Saini upate noti

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
Usaini mkataba, upewe mengi manoti,
Tupe mgodi wa shaba, wenye ya kudumu hati,
Masharti yote saba, yapite kimkakati,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Utalindwa kisiasa, mkataba kisaini,
Tutakupa nyingi pesa, Leo na huko mbeleni,
Huna kitu utakosa, mkataba kisaini,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Ndoa za moja jinsia, usizipinge saini,
Mashoga wote pokea, uwape haki nchini,
Hiyo yako familia, italindwa kwa thamani,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Fungua benki ulaya, Amerika na Asia,
Fedha hazitopoteya, tisini asilimia,
Ukizorota afiya, bure tutakutibia,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Tujali sisi wazungu, sisi kwako kila kitu,
tapewa mengi mafungu, yenye vya thamani vitu,
Utalindwa kwa uchungu, sibiwe maburungutu,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Toka leo toka sasa, kwetu rafiki mzuri,
Tutakongeza mapesa, saini hapa mhuri,
Yeyote akikutesa, kwetu huyo ni muhari,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Ile mbuga nzuri tupe, ili sisi tumiliki,
Uhamishe wale kupe, fidia walipwe laki,
Wabishi fimbo uwape, wale wanodai haki,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Utupe hiyo bandari, miaka mia tisini,
Utie hapa muhuri, kubali yote jamani,
Tapewa mengi magari, yaso idadi nchini,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Na lile pori tengefu, tupe tujenge hoteli,
Tutajenga jengo refu, livute watu wa mbali,
Watu wa hapa wachafu, kwingia tusikubali,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Shime saini haraka, watu wasibumburuke,
Lugha iwe ya kichaka, kwa watu sitambulike,
Wale kianza ropoka, shimoni ukawazike,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Siri hii itunzeni, wananchi wasijue,
Zungusha wazungusheni, wakitaka watambue,
Ngonjera waimbieni, wapumbae wazubae,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 11/12/2023
 
SAINI UPEWE NOTI

Usaini mkataba, upewe mengi manoti,
Tupe mgodi wa shaba, wenye ya kudumu hati,
Masharti yote saba, yapite kimkakati,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Utalindwa kisiasa, mkataba kisaini,
Tutakupa nyingi pesa, Leo na huko mbeleni,
Huna kitu utakosa, mkataba kisaini,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Ndoa za moja jinsia, usizipinge saini,
Mashoga wote pokea, uwape haki nchini,
Hiyo yako familia, italindwa kwa thamani,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Fungua benki ulaya, Amerika na Asia,
Fedha hazitopoteya, tisini asilimia,
Ukizorota afiya, bure tutakutibia,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Tujali sisi wazungu, sisi kwako kila kitu,
tapewa mengi mafungu, yenye vya thamani vitu,
Utalindwa kwa uchungu, sibiwe maburungutu,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Toka leo toka sasa, kwetu rafiki mzuri,
Tutakongeza mapesa, saini hapa mhuri,
Yeyote akikutesa, kwetu huyo ni muhari,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Ile mbuga nzuri tupe, ili sisi tumiliki,
Uhamishe wale kupe, fidia walipwe laki,
Wabishi fimbo uwape, wale wanodai haki,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Utupe hiyo bandari, miaka mia tisini,
Utie hapa muhuri, kubali yote jamani,
Tapewa mengi magari, yaso idadi nchini,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Na lile pori tengefu, tupe tujenge hoteli,
Tutajenga jengo refu, livute watu wa mbali,
Watu wa hapa wachafu, kwingia tusikubali,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Shime saini haraka, watu wasibumburuke,
Lugha iwe ya kichaka, kwa watu sitambulike,
Wale kianza ropoka, shimoni ukawazike,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Siri hii itunzeni, wananchi wasijue,
Zungusha wazungusheni, wakitaka watambue,
Ngonjera waimbieni, wapumbae wazubae,
Saini hu mkataba, upewe mengi manoti.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 11/12/2023
 

Attachments

  • 1710778949708.jpg
    1710778949708.jpg
    337 KB · Views: 1
Nae kweli akasain,manoti mengi ajazwe,
Mwewe nao Kwa macho wakaona,
Wakawasanua maamuma,Tunu twapigwa,

Ngoma nayo ikalia,ikawashtua maaamuma usingizini.
Vipepeo wakaamua Kwa mwenyezi aende mapema,asije maliza urithi wote,

Tunaanza na tabasamu,halafu na yeye atafuata.
Ni Bora mmoja akaenda,tukaponya urithi wetu.

Vipepeo hawataki utani,na kazi wameanza!
 
Back
Top Bottom