Said Ngamba alias 'Mzee Small wa Ngamba' afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Taarifa tulzozipata hivi punde kuwa muigizaji Said Ngamba au Mzee Small Amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu.

Mzee Small alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa kipindi kirefu.

Chanzo cha taarifa hizi ni Mtoto wake wa kiume Mahmudu (Mongamba) ambaye anadai Baba yake alipelekwa hospitali ya Muhimbili Jumamosi Tar 7 Juni (jana), muda wa saa mbili asubuhi baada ya kuzidiwa. Ameeleza kwamba alishinda naye kutwa nzima ila ilipofika saa 4:09 usiku akafariki akiwa mikononi mwake.

Said Ngamba au Mzee Small (amezaliwa mw. 1955) na alikuwa msanii wa maigizo na vichekesho nchini Tanzania.

Mungu ampe pumziko jema la milele


Said-Wangamba.jpg



HISTORIA YAKE FUPI

Jina lake ni Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (58). Amezaliwa mwaka 1955. Alikuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo hapa Bongo.

Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila ulipozungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.

Mzee Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono' (kwa sasa na yeye ni marehemu).

Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small ametumika katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.

Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.

Baadaye aliibuka na kitu kingine kikali kilichokwenda kwa jina la Nani Kama Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali wengine kama King Majuto, Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa Bongo.

Mzee Small ndiye alikuwa mmiliki wa kundi la sanaa linalojulikana kama Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.

Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini mkongwe huyo hakuwa na mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichofanya ni kurekodi na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano maalum.

Kutokana na vichekesho, Mzee Small alikuwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma alikuwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani alijua kinachoendelea kuwa ni kazi tu.

Mzee Small ameacha watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike.

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

attachment.php

[h=2]Rais JK akiwasili kwenye msiba wa marehemu Said Ngamba a.k.a Mzee Small[/h]
 
rip...

----------------------
PICHA ZA MATUKIO KATIKA MAZISHI

MAMIA WAMZIKA MSANII MKONGWE WA MAIGIZO NCHINI MZEE SMALL



IMG_4686.JPG

Msafara wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwaajili ya Kumpumzisha Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu Mzee Small
IMG_4692.JPG

Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza) likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye Makaburi ya Segerea jioni Hii
IMG_4698.JPG

Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea


IMG_4711.JPG

IMG_4716.JPG

Vijana wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small
IMG_4743.JPG

Vijana wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small wakielekea kwenye Makaburi ya Segerea Jioni Hii.
IMG_4664.JPG

Watu mbalimbali wakisubiri Mwili wa Marehemu kuwasili katika makaburi ya Segerea
IMG_4665.JPG

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akiwasilika katika eneo la Makaburi ya Segerea jioni hii kwaajili ya kumzika Mzee Small
IMG_4770.JPG

IMG_4776.JPG

Mwili wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.
IMG_4661.JPG

Watu mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika Mzee Small. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
IMG_4739.JPG

Umati wa watu wakielekea Kupokea Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small wakati ulipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Segerea.
IMG_4760.JPG

IMG_4668.JPG

IMG_4788.JPG

IMG_4792.JPG

Wanahabari wakitafuta taswira katika mazishi ya Mzee Small katika Makaburi ya Segerea
IMG_4666.JPG

IMG_4671.JPG

IMG_4723.JPG

IMG_4795.JPG

IMG_4798.JPG

IMG_4801.JPG

IMG_4804.JPG

IMG_4819.JPG

IMG_4824.JPG

IMG_4834.JPG

IMG_4838.JPG

IMG_4841.JPG

IMG_4843.JPG

IMG_4749.JPG

IMG_4759.JPG


Picha Zote na Josephat Lukaza
 
dah!! r.i.p mzee small.. haya sasa mbona majanga bongo muvi
 
habari za kusikitisha ni kwamba mzee small amefariki dunia hospitalini muhimbili kwa ugonjwa wa presha.source instagram page ya zamaradi mketema na tovuti ya global publishers.
 
mzee small alikuwa anaumwa muda sana aliomba pia msaada sana wa kutibiwa, utaskia michango ikatayo changishwa sasa.r.I.p.mzee small
 
Dah another Leaders Saga

Rip.....ila huyujamaamara sita anasemewa kafa afi ngojanisubirndugu
 
Kuna taarifa nilozozipata hivi punde kuwa muigizaji Said Ngamba au Mzee Small Amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu.
Natanguliza pole kwa wafiwa.

unauhakika mpaka utoe RIP?

tujijengee utamaduni wa kutotoa RIP mpaka habari iwe cinfirmed... huku ndo kuchuliana
 
Back
Top Bottom