Sabodo: Sina mpango wa kuhama CCM; Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania


thursday, 20 october 2011 19:27 newsroom


* awakana chadema, awaonya watanzania

mfanyabiashara maarufu nchini, jaffer sabodo, amesema hajahama na wala hana mpango wa kukihama chama cha mapinduzi (ccm), ambacho amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40.

Sabodo alisema baadhi ya kauli kali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya ccm, hazina maana kuwa anaichukia, isipokuwa zinalenga kukikosoa chama ili kiendelee kuwa imara katika kuwaongoza watanzania na kuharakisha maendeleo yao. Hayo aliyasema jana alipozungumza na naibu katibu mkuu wa ccm (bara), john chiligati nyumbani kwake, upanga, dar es salaam na kuwataka wana ccm na wananchi kwa jumla wasimwelewe vibaya.

"siwezi kuondoka ccm ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, ccm bado chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona chama changu kikiteketea," alisema sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha ccm ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, “vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi.”

alitoa toa wito kwa wananchi kutofanya makosa ya kufanya majaribio ya kuwapa ridhaa wapinzani kuunda serikali. "nawaomba watanzania wenzangu, tusifanye majaribio ya kuwapa chadema au chama kingine chochote zaidi ya ccm kuongoza serikali kwa kuwa havina uzoefu, hatuwezi kufanya majaribio ya kuliweka rehani taifa," alisema mfanyabiashara huyo.

Kuhusu msaada wa sh. Milioni 100 alizotoa hivi karibuni kwa chadema za kuchimba visima vya maji, alisema ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm kwa kuwa visima vitakavyochimbwa vitasaidia wananchi wote bila kujali itikadi zao za siasa.

alisema amepanga kuchimba visima 200 katika majimbo yote nchini, bila kujali wabunge wa majimbo hayo wanatoka vyama gani kwa kuwa lengo lake ni kuwasaidia watanzania na kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya ccm.

naibu katibu mkuu wa ccm, chiligati alimshukuru sabodo kwa kutoa msimamo wake huo kwa kuwa unamaliza minong'ono ya baadhi ya wanachama wa ccm na wananchi kwa jumla juu ya msimamo wa mfanyabiashara huyo ndani ya chama.

"nitawajulisha wanachama wenzako wa ccm na wananchi kwa jumla, kwamba bado uko nao kwa hali na mali ndani ya chama chetu kwa ajili ya ustawi wa taifa letu, kauli yako imemaliza minong'ono kwamba umehama au una mpango wa kuhama ccm," alisema.
.
habari mchakachuo!
 
Nimeiona habari hii kwenye Gazeti la Habari leo pia! Dah Mhindi sio mtu wa kumuamini leo anaiponda Chadema utadhani haijui kabisa! Chadema kwa hili mmedhalilishwa sana na Sabodo kweli pesa ni mbaya!
 
Nimeiona habari hii kwenye Gazeti la Habari leo pia! Dah Mhindi sio mtu wa kumuamini leo anaiponda Chadema utadhani haijui kabisa! Chadema kwa hili mmedhalilishwa sana na Sabodo kweli pesa ni mbaya!

Chadema kudhalilishwa ?
Hebu hapa ndipo nani kawadhalilisha wana CCM na watanzania wote wa vyama vyote na wasio kuwa na vyama

-Barabara hakuna hadi mjini Dar
-Umeme muda wowote hakuna uhakika
-Umeme kukosekana uwanja wa ndege wa kimataifa
-Cement bei juu kisa umeme hakuna
-Serikali inasimamia ulanguzi wa Sukari kwenye kenya , polisi na TRA
-Hakuna madawa hosp
-Hakuna wodi na vitanda wanalala chini wagonjwa
-Shule za kata ni aibu ambazo ndiyo wewe umesoma huko ndiyo maana akili yako ni matope kama kata
-Nyamongo wanauawa polisi wa CCM kisa mali zao
-Getita yale yale
-Ufisadi wa kutisha
-Polisi kuwabambikia kesi walala hoi
Niendelee kaka ? Yako mengi ya kudhalilisha yamefanywa na yanafanywa na CCM na serikali yake .
 
Wakuu, nimejaribu kuifuatilia hiyo habari nimeona ni crap. Haina mashiko. Haijawahi kusemwa na kiongozi yeyote wa CHADEMA kwamba Mzee Sabodo amehamia au anampango wa kuhamia CHADEMA. Mzee mwenyewe siku zote amekuwa akisema yeye ni kada wa CCM, ila anapendezwa na mikakati ya ukombozi wa wanyonge wa TZ inayoendeshwa na CHADEMA. Ndiyo maana amekuwa akitoa pesa mara kwa mara ili kufanikisha mipango ya CHADEMA. Sasa hilo suala la kuihama CCM au kuwakana CHADEMA limetokea wapi. Wanahabri, please stick to ethics.
 
Kwa nini Chadema wanapokwenda kukutana na hawa makada wa CCM wasiende na waandishi wao wa habari warecord wanachosema?Hii ilishatokea tena wakati Chadema walipokwenda Butiama tulisoma walichosema familia ya Nyerere baada ya siku chache Makongoro hakakanusha.Hapa hauwezi kujua kama Sabodo ni mnafiki au mwandishi ni mwongo.
 
Hakika tumesema mengi sana kuhusu huyu SABODO na thread inayosema "Sabodo kumchangia mgombea wa CHADEMA millioni 500 [Bofya Hapa]" na CDM bofya hapa HAKIKA CHADEMA MMEENZA KUONA MCHEZO WENU.


Haya WANACHADEMA mliokua mnamtetea OOOOOOOOOOOOOOOH MZZEEEEEEEEEEEEEEEEE SABBBBBBBBBBBBOOOOOOOOOOOOOOOOOODO

EEEEEEEEEHEEEEEEEEEEEEEE LETENI STORY TUSIKIE.NABADO ENDELEEEEEEEEEEEENI KUAMINI KUWA MTAFANIKIWA KUPITIA PESA ZA WATU MATAJIRI. MIMI BINAFSI NAAMINI MTAFANIKIWA KUPITIA WATU WATAKAVYOJITOA KWA DHATI KWA CHAMA CHENU.TENA PESA NZURI KWENU NI HIZI ZA WANACHAMA WALALA HOI LA JASHO MITAANI KWA MAANA PESA HIZO ZIMEPATIKANA KWA JASHO HALALI,NA SI PESA ZA WAHINDI WALIOWATUMIKISHA WAKINA SANJA NA JUMA BOY.
 
Kwenye thread ya sabodo kuchangia chadema Millioni 500 wengine tulichangia ifuatatavyo

Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafuteni vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.

Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.

Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao pia wako katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Kama chadema ni makini Watch Out.

Hakika wengine tunatoa taadhari hata CCM waliaanza hivyo hivyo,uzuri wakati CCM wanatoka huko chadema ndio wanaingia huko anyway inafikia sehemu wengine wataamini kuwa CCM ndie baba wa mageuzi hivyo siku zote kitaendelea kuwa chama kisicho na mmbadala kwa kuwa wanatumia udhaifu wa vyama vya siasa na sayansi ya siasa za bongo kuendelea kutawala.Ukipokea ujue kuwa kunakutoa.

Tumesema kwa kuwa time will tell.

Ikafuata shutuma dhidi ya uchangiaji nikaibuka na hiii

Uliona wapi adui yako anakupa silaha umpige !!!!!!!! Please tathmini,Yanga na Simba walikuwa wanapokea Pesa toka kwa wafadhili matokeo yake timu hizo zimestuka sasa kwani ulipofika wakati wa kupanga timu [safu] kwa ajili ya mechi kama mfadhiili ana interest na mechi husika ana wazuia wachezaji aliowalipia kwenye usajili kisha timu inaingia matatizoni kwa wachezaji kususia mechi na migogolo isiyoisha.

Kupokea kwa chama cha siasa kitawafanya wapumbazike na kushindwa kutafuta njia genuine za kujiingizia kipato cha kuendeshea chama matokeo yake watawategemea wafadhili ambao kwa siku isiyo na jina wafadhili wata pull out na kuwaacha chadema kwenye uhitaji mkubwa sana wa kifedha na majukumu ya kukamilisha kupitia fedha hizo na kuzingatia wamebweteka na hapo ndio the sinking boat will loose the direction and its where the hunter become hunted.

Tukaendelea
Kwenye nyekundu kimbunga your right,chadema wafikilie kama walivyofikilia swala la madiwani wa arusha.


Sasa hapa sasa tena naona wengine wameanza kuleta yao kuwa katishwa na CCM you guys acheni kutuyumbisha na ujinga huo mboana haya mambo yako wazi.Ukitaka kujua hya mambo yako wazi maamuzi sahihi ni kufanya mambo sahihi kitendo cha Chadema kutokuunda umoja na CCM kwenye Local Government ndio msimamo wenye kuonyesha kuwa wanajitegemea na umezaa positive image na kuimbua challenge halisi na sasa kila mtu kajua ukweli uko wapi.

CCM walishapita huko wanakujua sana nyie chadema ndio mnaluid huko nani majanja kuliko mwenzie,wajifunze kusikia sauti za umma kabla ya kulipuka kufanya mambo.
 
kUMBE NI GAZETI UCHWALA!!!! HIVI SIKU HIZIHILI GAZETI LINANUNULIWA AU ANALINUNUA JK NA NAPE WAKE MAANA KILA NIKIENDA KWENYE VIBANDA VYA MAGAZETI NAKUTA MAGAZETI KAMA MWANANCHI, TZ DAIMA, MWANAHALISI, NIPASHE YAMEISHA ILA HILI UHURU NAKALA ZIMERUNDIKANA ,,,NADHANI HATA WAUZAJI WATAKATAA KUYANUNUA MAANA NAJUA YANAWAPA HASARA,, VIVAAAAA
ni kweli, nawashauri wagawe bure kwa mabalozi wao wa nyumba kumi kumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom