Sabodo anaisaidia au anaiogopa chadema?

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,976
784
Tangu Sabodo alipoanza kumwaga fedha CHADEMA kumekuwepo na makundi mawili yanayopingana wale wanaosema msaada huo unaonyesha kwamba Sabodo ni mzalendo na wale ambao wanasema Sabodo anajiandalia mazingira mazuri kwa kucheza karata zake vema endapo CHADEMA wanakamata dola.

Mara nyingi tumekuwa na hofu CCM inapopata msaada wa fedha kutoka kwa wafanyabishara lakini hofu hiyo hutuondoka CHADEMA inapopewa fedha na wafanyabiashara. Sabodo akitoa fedha CCM tumesikia makofi machache JF lakini akitoa fedha chadema makofi mengi.

Ni nini maana ya SABODO kutumikia vyama vya siasa viwili?

Kama SABODO amekosana na CCM anaogopa nini kujiondoa badala ya kuwa kama mwanamke mwenye mabwana wawili?

Je SABODO hajatumwa na CCM kuibomoa CHADEMA?
 
Mkuu , Defensive mechanism. Anasoma alama za nyakati si unajua tena mambo ya ufuaji wa fedha haramu (Money Loundering). Kapata utajiri akiwa CCM, anasaidia CDM akiwa CCM. Nadhani jibu liko wazi Sabodo ama katumwa au anajaribu kuwa kama Sarafu(Pande mbili). Lakini swali la msingi tu hapa kwa Makamanda siku wakichukua nchi Sabodo watamueza? au nao wamewaonea wivu wenzao wa CCM(Wanataka kuwa na ROSTI YA HAMU) wao?
 
Mchezo anaocheza Sabodo kwa vyovyote vile utamletea matatizo.
Contribution yoyote kwa Chama au Vyama si msaada kwa jamii, hivyo inapaswa kulipiwa kodi.
Najua msaada kwa Chama tawala watafumba macho lakini kwa CDM ni lazima jamaa wa TRA wata mwingilia.
Mfano ukitoa millioni 100 basi inabidi kwa Pilato upelele millioni 30(30% tax on prifit).
Lakini kwa vile anazo bado pengine si tatizo
 
Tangu Sabodo alipoanza kumwaga fedha CHADEMA kumekuwepo na makundi mawili yanayopingana wale wanaosema msaada huo unaonyesha kwamba Sabodo ni mzalendo na wale ambao wanasema Sabodo anajiandalia mazingira mazuri kwa kucheza karata zake vema endapo CHADEMA wanakamata dola.

Mara nyingi tumekuwa na hofu CCM inapopata msaada wa fedha kutoka kwa wafanyabishara lakini hofu hiyo hutuondoka CHADEMA inapopewa fedha na wafanyabiashara. Sabodo akitoa fedha CCM tumesikia makofi machache JF lakini akitoa fedha chadema makofi mengi.

Ni nini maana ya SABODO kutumikia vyama vya siasa viwili?

Kama SABODO amekosana na CCM anaogopa nini kujiondoa badala ya kuwa kama mwanamke mwenye mabwana wawili?

Je SABODO hajatumwa na CCM kuibomoa CHADEMA?

Mkuu mimi nabaki mdomo wazi kwa kweli kuhusu SABODO, CCM na CHADEMA. CHADEMA na CCM paka na Panya, SABODO kwa CCM na CHADEMA mambo waaaa! Hili jambo limekaaje? LAKINI mimi naomba niwe na jicho la tatu. Inawezekana kabisa SABODO akawa anachukua tahadhari kutokana na biashara zake aidha kutokuwa halali au anatengeneza mazingira ya kutokuwa na biashara halali kwa baadae. Lakini pia SABODO anaweza kutumia mwanya huo kuendesha biashara haramu hivi sasa akiwa na kinga ya kisiasa kwamba endapo uhali wa biashara yake utahojiwa na vyombo vya dola basi kisingizio kiwe eti anaonewa kwa vile anakisaidia chama fulani cha siasa. Mwisho kabisa nimalizie kwa maandishi makubwa kabisa tena kwa kuya-bold ili JF tusijifanye hatujauona msatari huo kwamba, BADALA YA SABODO KUOGOPA MAMBO YANAWEZA KUWA KINYUME KABISA YAANI SABODO AKAOGOPWA kama ambavyo RA alivyokuwa akiogopa Chama, lakini hivi leo yeye ndiye anayeogopwa. Asanteni.
 
Je SABODO hajatumwa na CCM kuibomoa CHADEMA?

aisee kama ccm imemtuma huyo mhindi aibomoe chadema kwa kuwapa shs million 200 na kuwaahidi kuwajengea ofisi mpya za makao makuu mh...basi na mi naomba huyo mhindi atumwe kwangu kunibomoa anipige na shs million 20 za fasta fasta:shock:
 
Mjadara wa kipuuzi kabisa,mbona wakati anatoa CCM mlikuwa hamsemi?acheni wivu wa kijinga alaaa!!!.
 
Tangu Sabodo alipoanza kumwaga fedha CHADEMA kumekuwepo na makundi mawili yanayopingana wale wanaosema msaada huo unaonyesha kwamba Sabodo ni mzalendo na wale ambao wanasema Sabodo anajiandalia mazingira mazuri kwa kucheza karata zake vema endapo CHADEMA wanakamata dola.

Mara nyingi tumekuwa na hofu CCM inapopata msaada wa fedha kutoka kwa wafanyabishara lakini hofu hiyo hutuondoka CHADEMA inapopewa fedha na wafanyabiashara. Sabodo akitoa fedha CCM tumesikia makofi machache JF lakini akitoa fedha chadema makofi mengi.

Ni nini maana ya SABODO kutumikia vyama vya siasa viwili?

Kama SABODO amekosana na CCM anaogopa nini kujiondoa badala ya kuwa kama mwanamke mwenye mabwana wawili?

Je SABODO hajatumwa na CCM kuibomoa CHADEMA?

M4C ni movement inayopokea mchango wa pesa safi yoyote.
sasa kama unafatilia kwa makini, wanaochangia through M4C ni wengi sana kwa iyo hilo swala la sabodo ni swala linalohusu mamilioni ya watanzania wote wanaochangia chama hichi.
 
aisee kama ccm imemtuma huyo mhindi aibomoe chadema kwa kuwapa shs million 200 na kuwaahidi kuwajengea ofisi mpya za makao makuu mh...basi na mi naomba huyo mhindi atumwe kwangu kunibomoa anipige na shs million 20 za fasta fasta:shock:

mtu kama wewe unabolewa kwa t-shirt na kanga ya mama ako au mkeo upo hapo!
 
aisee kama ccm imemtuma huyo mhindi aibomoe chadema kwa kuwapa shs million 200 na kuwaahidi kuwajengea ofisi mpya za makao makuu mh...basi na mi naomba huyo mhindi atumwe kwangu kunibomoa anipige na shs million 20 za fasta fasta:shock:
Huo ni mtandao wa RA na ED ndo unajipenyeza ili mwisho wa siku mambo yale yale tuliokuwa tunapigia debe kuwa tunayakataa. Hivi unataka kuniambia kuwa mpaka hapo kuna tofauti kati ya CCM na CHADEMA kweli? CCM ukitoa herufi ya kati jibu= CM, CDM ukitoa herufi ya kati jibu=CM. Wafadhili wakuu wa CCM, wafanyabiashara, Wafadhili wakuu wa CDM, wafanyabiashara. Wanachama wengi wa CDM, kutoka CCM. Majina yao ya utani MAGWANGA kwa MAGAMBA, mule mule tu. Mbinu za ushindi zile zile iba niibe, piga nipige, tukana nitukane, hakuna anayejifanya mjinga. Mafahari wawili wanapogomba zinazoumia ni Nyasi na tutaimia weli.
 
mbona mnawasiwasi sana na huyu mzee wkt ashajizeekea hana cku nyingi huyo mwacheni atoe.[/QUOTE
SABODO hana kosa jamani, yeye ni mfanyabiashara, CDM kinamilikiwa na wafanyabiashara so ana haki ya kuwasaidia wafanyabiashara wenzake. Inawezekana akawa na hisa huko.
 
Mjadara wa kipuuzi kabisa,mbona wakati anatoa CCM mlikuwa hamsemi?acheni wivu wa kijinga alaaa!!!.
Ulikuwa na maana ya mjadala? Hiki kiswahili jamani mbona tunacho kila siku? au Jazba Mkuu. Tatizo siyo kusaidia CCM ama CDM , tatizo nini lengo lake? asichunguzwe biashara zake sasa au hata baadaye au au ni ongezeko la wafanyabiashara wanaosafisha peza zao. Hii ni hatari sana.
 
daah huyu jamaa sjamsoma kabisa ana nia gan na cdm aangaliwe kwa makini
si ajabu ni mamluki na hzo pesa anazotoa anapga biashara gani?
 
hehe ..mimi nafurahiaga mabusu anayopigwa sabodo na dr.slaa, last time slaa alimbusu sabodo shingoni alipotoa milioni 100 na kutoa ahadi ya kujenga visima kumi arumeru mashariki..siku sabodo akitoa milioni 500 si ndo slaa atamla denda kabisa..aibu..fedha fedheha..
 
Ulikuwa na maana ya mjadala? Hiki kiswahili jamani mbona tunacho kila siku? au Jazba Mkuu. Tatizo siyo kusaidia CCM ama CDM , tatizo nini lengo lake? asichunguzwe biashara zake sasa au hata baadaye au au ni ongezeko la wafanyabiashara wanaosafisha peza zao. Hii ni hatari sana.

Sasa lengo lake unaweza kulijua wewe? hakuna anayeweza kujua lengo lake hapa, inabaki kutoa mawazo binafsi tu yasiyo na mashiko. Mi sioni tatizo kama michango yake inawasaidia wananchi. Bora yeye hata kama hajalipa kodi lakini angalau wananchi wanapata visima vya maji. Sasa tatizo lako nini? au kwa sababu NCCR,UDP hawajapewa? Muda wao bado coz hata CDM wamefanya kazi kubwa hadi unaona sasa wanachangiwa. Hapa ni law of the jungle inatumiaka bana "Survival for the greatest"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom