Sababu za kutomwamini Prof.Lipumba

1. Anawaponda wapinzani wenzake.
2. Amechuja kwa kugombea mara ya nne.
3. Alishatumika na Serikali bila mafanikio.
4. Chama chake(CUF) kina makubaliano na CCM huko Zanzibar,wakati CCM kinakumbatia ufisadi/mafisadi.
5. Haamini kuchuka kwa bei ya bidhaa za ujenzi wakati malighafi inapatikana Tanzania.
NDIVYO NINAVYOONA WEWE JE ?

UNAUSHAHIDI GANI KAMA LIPUMBA ANAWAKANDIA WAPINZANI WENZAKE? NA CUF KWA TAARIFA YAKO INATISHA ANGALIA HAPA:

View attachment 15906HAPA NI KTK UWANJA WA JANGWANI JANA 28.10.10 HAIJAWAHI KUONEKANA KTK KAMPENI ZA MWAKA HUU SI CCM WALA CHADEMA WAFANYA MKUTANO KAMA HUU!!

NA HII INAKANUSHA YALE JF WALIOKUWA WAKIDAI KUWA CUF WANAIKIMBIA UWANJA WA JANGWANI!!!

UNAWACHA KUMSEMA MREMA UNABAKI KUMPAKAZIA LIPUMBA!! YATAWASHINDA!!!! GONGA HAPA UTASHANGAA: http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=11198
 
CUF imekaa kidini zaidi, hata Prof. mwenyewe kwenye mahojiano ITV alikubali kwamba chama chake kimekita kampeni zake zaidi kwenye maeneo yenye waislam wengi (Tanga, Pwani, Dar, Lindi, Mtwara, Tunduru, Tabora). Pia anashabikia dhana potofu kwamba Waislamu wanakandamizwa hasa katika kupewa elimu hivyo kunadi ajenda ya Haki Sawa inayoendeleza chuki kati ya dini mbili kubwa hapa nchini. Anachangia mgawanyiko zaidi kuliko kuleta umoja wa kitaifa anaouhubiri.

mkuu umenena, hakika kitendo chake cha kuonyesha kuwa waislam wanaonewa hivyo ndo maana wengi wa wana cuf ni waislam (siku ile itv), ni kitendo kibaya sana na ni mdini hana maana. hatufai kabisa na atakufa tu bila kupata urais. badala ya kuwaunganisha watz anawagawanya, mtu gani huyu? yeye mwenyewe kasoma shule za mission, waislam wanaonewa namna gani wakati shule zetu za mission zilizomsomesha kikwete na yeye mwenyewe zilinyang'anywa na selikali ili kuwahudumia watu wote wakristo kwa waislam? nyerere asingefanya hivyo, waislam wangapi wangekuwa wasomi?waarabu walioleta dini yao wamejanga shule ngapi tangu iislam uanze tz? hapa ndo huwa naona akili za prof bora hata za mwalimu wa shule ya msingi.
 
Back
Top Bottom