Safari za vigogo zalitafuna taifa

Safari za vigogo zalifilisi taifa
• Kwa mwaka mmoja tu 'zimetafuna' sh bil. 28

na Rahel Chizoza, Dodoma
Tanzania Daima


amka2.gif
WAKATI wananchi wakihoji na kulalamikia wingi wa safari za viongozi, hususan zinazomhusu Rais Jakaya Kikwete, imedhibitika ziara zimekuwa zikiligharimu taifa mamilioni ya fedha.
Ukweli huo, umethibitika juzi wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano, Bernard Membe, alipokuwa akisoma bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2010/11, bungeni mjini Dodoma.
Hatua hiyo, imetokakana na safari hizo kutumia kiasi cha sh bilioni 28 za Kitanzania, licha ya kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa na watu wa kada tofauti.

Waziri Membe, alisema fedha hizo zimetumika katika mwaka wa fedha 2009/2010 tu.
Waziri Membe, alisema kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ameagiza kuangaliwa upya orodha ya watu wanaoongozana na viongozi katika safari hizo.

Alisema mpaka sasa, serikali iko kwenye mchakato wa hatua za mwisho wa kupunguza orodha ya watumishi wa serikali wanaosafiri nje na viongozi.

Waziri Membe, alisema fedha zilizotumika ni nyingi, ingawa zilikuwa na umuhimu kwa taifa.

Alisema idadi ya watu na orodha maalum inayoandaliwa kwa ajili ya kuongozana na viongozi wakati wa ziara za nje, itahusu ziara za Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu.

Alisema safari hizo, zimekuwa na manufaa kwa uchumi wa nchi kwani wakati mwingine wamekuwa wakisafiri kwa lengo la kwenda “kuhemea” kwa wahisani na marafiki wa Tanzania.
Alisema, safari hazipaswi kuchukuliwa kama ni anasa kwa viongozi, kwani zimekuwa ni sehemu ya shughuli za kiutendaji za viongozi hao wakati zingine zimekuwa ni mialiko ya mikutano ya kimataifa.

Katika hatua nyingine, Waziri Membe amewaonya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na kutamka kuwa atamfukuza nchini balozi yeyote atakayebainika kufanya kazi za vyama vya siasa nchini.

Alisema kazi za mabozi ziko wazi na kila mmoja anafahamu wajibu wake na kubainisha kuwa kufanya kazi na vyama vya siasa au kuvichangia kunaruhusiwa, lakini kinachokatazwa ni kufanya kazi za vya vyama vya siasa.

Akizungumza kwa ukali, Waziri Membe alisema hatasita kumfukuza balozi yeyote atakayesaidia chama chochote cha siasa mbinu za kukimaliza chama kingine kiwe chama tawala au cha upinzani.

“Natoa onyo kwa mabalozi kutoka nchi mbalimbali, nitamfukuza mtu hata kesho kama atakiuka taratibu zetu, isome akili yangu na isome midomo yangu kwa hili nitakuwa mkali maana mgeni hawezi kuja kwako na kukuingilia mpaka jikoni halafu unyamaze,” alisema Membe kwa ukali.

Alisema wapo mabalozi waliotoa misaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi lakini hivi sasa wanataka kutoa masharti na kubainisha kuwa Tanzania haitakuwa tayari kwa jambo hilo na kutamka kuwa yeyote mwenye nia ya kutoa msaada kwa masharti asitoe kabisa. Alibainisha kuwa katika suala la uchaguzi, Tanzania inapaswa kuachwa yenyewe iamue chama gani kiongoze kwa kuzingatia demokrasia kupitia mfumo wa kupiga kura.
 
sio safari za nje tu bali hata safari za kulazimisha za ndani ambapo viongozi kibao hujiandikia posho almaarufu 'night'
 
hivi watu walipokuwa wakipiga kelele walifikiri ni wenda wazimu?

safari za nje, za ndani, seminar znahujumu taifa
 
Back
Top Bottom