Saikolojia: Waelewe Wanaume (Understand Men)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
Waelewe/Wafahamu Wanaume (Understand Men)
upload_2018-5-17_13-59-45-png.779839

Habari za muda kidogo wasomaji wa makala ninazoziandika hasa kuhusu saikolojia na maisha karibu katika makala inayohusu kuwaelewa wanaume.

Niombe radhi kwa kushindwa malizia makala kama mbili sababu kubwa ni baada ya kupata ushauri kutoka kwa wasomaji wangu na watu wangu wa karibu.

Malengo ya makala hii nimejikita katika dhana ya msingi ya kumuelewa mwanaume na hili itasadia katika kuongeza hekima kati yetu sisi wanaume wenyewe kwa wenyewe katika kujielewa na pia wanawake kupata mwanga kuhusu mwanaume kihasili hasa tabia na mwenendo wao.

Kuwa mwanasaikolojia kunakupa ufahamu wa aina nne juu ya tabia za mwanadamu ikiwepo (i) kuelewa tabia, (ii) kuielezea tabia (iii) kuitabiri tabia na (iv) kuidhibiti au kuiendesha tabia (control). Hivyo kuna mambo mengi siwezi kufunguka kwa sababu maalum sababu ntakuwa nabomoa badala ya kujenga hivyo kuwa na tahadhari kwangu ni muhimu sana kuliko mambo mengine.

Hivyo kadili utakavyokuwa unatafakari unaposoma na kuingia ndani katika haya niliyoyandika ndipo utazidi kufahamu tabia nyingi na kwa upana kuhusu Mwanaume katika maisha ya ndoa, mahusiano, kiuchumi na pia jamii na tamaduni.

hivyo pia kupata busara na akili ya kuishi na mwanaume katika familia na mahusiano pasipo mifarakano au mikwaruzano ya mara kwa mara kupitia elimu hii na kuwaelewa pindi unapochukua tahadhari nao.

TAFSIRI MWANAUME.

Mwanaume ni mtu aliye na jinsia ya kiume. (Kamusi ya kiswahili karne ya 21) pia Mwanaume au mvulana mwenye aina tabia sifa kama vile uwezo na ujasiri au ushupavu.

ASILI YA MWANAUME

i. Wanadini imani zenye mzizi ya Abrahamu (Ukristo, Uyahudi na Uislamu).

Katika imani zenye mizizi ya abrahamu yaani ukristo uyahudi na uislamu inaeleza mwanaume au chimbuko la mtu mwanaume linatokana na uumbaji wa Mungu na mwanaume wakwanza alikuwa Adam alipewa kutawala viumbe vingine, kutunza bustani na msaidizi wake ni mwanamke Eva.

Katika nadharia hii kuna vitu vitatu vinajitokeza hasa kuhusu mwanaume

a) Asili ya mwanaume ni kutawala (dominate).

b) Mwanaume ni kiongozi (leader).

c) Mfanyaji kazi kiasili. (worker)

ii. Wanamapinduzi/wanaubadilikaji (Wanasayansi na wasioamini katika Mungu)

Dhana hii ya wana mapinduzi katika kutafsiri mwanaume ilihasisiwa na mwanabaiolojia Charles Darwin mnamo karne ya 19 hii kikmueleza mwanaume asili yake ni kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyochukua miaka mingi hivyo mwanadamu mwanaume ni mnyama au kiumbe jamii

Unaposema au kueleza dhana hii katika muktadha wa msamiati Jamii ni lazima kila jamii kiasili ina mpangilio Fulani kuitambulisha hasa za wanadamu ikiwemo uongozi na mfumo wa sheria flani zenye kubeba utambulisho wa jamii hizo.

Kutokana na dhana ya unyama unapata vitu vinavyojitokeza

a) Mwenye nguvu mpishe.

b) Kupambana kwa ajili ya rasiliamali wakati wote ( resource) ili uendelee kuwepo.

c) Samaki mkubwa ni halali kumla mdogo ili aendelee kuwepo.

iii. Tafsiri ya jumla inayopatikana.

Hivyo tunapoangalia katika utangulizi hasa katika kufahamu tafsiri na asili ya mwanaume kutokana na vyanzo vya imani pamoja na wanasayansi utagundua zipo sifa ambazo ni za kiasili na pia kibaiolojia na kisaikolojia ambapo nadharia zote hizi mbili za dini na wanasayansi au wanaubadilikaji wanazitaja.

Kila mwanaume anazo ila katika kujidhihirisha kwake kwa kila mwanaume ni tofauti kutokana na nidhamu ambazo kila mwanaume anazipata kupitia tamaduni imani malezi pamoja na mazingira anayokulia au kuwepo.

iv. Tofauti ya mwanaume (manhood) na uanaume (masculinity).

Mtakubalina na mimi katika haya machache hasa napotumia msamiatikuwa mwanaume” kigezo cha kitamaduni katika mtazamo wa jamii mbalimbali. Leo hii kuna msemo unaibuka hapa nyumbani Tanzania kwenye uhususani kwenye mitandao kuhusu “mwanaume wa dar” na “wa mikoani” huku wakijaribu kutofautisha kwa namna tofautitofauti.

Mtazamo wa uanaume ni tofauti katika jamii mbalimbali mfano kuna jamii nyingine sifa mojawapo ya uanaume inajumuishwa na suala la kutahiriwa na nyingine kutotahiriwa, zipo zinazosema uanaume kuwa na wake wengi na nyingine kuwa na mke mmoja, pia zipo zinazovuka mipaka hata kusema kulia sio uanaume.

Hivyo ni vigezo tu lakini ni vya kitamaduni zaidi na lengo la makala hii ni kuangazia zile za kiasili yaani mwanadamu wanaume anapozaliwa anakuwa nazo ila nidhamu anayojifunza ndio inamsaidia kumtofautisha kimaamuzi katika kujidhihirisha kwa tabia hizi.

FAHAMU TABIA NA UASILI NDANI YA MWANAUME.

Hizi tabia haijarishi taifa kabila jamii tamaduni ila kinachotofautisha ujihidhihirishaji ni ni nidhamu ya ujidhibiti au kujizuia “self control” kunakotokana na malezi, tamaduni, mazingira na imani.

1. Kutungwa kwa mimba.

Tulifundishwa katika ngazi mbalimbali za kielimu kuhusu Kromosomu tafsiri rahisi hili azaliwe mtoto mwanaume ina maana baba anapotoa mbegu ya kiume yenye kromosomu X ina maana mtoto anakuwa wa kiume sababu mama (mwanamke) yeye huwa na kromosomu X tu ila mwanaume yeye anazo zote mbili yaani ile kromosomu X na Y hivyo kuzaliwa mtoto wa kike au wa kiume hutegemea baba anatoa kromosomu gani.

(Unapata jibu mwenye kusababisha mtoto azaliwe wakike au wa kiume ni baba (mwanaume)

Hivyo kromosomu XY (Mwanaume) inaelezwa na wanasayansi kuwa na mapungufu kutokana na Y hivyo si sawa na hile yenye XX (Mwanamke).
upload_2018-5-17_14-0-15-png.779846

(Picha inayoonesha shughuli watoto wa kiume wanajishughulisha wakiwa katika umri)

Hivyo mapungufu hayo yanafanya pia idadi ya wanaume kuwa wachache kuliko wanawake. wanaoweza kuhimili kuishi “survive” wakiwa watoto na kukua ni wakike kuliko wakiume kwa mujibu wa tafiti.

Ijapokuwa watoto wanazaliwa wengi wakiume kuliko wakike. lakini shughuli, michezo ya hatari na majukumu hasa kwa watoto wakiume katika jamii mbalimbali inasababisha watoto wakiume kuwa katika hatari nyingi na mazingira hayo, na hivyo idadi yao kuwa chache sana ukilinganisha na wale wa kike.
upload_2018-5-17_14-0-30-png.779847

(Picha inayoonesha shughuli ambazo watoto wakike wanajishughurisha muda mwingi wakiwa na umri mdogo mmoja kambeba mdogo wake na wapo karibu na jiko nyuma yao)

Changamoto hii mara nyingi hujidhihirisha wakati wa kipindi cha kuoa na kuolewa sababu watoto wakike pia wanapofikia kipindi hiki mapema tofauti na wa kiume na hapo uchache ndipo unajidhihirisha.

2. Akili ya mwanaume na uongeaji.

“Kuna msemo mmoja unasema wanawake zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo ni umbea lakini wanaume zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo wao wanapashana habari”
upload_2018-5-17_14-0-43-png.779849

(Tafiti zinabainisha kwa siku mwanaume huongea maneno 7000 na mwanamke uongea maneno 20,000)

Katika kipengele hiki tunajifunza kifiziolojia utendaji wa ubongo wa mwanaume unaegemea sana katika upande wa kushoto na wanawake kwao ni upande wa kulia.

Utendaji wa akili hasa katika upande wa kushoto tunauita wenye kuwezesha fikra na mawazo mantiki “logic” na wenye uchanganuzi sana wa mambo.

lakini ule wa upande wa kulia wenyewe uwezo katika fikra au mawazo ya ubunifu, uelewa wa masuala kiasili (shuku)

Kwahiyo kwa dhana hii utajifunza kuwa mwanamke huwa muongeaji sana kuliko mwanaume hilo ni suala la kimaumbile.

Pia mwanamke anauelewa mkubwa sana wa kiasili “intuitive thinking” kushinda mwanaume na ndio sababu mtoto wa kike kumtuma akakuelewa akiwa mtoto wa miaka mitatu ni mkubwa kuliko kwa mtoto wa kiume.

Mtoto wa kike hata unaweza muachia mtoto mdogo akakaa nae akamuangalia bila shida yoyote.

Pia uwezo wa kuanza kuongea kwa mtoto wa kike anaanza mapema kuliko wa kiume.

Pia unajifunza suala jingine hasa katika mahusiano mwanamke anafikia ukomavu wa kifikra na mawazo akiwa na miaka 22 na anaweza kuolewa na akatunza familia vizuri wakati kwa mwanaume ni kuanzia umri wa miaka 27 ndio anafikia kiwango hicho cha kukua kifikra.

Mwanamke na mwanaume wanapolingana kiumri kiasili mwanaume ni mdogo kwa mwanamke.

Unajua sasa kwanini mwanaume anachoshwa haraka na mwanamke anaeongea sana?

3. Ukali (Aggressiveness).
upload_2018-5-17_14-1-2-png.779851

(Wavulana wakipigana, tazama wanaowagombelezea wakike anamaanisha kuwaachanisha lakini wakiume anafanya kwaajili ya picha wengine wakiume wanashuhudia pambano)

Tafsiri ya neno aggressive inapokuja katika lugha ya Kiswahili haileti ladha kamili hasa katika upande wa saikolojia ijapukuwa inatoa muelekeo wa kidhana

Aggressive ni “ushari”, “gomvi”, “chokozi” “jeuri” na tafsiri nyingine ni “kutaka maendeleo”.

Hivyo kila mwanaume ana hali hii kiasili himo ndani yake ila kujitokeza kwake kunatokana na nidhamu katika imani tamaduni au mazingira huo unakuwa ndio msingi wa kujidhibiti au kujiachilia.

Kwanini basi hali hii hipo kwa wanaume? Sababu ya homoni inayoitwa Testosterone homoni hii huwa katika viungo vya uzazi wa mwanaume na ndio inayomtofautisha mwanaume kitabia na mwanamke.
upload_2018-5-17_14-1-22-png.779854

(Donald Trump anaelezwa kuwa ni moja ya watu wenye viwango vingi vya testosterone katika mwili wake)

Je nini kinachotokea homoni hii inapozidi? Tafiti zinabainisha kuwa wengi wenye homoni hii iliyozidi huwa na hali ya kupambana sana kimaisha homoni hii inafanyika kama kumpa motisha ndani yake. Ndio maana matajiri au mabosi wengi huwa ni wakali na pia wengi ni wanyanyasaji wa kijinsia “womanizer” sababu tafiti wengi huwa wana homoni hii iliyozidi.

Lakini changamoto hasa watu wengi sana wanaozidiwa na homoni hii hasa maeneo ya afrika na asia huishia kuwa na wanawake wengi.

Na pia kuwepo kwa homoni hii kunasababisha pia matukio mengi ya uharifu kwa mujibu wa takwimu, matukio ya uharifu utekelezwa kwa asilimia kubwa na wanaume kuliko wanawake.
upload_2018-5-17_14-1-37-png.779857

(Swali kwa wasomaji wajinsia zote? Je sinema gani kati ungepata shahuku ya kuanza itazama )

Pia kujidhihirisha kwa homoni hii inafanya wanaume wengi sana kupenda michezo au filamu zenye mapigano mfano Vita, ubabe, na michezo kama ngumi. Na hata kuwa washabiki sana pale mazingira ya ugomvi unapotokea kuliko kusuluhisha au kuamulia.

4. Utawala (Dominance)
upload_2018-5-17_14-2-5-png.779859

(Picha askari wa uingereza wakielekea vitani pembeni ni wake zao (mtoto akimkimbilia baba yake). Kwa karne nyingi matukio ya vita yalihamasishwa kwa kauli mbiu ya wanaume kupigania uhuru wao, wake na vizazi vyao dhidi ya maadui wa nje.)

Tafsiri yake ni kitendo cha kuwa na amri juu ya au amuru au mamlaka. Kama nilivyojaribu kupitia nadharia mbili ya asili ya mwanadamu hasa mwanaume zote kwa pamoja zinabainisha kuwa kila mwanaume anakitu kutawala ndani yake haijalishi umri wake.

Kupitia nadharia hii mwanaume kiasili anawajibika kwa ajili ya jamii yake katika kuilinda na kuipigania dhidi ya matukio mbalimbali katika ulimwengu mfano uharifu, majanga na vita

mfano Baba ujiona anawajibika kwa ajili ya familia yake mkewe na watoto pia kila kijana wa kiume hujiona ana wajibu kuwalinda dada zake. Hivyo suala hili ni la kiasili kabisa.

Hivyo katika hili unapata kufahamu kwanini jamii nyingi zina tamaduni mfumo dume yaani zinazowapa wanaume kipaumbele au mazingira pendelevu.

Utajifunza kosa kubwa mwanamke analolifanya kwa mwanaume ni pale kumvunjia heshima au kutomuheshimu mume wake au kaka yake au mtu yoyote kaitka jamii ambaye ni jinsia ya kiume.
upload_2018-5-17_14-2-22-png.779862

Ukitaka kuutikisa moyo wa mwanaume kwa muda muoneshe kumheshimu (hii kwa wanawake).

Pia kwa sababu hii utagundua kuna jambo linajichipuza nalo ni “Wivu” hivyo si jambo la kawaida kukuta mwanamke ameolewa na wanaume watatu wakaishi pamoja lakini mwanaume kuoa zaidi ya watatu ni jambo la kawaida kwa tamaduni nyingi duniani.

Pia utafahamu wanaume kwanini huwa hawaaminiani wao kwa wao kuhusu mwanamke.

Wivu ni kitu kipo pia kwa kila mwanaume.

5. Mwanaume huvutiwa kwa kutazama.
upload_2018-5-17_14-2-39-png.779864

(Picha ya mchoro inayomuonesha mfalme Daudi akimwangalia mwanamke anayeoga (Mke wa kamanda wake “Uria Mhiti”) baadaye alimtwaa na kuwa mke wake baada kutengeneza mazingira ya Uria Mhiti kuuliwa vitani Ghadhabu na adhabu ya Mungu ikawaka juu ya nyumba ya Mfalme Daudi.)

Picha ya kielelezo hiki nimemtumia Mfalme Daudi kama kielelezo kuwa mwanaume yoyote anaweza kukumbana na hali ya uzinzi au uasherati kama akijisahau katika nidhamu ya kudhibiti macho yake.

Niliwahi kumsikia dada mmoja ambaye alikuwa na ghadhabu sana kutokana na tabia ya mchumba wake, hasa wanapotoka yaani ni rahisi sana kugeuka geuka wanapopita wadada wengine kwahiyo alishindwa mvumilia kabisa kutokana na mara kwa mara kuongea nae laikini tabia hiyo ilikuwa inajirudia baada ya muda hivyo aliafikia kuachana nae na kuvunja uchumba.

Labda nirejee sehemu ya utaangulizi nilipoeleza kuwa utofauti wa wanaume na asili yao hutokana na nidhamu ambazo kila mwanaume anazipata anafundishwa anajifunza kupitia tamaduni, imani na malezi pamoja na mazingira anayokulia au kuwepo.
upload_2018-5-17_14-2-54-png.779867

Hivyo tamaa ya kuvutiwa kwa mwanaume hasa kwa wa jinsia nyingine ina nguvu sana machoni, ila kila mwanaume ana nidhamu ya kujidhibiti kwa namna tofautitofauti.

a) Mwanaume ni rahisi kumpenda mtu kwa uzuri au kwa kumuona tu lakini kwa mwanamke yeye anaegemea sana hisia zake na mara nyingi hisia utegemea ukaribu wa kipindi Fulani au kwa kusikia tu habari za mtu Fulani. Lakini mwanaume inamtokea tu kwa kuona sababu tamaa ya wanaume hipo machoni.

b) Vilevile utajifunza kwanini wanawake wengi hupoteza mvuto kwa wanaume zao baada ya kuwaoa? Sababu wanawake wengi hawafahamu mawanaume huvutiwa na muonekano (physical appearance) na wanawake wakishaolewa huwa wanaacha kujari muonekano wao tena mbele za wanaume zao.

c) Pia kwa kigezo hiki unajifunza kwanini wanaume hunaswa kirahisi na wanawake wanaovaa nguo za utata na kujiremba lakini wake zao wanapoondoka baada ya mifarakano hupata tabu sana na kujaribu kutafuta suruhu nao baada ya kutafakari sana kuhusu kutaka na kupenda kupi muhimu.

Sababu moyo wa mwanaume hutamani wengi lakini upendo wake huwa sehemu moja.
(Pia tunajifunza katika vitabu vya imani kupitia mtoto wa kwanza Reubeni wa mzee Yakobo (Israel) alivyojikuta akiingia katika mahusiano ya kimapenzi na mama yake Mdogo Bilha ambaye ni mke mdogo wa baba yake).

Hivyo ni muhimu sana kwa kijana wa kiume kujifunza kuwa na nidhamu ya udhibiti wa macho yako itakujenga katika nidhamu ya kuutawala mwili wako kihisia si kila kitu lazima utazame tu kama hupo katika maisha ya kimalengo juu ya kesho yako (si vijana wengi wakiume wanaishi kimalengo).

Kijana wa kiume kuna mazingira mengine huwa yanatokea usijiamini kupita kiasi, sababu Duma na swala hawawezi kuishi kwa karibu halafu lisitokee lakutokea.
6. Shawishi au shawishika (Persuade)
upload_2018-5-17_14-3-11-png.779869

(Picha hii inaonesha tukio la kijamii linalohusu upimaji wa afya. Angalia je waliojitokeza kuhudhuria idadi hipi ni kubwa? katika ya wanaume na wanawake.)

Wengi tunaoudhuria katika shughuli mbalimbali za kijamii mfano zili zinazohusisha labda uchangiaji damu, upimaji wa afya, semina, misiba, mikutano ya kidini utagundua idadi kubwa sana ya wahudhuriaji wakubwa au kwa idadi kubwa ni wanawake kuliko wanaume.

Kama ujawahi fanya tafiti hiyo hanza kuanzia sasa kama ni kanisani (sababu jumuiya hii uwachangamanisha watu wa jinsia zote mahali pamoja) tofauti na jumuiya za imani nyingine. utagundua kundi la wanawake huwa ni kubwa sana. Basi umeshawahi jiuliza kwanini?

Kama nilivyoelezea pia katika sababu mojawapo inayowatofautisha wanaume na wanawake kiakili wanaume hutumia zaidi sehemu ya ubongo wa kushoto. Hivyo kumshawishi mwanaume katika shughuli za kijamii kunahitaji sana sababu za kimantiki katika fikra zake na za kujitosheleza au pengine kama kuna manufaa au kumuinulia shauku.

Hivyo muhimu cha kufanya kama unaosoma ujumbe huu ni mwanamke umeolewa fanya hivyo vya msingi kwanza baada ya yeye kuona manufaa, mantiki au kupatwa na shauku basi utamvuta lakini kumbembeleza au kumlazimisha hakuwezi kuleta muafaka anaweza kufanya kukufurahisha tu kwa muda huo lakini si kwa kudhamiria.
upload_2018-5-17_14-3-39-png.779873

Hata katika saikolojia ya matangazo sababu njia moja ya kujaribu kushawishi jinsia zote katika biashara hutumia wanawake wazuri ili kupata uangalifu wa mwanaume katika kuuza na kutangaza bidhaa zao.
****************************************************************************
Pia ili huweze kufuatilia vizuri mafundisho haya kuhusu Saikolojia na maisha ni vizuri kama utaanza ni follow katika akaunti yangu “Education mentor” niombe radhi tu kwa wale walioniomba kuwatag hinaniwia vigumu kukumbuka majina yote.

Na pia kuhusu Maswali yoyote ya kisaikolojia na maisha unaweza niuliza PM na mimi ntayajibu kwa mfumo wa makala au “mada”.

KUHUSU MWANDISHI,

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Vitabu vinavyohusu Falsafa na maisha, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).

Makala nyingine alizoandika Education Mentor..
Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda

Saikolojia: Sababu zinazosababisha magonjwa ya akili ambazo wengi hawafahamu. (psychological disorder)

Saikolojia:Jifunze mambo yakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (Case study Finland)

Saikolojia: Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (sehemu ya pili)

Saikolojia: Fahamu magonjwa ya kisaikolojia, dalili,tabia na mifano.(Case study Tanzania)

Saikolojia: Je Nimlipizie kisasi au nimsamehe?. (Vita visivyoisha vya Afghanistan)
 
Waelewe/Wafahamu Wanaume (Understand Men)
upload_2018-5-17_13-59-45-png.779839

Habari za muda kidogo wasomaji wa makala ninazoziandika hasa kuhusu saikolojia na maisha karibu katika makala inayohusu kuwaelewa wanaume.

Niombe radhi kwa kushindwa malizia makala kama mbili sababu kubwa ni baada ya kupata ushauri kutoka kwa wasomaji wangu na watu wangu wa karibu.

Malengo ya makala hii nimejikita katika dhana ya msingi ya kumuelewa mwanaume na hili itasadia katika kuongeza hekima kati yetu sisi wanaume wenyewe kwa wenyewe katika kujielewa na pia wanawake kupata mwanga kuhusu mwanaume kihasili hasa tabia na mwenendo wao.

Kuwa mwanasaikolojia kunakupa ufahamu wa aina nne juu ya tabia za mwanadamu ikiwepo (i) kuelewa tabia, (ii) kuielezea tabia (iii) kuitabiri tabia na (iv) kuidhibiti au kuiendesha tabia (control). Hivyo kuna mambo mengi siwezi kufunguka kwa sababu maalum sababu ntakuwa nabomoa badala ya kujenga hivyo kuwa na tahadhari kwangu ni muhimu sana kuliko mambo mengine.

Hivyo kadili utakavyokuwa unatafakari unaposoma na kuingia ndani katika haya niliyoyandika ndipo utazidi kufahamu tabia nyingi na kwa upana kuhusu Mwanaume katika maisha ya ndoa, mahusiano, kiuchumi na pia jamii na tamaduni.

hivyo pia kupata busara na akili ya kuishi na mwanaume katika familia na mahusiano pasipo mifarakano au mikwaruzano ya mara kwa mara kupitia elimu hii na kuwaelewa pindi unapochukua tahadhari nao.

TAFSIRI MWANAUME.

Mwanaume ni mtu aliye na jinsia ya kiume. (Kamusi ya kiswahili karne ya 21) pia Mwanaume au mvulana mwenye aina tabia sifa kama vile uwezo na ujasiri au ushupavu.

ASILI YA MWANAUME

i. Wanadini imani zenye mzizi ya Abrahamu (Ukristo, Uyahudi na Uislamu).

Katika imani zenye mizizi ya abrahamu yaani ukristo uyahudi na uislamu inaeleza mwanaume au chimbuko la mtu mwanaume linatokana na uumbaji wa Mungu na mwanaume wakwanza alikuwa Adam alipewa kutawala viumbe vingine, kutunza bustani na msaidizi wake ni mwanamke Eva.

Katika nadharia hii kuna vitu vitatu vinajitokeza hasa kuhusu mwanaume

a) Asili ya mwanaume ni kutawala (dominate).

b) Mwanaume ni kiongozi (leader).

c) Mfanyaji kazi kiasili. (worker)

ii. Wanamapinduzi/wanaubadilikaji (Wanasayansi na wasioamini katika Mungu)

Dhana hii ya wana mapinduzi katika kutafsiri mwanaume ilihasisiwa na mwanabaiolojia Charles Darwin mnamo karne ya 19 hii kikmueleza mwanaume asili yake ni kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyochukua miaka mingi hivyo mwanadamu mwanaume ni mnyama au kiumbe jamii

Unaposema au kueleza dhana hii katika muktadha wa msamiati Jamii ni lazima kila jamii kiasili ina mpangilio Fulani kuitambulisha hasa za wanadamu ikiwemo uongozi na mfumo wa sheria flani zenye kubeba utambulisho wa jamii hizo.

Kutokana na dhana ya unyama unapata vitu vinavyojitokeza

a) Mwenye nguvu mpishe.

b) Kupambana kwa ajili ya rasiliamali wakati wote ( resource) ili uendelee kuwepo.

c) Samaki mkubwa ni halali kumla mdogo ili aendelee kuwepo.

iii. Tafsiri ya jumla inayopatikana.

Hivyo tunapoangalia katika utangulizi hasa katika kufahamu tafsiri na asili ya mwanaume kutokana na vyanzo vya imani pamoja na wanasayansi utagundua zipo sifa ambazo ni za kiasili na pia kibaiolojia na kisaikolojia ambapo nadharia zote hizi mbili za dini na wanasayansi au wanaubadilikaji wanazitaja.

Kila mwanaume anazo ila katika kujidhihirisha kwake kwa kila mwanaume ni tofauti kutokana na nidhamu ambazo kila mwanaume anazipata kupitia tamaduni imani malezi pamoja na mazingira anayokulia au kuwepo.

iv. Tofauti ya mwanaume (manhood) na uanaume (masculinity).

Mtakubalina na mimi katika haya machache hasa napotumia msamiatikuwa mwanaume” kigezo cha kitamaduni katika mtazamo wa jamii mbalimbali. Leo hii kuna msemo unaibuka hapa nyumbani Tanzania kwenye uhususani kwenye mitandao kuhusu “mwanaume wa dar” na “wa mikoani” huku wakijaribu kutofautisha kwa namna tofautitofauti.

Mtazamo wa uanaume ni tofauti katika jamii mbalimbali mfano kuna jamii nyingine sifa mojawapo ya uanaume inajumuishwa na suala la kutahiriwa na nyingine kutotahiriwa, zipo zinazosema uanaume kuwa na wake wengi na nyingine kuwa na mke mmoja, pia zipo zinazovuka mipaka hata kusema kulia sio uanaume.

Hivyo ni vigezo tu lakini ni vya kitamaduni zaidi na lengo la makala hii ni kuangazia zile za kiasili yaani mwanadamu wanaume anapozaliwa anakuwa nazo ila nidhamu anayojifunza ndio inamsaidia kumtofautisha kimaamuzi katika kujidhihirisha kwa tabia hizi.

FAHAMU TABIA NA UASILI NDANI YA MWANAUME.

Hizi tabia haijarishi taifa kabila jamii tamaduni ila kinachotofautisha ujihidhihirishaji ni ni nidhamu ya ujidhibiti au kujizuia “self control” kunakotokana na malezi, tamaduni, mazingira na imani.

1. Kutungwa kwa mimba.

Tulifundishwa katika ngazi mbalimbali za kielimu kuhusu Kromosomu tafsiri rahisi hili azaliwe mtoto mwanaume ina maana baba anapotoa mbegu ya kiume yenye kromosomu X ina maana mtoto anakuwa wa kiume sababu mama (mwanamke) yeye huwa na kromosomu Y tu ila mwanaume yeye anazo zote mbili yaani ile kromosomu X na Y hivyo kuzaliwa mtoto wa kike au wa kiume hutegemea baba anatoa kromosomu gani.

(Unapata jibu mwenye kusababisha mtoto azaliwe wakike au wa kiume ni baba (mwanaume)

Hivyo kromosomu XY (Mwanaume) inaelezwa na wanasayansi kuwa na mapungufu kutokana na X hivyo si sawa na hile yenye YY (Mwanamke).
upload_2018-5-17_14-0-15-png.779846

(Picha inayoonesha shughuli watoto wa kiume wanajishughulisha wakiwa katika umri)

Hivyo mapungufu hayo yanafanya pia idadi ya wanaume kuwa wachache kuliko wanawake. wanaoweza kuhimili kuishi “survive” wakiwa watoto na kukua ni wakike kuliko wakiume kwa mujibu wa tafiti.

Ijapokuwa watoto wanazaliwa wengi wakiume kuliko wakike. lakini shughuli, michezo ya hatari na majukumu hasa kwa watoto wakiume katika jamii mbalimbali inasababisha watoto wakiume kuwa katika hatari nyingi na mazingira hayo, na hivyo idadi yao kuwa chache sana ukilinganisha na wale wa kike.
upload_2018-5-17_14-0-30-png.779847

(Picha inayoonesha shughuli ambazo watoto wakike wanajishughurisha muda mwingi wakiwa na umri mdogo mmoja kambeba mdogo wake na wapo karibu na jiko nyuma yao)

Changamoto hii mara nyingi hujidhihirisha wakati wa kipindi cha kuoa na kuolewa sababu watoto wakike pia wanapofikia kipindi hiki mapema tofauti na wa kiume na hapo uchache ndipo unajidhihirisha.

2. Akili ya mwanaume na uongeaji.

“Kuna msemo mmoja unasema wanawake zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo ni umbea lakini wanaume zaidi ya watatu wanapokuwa katika mazungumzo wao wanapashana habari”
upload_2018-5-17_14-0-43-png.779849

(Tafiti zinabainisha kwa siku mwanaume huongea maneno 7000 na mwanamke uongea maneno 20,000)

Katika kipengele hiki tunajifunza kifiziolojia utendaji wa ubongo wa mwanaume unaegemea sana katika upande wa kushoto na wanawake kwao ni upande wa kulia.

Utendaji wa akili hasa katika upande wa kushoto tunauita wenye kuwezesha fikra na mawazo mantiki “logic” na wenye uchanganuzi sana wa mambo.

lakini ule wa upande wa kulia wenyewe uwezo katika fikra au mawazo ya ubunifu, uelewa wa masuala kiasili (shuku)

Kwahiyo kwa dhana hii utajifunza kuwa mwanamke huwa muongeaji sana kuliko mwanaume hilo ni suala la kimaumbile.

Pia mwanamke anauelewa mkubwa sana wa kiasili “intuitive thinking” kushinda mwanaume na ndio sababu mtoto wa kike kumtuma akakuelewa akiwa mtoto wa miaka mitatu ni mkubwa kuliko kwa mtoto wa kiume.

Mtoto wa kike hata unaweza muachia mtoto mdogo akakaa nae akamuangalia bila shida yoyote.

Pia uwezo wa kuanza kuongea kwa mtoto wa kike anaanza mapema kuliko wa kiume.

Pia unajifunza suala jingine hasa katika mahusiano mwanamke anafikia ukomavu wa kifikra na mawazo akiwa na miaka 22 na anaweza kuolewa na akatunza familia vizuri wakati kwa mwanaume ni kuanzia umri wa miaka 27 ndio anafikia kiwango hicho cha kukua kifikra.

Mwanamke na mwanaume wanapolingana kiumri kiasili mwanaume ni mdogo kwa mwanamke.

Unajua sasa kwanini mwanaume anachoshwa haraka na mwanamke anaeongea sana?

3. Ukali (Aggressiveness).
upload_2018-5-17_14-1-2-png.779851

(Wavulana wakipigana, tazama wanaowagombelezea wakike anamaanisha kuwaachanisha lakini wakiume anafanya kwaajili ya picha wengine wakiume wanashuhudia pambano)

Tafsiri ya neno aggressive inapokuja katika lugha ya Kiswahili haileti ladha kamili hasa katika upande wa saikolojia ijapukuwa inatoa muelekeo wa kidhana

Aggressive ni “ushari”, “gomvi”, “chokozi” “jeuri” na tafsiri nyingine ni “kutaka maendeleo”.

Hivyo kila mwanaume ana hali hii kiasili himo ndani yake ila kujitokeza kwake kunatokana na nidhamu katika imani tamaduni au mazingira huo unakuwa ndio msingi wa kujidhibiti au kujiachilia.

Kwanini basi hali hii hipo kwa wanaume? Sababu ya homoni inayoitwa Testosterone homoni hii huwa katika viungo vya uzazi wa mwanaume na ndio inayomtofautisha mwanaume kitabia na mwanamke.
upload_2018-5-17_14-1-22-png.779854

(Donald Trump anaelezwa kuwa ni moja ya watu wenye viwango vingi vya testosterone katika mwili wake)

Je nini kinachotokea homoni hii inapozidi? Tafiti zinabainisha kuwa wengi wenye homoni hii iliyozidi huwa na hali ya kupambana sana kimaisha homoni hii inafanyika kama kumpa motisha ndani yake. Ndio maana matajiri au mabosi wengi huwa ni wakali na pia wengi ni wanyanyasaji wa kijinsia “womanizer” sababu tafiti wengi huwa wana homoni hii iliyozidi.

Lakini changamoto hasa watu wengi sana wanaozidiwa na homoni hii hasa maeneo ya afrika na asia huishia kuwa na wanawake wengi.

Na pia kuwepo kwa homoni hii kunasababisha pia matukio mengi ya uharifu kwa mujibu wa takwimu, matukio ya uharifu utekelezwa kwa asilimia kubwa na wanaume kuliko wanawake.
upload_2018-5-17_14-1-37-png.779857

(Swali kwa wasomaji wajinsia zote? Je sinema gani kati ungepata shahuku ya kuanza itazama )

Pia kujidhihirisha kwa homoni hii inafanya wanaume wengi sana kupenda michezo au filamu zenye mapigano mfano Vita, ubabe, na michezo kama ngumi. Na hata kuwa washabiki sana pale mazingira ya ugomvi unapotokea kuliko kusuluhisha au kuamulia.

4. Utawala (Dominance)
upload_2018-5-17_14-2-5-png.779859

(Picha askari wa uingereza wakielekea vitani pembeni ni wake zao (mtoto akimkimbilia baba yake). Kwa karne nyingi matukio ya vita yalihamasishwa kwa kauli mbiu ya wanaume kupigania uhuru wao, wake na vizazi vyao dhidi ya maadui wa nje.)

Tafsiri yake ni kitendo cha kuwa na amri juu ya au amuru au mamlaka. Kama nilivyojaribu kupitia nadharia mbili ya asili ya mwanadamu hasa mwanaume zote kwa pamoja zinabainisha kuwa kila mwanaume anakitu kutawala ndani yake haijalishi umri wake.

Kupitia nadharia hii mwanaume kiasili anawajibika kwa ajili ya jamii yake katika kuilinda na kuipigania dhidi ya matukio mbalimbali katika ulimwengu mfano uharifu, majanga na vita

mfano Baba ujiona anawajibika kwa ajili ya familia yake mkewe na watoto pia kila kijana wa kiume hujiona ana wajibu kuwalinda dada zake. Hivyo suala hili ni la kiasili kabisa.

Hivyo katika hili unapata kufahamu kwanini jamii nyingi zina tamaduni mfumo dume yaani zinazowapa wanaume kipaumbele au mazingira pendelevu.

Utajifunza kosa kubwa mwanamke analolifanya kwa mwanaume ni pale kumvunjia heshima au kutomuheshimu mume wake au kaka yake au mtu yoyote kaitka jamii ambaye ni jinsia ya kiume.
upload_2018-5-17_14-2-22-png.779862

Ukitaka kuutikisa moyo wa mwanaume kwa muda muoneshe kumheshimu (hii kwa wanawake).

Pia kwa sababu hii utagundua kuna jambo linajichipuza nalo ni “Wivu” hivyo si jambo la kawaida kukuta mwanamke ameolewa na wanaume watatu wakaishi pamoja lakini mwanaume kuoa zaidi ya watatu ni jambo la kawaida kwa tamaduni nyingi duniani.

Pia utafahamu wanaume kwanini huwa hawaaminiani wao kwa wao kuhusu mwanamke.

Wivu ni kitu kipo pia kwa kila mwanaume.

5. Mwanaume huvutiwa kwa kutazama.
upload_2018-5-17_14-2-39-png.779864

(Picha ya mchoro inayomuonesha mfalme Daudi akimwangalia mwanamke anayeoga (Mke wa kamanda wake “Uria Mhiti”) baadaye alimtwaa na kuwa mke wake baada kutengeneza mazingira ya Uria Mhiti kuuliwa vitani Ghadhabu na adhabu ya Mungu ikawaka juu ya nyumba ya Mfalme Daudi.)

Picha ya kielelezo hiki nimemtumia Mfalme Daudi kama kielelezo kuwa mwanaume yoyote anaweza kukumbana na hali ya uzinzi au uasherati kama akijisahau katika nidhamu ya kudhibiti macho yake.

Niliwahi kumsikia dada mmoja ambaye alikuwa na ghadhabu sana kutokana na tabia ya mchumba wake, hasa wanapotoka yaani ni rahisi sana kugeuka geuka wanapopita wadada wengine kwahiyo alishindwa mvumilia kabisa kutokana na mara kwa mara kuongea nae laikini tabia hiyo ilikuwa inajirudia baada ya muda hivyo aliafikia kuachana nae na kuvunja uchumba.

Labda nirejee sehemu ya utaangulizi nilipoeleza kuwa utofauti wa wanaume na asili yao hutokana na nidhamu ambazo kila mwanaume anazipata anafundishwa anajifunza kupitia tamaduni, imani na malezi pamoja na mazingira anayokulia au kuwepo.
upload_2018-5-17_14-2-54-png.779867

Hivyo tamaa ya kuvutiwa kwa mwanaume hasa kwa wa jinsia nyingine ina nguvu sana machoni, ila kila mwanaume ana nidhamu ya kujidhibiti kwa namna tofautitofauti.

a) Mwanaume ni rahisi kumpenda mtu kwa uzuri au kwa kumuona tu lakini kwa mwanamke yeye anaegemea sana hisia zake na mara nyingi hisia utegemea ukaribu wa kipindi Fulani au kwa kusikia tu habari za mtu Fulani. Lakini mwanaume inamtokea tu kwa kuona sababu tamaa ya wanaume hipo machoni.

b) Vilevile utajifunza kwanini wanawake wengi hupoteza mvuto kwa wanaume zao baada ya kuwaoa? Sababu wanawake wengi hawafahamu mawanaume huvutiwa na muonekano (physical appearance) na wanawake wakishaolewa huwa wanaacha kujari muonekano wao tena mbele za wanaume zao.

c) Pia kwa kigezo hiki unajifunza kwanini wanaume hunaswa kirahisi na wanawake wanaovaa nguo za utata na kujiremba lakini wake zao wanapoondoka baada ya mifarakano hupata tabu sana na kujaribu kutafuta suruhu nao baada ya kutafakari sana kuhusu kutaka na kupenda kupi muhimu.

Sababu moyo wa mwanaume hutamani wengi lakini upendo wake huwa sehemu moja.
(Pia tunajifunza katika vitabu vya imani kupitia mtoto wa kwanza Reubeni wa mzee Yakobo (Israel) alivyojikuta akiingia katika mahusiano ya kimapenzi na mama yake Mdogo Bilha ambaye ni mke mdogo wa baba yake).

Hivyo ni muhimu sana kwa kijana wa kiume kujifunza kuwa na nidhamu ya udhibiti wa macho yako itakujenga katika nidhamu ya kuutawala mwili wako kihisia si kila kitu lazima utazame tu kama hupo katika maisha ya kimalengo juu ya kesho yako (si vijana wengi wakiume wanaishi kimalengo).

Kijana wa kiume kuna mazingira mengine huwa yanatokea usijiamini kupita kiasi, sababu Duma na swala hawawezi kuishi kwa karibu halafu lisitokee lakutokea.
6. Shawishi au shawishika (Persuade)
upload_2018-5-17_14-3-11-png.779869

(Picha hii inaonesha tukio la kijamii linalohusu upimaji wa afya. Angalia je waliojitokeza kuhudhuria idadi hipi ni kubwa? katika ya wanaume na wanawake.)

Wengi tunaoudhuria katika shughuli mbalimbali za kijamii mfano zili zinazohusisha labda uchangiaji damu, upimaji wa afya, semina, misiba, mikutano ya kidini utagundua idadi kubwa sana ya wahudhuriaji wakubwa au kwa idadi kubwa ni wanawake kuliko wanaume.

Kama ujawahi fanya tafiti hiyo hanza kuanzia sasa kama ni kanisani (sababu jumuiya hii uwachangamanisha watu wa jinsia zote mahali pamoja) tofauti na jumuiya za imani nyingine. utagundua kundi la wanawake huwa ni kubwa sana. Basi umeshawahi jiuliza kwanini?

Kama nilivyoelezea pia katika sababu mojawapo inayowatofautisha wanaume na wanawake kiakili wanaume hutumia zaidi sehemu ya ubongo wa kushoto. Hivyo kumshawishi mwanaume katika shughuli za kijamii kunahitaji sana sababu za kimantiki katika fikra zake na za kujitosheleza au pengine kama kuna manufaa au kumuinulia shauku.

Hivyo muhimu cha kufanya kama unaosoma ujumbe huu ni mwanamke umeolewa fanya hivyo vya msingi kwanza baada ya yeye kuona manufaa, mantiki au kupatwa na shauku basi utamvuta lakini kumbembeleza au kumlazimisha hakuwezi kuleta muafaka anaweza kufanya kukufurahisha tu kwa muda huo lakini si kwa kudhamiria.
upload_2018-5-17_14-3-39-png.779873

Hata katika saikolojia ya matangazo sababu njia moja ya kujaribu kushawishi jinsia zote katika biashara hutumia wanawake wazuri ili kupata uangalifu wa mwanaume katika kuuza na kutangaza bidhaa zao.
****************************************************************************
Pia ili huweze kufuatilia vizuri mafundisho haya kuhusu Saikolojia na maisha ni vizuri kama utaanza ni follow katika akaunti yangu “Education mentor” niombe radhi tu kwa wale walioniomba kuwatag hinaniwia vigumu kukumbuka majina yote.

Na pia kuhusu Maswali yoyote ya kisaikolojia na maisha unaweza niuliza PM na mimi ntayajibu kwa mfumo wa makala au “mada”.

KUHUSU MWANDISHI,

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Vitabu vinavyohusu Falsafa na maisha, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).

Makala nyingine alizoandika Education Mentor..
Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda

Saikolojia: Sababu zinazosababisha magonjwa ya akili ambazo wengi hawafahamu. (psychological disorder)

Saikolojia:Jifunze mambo yakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (Case study Finland)

Saikolojia: Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (sehemu ya pili)

Saikolojia: Fahamu magonjwa ya kisaikolojia, dalili,tabia na mifano.(Case study Tanzania)

Saikolojia: Je Nimlipizie kisasi au nimsamehe?. (Vita visivyoisha vya Afghanistan)

Mkuu hapo kwenye Chromosome umechanganya ,mwanamke ana chromosome XX na mwanaume ana Chromosome X and Y ,kwahiyo XX mtoto atakuwa wa kike na XY mtoto atakuwa wa kiume
 
Back
Top Bottom