Sahihisho: CCM haijapungua mvuto

mjogoro

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
882
652
wana jf, salaamKufuatia wimbi la mageuzi ya kisiasa kushika kasi hapa nchini, baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa wamesikika kwa nyakati tofauti wakisema kuwa eti CCM imepungua mvuto mbele ya jamii. lakini mimi napingana vikali na mtazamo huu kwani naamini kuwa CCM haijawahi kuwa na mvuto wowote kwa jamii. CCM ni ileile haikuwahi kuwa na lolote na sasa haina lolote. kinachotokea sasa ni matokeo ya mwamko wa wananchi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo mustakbali wa maisha yao na maendeleo kwa ujumla.
 
huo ukweli dhahiri........watu wa sasa ni wapya taifa limezaliwa upwa....hata kibiblia ni mwaka wa jubilii yani mwaka wa matengenezo......(miaka 50) amabayo tuliazimisha mwaka jana mwaka wa 50 tangu uhuru...
 
Well said mkuu. Ila inabidi nguvu ya mapambano iongezeke hii vita si lelemama...
 
mjogoro, iliwahi kuwa na mvuto japo ulikuwa ni wakulazimishwa na watu waliamini hakuna nyingine zaidi yake. Sasa watu wanataka kujaribu wengine. Ni sawa na mzazi anapopata mtoto wa pili au zaidi, hupunguza kumjali yule wa kwanza na upendo zaidi kuamia kwa yule wa pili.
 
Last edited by a moderator:
Waacheni wafu wazikane wao kwa wao, mbona mnawasumbua CCM? Msiwaamshe
 
Ni kweli CCM haijapungua mvuto bali imepungua wanachama!
 
Hii noma ipo nchi nzima, ccm imechokwa mpaka nyumbani kwa Jk.
 
kweli kabisa na nguvu za ziada zinaitajika kuwaamsha wengi ambao hawajajua ukweli kwamba watabzania walitakiwa wawe katika hali gani toka tulipopata uhuru
 
Kikwete mwenyewe kaichoka ccm kama ulisikia hotuba yake miy mosi utaamini maneno yangu.
 
Back
Top Bottom