Sababu za CHADEMA kuukataa Mswada wa Sheria ya Katiba (VIDEO)

Hii ni shule iliyotakiwa kuwa publicity enough na wanahabari ili kupanua uwelewa na wananchi juu ya sheria hii na hoja ya CDM, Manake ninaamini kuwa wabunge wengi wa ccm wameipigia makofi tu bila hata kujua maudhui ya mswaada wenyewe.
 
Haya maelezo ya CHADEMA yni ya msingi kabisa kabisa la sivyo hiyo 'KATIBA MPYA' ya CCM si ajabu ikaishia kutungwa tu na wachumba, mashemeji pamoja na maswahiba wachache wa hapa na pale endapo Watanzania tutaridhia huu muswada kuhodhisha mchakato mzima mikononi mwake mtu mmoja tu Tanzania nzima hii eti kwaa sababu tu ni rais.

Ni ukweli usiochezeka kukasimu haki zetu za kikatiba kwake kutufanyia hiyo kazi na sana sana ukaidi huo ukiendelea basi watu tutakutana kote mitaani kwa kutumia nazo haki zetu kuandamana kwa kipindi kisichojulikana vile kwenye mahakama endapo wengine watabainika madaraka ya kiserikali yatakua yamewapanda kichwa kiasi ch kutamani kudandia hata nalo hili letu wenyewe wananchi kushikilia ushukani kujitungia katiba kwa namna tupendezwavyo.
 
Back
Top Bottom