Sala ya Baba Yetu inasema “usitutie majaribuni”. Je, Mungu anaweza kufanya hivyo?

Wadau kwa Wakristo katika ile Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni kuna maneno yanasomeka kuwa " Usitutie Majarubuni bali utuokoe na yule Muovu."Swali langu je Mungu anaweza kututia Majaribuni?Mie naamini Mungu anatupenda je anaweza kutufanyia hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiswail kina uhaba wa maneno ila Mungu hamjaribu MTU Bali anampima kama amefika level flan akuinue zaidi, kama vile shulen twapewa mitian tuvuke madarasa..i

Kimbembe ni shetan yeye akikujaribu nia yake akuangushe ushindwe kuendelea mbele japokua hawez kufanya HVO bila kibali cha Mungu..na Mungu akimpa kibali ujue ameshapima hlo jaribu na ameona unalimudu kabisa HVO ukishindwa na kwa ujinga wako.
 
Kwa hiyo shetanu huomba kibali kwa Mungu ili akujaribu,,,,ukishindwa basi ni moja ya mapungufu yako ambayo Mungu alikuumba pamoja nayo na Mungu mwenye analifahamu hilo kabla hujazaliwa!!!!!!

Lakini baada ya kushindwa hilo jaribu Mungu atakuhukumu !!!???
Hakuna aombaye apitie majaribuni isipokuwa ni njia mojawapo shetani hushitaki Watu wa Mungu kuwapima imani na huomba kibali kwa Mungu kama ilivyokuwa kwa Ayubu.

Kumbuka "imeandikwa usimjaribu Mungu wako" so ikiwa unapitia majaribu tambua uko kwenye kipimo cha imani lkn Mungu hujivunia wakati huo ikiwa utasimama imara hadi utaposhinda jaribu lako kuwa jns gani unamtegemea na kumuamini Mungu ktk kila jambo hata upitapo ktk uvuli wa mauti.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hyo jamaa itakua ni washkaji wazuri tu si ndio
Ndio apo ninapoamini kuwa Mungu na shetani kuna kipindi wanakubaliana kwenye bahadhi ya mambo lakini vile vile shetani ana mamlaka ya ndani ila kuna bahadhi ya vitu hawezi kuvifanya hadi aombe ruksa kwa Mungu mfano kama Tanzania na Zanzibar. Zanzibar wana mamlaka yao ya ndani lakini bahadhi ya mambo lazima waombe ridhaa ya serikali kuu (Tanzania)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kwa kilugha inanoga zaidi “and lead us NOT into temptations, but deliver us from evil”.
Huwa tunamuomba Mungu atuongoze kwenye njia ambayo itatuepusha kukutana na vishawishi vinavyoweza kututia majaribuni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wadau kwa Wakristo katika ile Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni kuna maneno yanasomeka kuwa " Usitutie Majarubuni bali utuokoe na yule Muovu."Swali langu je Mungu anaweza kututia Majaribuni?Mie naamini Mungu anatupenda je anaweza kutufanyia hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaweza tena ukishinda hayo majaribu anakupa darajakubwa sana before and after death..
Speaking of death sio kitu vibaya alieshinda majaribu
 
Mwanadamu mwenye kumcha mwwnyezi Mungu ni lazima ajue utofauti wa giza na Mwanga.Uwezi kujua giza linafafanaje na linatofauti gani na mwanga bila kutiwa katika hilo giza.Majaribu yatokayo kwa Mungu yanalengo la kukuonyesha Mungu anafananaje na ana nguvu gani.Yana lengo la kukutoa kwenye level moja ya imani kwenda nyingine,uwezi kuesabiwa kuwa umekuwa kiimani bila mtu kuangalia majaribu uliyopitia na jinsi ulivyoyashinda.

Mwanadamu kila siku anatamani baraka nyingi za kiuchumi.Hizo baraka kuzifikia lazima upewe mitiani tena mingine mikubwa .Wale waliokusudiwa kuwa kwenye mamlaka makubwa watapata mitiani mikubwa.Uwezi kuwa na huruma kwa mwenzako kama hujawai kupitia hali anayopitia mwenzako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo ni kiswahili chetu kinashindwa kutofautisha..lkn kizungu kiko sawa kuna "temptation" na "test" ....


MUNGU anaruhusu "test" kwa maana km utafeli hiyo test hauwezi ingia dhambini,ila unakuwa umekosa nafasi ya kupanda daraja...lkn temptation ambayo huifanya shetani,lengo lake ni kukuingiza dhambini..

ayubu aliingia kwenye "test" lkn ndani ya test akaingia kwenye "temptation" pale mkewe alipoingiwa na shetani na kumwambia "mkufuru MUNGU ukafe" hy ni temptation..wkt shetani anamwambia yesu "km ww ni mwana wa MUNGU" hakuwa anamtest bali alikuwa akifanya temptations..akiwa na maana km atakubaliana nae tuu,basi angemuingiza dhambini,hy ni km ile ya ile ya mke wa ayubu "mkufuru MUNGU ukafe"...jibu la yesu likamaliza utata wote ule "usimjaribu BWANA MUNGU wako" shetani akaishia hapo..kwa wale wenye kuuliza "je MUNGU alijaribuwa na shetani?" jibu ni "ndio" na ndipo tunaona shetani aki "ufunga" mdomo wake alipokumbushwa kuwa "anakufuru" anapojaribu kumjaribu BWANA MUNGU wake...

ngoja niishie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msamiati wa Kiswahili bado ni mdogo.
Jaribu 1 = testing
Jaribu 2 = temptation
Zipo tofauti kati ya testing - dokimazo
Na temptation (peirazo)

Testing (Jaribu) - Uratibiwa na Mungu ili kupima na kukomaza imani zetu. Mungu kamwe hafanyi temptation kwa kiumbe chake (Yakobo 1:13) pia hata Yeye hajaribiwi (Shetani, husimjaribu BWANA Mungu wako).
Ibrahimu, Ayubu, Waizraeli ... wote walijaribiwa (Dokimazo) - angalia 17:10, Zaburi 26:2, Kumbu 8:1-2.

Temptation (Jaribu) - Uratibiwa na Shetani kwenda kwa binadamu ili atende dhambi.
Angalia: 1 Wathesalonike 3:5, 1 Wakor 7:5.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja niongeze kidogo mkuu.

TESTING ambayo MUNGU MWENYEZI anaifanya kwa mja wake huishia na matokeo chanya.Mwishowe anashinda.Anavuka ngazi moja kwenda ya juu zaidi.

TEMPTATION ambazo shetani anazifanya kwa mwanadamu Mara nyingi huwa na mwisho mbaya.Binadamu Kama sio mcha MUNGU wa kweli anaanguka na kutenda dhambi.Endapo MUNGU MWENYEZI ataingilia kati, hii temptation itafeli.

KWA MCHA MUNGU WA KWELI TEMPTATION NA TESTING VYOTE ANASHINDA MAANA MUNGU MWENYEZI ATAMWOKOA KWA VYOTE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu aliruhusu mtumishi wake Ayoub ajalibiwe.
Wakati mwingine majaribu hayana budi kuja ili kuzipima imani zetu kwa Mungu mwenyezi.
Na tunapoomba asitutie majaribuni tunamaanisha sisi ni dhaifu atuzidishie imani
Yeah.
Wakati mwingine Mungu utujaribu ili kufunua mioyo yetu na kuweka wazi dhamira zetu mbaya. Mfano: Mara baada ya Kaini kumuua Abel nduguye, Mungu alimjaribu (testing) Kaini kwa kumuuliza, "Yu wapi Abel nduguyo?"; si kwamba Mungu alikuwa hajui aliyofanya Kaini, Mungu alijua sana tu, but alitaka Kaini dhamiri yake moyoni imshtaki yeye mwenyewe kuwa alitenda jambo baya mbele za Muumba wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau kwa Wakristo katika ile Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni kuna maneno yanasomeka kuwa " Usitutie Majarubuni bali utuokoe na yule Muovu."Swali langu je Mungu anaweza kututia Majaribuni?Mie naamini Mungu anatupenda je anaweza kutufanyia hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kinaweza kumpata mtu kama Mungu hajaruhusu. Hili limewekwa wazi kwenye kisa cha Ayubu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu aliruhusu mtumishi wake Ayoub ajalibiwe.
Wakati mwingine majaribu hayana budi kuja ili kuzipima imani zetu kwa Mungu mwenyezi.
Na tunapoomba asitutie majaribuni tunamaanisha sisi ni dhaifu atuzidishie imani
Na hapa ndipo Mungu aliponivuruga zaidi ufahamu baada ya kukaa na shetani na kufanya nae mazungumzo kwamba amtese ayubu ila asimuue.

Sasa ina maana Mungu na shetani wana ushkaji na ukaribu hadi kiasi cha kupiga story? Hawa wakuu isije kuwa wanaelewana fresh tu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom