Safari siyo kifo.......Babu DC !!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,599
Bandugu bapendwa, safari siyo kifo na Mungu siyo Athumani wala Abdallah!

Babu DC karudi salama
Kamkuta bibi mzima kama malaika
Hakuna uchakachuaji hata kidogo
Wajukuu hawajambo wote?
NasiKia baadhi wamekuMbwa na mafuriko
DA kapatwa na jinamizi gani?
AD naye vipi?

Nasubiri kusikia mengi...
Nambie kama nyumba haijachomwa moto
Tena kwa maji ya uvuguvugu
The Finest fanyara hima,
Mtoe babu wasiwasi
Hebu mweleze babu
Kondoo wote wako salama?
Judith na Kashaija butege
Mwimbie babu shairi
Atulize roho yake, na kuvuta kiko kwa raha zake,

Babu DC 1947!!
 
Karibu sana DC mie niko salama ila niliamua kuchukua likizo ya muda mfupi kidogo.
 
Welcome back comrade.....Miss Judith anatunoa namna ya kutongoza.....
 
Karibu sana DC mie niko salama ila niliamua kuchukua likizo ya muda mfupi kidogo.

Hivi ile ban ulikua umepewa ulikua umeamua kuchukua Likizo. ulisababisha Jamvi likafurika Thread za kuuliza kulikoni.
Halafu nyie mods hamkututendea haki, ina maana m2 hawezi kuchukua likizo bila kuomba ban?
 
Babu umejuaje kama bibi hajachakachuliwa?
karibu tena

Halafu wewe......? Inaonekana huna uchungu na afya ya babu.....!! Kwani umesahau kuwa tunatakiwa kuishi kwa kanuni ya imani?

Hebu basi fanya juhudu za makusudu kuturudishia ile avatar yetu tukufu...Hii ya uchakachuaji hailipi!!
 
Karibu sana DC mie niko salama ila niliamua kuchukua likizo ya muda mfupi kidogo.

Kama uliomba mapumziko kwa nini unataka kumpandisha babu pressure? Siku nyingine toa taarifa. Vinginevyo babu ataanza kutumia silaha yake ya mwisho kuwashushia laana wajukuu wasiomtakia mema!

Hivi ile ban ulikua umepewa ulikua umeamua kuchukua Likizo. ulisababisha Jamvi likafurika Thread za kuuliza kulikoni.
Halafu nyie mods hamkututendea haki, ina maana m2 hawezi kuchukua likizo bila kuomba ban?

Umeona eehh... Kama mtu kaomba si tuambiwe basi??
 
Nimeamini unanipenda thanks pata hii basi

The Following 2 Users Say Thank You to vivian For This Useful Post:

Dark City (Today), Dena Amsi (Today)​
 
Kama uliomba mapumziko kwa nini unataka kumpandisha babu pressure? Siku nyingine toa taarifa. Vinginevyo babu ataanza kutumia silaha yake ya mwisho kuwashushia laana wajukuu wasiomtakia mema!

Umeona eehh... Kama mtu kaomba si tuambiwe basi??

Nilitoa taarifa labda zilichelewa kufika usijali Babu.
 
Karibu sana babu yangu, nilikumisi kupita maelezo, pole kwa safari babu. Karibu na chai hapa!!
 
Karibu sana babu yangu, nilikumisi kupita maelezo, pole kwa safari babu. Karibu na chai hapa!!

LD....yaani we acha tu!

Ni afadhali kwenda lupango kwa masaa 48 kuliko kuliko kuikosa JF especially hili jukwaa la wajukuu hata kwa saa 1. Siwezi kueleza nikaeleweka taabu alizokumbana nazo babu!!

Bora nimerudi salama....chai ya babu weka sukari kiduuuuchu tu, he will be very happy!
 
Pole sana Babu haitatokea tena

Sawa sawa kajukuu kazuri,

Hebu basi nambie..hawa wajukuu wengine wameenda kuchezea wapi?

Yuko wapi the Finest, wapi Teamo, Maty, AD, Rose, Musinga, MJ1, Judith, BE.....

Shangazi yao Nyamayo naye je? Babu mwenzangu Asprin (2 kutwa mara 3) naye kapatwa na maswahibu gani?

Hebu endelea bas DA!!
 
TF toka atoke asubuhi hajarudi, Teamo alirudi kunywa chai hajarudi tena ,Maty hata chai hajanywa, AD kaomba BAN, Rose kaenda kwa shangazi gongo la mboto, Musinga anarudi kesho alikuwa morogoro, MJ1 nimemwona asubuhi alivyoamka , Judith nimemwona kule mtaa wa pili anacheza, BE ndo umeniua kabisa tangu nirudi namtafuta simpati kabisa mpaka nimechanganyikiwa.

Nyamayao nilikuwa nae sasa hivi tu alikuwa kwa mama wa kambo, Asprin alikuwepo asubuhi mahali fulani anazimua na mama wa kambo
 
Back
Top Bottom