Edson Carrington
JF-Expert Member
- Oct 30, 2022
- 216
- 634
Kwanza nianze na salamu kwa wana JF wote nikiamini ni wazima na mnaendelea vizuri.
Pili niende moja kwa moja kwenye muktadha wa uzi huu kuwa hauna nia ya kudharau, kupotosha au kuchochea suala lolote la udini wala siasa.
Moja kwa moja tukienda kuangazia sakata linaloendelea huko magharibi mwa dunia, linalohusu mataifa mawili yaliyo kwenye mgogoro wa kihistoria duniani Palestine na Israel, ambapo kihistoria inaonyesha haya ni mataifa yanayowakutanisha ndugu wawili (Ismaili na Yakoub) kwenye chimbuko lao kutoka kwa baba yao (Ibrahim).
Na pia tukiangazia haswa kwenye sakata hili utagundua chimbuko kuu ni ardhi ya ukanda wa GAZA inayogombewa kati ya mataifa haya mawili enzi na enzi.
Sakata hili limezua vita vya mara kwa mara vikiambatana na vifo kwa kiasi kikubwa sana. Huku mhanga mkubwa akiwa Palestine ambaye amekuwa kama mdogo kwa Israel.
Lakini pia tukiangalia upande wa imani kati ya mataifa haya utagundua ni dhahiri ni moja ya vitu vinavyochochea vita hii, ambapo kwa macho ya kawaida huwezi liona suala hili lililojificha. Hii isingekuwa vita kubwa duniani kama ingehusisha mataifa yenye idadi kubwa ya watu wenye mchanganyiko wa dini. Kwani isingepelekea baadhi ya watu kutaka ingilia kwa kigezo cha imani.
Kiukweli Uislamu umeshamiri kwa kiasi kikubwa sana kwa upande wa Palestine.Na hawa ni watu wanaoamini kwa Allah S.W na mtume wake S.A.W
Na pia kwa upande wa Israel utagundua kuwa wengi wao wana asili ya kiyahudi toka enzi na enzi mpaka sasa. Hawa ni watu wasiokuwa na dini na wasioamini uwepo wa nguvu iitwayo Mungu, wanaamini hakuna Maisha baada ya kifo (Na ndio maana huogopa zaidi kifo), ushoga, uasherati nk. Watu hawa hufahamika kama makafiri kwa upande wa Palestine.
Kutokana na kanda hizi kushamiri kwa imani hizi imetengenezeka dhana inayo ashiria vita hii ni kati ya waislamu na makafiri kwa upande wa dunia na hii inajengeka maeneo mbalimbali duniani. Kwa upande wa uislamu huamini kuwa waislamu wote ni ndugu duniani, na tatizo linapomkuta muislamu mwenzako unapaswa kuwajibika kumsitiri mwenzako.
Uislamu pia huamini kuwa kuna aina mbili za dini hapa duniani kwani ni uislamu na ukafiri, na hili ndilo linalojidhihilisha kwani tayari vita hii imegawa watu wengi duniani kwenye pande mbili. Baadhi ya watu wameonekana kusupport upande fulani kutokana na imani tu kati ya mataifa haya. Kwani si ajabu baadhi ya watu wamekuwa wakisupport upande fulani ili kuikandamiza dini fulani.
Ukipita mitandaoni utakuta kila mtu ana upande wake, huyu Israel na huyu Palestine, huku kiini kikuu kikiwa ni dini zilizonyuma ya mataifa haya. Ambapo huwezi mkuta akiliongelea hili lakini ni dhahiri kabisa.
Lakini baada ya yote, sote ni binadamu na kikubwa tuombe salama kwani vita sio ya kushabikia kwani wanaoumia ni binadamu kama sisi.
Mwenyezi Mungu ndie ajuaye yote kuhusu sisi, hatuna haja ya kumwachia yeye kwani asemayo kwenye vitabu tunayaona kwa macho.
Ngoje tukae tuendelee kuangalia.
Sent using Jamii Forums mobile app