... Well said mkuu, but uache ku quote whole text unasumbua Watumiaji wa simu.Binafsi nasema changamoto walio nayo madereva wa tax nchini ni bei languzi wanazokutajia kama mteja.
Mfano.. Uber kutoka posta to airport ni sh10,000 assuming hakuna foleni wakati tax ya kawaida usipungukiwe elfu 25. So madereva tax wajitathmini kabla ya hilo kwanza.
Duniani ktk nchi zilizoendelea tabia ya madereva wetu hawa hawawezi kufanya kazi kwani wao wamezoea kuvizia wateja kama sehemu huijui driver wa uber anakufikisha bila kukuyumbisha kwenye malipo lakini ikitokea kwa normal tax driver kama ni karibu basi atakuzungusha weee ili ujue ni mbali. Nakumbuka enzi nasoma kutoka njombe mjini hadi njombe sec (njoss) nauli elfu 2 lakini dereva atakuzungusha ilimradi utoe elf10.
Sasa katika hili wenzetu uber wanakaunti distance na time angalia mfano hapo kwa hiyo kwa abiria hakuna tena mda wa kujadili bei.
Pia Usalama. kama umesahau mzigo wako unakuwa salama wakati hizi tax za kawaida unakuwa huna taarifa za gari ulikuwa umepanda iliwemo namba ya dereva.
Kwa ujumla madereva wetu wana shida na wanahitaji kubadilika sana na mfumo wao wa kizamani huo lasivyo dunia itawapita .
Afu hata issue ya mabasi ya mwendo kasi mi sikuona sababu ya kuondoa daladala za kawaida. Wangeachwa washindane katika kutoa huduma, ingekua poa sana kwetu sisi Wateja.Kwa nini nilipe shs 20,000 badala ya sh 10,000 kwa sababu tu nataka kulisaidia taifa? Hapa nalisaidia taifa au dereva taxi anayenigonga nauli? Nimelipa Uber shs 14,000 toka airport mpaka Ubungo saa 7 usiku wakati hapo airport taxi wangenichaji shs 40,000!!. Ma taxi drivers waache kulalamika. Ushindani ni bora kwa mtumiaji.
kumbe we mbebez una upeo mdogo hivyo au kwa kuwa umehongwa hicho ki vits bas huthamini maslahi ya madereva taksi. mbebez wa bongo mna shida sanaSioni ubaya wala tatizo la Uber kuwepo nchini.
Na ningependa kuwaona na Lyft nao wakija pia.
Badala ya watu wa teksi kulalamika, ingekuwa vyema wangejiangalia na kuboresha zaidi huduma yao ili iweze kwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia na hivyo kuweza kushindana na makampuni kama Uber.
Ridesharing ndo habari ya dunia kwa sababu.
So either get with the program or get the hell out.
Sio lazima Uber,iondolewe,hata tigo wameanzisha yao inaitwa Twende,Uber inasaidia sana kwanzaMpendwa,
Tuwe tunajitahidi kujiongeza kabla ya kuwa wajuaji wa kuwaelimisha wengine. Unadhani nimekurupuka tu kuandika hili? Aliyekuambia Uber ninsoftware tu ni nani rafiki yangu? Tumia vema hata internet tu itakusaidia kufahamu mambo kwa undani kabla ya kuwaona wenzako washamba
sikumbuki nilipanda lini mara ya mwisho no offense lakiniSi upande daladala nauli tsh 400/- tu
Sio upeo mdogo,_hawa madereva wa Taxi zakawaida,walitutesa sana,kwanza hawapunguzi bei,wanaringa,hata kama una mgonjwa au mzazi,hawajui hilo.kumbe we mbebez una upeo mdogo hivyo au kwa kuwa umehongwa hicho ki vits bas huthamini maslahi ya madereva taksi. mbebez wa bongo mna shida sana
We mbwiga ili uuze chakula ni lazima kikaguliwe na mamlaka za unaotaka kuwauzia hicho chakula. Wanalinda afya ya mwananchi wao.Ndugu yangu,
Nipanic kwa lipi? Mjadala na kutoa mawazo? Labda lingine. Nikipanikishwa na majadala na chaki imenishinda
Mimi nimereact kwenye maoni yako kama wewe ulivyoaract kwenye yangu na ni baada ya kuona maoni yako yanajenga hoja nje ya hoja zangu. Ukisoma ujumbe wangu una mambo kama sita ambayo nilidhani wewe na wengine mwaweza kuyaona humo. Ngoja nikusaidie kukuweke summary:
MOJA: Tuna tatizo la ubora wa huduma za Taxi na ni sahihi kabia kutafuta njia za kukabiliana na hili tatizo.
PILI: Pili, pamoja na uwepo wa tatizo hili sio sahihi kuruhusu kampuni za nje kuwekeza kwenye sekta ndogo kama usafiri wa taxi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa na kutegemewa na watu wa kipato cha chini (hili nimefananua vema kwenye ujumbe ni kwanini)
TATU: Nchi zote duniani (hasa zilizoendelea) zina sera ya kulinda ajira na biashara za watu wake. Ndio mana nimeuliza unadhani kwa nini wewe machungwa yako na maembe na maziwa huruhusiwi/huwezi kuja kuyauza Ulaya
NNE: Kwa kutumia maarifa haya haya ya uwezekano wa kuboera huduma kwa kutumia teknolojia, tunaweza kufanya hivyo kwa kuboresha usafiri wa Taxi DSM. Kwanza kuonfokana na mfumo wa kienyeji wa kumiliki na kutoa huduma na pili kutumia mifumo itakayosaidia kuongeza ufanisi na kupunguza bei. Hatuhitaji makampuni ya nje kuwekeza kwenye taxi ili tupate akili za kuwa na ushindani.
TANO: Tutumie wataalamu wetu kutengeneza mifumo ya kumanage huduma ya Taxi (na zingine pia) maana tunao na wanaweza. Na tukifanya hivyo tutakua tumefanya zaidi ya kuboresha huduma za usafiri wa taxi
SITA: Viopngozi watumie watafiti/wasomi/wagunduzi wetu kama sehemu ya mikakati yao ya kutafuta suluhisho endelevu la changamoto zetu hilo la Taxi likiwa mojawapo.
Haya nilitegemea yawe wazi kwa mtu aliyesom aujumbe wangu kabla ya kuanza kutoa lugha za sijui siifahamu Uber, sijafanya research, ni mjinga, nk.
uber mkombozi sana, sa nyingine unajisikia vibaya unatamani kupanda taxe ila wakikutajia bei unahisi kupona na kwenda kupanda daladala.unakosea, uber ni mkombozi katika huduma hii ya usafiri, inawezekana na wewe ni mmoja wa madereva tax mnaotaka kunyonya wananchi, ilifikia hatua kupanda taxi si huduma tena ni kama anasa, hatuwezi kuikimbia teknologia, sio wewe wala makonda mtazuia hili...kwani hao madereva wa uber ni wamarekani?si watanzania wenye magari yao?wanapata faida au hawapati?kodi inalipwa au hailipwi?kwanini hao madereva kama wanataka kutoa huduma nafuu wasijiunge na uber kama lengo lao ni kumsaidia mtanzania mwenzao na si kumnyonya?hii ishu ina conflict of interest...kama ukitumia taxi ya wabongo unalipa 30,000 na ukitumia uber unalipa 10,000 ni kipi bora?acheni mambo yenu kutuongezea machungu ya maisha
we nae mbebez tu. hebu soma tena maelezo ya mtoa mada kabla hujajibu kwa haraka kama umemiss dudyu vileSio upeo mdogo,_hawa madereva wa Taxi zakawaida,walitutesa sana,kwanza hawapunguzi bei,wanaringa,hata kama una mgonjwa au mzazi,hawajui hilo.
Ukisahau mzigo,ndio basi,humpai tena.
Mkuu mimi nimekuelewa sana. Nilikuwa najaribu kuondoa fikra potofu kwamba maslahi yako yameguswa ktk hili suala la Uber. Ndio nikatoa pendekezo kama kuna chembe yeyote ya kukutilia shaka basi ingekuwa ni kuihusisha na taaluma/fani yako. Sasa nilivyoisoma jamii ya wana JF ni kosa kubwa kusifu au kukubali jambo lolote liwe jema au baya toka kwa Paul Makonda au kwa mtu aliemteua nafasi anayoshikilia serikalini. Kama ungeanza kumponda Mh. Makonda na serikali ungepata kuungwa mkono sana na pengine ungegeuka shujaa bila kujali mantiki ya hoja zako na maslahi mapana ya taifa hasa watanzania wa hali ya chini.Ndugu yangu sihitaji deal lolote na wala sina kampuni ya kuunda mifumo. Sina biashara yoyote hata ya kuuza sambuza wala ya kuendesha baiskeli. Ila ninawajibika kwa nchi yangu kutoa mchango wa mawazo na utaalamu wangu kwa ajili ya manufaa ya watu wake. Mchango wa fikra ndio jukumu kubwa tulilopewa na nchi yetu bila kujali wako wataoana ni za kipuuzi au zina mashiko. Na michango kama hii ya mijadala ni sehemu tu.
Pili michango mingi inayotolewa hapa inaonesha tuna udhaifu mkubwa sana kama jamii. Kwamba mtu hawezi kutoa maoni na ushairi wake juu ya jambo fulani hadi awe na maslahi nalo. Nazidi kumuelewa Rais JPM kwa nini anatuambia nchi ilishabadilishwa kuwa deal maana kila mtu anadhani mwingine anayongea yanatokana na maslahi binafsi. Kwa hiyo tunatakan watu waogope kutoa mawazo yao kwa sababu wataonekena wana maslahi? Ni taifa la watu gani liso na tofauti ya mawazo na mitazamo katika mambo yahusuyo maslahi ya watu wake? Munataka akina Uber tu ndio waje wawasaidie kuwaza na kuwapa solutions za matatizo yetu?
Bado najifunza
Sioni ubaya wala tatizo la Uber kuwepo nchini.
Na ningependa kuwaona na Lyft nao wakija pia.
Badala ya watu wa teksi kulalamika, ingekuwa vyema wangejiangalia na kuboresha zaidi huduma yao ili iweze kwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia na hivyo kuweza kushindana na makampuni kama Uber.
Ridesharing ndo habari ya dunia kwa sababu.
So either get with the program or get the hell out.
Noma
Kama andiko hili ni la Mwalimu tunaempa wadogo zetu awatoe ujinga, sishangai kwanini kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaopata zero inaongezeka....
Na walimu wa dizaini hii ndio sababu ya kwanini serikali hailipi deni lenu miaka nenda rudi...
Kutoka Ubungo mpaka mwenge niliwahi kupanda taxi kwa shilingi 25,000 ... Leo kwa umbali huo huo nilipanda uber taxi kwa shilingi 8500/=...... Ni kichaa tu ndio anaweza asione tofauti yoyote hapo....
Mlizoea kula msivyopaswa kula na acheni kulia lia kuweni wabunifu kwenye taxi zenu msitegemee Huruma ya serikali.... Nchini kenya kampuni ya uber wameweka mpaka helicopter , sijaona wanalalamika hovyo hovyo, ila tunaona daladala zao wanavyozifanyia ubunifu .. Wanaweka mpaka WiFi.... Na nyie kuweni wabunifu mwisho wa siku mteja ndio muamuzi wa mwisho kuangalia Huduma bora yenye gharama nafuu...
Ilifikia nauli ya taxi humu humu dar inazidi nauli ya kutoka dar mpaka mtwara... Tuachieni uber kama mnaona hamuwezi kuwa creative kalimeni....
Serikali kwa maana ya Kodi na gharama nafuu kwa msafiri.Hivi uwepo wa Uber nchini unamnufaisha nani kwani?