Sadaka ni nini? Je Kanisani inatolewa Sadaka kwa mujibu wa andiko gani la Agano Jipya?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Kama nilivyouliza Kwenye kichwa cha thread

Niko Hapa kujifunza na kupata maarifa zaidi

Nawatakia Dominica Njema 😀
 
Nenda kanisani, leo ni Epifania, sherehe ya mwana wa Mungu kujifunua kwa mataifa, nao kumtolea sadaka kupitia zawadi za Mamajusi
 
Sadaka ni michango au zawadi inayotolewa kwa hiari kwa madhumuni ya kidini au kijamii. Katika Kanisa, sadaka hutolewa kama sehemu ya ibada na kuchangia kazi za kanisa. Katika Agano Jipya, mafundisho mengi kuhusu kutoa sadaka yamejikita katika mafundisho ya Yesu na maandiko mengine.

Moja ya mafungu yanayohusu kutoa sadaka linapatikana katika Injili ya Mathayo 6:2-4, ambapo Yesu anawahimiza watu kutoa sadaka kwa unyenyekevu na kwa siri, bila kujionyesha mbele za watu. Pia, mafundisho mengine yanapatikana katika barua za mitume, kama vile 2 Wakorintho 9:7, ambayo inasisitiza umuhimu wa kutoa kwa furaha na moyo wa ukarimu.

Sadaka pia inajadiliwa katika maandiko mengine ya Agano Jipya, na misingi ya kutoa sadaka inategemea zaidi maadili ya Kikristo na wito wa kujitolea kwa ajili ya Mungu na wenzetu wenye uhitaji.
 
SADAKA NI NINI ?

Sadaka ni Ibada kamili kati yako wewe na MUNGU
aliyekuumba,unamtolea MUNGU ili sadaka yako
inene kama ya Abeli.na ili sadaka yako inene
mbele za MUNGU, kwanza mtu asijue umetoa
kiasi gani. Ukisoma katika injili ya Mathayo 6:
(2-4) inaelezea usishauriwe na mtu, hata
mtumishi, utoe kiasi gani.

Sadaka za michango hizo hazimuhusu
MUNGU, sadaka za kuahidi, madeni, Imani, eti
ukipata ulete na zote hata ukombozi siyo za
mpango wa MUNGU, huu ni ujanja wa shetani
ameliteka kanisa na kubadili mpango wa MUNGU
ili wewe usifanikiwe na ushiriki kufanya haya
ambayo hajaruhusu upate dhambi.
Ukiambiwa toa mpaka iume usifanye hivyo,
haipokelewi .Toa kwa furaha, YESU hanyan’ganyi
pesa kama ilivyo makanisani siku hizi, huyo ni
shetani na anayefanya hivyo ndani ya moyo wake
mtumishi huyo anayo roho ya kuasi na tamaa juu
ya pesa.
Ukifuatwa kudaiwa pesa labda mfano wa kununua
kitu, mfano kinanda,gari, mabati, usitoe YESU siyo
omba omba na hana shida kama ni mpango wake
ataleta watu watafanya tena kwa furaha. Ukitoa
haubarikiwi ni sawa na kutupa jalalani,
ameniambia YESU niuambie ulimwengu wote
ubadilike awarudi sasa, na utukufu wake wa
mwisho ndio huu sasa umeanza ni kweli tuu
mpaka aje na kuharibu uovu wote.
Ukikuta madhabahu inachangisha au kukopa benki
–hapo hayupo na sadaka zenu zinapotea,
YESU halipi riba, leo analazimishwa kulipa riba,
hapo ni shetani amekunja nne anawachuna, YESU
hakopi wala kulipa riba, leo hii iweje kanisa likope
benki? Sio kanisa lake, hata kama jina lake
linatajwa hapo ni machukizo. ( Marko 7: 6-7)
  • inapokopa benki – mfu
  • inatoa huduma za kiroho kwa pesa – mfu
  • madhabahu inayofanya kazi za biashara –
mfu
- kazi ya kanisa la YESU siyo kufanya
biashara, huoni majibu unakaa hapo miaka nenda
rudi haupo kiroho wala kimwili.
- Utaona ni mateso magonjwa, umasikini
ufukara tuu ndio unaokujaa.
- Ukiona nguvu za giza zinakutesa na
hazikutoki ujue hapo ni mfu.
- Inamatabaka, viongozi ni washirikina, hapo
Uni pesa tu.

TAFAKARI MANENO YA MUNGU SI MWANADAM
 
Marko 12:41-44

41 Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha.
42 Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.

43 Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote!
44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”
 
Kama nilivyouliza Kwenye kichwa cha thread

Niko Hapa kujifunza na kupata maarifa zaidi

Nawatakia Dominica Njema 😀

Zipo sehemu nyingi sana...

Luka 11
40 Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?

41 Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.

Matendo ya Mitume 10
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
 
Wataendaje wasipopelekwa? Sadaka ni muhimu kupelekwa INJILI, kuhudumia maskini wasojiweza na wajane wa Kanisa, yatima nk nk.

Yesu pia alikuwa akipokea sadaka, mhasibu alikuwa Yuda.
 
Back
Top Bottom