Sababu nyingine ya kutomchagua Kikwete

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Tumeshaona mara nyingi mambo ya serikali yakishughulikiwa na familia ya Kikwete. Pamoja na kusemwa sana hadharani, ndio kwanza familia hii inaendelea na mtindo huo. Mfano mmoja ni huu:
...................................................................................................................................

JK atasuluhisha migogoro ya mipaka - Mama Salma

Na Lulu George
21st September 2010

Salima%20k%286%29.jpg

Mama Salma Kikwete ambaye ni mke wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema chama hicho kikishinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, serikali yake itatatua migogoro ya mipaka.

Amesema migogoro ya mipaka ni miongoni mwa kero zinazowaathiri wananchi wengi, hivyo utatuzi wake utafanyika ndani ya miaka mitano ijayo.
Mama Salma aliyasema hayo jana mjini hapa, wakati akizungumza na wanachama wa CCM, kupitia Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT) katika wilaya ya Tanga.

Alisema, serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha inatatua kero zinazoikabili jamii likiwemo suala la migogoro ya mipaka.
Hata hivyo, Mama Salma alisema kero ya migogoro ya mipaka limeanza kushughulikiwa na serikali ya CCM kupitia ofisi ya Waziri Mkuu.

"Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba changamoto mbalimbali zinazowakabili zinatatuliwa, ikiwemo ile ya migogoro ya mipaka…suala hili lipo kwa Waziri Mkuu na tayari linashughulikiwa na punde utatuzi utapatikana,"alisema.
Pia Mama Salma alisema katika miaka mitano ijayo, serikali itaongeza mtaji kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Pia Mama Salma alisema serikali itatekeleza mpango wa ufufuaji na kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo, ili kuharakisha kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi.

CHANZO: NIPASHE
 
Tumeshaona mara nyingi mambo ya serikali yakishughulikiwa na familia ya Kikwete. Pamoja na kusemwa sana hadharani, ndio kwanza familia hii inaendelea na mtindo huo. Mfano mmoja ni huu:
...................................................................................................................................

JK atasuluhisha migogoro ya mipaka - Mama Salma

Na Lulu George
21st September 2010

Salima%20k%286%29.jpg

"Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba changamoto mbalimbali zinazowakabili zinatatuliwa, ikiwemo ile ya migogoro ya mipaka…suala hili lipo kwa Waziri Mkuu na tayari linashughulikiwa na punde utatuzi utapatikana,"alisema.
Pia Mama Salma alisema katika miaka mitano ijayo, serikali itaongeza mtaji kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Pia Mama Salma alisema serikali itatekeleza mpango wa ufufuaji na kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo, ili kuharakisha kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi.

CHANZO: NIPASHE

Huyu maza kapinda kweli....

Yaani anatamka neno "Serikali" kirahisi kama yeye ni rais au waziri. Bora hata angetumia sentensi "mume wangu".

Alisoma wapi huyu??
 
Kuna mapinduzi nini?
Mbona hii hali inatisha sasa.
Yaani haambiwi akasikia kwamba hatumtaki aendelee na huo mchezo mchafu wa kujiingiza au kusema kama yeye ni mmojawapo wa watendaji wakuu serikalini.
 
Mwalimu wa shule ya msingi, Kinyama.

Hahahaaa, umenikubusha- Saa imefika ya kwenda nyumbani- MAMA amepika wali wa nyama piipi uleule kwaheri.............kwaheriii ya kuonana keshoooo!!!
 
miaka mitano mliokuwa madarakani hamkuyaona hayoo mnayo ahidi kwa sasa...?

mlikuwa mnashinda angani kama POPO. ule muda uliopoteza kwenda kuangalia MATITI kwa king mswati ungeutumia kuwasaidia hao..!
 
Kwanza aache kutumia Chama chakee kikishinda uchaguzi, atumie familia yake ikishinda uchaguzi huu maana hizi siyo kampeni za ccm ni JK & Family Co. Unlimited.
 
Jk alisha sema urais jambo binafsi, sitashangaa kwa awamu yake ya mwisho kama atamchagua kmewe kuwa waziri wa maendeleo ya wanawake jinsia na watoto. Na inashangaza mahakama kuu kukataza mgombea binafsi, wakati huo huo wamekaa kimya wakishuhudia familia inajinadi kupigapigania kuingia ikulu.
 
Back
Top Bottom