MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Tangu Sabodo alipoanza kumwaga fedha CHADEMA kumekuwepo na makundi mawili yanayopingana wale wanaosema msaada huo unaonyesha kwamba Sabodo ni mzalendo na wale ambao wanasema Sabodo anajiandalia mazingira mazuri kwa kucheza karata zake vema endapo CHADEMA wanakamata dola.
Mara nyingi tumekuwa na hofu CCM inapopata msaada wa fedha kutoka kwa wafanyabishara lakini hofu hiyo hutuondoka CHADEMA inapopewa fedha na wafanyabiashara. Sabodo akitoa fedha CCM tumesikia makofi machache JF lakini akitoa fedha chadema makofi mengi.
Ni nini maana ya SABODO kutumikia vyama vya siasa viwili?
Kama SABODO amekosana na CCM anaogopa nini kujiondoa badala ya kuwa kama mwanamke mwenye mabwana wawili?
Je SABODO hajatumwa na CCM kuibomoa CHADEMA?