SoC01 Sababu za watu kuwa walevi wa Pombe, namna ya kuachana na tabia hiyo na faida za kutokunywa Pombe?

Stories of Change - 2021 Competition

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
418
630
Utangulizi:

Ulevi wa pombe limekuwa ni janga linaloitafuna sana jamii yetu kutokana na kusababisha matatizo mengine mengi zaidi ikiwemo umaskini, migogoro kwenye ndoa, ugomvi na hata mauwaji, watu kufukuzwa kazi , matatizo ya kiafya na mengineyo mengi.

Pamoja na matatizo yote hayo lakini bado walevi wanaongezeka kila uchao, Pengine ni kutokana na serikali na jamii nzima kutolitilia maanani suala hili na au ni wahusika kutojua wafanye nini ili kujinasua na janga hili.

Hivyo katika makala haya nitajadili chazo cha watu wengi kuwa walevi wa pome,mbinu unazoweza kuzitumia ili kuacha pombe na faida za kuacha tabia hiyo.

Nini Chanzo Cha watu wengi kuwa walevi wa pombe?

Watu wengi huingia katika ulevi wa pombe kutokana na sababu nyingi zikiwemo za kiuchumi, kimazingira na kijamii, kama ifuatavyo:-

Kupoteza kazi, kuporomoka au kufilisika kiuchumi:

Uchuguzi unaonyesha kuwa sehemu kubwa ya watu waliojiingiza katika ulevi wakiwamo wasomi na watu wa makundi mbalimbali huwa ni kutetereka kwa hali zao za kiuchumi kama vile kufilisika mitaji yao ya biashara au kupoteza kazi au vyeo vikubwa maofisini.

Hali hizi zote huwatokea watu katika namna ya bila wao kutarajia au kujiandaa na hivyo kukosa uwezo wa kuhimili mtikisiko huo bila kukumbwa na msongo wa mawazo.

Wengi wao huwa si wepesi wa kuipokea hali hiyo na kuacha maisha mapya yaendelee bali hukumbwa na msongo mkubwa wa mawazo kila wakati.

Hivyo ili kujaribu kuepuka mawazo mengi zaidi mtu huamua kuanza kunywa pombe kama njia ya kumfanya ayasahau masahibu yaliyomsibu.

Mfarakano wa kifamilia au kupoteza ndoa:

Migogoro na mifarakano katika familia zetu hutufikisha mahala tukajikuta tunaanzisha tabia ambazo mtu hukuwahi kuwa nazo wala kufikiri kuja kuwa nazo.

Mathalani mtu aliyepoteza ndoa katika mazingira ya kutatanisha hujikuta akikosa mwelekeo na kubaki kuwa na msongo wa mawazo kila wakati, matokeo yake huamua kujiingiza kwenye ulevi wa pombe kama njia ya mkato ya kumfanya ayasahau madhila yaliyompata.

Kupewa majukumu makubwa ya kiofisi au kitaasisi:

Watu wengi wanapopewa majukumu makubwa ya kiofisi hujikuta katika wakati mgumu wa kuandamwa na mawazo mengi ya kila wakati wakijaribu kuwaza jinsi gani wafanye ili taasisi iweze kukuwa na kustawi kukidhi matarajio waliyojiwekea.

Mathalani taasisi zinazojiendesha kibiashara matarajio yake huwa ni kukuza mtaji kwa kufanya biashara na huduma zinazoiletea taasisi faida kubwa. Katika mazingira haya mkuu wa taasisi anatakiwa kuwaza na kubuni mbinu na mikakati ya kuiwezesha taasisi yake kufikia malengo hayo.

Hali kama hii humfanya mhusika ajikute anaanza kutumia pombe kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo kichwani akijaribu kujiepusha na hatari ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari na mengineyo hasa kama taasisi husika haifanyi vizuri.

Kujiweka jirani muda mwingi na walevi wa pombe:

Kuna watu wengi wamejikuta wanajiingiza katika unywaji wa pombe kutokana na kuzungukwa na washirika wake wa kazini au katika biashara ambao ni walevi wa pombe.

Kutokana kuwa na mazingira ya ukaribu na watu wa aina hii, mtu hujikuta akishawishika au kushawishiwa kuanza tabia ya ulevi wa pombe.

Kuiga au kufuata mkumbo:

Vijana wengi a hasa wanafunzi wa shule na vyuo huona fahari sana wanapojiona wamelewa pombe, Hujiona kama vile ni watu wanaofanya mambo ya kikubwa na hivyo kujiona kama vile wao ni wakubwa sana kuliko wenzao ambao sio walevi.

Kutokana na mtazamo huu baadhi ya wanafunzi nao hujiingiza kwenye vitendo vya ulevi ili nao waweze kusifiwa na kuonekana mbele ya jamii ya wanafunzi wenzao kuwa nao ni wakubwa au ni mafahari.

Kufanya sana shughuli zinazohusiana na pombe:

Kuna wakati mtu hujikuta akianguka katika ulevi wa pombe kutokana na kujishughulisha za utengenezaji ama uuzaji wa pombe.

Mathalani, watu wanaofanya kazi katika viwanda vinavyozalisha pombe hulazimika kuonja pombe yao mara baada ya kuizalisha kabla ya kuipakia katika chupa /vifungashio ili kujiridhisha na ubora wa bidhaa yao. Hivyo kwa wafanyakazi wa mazingira kama haya ulevi wa pombe kwao huwa ni kawaida.

Kurithi tabia kutoka kwa wazazi:

Kuna baadhi ya wazazi ambao ni walevi wa pombe nao pia hurithisha tabia hizi kwa watoto wao. Hali hii hutokana na wazazi hawa kufanya vitendo hivi vya ulevi mbele za watoto wao bila kukumbuka kuwa vina athiri watoto kisaikolojia na kitabia, Hivyo watoto nao hujikuta wanakuwa wepesi wa kuanza kufanya vitendo hivyo wakijiona kamakwamba wana baraka za wazazi wao.

Mbinu za kuachana na ulevi wa pombe:.

Mbinu zifuatazo zinaweza kumsaidia mtu yeyote katika mazingira yoyote kuacha ulevi wa pombe na akabaki salama kama ifuatavyo;-

Kujiweka bize muda wote na shughuli au mazowezi:

Kujiweka bize muda wote na shughuli au mazowezi huifanya akili yako ijikite zaidi na kile unachokuwa unakifanyia kazi kwa muda huo badala ya kukumbuka vile vya nyuma.

Mbinu hii husaidia sana kupunguza msongo wa mawazo kwa watu waliokumbwa na madhila mbalimbali kama vile kupotezakazi, ndoa au kufilisika mtaji wa biashara na mengineyo.

Jambo la kufanya ni kupanga ratiba yako ya shughuli katika mtiririko utakaokufanya usipate muda wa kukaa bila shughuli. Ikitokea huna shughuli , unga ratiba ya kufanya mazoezi mepesi ya viungo kila wakati.

Ukipewa majukumu makubwa shirikisha wataalamu kupata matokeo mazuri:

Kwa wale wanaokumbwa na msongo wa mawazo kutokana na majukumu makubwa ya kitaasisi, huna haja ya kuitumia pombe kama suluhisho, bali shirikisha wataalamu walio katika fani husika, mfano wataalamu wa miradi, wataalamu wa masoko n.k.

Wape malengo na waeleze unataka kupata matokeo gani katika mradi au huduma za biashara ya taasisi yako, na unata wao washughulike na kitu gani? Kisha wawezeshe kwa vitendea kazi na mazingira bora.

Uwapo nyumbani tumia sehemu ya muda wako kuzungumza na mwenzi wako , watoto wako na kufanya mazowezi ili kuuweka mwili bize na usitowe nafasi ya kukaa na kuzubaa kuanza kufikirisha kichwa kupita kiasi.

Epuka habari au mazingira yanayoshawishi ulevi:

Iwapo katika ofisi yako au biashara zako unaona unazungukwa na watu wengi ambao ni walevi wa pombe, basi, kama ni ofisini nyanyua sheria na kama ni kwenye biashara basi tafuta washirika wengine. Ukibaki na msimamo huo siku zote hata wao watakosa hamu ya kuleta habari za ulevi mbele yako.

Jiwekee malengo binafsi na jisimamie wewe mwenyewe:

Mara nyingi watu wanaojiingiza katika ulevi wa pombe kwa kufuata mkumbo huwa ni watu wasiokuwa na malengo binafsi na hivyo wanayumbishwa kirahisi na tabia za watu wengine.

Ili kuvuka vyema katika wimbi hili ni muhimu hasa kwa vijana kujiepusha na makundi ya watu wenye tabia zisizofaa.

Fanya shughuli zako kitaalamu achana na mazoea:

Kwa wale wafanyakazi wa viwanda vya kutengeneza pombe, bado wanayo nafasi ya kuacha kunywa pombe kwa lego la kupima uora na adala yake watumie vifaa maalumu.

Hivi sasa kuna uvumbuzi wa vifaa vya kisayansi vinavyoweza kutumika kupimia ubora wa pombe ikiwemo kiwango cha kilevi na uwiano wa vile ulivyochanganya kutengeneza hiyo pombe na ukapata majibu sahihi bila kunywa hiyo pombe mdomoni.

Nini faida za kuacha kunywa pombe?

Huimarisha afya ya mwili na akili:


Utafiti unaonyesha kuwa, mlevi yeyote wa pombe yuko katika hatari ya kuugua aina 40 za magonjwa, ikiwemo saratani, magonjwa ya moyo,Figo,Ini, akili na mengineyo yasiyoambukiza. Hivyo uamuzi wa kuacha ulevi wa pome unakuweka mbali kabisa a hatari hizi.

Huimarisha uchumi na kuwezesha kufanya miradi ya maendeleo:

Watu wengi wanaojihusisha na ulevi wa pombe huelekeza fedha zao nyingi kwenye kugharamia pombe kila siku , hivyo basi hatua ya kuacha pombe husaidia kubana bajeti na kuongeza ziada ya fedha ambayo husaidia kufanya mambo mengine ya maendeleo.

Huongeza uwezo wa kufikiri kwa utulivu na kuamua mambo kwa busara:

Pombe kwa kawaida huathiri zaidi ubongo na uwezo wa binadamu kujitambua anapokuwa akifanya jambo flani.

Hivyo basi kuacha kunywa pombe huwezesha akili ya mtu kutulia na kufanya kazi sawasawa muda wote.

Hupunguza mifarakano na kuleta amani katika jamii:

Ulevi wa pombe ndio husababisha ugomvi na kuleta mifarakano katika familia, Hivyo hatua ya kuacha kunywa pombe husaidaia sana kuimarisha amani na upendo katika familia zetu.

Huimarisha nidhamu na utendaji kazi nyumbani na maofisini:

Ulevi wa pombe huchangia sana kumfanya muhanga kushindwa kufanya shughuli zake kwa utulivu na badala yake muda wote huwaza kunywa pombe na hivyo hushindwa kutimiza vema majukumu yake ya kila siku.

Matokeo yake huwa ni kupoteza kazi na kubakia akihangaika mitaani. Hivyo kuacha ulevi wa pombe ni hatua moja muhimu sana katika kulinda pia ajira ya muhusika.

Hupunguza uchakavu wa mwili na kuongeza uimara na unadhifu:

Mbali na madhara ya ndani ya kiafya, pombe pia huchakaza na kulegeza uimara wa mwili wa mhanga, kwani walevi wengi hula chakula kidogo sana bila kujali mahtaji ya mwili.

Hivyo basi hatua ya kuacha ulevi wa pombe husaidia kuimarisha mwili na kupunguza uchakavu unaomfanya mhanga kuonekana kuwa na sura na umbile lisilowiana na umri wake halisi.



Hitimisho:

Kwakua madhara ya ulevi wa pome yamekuwa yakiathiri jamii yetu nzima ya Watanzania wote wakiwemo wasiokunywa wala kutengeneza pome hiyo, hivyo ni jukumu letu sote kama taifa kujenga mazingira rafiki yatakayosaidia kupunguza ulevi na kundi la walevi katika jamii yetu.

Nyenzo muhimu katika kufanikisha hili ni kutoa elimu kwa walevi wote itakayowahamasisha kuachana na tabia hizo hasa kwa kutambua hasara za ulevi wa pombe na faida za kuachana na utamaduni huo.
 
Karibuni wadau tusaidiane kuwaelimisha watumiaji wa pombe, ili tuwaokoe na majanga yanayoweza kuepukika!
Ukisoma huu uzi usisahau pia kwenda kuupigia kura! Thanks, May God Bless You All!
 
Mkuu umeandika kitu kinachogusa jamii zetu Kwa mapana kabisa,kiafya,kifamilia,kiuchumi na kazi za kila siku.

Watu wengi wameyumba kwenye hayo niliyoyataja kisa pombe, wamepata na kupeleka magonjwa kwenye familia zao kutokana na msukumo wa pombe.

Pombe ni rahisi sana kuanza,ila kuacha ni shughuli pevu, Wengi walianza Kwa kuonja wadau wanapokunywa,wengine walianzia kwenye cocktail ya juice wanachanganyiwa pombe bila kujua especially akina dada mwisho wa siku wanajikuta walevi kupindukia.

Nakumbuka Kuna bwana mdogo alihamia mtaani kwetu alikua hajawahi kunywa toka amezaliwa,ila company ilimponza akatumbikia humo.

Solution ya kuacha pombe

no.1.Muombe Mungu sana,yaani Jishike kwenye Imani yako sawasawa na Ukitoka kwenye mihangaiko yako usipite kokote kunako company ya pombe,nenda home straight take a bath,kula chakula,hapa utaona uvivu wa kutoka.

2.Tengeneza mazoea ya kuangalia filamu,ikibidi na familia au wife,hii itakusaidia siku umechelewa atakukumbusha kuhusu filamu yenu.

Kama uko bachelor tengeneza mazoea ya kuangalia move uwe addicted upande huu.

3.Jenga mazoea ya kupata chai wakati wa jioni iwe ya viungo au maziwa.Kahawa ni nzuri Kwa kua ina caffeine itakufanya uwe addicted kiasi.

4.Tengeneza mazingira ya kufanya mazoezi kila jioni,ukiweza kufanya evining walking na wife au familia itakua safi.

5.Tafuta baba /mama/kaka/dada wa kiroho ambaye utakua unapata wasaa wa kumtembelea japo mara moja Kwa mwezi mkawa mnabadilishana mawazo.(Akiwa baba au mama wa kiroho itakua safi zaidi Kwa kua hawa wana experience na Maisha kuliko wewe.

6.Anzisha mradi nyumbani mfano ufugaji wa kuku,bata,mbwa kwa Ajili ya biashara ambao ukirudi jioni watakukeep busy.

7.Anzisha bustani ya mbogamboga,kama eneo ni dogo unaweza kupanda kwenye makopo,ndoo,mifuko ya plastic (utapata fresh vegetables ambazo ni salama)

8.Tenga muda na wanao,angalia home work zao,piga hadith nao(itakufanya uwafahamu vizuri watoto wako na huku wakijifunza siha njema)

9.Jenga mazoea ya kufanya usafi mwenyewe,unaweza kufua,kufuta home appliances, cobwebs, na mda mwingine kuosha gari yako mwenyewe (Hii itafanya akili ichangamke,na ni sehemu ya mazoezi ya mwili)Binadamu tunapenda kupongezwa ama kujipongeza wenyewe utakavyomaliza kazi zako na kujipongeza basi mwili hupata furaha na kuchangamka kwelikweli.

10.Jenga mazoea ya kulala mapema(Inaimarisha afya ya akili,unaamka mwili ukiwa fresh wenye nguvu na tayari Kwa kazi Mpya ya siku Mpya,Inaimarisha afya ya moyo na uzazi Kwa wale Wana ndoa.

11.Kwa walioa, hakikisha mnakutana kimwili walau mara mbili Kwa week,ukishindwa kabisa mara moja Kwa week,kama wote ni wazima hamuumwi(Inaimarisha afya ya akili,Moyo,Mishipa ya damu,inakufanya unakua na furaha na mcheshi wakati wote).

12.Jitahidi usiwe ni mtu wa kununua kila kitu, jitahidi usikope unnecessary yaani usiwe na madeni madogomadogo, ridhika na ulichonacho, kama hali haikuruhusu kula nyama kula mboga za majani, siku ukikaa fresh basi utakula nyama.(Hii itakupunguzia mawazo ya madeni madogomadogo na itaiacha akili yako kua fresh wakati wote,hakuna kitu kinaumiza kama madeni).

13.Epuka michepuko wengi wametumbukia kwenye pombe Kwa sababu ya michepuko(pombe inatumika kuondoa aibu na kuongeza ujasiri.

Pia ukiepuka michepuko itakupunguzia mabukizi ya magonjwa.

14.Usiwe na malengo makubwaa sana(High expectations)itakufanya ujutie usipokamilisha malengo yako na kuona solution ni kulewa.

Amini Kila jambo na wakati wake, Just remember a story of bawbaw seed. (Grow slow, ambitious, wisely, consistent, strong and You will enjoy the fruits of Your hands works.

Mungu Atubariki sote.Amen.
 
Back
Top Bottom