Sakata la Lwakatare na sababu 2 za uthibitisho wa Mtonyaji Serikalini kuihujumu CHADEMA

hauamini? cdm ni chaguo la wengi we mamluki.

Wewe ni usiku wa giza; huji utokako wala uendako! Mtakesha sana humu JF, MTAANDAMANA SANA, MTATUKANA SANA, MTAFANYA FUJO SANA, MTATEKA WAANDISHI WA HABARI SANA, LAKINI IKULU MTAISIKIA REDIONI TU NA KWENYE TV. LABDA BAADA YA MIAKA 500 NDIO MTACHUKUA NCHI NA MAGWANDA YENU HAYO ILI MUWEZE KUJINEEMESHA NA KUIJENGA VIZURI KILIMANJARO. Hamuwezi kushinda Urais wa TZ bila kura za Zanzibar kama sehemu ya Muungano; na siioni CHADEMA Zanzibar mieeeeeh!
 
Worry not, kuna mambo kadha wa kadha yamebadilika kuanzia wakati ule mpaka sasa.
Mosi, Imani ya wananchi kwa serikali ya ccm imepungua sasa kuliko wakati ule. Waliposema CUF ni chama cha kidini na kigaidi ccm walikuwa wanaaminika na hivyo wananchi wakaamini kwamba CUF ni mbaya. Not now any more.

Pili, Chadema kimkakati iko vizuri zaidi na tumejifunza kutokana na makosa ya CUF tuko vizuri kujibu tuhuma za ccm.

Tatu, watumishi wa Umma kwenye kila ngazi sasa hawako tayari kuburutwa na serikali. Mfano, si polisi wote utawatuma na wakakubali kufanya uhalifu wo wote dhidi ya Chadema kama wakati ule. Siku hizi wana hoji na wanajua watakuja kuwajibishwa mbele ya safari.
KAMA ULIYOANDIKA MNA UHAKIKA NAYO HONGERENI SANA. Ila , 2015 MSIJE MKASHANGAA GAMBA LINARUDI TENA IKULU. CCM 2015-USHINDI NI LAZIMA!
 
Nashukuru kwamba umejua hii ni movie ya ukweli - it about life or death.

Ndugu zangu hii movie ni ya kweli

sasa dawa yao ni moja tu

Kila wanalopanga kesho walikute mtaani tena peupeee. Ndugu wanamapinduzi mlioko ndani hakikisheni kila siri inawekwa mezani na ndipo huyu shetani ccm atakuwa ameaibika.

hatulali mpaka kieleweke.

 
Ndugu zangu hii movie ni ya kweli

sasa dawa yao ni moja tu

Kila wanalopanga kesho walikute mtaani tena peupeee. Ndugu wanamapinduzi mlioko ndani hakikisheni kila siri inawekwa mezani na ndipo huyu shetani ccm atakuwa ameaibika.

hatulali mpaka kieleweke.

Ni dawa nzuri sana... Maana katika hali ya kawaida, kama siri yako unaisikia nje na hata hujui imetokaje, basi kinachofuata unanyamaza maana huwi na uhakika hicho unachowaza kama bado hakijaingia mtaani kabla ya utekelezaji
 
Ndugu yangu ya kijijini ndio acha kabisa, usione watu wamejazana ukafikiri ni wapenzi wa chama, hao wanakuja kushangalia helkopta. Ni rahisi sana kubadili mawazo ya watu wanao ishi mjini lakini wa kijijini sio rahisi. Bila shaka wewe huna ndugu kijijini ndio maana unasema haya. Watanzania bado wanachagua mtu kutokana wanavyo shauriwa na mwenyekiti wa kijiji. Usimshangae mbunge wa ccm anae wapigia magoti wapiga kura ndugu yangu, hayo ndio mambo yanayo takiwa kijijini.


kwahyo mnaona ujanja kuwapgia magoti na kisha kuwaacha na nyie kuhamia Dar? Na kuwaacha wakiteseka maji hawana, usafiri baiskel,wanaporwa haki na ardhi zao na wawekezaji wa madin na wakulima wakubwa polis ndo ma hakimu huko si ndio?
Mkuu wa kaya mwenyewe ndo aliyeanzsha usemi akili za kuambia changaya na zako kwhyo unataka kutuambia kuwa wavjijin ni wapumbavu? Hawaelew maana ya usemi huu! Wewe unasema kuwa wanashauriwa na mwenykiti tu! Hivi wao hawaoni kinachoendelea shida zilivyo, hawaon kuwa mbunge wao tokea wamemuona siku ya kuomba kura tena mara 1 mtaani kwao mpaka leo hata sura ya mbunge kwa Tv/kuisikia saut redion kimya na sura wameisahau, n.k
na kama hujui hamna sumu mbaya kama ikasambaa vijjin wakishauriana kilugha kura hampati hata muende mkalale chin ya viatu vyao!!
Embu njoo Geita mwekezaji amepora wanakijiji ardhi,nyumba na hadi baadhi ya kata shule ipo ndan ya mgodi polc kama kawa ndo watumia baba,mama na watoto wanakaa ktk hema la makalatasi na maboksi ambalo kuvaa nguo ni kuachiana!!! Mimi sio mshabiki wa siasa lkn nataka mapindizi ya kuiscan nchi hii dhidi ya mavirus amabayo ni magumu kufa kwa kuyambia yaache kuharibu files!!!
Yanataka tu-ping kwa command
ila kaa ukijua tokea utoto wako mpka sasa
KUWA HAKI HAIOMBWI!!..
 
nipeni muda tu! Nitairusha hapa!
za mchana wanajanvi GT jana niliomba radhi kwa kutokuweza kuleta data ambazo Mkuu Awenda aliniomba nitupie huku na yenyewe ni kama hivi :


 
Last edited by a moderator:
...
B) Mbinu ya tatu ilikuwa ni kuibatiza CCM au kuibadilisha CCM kwa kuanzisha chama kipya.
Wakati ule nilipoleta habari ya mtonyaji kwamba kuna mkakati wa ndani kabisa wa kuibadilisha CCM au kuibatiza CCM watu hawakunielewa hata kidogo. Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa ktk mitandao ya kijamii iliyomnukuu msajiliwa vyama akisema kwamba, ofisi yake inaandaa mswada wa sheria wa kuruhusu vyama kuungana. Baada ya tamko hilo nadhani sasa ninaeleweka zaidi kuliko wakati ule nilipokuwa naleta taarifa za mtonyaji.
Ikumbukwe, huko nyuma serikali ya CCM ndo iliyokwamisha sheria ya vyama kuungana. Sasa, iweje sheria hiyo ikaletwa na serikali ile ile ya CCM? Huu ni uthibitisho wa taarifa za mtonyaji wangu ya kuibatiza CCM kwa jina jingine au kuanzisha muungano na chama kingine ili jina CCM lililochokwa libadilishwe.
Huu ni mkakati unafanywa na viongozi wa CCM na idara kwa siri sana kwa muda mrefu.

Swali ni Je, watafanikiwa kuizuia CHADEMA kuingia Ikulu 2015. Jibu langu ni Hapana – hawataweza. LET US WAIT AND SEE.
Mkuu Aweda,
Hii kitu niliishitukia tangu Mbatia alipopewa ubunge. Sasa hivi kuna mbinu za kimkakati kukijenga NCCR. Muungano huo ukitokea, utakuwa wa hawa wawili.
 
Hizi hadhithi mnazo leta ni za kutafuta huruma kutoka kwa wananchi, siasa hizo zilisha pitwa na wakati, wapiga kura hawatazami hayo tena wao wanatazama msimamo wa chama. Kwa jinsi mlivyo leo mkipewa serikali basi kuna wabunge watapewa wizara tatu kutokama na ufinyu wa viongozi. Chama kina wasomi wa kuhesabu na vijana wasio na utaalamu wowote.
Kwani sasahivi kuna ufanisi gani katika wizara zilizovunjwavunjwa na kuwa nyingi kisha kupewa mawaziri ambao wameshindwa kuziendesha zaidi zinakula tu kodi za wananchi kwa kuongeza bajeti za uendeshaji? Mi sioni tabu mana kichwa kimoja cha chadema kinaweza kuongoza wizara zaidi ya tatu! Mfano, Sayansi na elimu ya juu inaungana MoEVT+utamaduni na michezo. Alafu kwa utendaji kazi wa John Mnyika hata akimuunganishia wizara tano za sasa atazinyoosha tu! Wakati wa chama tawala kila wakijitahid kugawa wizara lakini bado mawaziri wao wana-underperform tu! Hivyo wingi si hoja bali uwezo.
 
EE Mungu wa rehema,turehemu!Wanao miaka 50 tunakunywa maji yenye kinyesi na tunapata kipindupindu,wanao hata hapa jijini tunakaa chini sakafuni ili kujisomea,wenzetu wa sekondari za kata kuna waalimu 2 kwa watu 1000 sote tutapata diivisheni sifuri,hospitalini'dispensarini/vituo vya afya/na rufaa za hospitalini hakuna watumishi,tunachinjwa na visu-siku nyingine kama unatakiwa kichinjwa mguu wanakuchinja kichwa na kama ni kichwa basi wanakuchinja mguu-malaria inatuangamiza hadi eti JOJI BUSHI ametuonea huruma akatufadhili kila kitanda kipate chandarua chenye dawa.Madini,wanyama pori,maliasili na takrima zote ulizotukirimia tunaporwa mchana kweupee,na yeyote anayefurukuta kuuliza kwa nini tunakula kinyesi,kwa nini tunasomea mchangani,kwa nini malaria inatumaliza na kwa nini hasa tunaitwa maskini ,huyu wenye NGUVU WANAMWITA GAIDI!EE Mungu mmoja wao alituachia falsafa tukashindwa kutafsiri na kuitumia :MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE-Mwenyezi MUNGU TUPE NGUVU ZA KUWEZA KULETA MABADILIKO,UVUMILIVU KUKUBALIANA NA YALE TUSIYOWEZA KUBADILISHA,NA HEKIMA ITOKAYO KWAKO YA KUTUONGOZA KUJUA TOFAUTI YA TUNAYOPASWA KUBADILISHA NA TUNAYOPASWA KUVUMILIA!
 
Leo kumekuwa na mabandiko mbalimbali humu ndani yakielezea jinsi Joseph Ludovick Rwezaura anavyojulikana(bandiko la Mtela Mwampamba). Pia lipo bandiko la Ben Saanane linalopendekeza kuhojiwa kwa Zitto Juliana Shonza Mchange Mwigulu Nchemba,na Festo Sanga kuhusu kuhusika kwao katika sakata la Alfred Lwakatare,Ludovick na mengine ya namna hiyo.

Ikumbukwe kuwa suala la Lwakatare na 'mwenzake' lilianzia kwenye clip ya video iliyobandikwa youtube na kuwekwa humu na hugochavez. Na ikumbukwe pia kuwa,Ludovick amesikika akitajwa kwenye clip hiyo huku Lwakatare akitoa maelekezo ya 'kinjama-njama'

Ilipowekwa tu,clip hiyo ilipingwa sana kuwa ni batili kwa sababu kem kem za wanajamvi. Wapo wachache walioiamini tangu mwanzo.

Kuendelea kuwataja watu wanaohusika na 'hujuma' hiyo dhidi ya Lwakatare,Ludovick na CHADEMA kwa ujumla ni kuiamini clip hiyo na wanajamii wanahitaji mwendelezo wake? Kwanini isisimamiwe pale pale kuwa clip ni feki na ni ubambikizi wa mashtaka kwa Lwakatare na Ludovick?

Tujadili...
 
Back
Top Bottom