Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,641
- 46,295
Wayahudi au wengine wakiwaita mazayuni ni watu ambao wameishi Palestina/Israel tangu takribani miaka 1200 kabla ya Kristo. Historia yao ni ndefu sana na ipo katika vitabu vya dini na visivyo vya kidini kuonyesha wamekuwepo hapo walipo sasa kwa muda wote. Hapo Israel ndio nyumbani kwao hasa.
Tawala au Himaya mbalimbali zimekuwa zikiwafukuza na kuwatawanya duniani kote lakini wamekuwa wakirudi, na hata katika huko kutawanywa kwao sio wote huondoka katika ardhi yao.
Tofauti na jamii nyingine Wayahudi ni watu wasiojichanganya au kupoteza mila na tamaduni zao popote wanapokwenda jambo mojawapo linalowafanya kuwa walengwa rahisi wa chuki katika maeneo wanayofikia.
Baada ya wengi wao kutawanyika kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali karne ya 20 kwa sababu nyingi walijikita na kujielekeza kurudi kwa wingi katika ardhi ambayo wazazi wao waliishi kwa karne zote. Hapo ndipo vurumai za kila aina zilipoanza lakini baya zaidi ni kwamba waliokuwa wakifikiria hiyo ardhi yote ya Israel ni yao, Wapalestina na Waarabu wengine walikataa kata kata kuwatambua kama ni sehemu ya ardhi hiyo.
Waarabu wakiwa na msimamo mkali walikataa mpango wa Umoja wa mataifa wa azimio 181 wa mwaka 1947 kuunda mataifa mawili ya Israel na Palestina. Israel walichofanya wakachukua sehemu yao na kuanza kujitanua hata katika maeneo ya Wapalestina nyakati za viongozi wenye msimamo mkali kama huyu Benjamin Netanyahu waziri wao mkuu wa sasa.
Huu mgogoro umeshapelekea hata kuuwawa kwa waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin mwaka 1995 na Muisrael mwenye msimamo mkali kutokana kuonekana kwamba alikuwa akiurejea mpango wa mataifa mawili kupitia Oslo Accords kwa nguvu sana.
Kuna wakati Mahomoud Abbas,kiongozi wa Wapalestina upande wa West Bank aliwahi kusema yalikuwa ni makosa makubwa kwao Wapalestina na Waarabu kuukataa mpango wa UN wa mataifa mawili wa mwaka 1947.
Pia watu wenye msimamo mkali upande wa Israel kama Waziri mkuu wa sasa, Netanyahu wamekuwa wakifanya jitihada zote kuhakikisha suala la mataifa mawili Halifanikiwi pia, mpotezaji mkubwa katikati ya haya yote amekuwa Palestina kwa sababu imeendelea kudhoofika huku Israel ikipata nguvu zaidi na kuwa mtawala wa eneo lote.