Elections 2010 Sakata la mauaji ya Dereva wa CCM Maswa na hatima ya Shibuda

Makamba alikuwa kule siku ya tukio, bila shaka yeye ndiye aliyeingineer haya mambo yote. Lakini Mungu akiwa upande wetu ni nani atakuwa kinyume na sisi? Tuzidi kumwomba Labuka.
unajua ukimwangalia makamba. ana taswira ya mtu asiyefaa kuwa rafiki.
NI MWANAJESHI na ana kiu ya kuua
anaua demokrasia kwenye chama chake na nchini

Hiyo haitatokea NEc sio wajinga wa kiasi hicho ,TBc wanahalarisha Shibuda kuchukua jimbo hata kama hatarudi kwenye kampeni mpaka siku ya mwisho madiwani waliosimama kwa tiketi ya Chadema waendeleze libeneke,viongozi wa chadema wasiowagombea wakaweke kambi kule wasaidiane na madiwani kuendeleza kampeni
Pale wenyewe CCm limewakauka baada ya mgombea wao kumkata ngwara OCD akiwa amevaa nembo ya Taifa na kumuachia akidunda tuu ,manake nini wanachi wataendelea kuwakata ngwara mapolisi kwa kiasi wanachotaka wakijua RPc hatafanya lolote kwa sababu ni mambo yao ,hasira hasara wangeacha sheria ichukue mkondo wake badala ya kupindisha sheria kwa ajili ya kumkoa mtu wananchi wanajua mbivu na mbovu haki ya mtu haipotei
 
Hizo habari umezipata wapi - kwamba kaambiwa ajitoe ubunge?

Well, kama NI KWELI naona wanachemka tu. Si anaweza kukubali kwamba anajitoa then akifika kitaa anauchuna. Watamrudisha ndani?
husemi bila ya kusaini fomu kaka! hatuendi kirahisi rahisi namuna hiyo bro. unadondoka signature! mambo yanakwisha
 
Haiingii akilini kuona Shibuda anakamatwa haraka na hata kule kuhisiwa kuwa hajakamatwa OCD apigwe na bado aliyempiga asichukuliwe hatua. Kwa kuwa Shibuda alikuwa kwenye eneo jingine mbali na tukio na hata alikuwa akiwa kwenye uwanja wa mkutano umbali wa kilometa moja lakini bado ananganganiwa inatia wasiwasi. Kwa kuwa kifo kilichotokea kilipaswa kuchukuliwa kuwa ni matukio ya vurugu na wale waliokuwa eneo la vurugu wangepaswa kukamatwa na kuhojiwa bila kuwa na ulazima wa kumkamata mgombea aliyekuwa mbali na ambaye wala hajasikika akitamka maneno ya uchochezi.

Kuna kila sababu ya kufikiria kuwa kuna jambo juu ya kifo hiki. Ni kawaida mwanadamu kufikiri na kujaribu kupata majibu kwa kila swali lenye utata ili kujiridhisha kuwa mkondo unaofuatwa wa haki.

KATIKA HALI YA KAWAIDA NA YA KUTAKA UKWELI KUJULIKANA NA KWA KUWA KUNA VIFO VENYE UTATA VIMEKUWA VIKITOKEA NDANI NA NJE YA CCM KATIKA NYAKATI KAMA HIZI AU KATIKA MAZINGIRA TATANISHI KUNA HAJA YA MAKAMBA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM MASWA KUKAMATWA.

Ninajua watu wengi wanaweza kwa haraka kupuuza madai yangu lakini kwa akili ndogo watu wa kawaida wanaweza kujiuliza maswali kadhaa ambayo kuna haja ya kuthibitishiwa bila wasiwasi kuwa ni kweli au sio kweli.

Kuna mambo yaliyowahi kutokea kwenye chama cha mapinduzi yaliyoacha maswali hadi leo. Horace Kolimba aliwahi kufa akihojiwa na hadi leo wale waliokuwa wanamhoji hawakuwekwa ndani.
Leo anauawa mtu wakati mgombea wa CHADEMA YUKO KWENYE MKUTANO UMBALI WA KILOMETA MOJA YEYE ANAWEKWA NDANI.
1. Je ingewezekanaje Shibuda kujua kuwa kuna watu watapita na wakifika hapo watashuka kujisaidia hivyo atume watu wakamuue?
2.Kati ya Makamba, mgombea ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi kupitia CCM, Robert Kisena na SHIBUDA ni nani ambaye alijua kuwa dreva wa Kisena atapita maeneo hayo na kwa muda huo?

3. Je hatujawahi kuona CCM ikijaribu kutumia kifo cha Mtu kupata ushindi wa kura huko Tarime?

4. Kwa kuwa Makamba alifika eneo la tukio na pia wao na Kisene walionyesha kuwa ni muhimu Shibuda kukamatwa haraka basi maswali ni kuwa tutajuaje kuwa wao wamehusika kwa njia moja au nyingine ili kuthibitisha kauli inayotolewa na JK kuwa vyama vya upinzani vinamwaga damu?

5. KULE KISENA KUMVAMIA NA KUMPIGA OCD "kwa kutokutekeleza maagizo , pengine na mpango"
Kunaacha maswali makubwa juu ya zinakotoka nguvu za mgombea wa chama cha mapinduzi kuwa juu ya sheria na kutokuchukiwa hatua. KUNA NGUVU GANI KUBWA INAYOOGOPWA KIASI CHA KULIFANYA JESHI LA POLISI LIDHARAULIWE KUWA NI KALI TU KAMA JAMBO LINAWAHUSU UPINZANI?
RAIS WETU MPENDWA , SIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA BILA UPENDELEO.

Tatizo la kutokusimamia sheria kuna siku itakuja kukugeuka nawe uathiriwe kukosa haki au faida kwakuwa haikufuata mkondo wake. Kama inawezekana Shibuda kukamatwa naomba uwezekano wa wao Makamba na Kisena kuhusika kwa sababu nilizozitaja zitumike kuwakamata na wahojiwe.

Naomba kutumia uhuru wangu wa kuwaza kwa sauti kubwa kuwa hata kama tunajaribu kuonyesha kuwa haya ni mazingira ya vurugu lakini Swali linabaki kuwa
a) Iweje watu washuke kujisaidia haja ndogo mahali penye watu?
b) Kama hapakuwepo na watu walitokea wapi kwa haraka?
c) Kama kweli waliwachokoza watu wa CHADEMA nani ajuaye aliyemuua kwa kitu chenye ncha kali?
d) Je mwili wa huyu umefanyiwa postmortum?
6. Bila aibu JK ameanza kutumia tukio hilo kulifanyia kampeni, hili nalo linaacha maswali mengi kuliko majibu. Nchi nyingine wanatumiaga umafia wa jinsi hizi maji yakiwafika shingoni.
7. Naomba mnifikishie ujumbe kwa Manumba na CHADEMA kuwa MAKAMBA AWEKWE NDANI NA KISENA au wahojiwe.
Kwa kuwa ni haki kuwa na mawazo haya basi ni muhimu yadhibitishe kuwa sio mawazo ya kweli.
Njia ya kudhibitiha kuwa hakuna hila juu ya kifo hiki na kuwa hakuna mchezo wa kutumia vurugu kupeleka picha mbaya kwa jamii naomba MAKAMBA NA KISENA wakamatwe kwa haki na wathibitishe kuwa hawakuhusika na mpango mchafu wowote.

Mwajiriwa mmoja wa kampuni kubwa ya ujenzi alikuwa anastaafu. Na kwa kuwa alikuwa mjenzi mzuri aliyeanza na kumaliza nyumba yote kwa ustadi mkubwa, mwajiri wake alimpenda sana.
Alimuomba aongeze muda ajenge nyumba moja zaidi kabla ya kustaafu. Alifanya hivyo na alipomaliza aliikabidhi nyumba ile iliyojengwa kwa ustadi na ubora wa hali ya juu.

Baada ya kupokea nyumba ile mwajiri alimwambia , naomba uongeze muda tena unijengee tena nyumba moja tu na hii itakuwa ya mwisho sitakuomba uongeze tena muda.

Yule jamaa akaona kuwa itakuwa mchezo dawa nitajenga hii vibaya akasirike aachane na mimi.
Akatumia vifaa duni na hata mafundi wa bei rahisi katika ujenzi na kiwango kilikuwa hakiridhishi.
Alipomaliza alienda kwa tajiri akampelekea funguo akisubiri akakague na kisha akasirike waachane.
KWA MSHANGAO AKAMWAMBIA, NYUMBA HII NDIYO ZAWADI YAKO NILIYOKUSUDIA KUKUPATIA.
CHUKUA FUNGUO HII NI MALI YAKO.
Ni muhimu mambo yafanyike kwa misingi ya haki. Unaweza kadhani unamaliza muda wako ukapinda sheria hatimaye ukakuta hukumaliza muda na ukaathiriwa na sheria ulizopinda. Au ukadhani unaongeza muda ukakuta huongezi na uonevu iliowafanyia wengine ukawa ni wewe kufanyiwa.
Kama CCM mkishinda uchaguzi mnataka kupokea nchi isiyo na sheria?
NASISITIZA HAKI ITUMIKE NA SIO SIASA KATIKA MAMBO YANAYOHUSU UHAI WATU.
Kama kweli Shibuda maehusika basi akamatwe na hata afungwe kama kuna ushahidi. Lakini kama shida ni visa vya kisiasa tu acheni huo mchezo.
:amen:
 
Kwa kweli kama ni njama za kupikwa, kumwaga damu ili kutumia njia hiyo kujinufaisha kisiasa, kama messeji iliyosambazwa siku ya jana kwamba CHADEMA wameamua kumwaga damu, ni UCHAFUZI WA ARDHI (NCHI) YETU. Kukimbilia kumkamata Shibuda, pasi na mazingira yoyote yanayoashiria kuwepo kwake katika tukio, si jambo jema kwa Watanzania wote.
 
Ndugu wanaJF hebu tuhabarisheni nini kianendelea kwenye jimbo la MASWA na hali ya kisiasa ya mpiganaji SHIBUDA. Jana tuu ilisemekana Manumba angeenda MAswa lakini hakuna taarifa zaidi juu ya sakata hilo. Kama ni njia ya kumtoa SHIBUDA kwenye kinyang`anyiro washindwe na walegeeee
 
HAKI INA KANUNI YAKE, ISPOONEKANA LEO ITAONEKANA TU SIKU MOJA NA HATIMAYE KUNA SIKU YA HUKUMU.

Matthew 10:26
"So do not be afraid of them. There is nothing concealed that will not be disclosed, or hidden that will not be made known.
 
Jamani wana jamii hivi ni halali Kwa Mh Chibuda kuwekwa ndani kwa maelekezo ya Kikwete? Hivi hii nchi hulka binafsi zinazidi utashi wa Sheria! Inakuwaje ahusishwe na mauaji ya dereva wakati hakuwepo katika tukio? Habari nilizopata Bw. Chibuda amepewa condition ya kuachiwa nayo ni kujitoa kugombea Ubunge kwa Chadema, sasa hii ni haki? kwanini wana jimbo wasiandamane kulazimisha aachiwe Mbunge wao? Uvumilivu unanishinda mie!

1. Shibuda ni mwana demokrasia wa kweli kwani alitaka kushindana na JK kwenye Urais ngazi ya chama
2. amehama CCM
3. ana mchango mzuri kwenye maendeleo ya nchi hii

Hivyo sababu kubwa ni visasi na JK ni nambari ONE kwa visasi Tanzania hii. Na ambaye ataamua hatima ya JK ni Mungu!
 
Proverbs 28:13
He who conceals his sins does not prosper, but whoever confesses and renounces them finds mercy.
 
Hapo hakuna uhusiano wowote kati ya kugombea ubunge na mauaji,mauaji ni kosa la jinai,linashughulikiwa kijinai,mambo ya kugombea ni masuala ya sheria za uchaguzi,tume ndo inaweza kumtoa asigombea kama amevunja sheria za uchaguzi.Kimazingira hakuna ushahidi kuwa amevunja sheria ya uchaguzi,kwanza alikuwa jukwaani wakati tukio linatokea.Pili kama taarifa zilivyosema wafuasi wa chadema walikuwa wanaelekea kwenye eneo la mkutano wa kampeni utakaofuata ndipo wakakutana na wafuasi wa ccm ambao haikujulikana walikuwa wanaelekea wapi.Kwa hiyo ukiangalia hapo unaona kuwa chadema hawakuwafuata ccm,bali ccm waliwafuata chadema,chukulia wamekutana kama ilivyosemwa,inakuwaje kofia isidondoke sehemu yoyote ile isipokuwa pale ambapo chadema wapo?Hii inaonesha kuwa ccm wamekuwa na tabia y uchokozi halafu wanakimbilia polisi maana wanajua polisi wameshapewa maelekezo na wakuu wa chama.
Kwa kuangalia mfululizo wa matukio ya ghasia yaliyotokea mpaka hivi sasa utagundua ccm wanatoa vijisababu tu ilimradi kujikosha wakati wanaingilia mikutano na misafara ya chadema waziwazi.Polisi nao wanawaacha tu wakijua fika ni nini kitatokea.Sasa mzaa mzaa hutumbuka usaha,walizoea mambo yataishia watu kujeruhiwa,lakini sasa ni maafa.
CCM wanafanya vibaya mno kuwatumia vijana kama chambo,sasa ona mtu anapoteza maisha halafu wao wanaona ni mchezo mzuri na kutake advantage,Ifikie hatua vijana wa ccm wakatae kuwa chambo kwani ni maisha yao na wakifa hakuna atakayewakumbuka.

Kesi iende mahakamani,hakuna atakayejitoa kwani mtuhumiwa wa mauaji hajitoi kugombea bali hupelekwa mahakamani,kama ingekuwa ni kujitoa kugombea basi Chenge asingekuwa anagombea.
inaumiza sana ila watanzania wanatakiwa walione hili na kuchukua hatua
 
haiingii akilini kuona shibuda anakamatwa haraka na hata kule kuhisiwa kuwa hajakamatwa ocd apigwe na bado aliyempiga asichukuliwe hatua. Kwa kuwa shibuda alikuwa kwenye eneo jingine mbali na tukio na hata alikuwa akiwa kwenye uwanja wa mkutano umbali wa kilometa moja lakini bado ananganganiwa inatia wasiwasi. Kwa kuwa kifo kilichotokea kilipaswa kuchukuliwa kuwa ni matukio ya vurugu na wale waliokuwa eneo la vurugu wangepaswa kukamatwa na kuhojiwa bila kuwa na ulazima wa kumkamata mgombea aliyekuwa mbali na ambaye wala hajasikika akitamka maneno ya uchochezi.

Kuna kila sababu ya kufikiria kuwa kuna jambo juu ya kifo hiki. Ni kawaida mwanadamu kufikiri na kujaribu kupata majibu kwa kila swali lenye utata ili kujiridhisha kuwa mkondo unaofuatwa wa haki.

Katika hali ya kawaida na ya kutaka ukweli kujulikana na kwa kuwa kuna vifo venye utata vimekuwa vikitokea ndani na nje ya ccm katika nyakati kama hizi au katika mazingira tatanishi kuna haja ya makamba na mgombea ubunge wa ccm maswa kukamatwa.

Ninajua watu wengi wanaweza kwa haraka kupuuza madai yangu lakini kwa akili ndogo watu wa kawaida wanaweza kujiuliza maswali kadhaa ambayo kuna haja ya kuthibitishiwa bila wasiwasi kuwa ni kweli au sio kweli.

Kuna mambo yaliyowahi kutokea kwenye chama cha mapinduzi yaliyoacha maswali hadi leo. Horace kolimba aliwahi kufa akihojiwa na hadi leo wale waliokuwa wanamhoji hawakuwekwa ndani.
Leo anauawa mtu wakati mgombea wa chadema yuko kwenye mkutano umbali wa kilometa moja yeye anawekwa ndani.
1. Je ingewezekanaje shibuda kujua kuwa kuna watu watapita na wakifika hapo watashuka kujisaidia hivyo atume watu wakamuue?
2.kati ya makamba, mgombea ubunge wa jimbo la maswa magharibi kupitia ccm, robert kisena na shibuda ni nani ambaye alijua kuwa dreva wa kisena atapita maeneo hayo na kwa muda huo?

3. Je hatujawahi kuona ccm ikijaribu kutumia kifo cha mtu kupata ushindi wa kura huko tarime?

4. Kwa kuwa makamba alifika eneo la tukio na pia wao na kisene walionyesha kuwa ni muhimu shibuda kukamatwa haraka basi maswali ni kuwa tutajuaje kuwa wao wamehusika kwa njia moja au nyingine ili kuthibitisha kauli inayotolewa na jk kuwa vyama vya upinzani vinamwaga damu?

5. Kule kisena kumvamia na kumpiga ocd "kwa kutokutekeleza maagizo , pengine na mpango"
kunaacha maswali makubwa juu ya zinakotoka nguvu za mgombea wa chama cha mapinduzi kuwa juu ya sheria na kutokuchukiwa hatua. Kuna nguvu gani kubwa inayoogopwa kiasi cha kulifanya jeshi la polisi lidharauliwe kuwa ni kali tu kama jambo linawahusu upinzani?
Rais wetu mpendwa , simamia utekelezaji wa sheria bila upendeleo.

Tatizo la kutokusimamia sheria kuna siku itakuja kukugeuka nawe uathiriwe kukosa haki au faida kwakuwa haikufuata mkondo wake. Kama inawezekana shibuda kukamatwa naomba uwezekano wa wao makamba na kisena kuhusika kwa sababu nilizozitaja zitumike kuwakamata na wahojiwe.

Naomba kutumia uhuru wangu wa kuwaza kwa sauti kubwa kuwa hata kama tunajaribu kuonyesha kuwa haya ni mazingira ya vurugu lakini swali linabaki kuwa
a) iweje watu washuke kujisaidia haja ndogo mahali penye watu?
B) kama hapakuwepo na watu walitokea wapi kwa haraka?
C) kama kweli waliwachokoza watu wa chadema nani ajuaye aliyemuua kwa kitu chenye ncha kali?
D) je mwili wa huyu umefanyiwa postmortum?
6. Bila aibu jk ameanza kutumia tukio hilo kulifanyia kampeni, hili nalo linaacha maswali mengi kuliko majibu. Nchi nyingine wanatumiaga umafia wa jinsi hizi maji yakiwafika shingoni.
7. Naomba mnifikishie ujumbe kwa manumba na chadema kuwa makamba awekwe ndani na kisena au wahojiwe.
Kwa kuwa ni haki kuwa na mawazo haya basi ni muhimu yadhibitishe kuwa sio mawazo ya kweli.
Njia ya kudhibitiha kuwa hakuna hila juu ya kifo hiki na kuwa hakuna mchezo wa kutumia vurugu kupeleka picha mbaya kwa jamii naomba makamba na kisena wakamatwe kwa haki na wathibitishe kuwa hawakuhusika na mpango mchafu wowote.

Mwajiriwa mmoja wa kampuni kubwa ya ujenzi alikuwa anastaafu. Na kwa kuwa alikuwa mjenzi mzuri aliyeanza na kumaliza nyumba yote kwa ustadi mkubwa, mwajiri wake alimpenda sana.
Alimuomba aongeze muda ajenge nyumba moja zaidi kabla ya kustaafu. Alifanya hivyo na alipomaliza aliikabidhi nyumba ile iliyojengwa kwa ustadi na ubora wa hali ya juu.

Baada ya kupokea nyumba ile mwajiri alimwambia , naomba uongeze muda tena unijengee tena nyumba moja tu na hii itakuwa ya mwisho sitakuomba uongeze tena muda.

Yule jamaa akaona kuwa itakuwa mchezo dawa nitajenga hii vibaya akasirike aachane na mimi.
Akatumia vifaa duni na hata mafundi wa bei rahisi katika ujenzi na kiwango kilikuwa hakiridhishi.
Alipomaliza alienda kwa tajiri akampelekea funguo akisubiri akakague na kisha akasirike waachane.
Kwa mshangao akamwambia, nyumba hii ndiyo zawadi yako niliyokusudia kukupatia.
Chukua funguo hii ni mali yako.
Ni muhimu mambo yafanyike kwa misingi ya haki. Unaweza kadhani unamaliza muda wako ukapinda sheria hatimaye ukakuta hukumaliza muda na ukaathiriwa na sheria ulizopinda. Au ukadhani unaongeza muda ukakuta huongezi na uonevu iliowafanyia wengine ukawa ni wewe kufanyiwa.
Kama ccm mkishinda uchaguzi mnataka kupokea nchi isiyo na sheria?
Nasisitiza haki itumike na sio siasa katika mambo yanayohusu uhai watu.
Kama kweli shibuda maehusika basi akamatwe na hata afungwe kama kuna ushahidi. Lakini kama shida ni visa vya kisiasa tu acheni huo mchezo.
:amen:

baada ya wapenzi wa chadema kuonyesha kukerwa na tukio hili jeshi la polisi limechukua hatua kali za kumkamata mgombea wa ccm kuhusika na tukio hili pia na wote wawili wako rumande. Ni imani yangu kuwa aliyepkuwa na ujasiri wa kumpiaga ngwara polsi mwenye cheo kikubwa kama ocd ndiye aliyepanga njama hizi na kupelekea kumwagaika kwa damu hiyo. Kama alivyosema dr slaa ccm ndio wenye uwezo wa kupanga vurugu, macahafuko na umwagaji damu na dalili za hali hiyo ni wagombea wa ccm kuwashambulia polisi.

Inastahili ocd aliyepigwa na rpc wa mkoa wa shinyanga aliyewajibu waandishi wa habari kuwa kupigwa kwa ocd ni suala binafisi kati ya ocd huyo na mgombea wa ccm wachukuliwe hatua za kinidhamua kwa kulidhalilisha jeshi la polisi kwa kumuongopa mgombea wa ccm kutokana na fedha zake
.
 
unajua ukimwangalia makamba. ana taswira ya mtu asiyefaa kuwa rafiki.
NI MWANAJESHI na ana kiu ya kuua
anaua demokrasia kwenye chama chake na nchini

Hivi kwanini nyie watu mnatafuta scapegoat kwa mambo mliyoyafanya wenyewe? To be a decent citizen, means owning up to your actions and be responsible about it. Sasa kila kitu mnaona mnaonewa. I mean, wafuasi wa Chadema wamempiga na kumuua dereva wa CCM--lakini Jambo Forum bado tu wanasema this was engineered by CCM. Come on. You can't possibly be this partisan.
 
CCM WAMWAGA DAMU MASWA

Katika kampeni za ubunge zinazoendelea Maswa magaribi kumetokea kifo cha dereva wa mgombea wa CCM (Robert Simon Kisena). Lakini hiki si kifo cha bahati mbaya ni kifo cha kupangwa na mgombea wa CCM anayeungwa mkono na Riziwani Kikwete, Makamba pamoja na Kikwete. Robert Kisena ambaye ni tapeli mkubwa anayejulikana kwa utapeli wake pia ni swahiba wa karibu wa Riziwani Kikwete.

Kulikuwa na mkutano wa CHADEMA uliokuwa unaendelea maswa magaribi huku gari moja ya chadema(land rover) ikiwa inazunguka maeneo ya karibu, ikiwa inawatangazia watu juu ya mkutano huo, ghafla ilitokea gari ya ccm(surf) ambayo ilitaka kuigonga gari ya chadema.

Gari ya chadema katika kukwepa ikatoka barabarani na mmoja ya watu waliokuwemo katika gari hiyo ya chadema aliangusha kofia hapo, na ikabidi ashuke kuichukua. Chadema waliposimamisha gari yao kuokota kofia ndipo CCM waliposhuka na kuanza kuwashambulia CHADEMA.

Watu wa CHADEMA kuona hivyo wakaanza kupiga kelele, wale CHADEMA waliokuwepo kwenye mkutano waliposikia wakaanza kuondoka kwenye mkutano kuelekea kwenye tukio. Huko kwenye tukio watu wa CHADEMA walianza kuwapiga mawe CCM mpaka wakakimbia na mmoja wao kukamatwa. Mgombea ubunge wa CHADEMA alitaarifiwa kuhusu kukamatwa kwa kada wa CCM na akawaambia watu wa CHADEMA wasimpige wampeleke kwake pale kwenye mkutano, na mwishowe alimkabidhi kwa polisi.

Cha ajabu yule dereva aliyekuwa anaendesha gari ya CCM iliyokimbia eneo la tukio, amefariki, na taarifa ya uongo inasema alikufa pale pale kwenye eneo la tukio. Lakini hii taarifa ya uongo inatokana na shinikizo la CCM kwa polisi na kwa vyombo vya habari. Ukweli ni kwamba yule dereva aliweza kuendesha gari mpaka kituo cha polisi na kuandika maelezo na baada ya hapo kupelekwa hospitali na kuekewa dripu ya maji.

Gari ya CCM iliyoshiriki kwenye tukio ilikamatwa baadaye na kukutwa haina damu hata kidogo, kwahiyo kuna uwezekanao mawe hayakumpata dereva au hayakumuumiza kiasi cha kutoka damu. Lakini taarifa iliyotoka inasema alikufa kwa kupigwa mawe na kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni. Ukumbuke dereva wa CCM akushuka kwenye gari na alikuwa amekaa kwenye kiti cha dereva chenye head-rest.

Ni ngumu kuelewa hicho kitu cha ncha kali kiliweza kumfikia vipi kisogoni wakati amekaa kiti cha dereva. Na huwezi kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni uendeshe gari mpaka kituo cha polisi kuandika maelezo. Inawezekana CCM walimmalizia huyu dereva ili kukuza hili jambo kiasi cha kufanya CHADEMA isiruhusiwe kushiriki uchaguzi maswa magharibi. Pia watu wanaomjua huyu Robert kisena (mgombea wa CCM) wanasema inawezekana kamtoa kafara dereva wake, hasa ukizingatia yeye Robert Kisena ni mshirikina sana.

Katika mazishi ya Dereva, ndugu wa dereva walimuomba Robert Kisena ushirikiano wa kifedha akawajibu mnataka kunigeuza mtaji. Ndugu wa marehemu walilikataa jeneza la CCM na kusema mgombea wa CCM kamtoa kafara ndugu yao. Riziwani Kikwete aliyekuwepo kwenye mazishi ya dereva huyo naye alipewa ukweli wake hapo kwenye mazishi, kuwa wanashirikiana na mgombea wa CCM kuwauzia watu bidhaa feki. Upo ushahidi wa picha wa haya yaliyosemwa hapa, pamoja na ushahidi wa picha unaonyesha mgombea wa CCM akimpiga OCD wa maswa.

Mgombea wa CCM ni Mnyarwanda hivyo kukosa ubinadamu ni hulka yake na hana undugu na dereva aliyekufa. Dereva aliyekufa anamuita mgombea wa CHADEMA mjomba. CCM wanaogopa SHIBUDA asishinde ubunge kwa vile ataweka mfano m’baya ambao utawafanya wale wanaonewa CCM au ambao hawakubaliani na ufisadi, wahamie CHADEMA.
 
Haya CCM, Ni Chama Hatari watafanya kila kitu kukaa Madarakani na kufuja Mali za Nchi Ya Tanganyika, wazanzibari makini haswa hawataki huo Umoja wanatama Mafuta kuwa yao hawataki mkono na ulafi wa Mafisadi Bara

Kweli Tanganyika itajengwa na Mwenye Moyo
 
Kwa kweli kama ni njama za kupikwa, kumwaga damu ili kutumia njia hiyo kujinufaisha kisiasa, kama messeji iliyosambazwa siku ya jana kwamba CHADEMA wameamua kumwaga damu, ni UCHAFUZI WA ARDHI (NCHI) YETU. Kukimbilia kumkamata Shibuda, pasi na mazingira yoyote yanayoashiria kuwepo kwake katika tukio, si jambo jema kwa Watanzania wote.

eeehh bana weee...kuna namna ya picha fulani vile naipata nikiunganisha dots kati ya tukio la mtu kuuwawa kule Maswa na kufuatiwa kwa zile message za kutoka kuzimu, inaelekea kweli Mzee Makamba aliona aende Maswa akatoe kafara mmoja wa watani zake na amefanikiwa, jamani tuombeeeeeee .........Amina

CCM WAMWAGA DAMU MASWA

Katika kampeni za ubunge zinazoendelea Maswa magaribi kumetokea kifo cha dereva wa mgombea wa CCM (Robert Simon Kisena). Lakini hiki si kifo cha bahati mbaya ni kifo cha kupangwa na mgombea wa CCM anayeungwa mkono na Riziwani Kikwete, Makamba pamoja na Kikwete. Robert Kisena ambaye ni tapeli mkubwa anayejulikana kwa utapeli wake pia ni swahiba wa karibu wa Riziwani Kikwete.

Kulikuwa na mkutano wa CHADEMA uliokuwa unaendelea maswa magaribi huku gari moja ya chadema(land rover) ikiwa inazunguka maeneo ya karibu, ikiwa inawatangazia watu juu ya mkutano huo, ghafla ilitokea gari ya ccm(surf) ambayo ilitaka kuigonga gari ya chadema.

Gari ya chadema katika kukwepa ikatoka barabarani na mmoja ya watu waliokuwemo katika gari hiyo ya chadema aliangusha kofia hapo, na ikabidi ashuke kuichukua. Chadema waliposimamisha gari yao kuokota kofia ndipo CCM waliposhuka na kuanza kuwashambulia CHADEMA.

Watu wa CHADEMA kuona hivyo wakaanza kupiga kelele, wale CHADEMA waliokuwepo kwenye mkutano waliposikia wakaanza kuondoka kwenye mkutano kuelekea kwenye tukio. Huko kwenye tukio watu wa CHADEMA walianza kuwapiga mawe CCM mpaka wakakimbia na mmoja wao kukamatwa. Mgombea ubunge wa CHADEMA alitaarifiwa kuhusu kukamatwa kwa kada wa CCM na akawaambia watu wa CHADEMA wasimpige wampeleke kwake pale kwenye mkutano, na mwishowe alimkabidhi kwa polisi.

Cha ajabu yule dereva aliyekuwa anaendesha gari ya CCM iliyokimbia eneo la tukio, amefariki, na taarifa ya uongo inasema alikufa pale pale kwenye eneo la tukio. Lakini hii taarifa ya uongo inatokana na shinikizo la CCM kwa polisi na kwa vyombo vya habari. Ukweli ni kwamba yule dereva aliweza kuendesha gari mpaka kituo cha polisi na kuandika maelezo na baada ya hapo kupelekwa hospitali na kuekewa dripu ya maji.

Gari ya CCM iliyoshiriki kwenye tukio ilikamatwa baadaye na kukutwa haina damu hata kidogo, kwahiyo kuna uwezekanao mawe hayakumpata dereva au hayakumuumiza kiasi cha kutoka damu. Lakini taarifa iliyotoka inasema alikufa kwa kupigwa mawe na kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni. Ukumbuke dereva wa CCM akushuka kwenye gari na alikuwa amekaa kwenye kiti cha dereva chenye head-rest.

Ni ngumu kuelewa hicho kitu cha ncha kali kiliweza kumfikia vipi kisogoni wakati amekaa kiti cha dereva. Na huwezi kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni uendeshe gari mpaka kituo cha polisi kuandika maelezo. Inawezekana CCM walimmalizia huyu dereva ili kukuza hili jambo kiasi cha kufanya CHADEMA isiruhusiwe kushiriki uchaguzi maswa magharibi. Pia watu wanaomjua huyu Robert kisena (mgombea wa CCM) wanasema inawezekana kamtoa kafara dereva wake, hasa ukizingatia yeye Robert Kisena ni mshirikina sana.

Katika mazishi ya Dereva, ndugu wa dereva walimuomba Robert Kisena ushirikiano wa kifedha akawajibu mnataka kunigeuza mtaji. Ndugu wa marehemu walilikataa jeneza la CCM na kusema mgombea wa CCM kamtoa kafara ndugu yao. Riziwani Kikwete aliyekuwepo kwenye mazishi ya dereva huyo naye alipewa ukweli wake hapo kwenye mazishi, kuwa wanashirikiana na mgombea wa CCM kuwauzia watu bidhaa feki. Upo ushahidi wa picha wa haya yaliyosemwa hapa, pamoja na ushahidi wa picha unaonyesha mgombea wa CCM akimpiga OCD wa maswa.

Mgombea wa CCM ni Mnyarwanda hivyo kukosa ubinadamu ni hulka yake na hana undugu na dereva aliyekufa. Dereva aliyekufa anamuita mgombea wa CHADEMA mjomba. CCM wanaogopa SHIBUDA asishinde ubunge kwa vile ataweka mfano m'baya ambao utawafanya wale wanaonewa CCM au ambao hawakubaliani na ufisadi, wahamie CHADEMA.

Mkuu tupe source,
 
Back
Top Bottom