Sababu nne za CHADEMA kushinda Igunga

Tuwahimize Viongozi wa vyama vyote kutamka bayana kukubaliana na matokeo wakiwa jukwaani.Watanzania wana mengi ya kufanyiwa baada ya uchaguzi na si siasa tu. Kumbuka Igunga kuna njaa. Wanainchi wanatakiwa kuendeleza kilimo.
 



Ni nini lakini kilitokea?


Kutokana na sababu nilizozitaja hapo juu, CHADEMA iliamua kujipanga kama jeshi la myamvuli. Ikaingia vitani ikiwa imedhamiria kuibana CCM kila kona. Iliweka mpango wa kufika Igunga mara tu baada ya kusikia habari kwamba Rostam Aziz alikuwa amejivua gamba; likatoka na ngozi na hatimaye kuvuja damu ya ubunge mpaka ikaisha.
Walipeleka timu ambayo imeishi ndani ya jimbo la Igunga siku 47 kabla ya kampeni za ubunge kuanza. Wakiwa Igunga wameweza kuweka mtandao wa chama ndani ya kata zote 26 na vijiji vyote 98.

Kinachotambulishwa kama jeshi la magaidi lililoingizwa na CHADEMA kutoka nje ya Igunga ni uwongo mtupu! Nimefuatilia jimbo zima nikagundua kwamba baada ya chama kukubalika mpaka ngazi ya vijiji, CHADEMA waliwahamasisha wanavijiji wote kujiundia kamati zao za ulinzi na usalama. Kwa hiyo katika kila kijiji na kitongoji, wananchi wa eneo hilo ndio walinzi na wana usalama wa CHADEMA. Hawaruhusu upuuzi wowote kwenye eneo lao.

Ni bahati mbaya kwamba CCM ilichukua vijana watanowatano kutoka kila kijiji ikawapeleka kwenye makambi ya kuwafundisha ugaidi ili waje wawashambulie wana CHADEMA na kung'oa mabango ya mgombea wao na bendera za chama hicho. Pia waliandaliwa kutumika kwa kushirikiana na vijana waliotoka nje ya jimbo hili kuwatisha wananchi wote wanaoiunga mkono CHADEMA na kuwalisha mkong'oto wale wote wanaokataa amri zao.

Lakini kwa kuwa CHADEMA inatumia wananchi wenyewe wa eneo husika kama walinzi, ina maana wanawafahamu vijana hao wote wanaotumiwa na CCM kigaidi. Vijana hao wanakabiliwa na nguvu ya umma ya kijiji mpaka wanashindwa kufanya lolote. Lakini pia inakuwa rahisi kuwakamata watu wote wanaojihusisha na kuihujumu CHADEMA. Mkuu wa wilaya aliyeamua kuisaidia CCM alinaswa vivyo hivyo na wananchi ambao walimripoti kwa viongozi wa chama. Mabalozi waliokuwa wanaandikisha kadi za kupiga kura walikamatwa kwa intelijensia ya nguvu ya umma kijijini.
Kwa ujumla CCM wamebanwa kila kona. CHADEMA wamekaba mpaka penalti na sasa CCM imekubali kuwa chama cha upinzani kwa kulalamika kila siku.

Kwa herini CCM!

hiyo ndo polisi jamii inayohubiliwa na IJP Mwema. kumbe si kila kitu akifanyacho mtu kinakuwa kibaya hata kama inaonesha baadhi ya mambo kaharibu.
IJP Mwema alifanya madudu Arusha akapelekea watu kuuwawa, lakini mkakati wake wa polisi jamii na ulinzi shirikishi umewasaidia CHADEMA.
 
Siku hii njema naisubiri kwa hamu. Ahsante mkuu kwa kutujuza, Nami niatingia vitani hivi karibuni
 
kaka nilikuwa busy na kutafuta mlo wa kila siku ...............................mimi siyo mwandishi wa makala hii nimetoa ufafanuzi wa hili katika post mojawapo

habari zinatabanaisha kuwa igunga ina wapiga kura 170,586 waliopiga kura uchaguzi uliopita ni chini ya asilimia hamsini,sasa wale ndugu zetu wa CUF wakitoa kile wanachoita mtaji wao wa wapiga kura 10,000 ingawa ni imani yangu idadi hii inaweza kupungua zinabaki 160,586.Hapa kuna la kujiuliza


je kwa nini idadi ndogo ilipiga kura?

je ni wangapi watapiga kura?

je kama ambao hawakupiga kura kura hawakuona umuhimu wa kupigia CCM kwa kukosa imani nao ja watapigia CUF ambao hawakuwapigia mwanzo?

Je wale waliopigia CUF au CCM kwasababu walikosa mbadala watapigia wapi?

Nimetazama vyama zaidi kuliko mgombea hapa tena kuna la kujiuliza CUF ni mgombea yule yule ila CCM na CDM ni wagombea tofauti?
Ahsante kwa majibu yako na tumekuelewa! kwani wewe uko Igunga? Na kama uko Igunga hebu basi tueleze wananchi wa Igunga wanalizu
ngumzia vipi tukio la watu wa ccm kuchoma moto vibanda vya nyumba yao kwa mikono yao wenyewe alafu wanawasingizia CDM? Sote tuna
jua hii yote ni janja ya ccm ili kutafuta huruma ya wananchi wa igunga siku ya upigaji kura, Je wewe kama uko Igunga wananchi wanalizungum
ziaje swala hili? wameaamini uongo wa ccm au wameukataa? tujuze mkuu
 
I frankly appreciate this analysis. You deserve all the credibility to be an international reporter. Very soon the long awaited for triumph, is nearly approaching. Maintain the spirit and keep the promise my fellow citizens. God bless us. Peopleeeeeeessssssssssss
 
Mguuuuuuuuuuuuu Sawaaaaaaaaa..!!!!!!! Mbeleeeee Tembeaaa....Kushot kulia...kushot kulia ...kushot kuliaaaaaa...Stop!! Mguu Pandeee.. Mguu Sawaaa...HESHIMA TOAAAAAA.......
 
[h=6]Mapambano yetu ni kulinda nchi yetu kwa kuwa na haki sawa kwa wote na uhuru wa kutoa mawazo na kushiriki katika ujenzi wa nchi. Walakini kwa sasa, hakuna haki sawa, bali tuna matabaka mawili makubwa , wenye nacho (hao mafisadi na ndio viongozi wetu) na masikini. Tufikirie kwa mapana, kizazi kijacho kitakuwa cha namna gani kama tutaendelea namna hii. Vijana msione au kuchukua haya mambo juu-juu tuu, hatari kubwa inakuja. Tutarudi kwenye utumwa wa kimawazo, kifikra na hatimaye kimwili. Tutatawaliwa na watanzania wenzetu na tutakuwa maskini zaidi ya tulivyo sasa kwani hakuna atakayejali mwanao anasoma nini shuleni, anakula nini nyumbani au anapona vipi magonjwa kwani watoto wao wote watakuwa nje ya nchi, wao watachuma na kuthamanisha maisha yao siyo YETU. TUSISUBIRI TUFIKE HUKO!
[/h]Kufanya dhambi kwa kukaa kimya wakati tunapaswa kupinga kwa njia zozote zile ni kuwa na Taifa la Watu WAOGA.
 
KHA VANCO - MYCIN! tafadhali tuambie asili ya jina lako..... naamini vanco itakuwa ni aina ya FANGASI YA KIFISADI ambayo wewer ni DRUG UNAYEHANGAIKA NAYO! - - - - TUNASUKURU SANA NA TUTAENDELEA KUSOMA TOKA KWAKO!!!
 
Hapa Jamani lazima tuwe makini si umeona Hakimu ya mahakama ya kazi alivyowaumbua, Mkuchika na Mkurugenzi wamebaki na Aibu!!! Na Bado mwaka huu lazima udhalimu wa ccm ukomeshwe Kama Libya waliweza kumwadabisha Gadafi aliyekuwa nawapatia Umeme, Maji , Hospitali na Shule bure ndio ije CCM inayotulipisha kila kitu, Lazima tumwadabishe mkoloni wetu ccm!
 
Tufikiri, then what is next?? Analysis tumefanya vya kutosha. Kuna sababu ya kuingia katika actions!
 
Nimekukubali Mkuu, hizo ndizo taarifa sahihi. Maana kila point ina justification. Keep it up, tupeeni uhondo wa yanayojiri Igunga.
 
Back
Top Bottom