Sababu 6 kwanini sitoenda kuhudhuria mazishi ya mbunge wangu Captain Komba

wewe ndio bure kabisa hivi mtu anayefahamika nchi nzima kwa uzalendo wake aje kutafuta umaarufu hapa !

yani huyu ngonyani ndo afahamike nchi nzima huwezi kuwa serious msaka tonge kwa udi wa kuchoma.na atahangaika sna paka arudi kwao akawaombe msamaha aliowatapeli yy eti usalama wa taifa atawapa ajira.
 
Tatizo hujui kwa nini watu huenda kuzika.Kuhudhuria Mazishi kwa mtu uliyemchukia sana ni muhimu.Uende ukashuhudie anavyozikwa utupie na udongo urudi umefurahi kuwa uliyemchukia kafa kweli na wewe umeshuhudia na kurusha udongo kwa hasira kwenye kaburi lake.

Halafu kafa kwani anakuona kuwa hujaenda kuzika? Wewe utakuwa na ugonjwa wa akili.Naomba yeyote mwenye namba za hospitali ya vichaa mirembe ampe huyu ngonyani amtumie kwenye simu yake ambayo kaiweka wazi.

Pumba nyingine bwana, yeye katoa sababu sita, wewe umetoa ngapi za kupinga?
 
Matthew 7:1-3

Judging Others

7 “Judge not, that you be not judged. [SUP]2 [/SUP]For with the judgment you pronounce you will be judged, and with the measure you use it will be measured to you. [SUP]3 [/SUP]Why do you see the speck that is in your brother's eye, but do not notice the log that is in your own eye?
 
Kanisa linatambua ndoa moja takatifu pekee ..na salome mke mkubwaameishi nae kwa zaidi ya miaka 30 sasa maana nakumbuka jubilei ya ndoa yao...kwahiyo ulitaka kanisa lisifanye ibada ya mazishi yake wasusie sio??
Kwa hiyo huyo mke wa pili hakuwa mke wa Komba na hao watoto waliotajwa,hakuna watoto wa mke wa pili je kama walibatizwa unadhani kanisa halikujua kuwa ni wa mke wa pili?.
Kama huko karibu na familia hii bila shaka unajua kuwa Komba alikuwa na wake wawili na kanisa kwa kutumia jumuia zake ndogondogo wanajua fika kuwa huyu bwana hakuwa tena kwenye ndoa ya mke mmoja.
Kama unavyoona huyo mke wa pili hakuwa nyumba ndogo bali mkewe wa pili rasmi ndio maana alikuwepo bega kwa bega na mke mwenzie Salome.
Kwa taarifa yako hizo jumuia ndio jicho la kanisa,na wako mitaa yote kwa hiyo walijua fika uwepo wa mke wa pili kwenye msiba,hata kabla ya msiba na walipashwa kulitaarifu kanisa kwa kichachoendelea huo ni utaratibu unaofanyika kwa wakristo wote na pindi inapodhihirika kuna kasoro za namna hiyo kanisa halishiriki mazishi.
 
1. Ni mtu ambaye ameifikisha nchi hapa ilipo kwa kusaidia kurubuni maskini wasio na elimu kwa vinyimbo vyake ili waichague CCM na kuwapiga vijembe wapinzani.

1. Ni mtu aliyehamia Dar badala ya kuishi Liuli au hata Nyasa, huku akijua kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi. Tena huko Dar hadi mtaa anaoishi ukapewa jina lake kwa umaarufu wake.

3. Ni mtu aliyetaka kulitumbukiza taifa ktk machafuko kwa kauli yake ya kuwa iwapo rasimu ya katiba ya jaji warioba ingepita "angeingia msituni kupigana".

4. Ni mtu ambaye hakupenda demokrasia hata kidogo na alitusi mara kadhaa vyama visivyo madarakani na kutoa lugha ya kejeli.

5. Ni mtu aliyemtukana sana jaji Warioba kuliko watu wote nchi hii. Alitoa matusi, kejeli na dharau dhidi ya jaji Warioba huku akiwa anajua/hajui kuwa mzee Warioba alikuwa "mjumbe" tu wa kile walichosema watanzania.

6. Mwanae Komba, Fred alijiunga na chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) punde tu alipomaliza kuchukua shahada yake pale SAUT na akamwelezea tabia ya baba yake kuwa ni "MBAYA" na miongoni mwa watu walioichukia demokrasia ni huyu marehemu

kwa lipi nipange safari kwenda nyumbani kumzika huyu jamaa? Sina wivu wala inda kwa ndugu yangu, mbunge wangu wa kule nyumbani wala chuki nae. "Ila ukweli hastahili kupata pole ya kifo wala faraja ya kifo kutoka kwa wazalendo na wapinga ukoloni weusi"

Shukrani a. Ngonyani

Machi 03, 2015

Dar Es Salaam

Ngonyani@naij.com/sirngonyani@gmail.com

+255 784 37 97 99

Kwa jinsi ulivyoongea,basi ningekushauri weka NIA gombea UBUNGE urudi nyumbani wamanda tunakuhitaji sana.............
 
Kwa hiyo huyo mke wa pili hakuwa mke wa Komba na hao watoto waliotajwa,hakuna watoto wa mke wa pili je kama walibatizwa unadhani kanisa halikujua kuwa ni wa mke wa pili?.
Kama huko karibu na familia hii bila shaka unajua kuwa Komba alikuwa na wake wawili na kanisa kwa kutumia jumuia zake ndogondogo wanajua fika kuwa huyu bwana hakuwa tena kwenye ndoa ya mke mmoja.
Kama unavyoona huyo mke wa pili hakuwa nyumba ndogo bali mkewe wa pili rasmi ndio maana alikuwepo bega kwa bega na mke mwenzie Salome.
Kwa taarifa yako hizo jumuia ndio jicho la kanisa,na wako mitaa yote kwa hiyo walijua fika uwepo wa mke wa pili kwenye msiba,hata kabla ya msiba na walipashwa kulitaarifu kanisa kwa kichachoendelea huo ni utaratibu unaofanyika kwa wakristo wote na pindi inapodhihirika kuna kasoro za namna hiyo kanisa halishiriki mazishi.

We unawazimu unachojaribu kufanya unajiridhisha tu tangu lini kanisa katoliki likatambua mitala?
 
1. Ni mtu ambaye ameifikisha nchi hapa ilipo kwa kusaidia kurubuni maskini wasio na elimu kwa vinyimbo vyake ili waichague CCM na kuwapiga vijembe wapinzani.

1. Ni mtu aliyehamia Dar badala ya kuishi Liuli au hata Nyasa, huku akijua kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi. Tena huko Dar hadi mtaa anaoishi ukapewa jina lake kwa umaarufu wake.

3. Ni mtu aliyetaka kulitumbukiza taifa ktk machafuko kwa kauli yake ya kuwa iwapo rasimu ya katiba ya jaji warioba ingepita "angeingia msituni kupigana".

4. Ni mtu ambaye hakupenda demokrasia hata kidogo na alitusi mara kadhaa vyama visivyo madarakani na kutoa lugha ya kejeli.

5. Ni mtu aliyemtukana sana jaji Warioba kuliko watu wote nchi hii. Alitoa matusi, kejeli na dharau dhidi ya jaji Warioba huku akiwa anajua/hajui kuwa mzee Warioba alikuwa "mjumbe" tu wa kile walichosema watanzania.

6. Mwanae Komba, Fred alijiunga na chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) punde tu alipomaliza kuchukua shahada yake pale SAUT na akamwelezea tabia ya baba yake kuwa ni "MBAYA" na miongoni mwa watu walioichukia demokrasia ni huyu marehemu

kwa lipi nipange safari kwenda nyumbani kumzika huyu jamaa? Sina wivu wala inda kwa ndugu yangu, mbunge wangu wa kule nyumbani wala chuki nae. "Ila ukweli hastahili kupata pole ya kifo wala faraja ya kifo kutoka kwa wazalendo na wapinga ukoloni weusi"

Shukrani a. Ngonyani

Machi 03, 2015

Dar Es Salaam

Ngonyani@naij.com/sirngonyani@gmail.com

+255 784 37 97 99

Usipohudhuria hatazikwa?
 
Marehemu Komba alikuwa mhuni tu! Halafu ile kaunda yake aliyokuwa akibambia nayo watoto wa watu kwenye sherehe ndo walimvalisha. Hapo walipatia ila kosa ni ule msalaba waliovalisha juu ya ile kaunda!
 
Ki ustaarabu tukubali Cpt John Komba is NO MORE haya mengine ni kati yake na MOLA wake.. sisi tusimuhukumu.
 
Shukrani A. Ngonyani

Attention Seeker... Cheap Popularity.. Low Thoughts...
Usitafute umaarufu wa kijinga wewe... Pamoja na yote binadamu atabaki kuwa binadamu tu... Huna haja ya kumuhukumu Komba... Wewe ukiwa kama nani katika mamlaka ya roho... Wewe umetenda mangapi ya kuwaudhi na kuwaharibia maisha toka uzaliwe mpaka hapo ulipo??? Unadhani una utakatifu wa kumuita Komba alikuwa mchafu...

Kama wewe ni Chadema (am inn as well) unadhani mtoto wa marehemu ambae ni Chadema mwenzio akisoma hapa atajisikiaje?? Kuna wakati mwingine tusitafute umaarufu wa kwenye mitandao huku nafsi zikitusuta...

Think before you act!!!!

Ngonyani wewe ni mjinga wa kutupwa,Komba kuish Dar na kupeleka huduma kwa wananchi wake haramu,wewe kuishi Dar na kuwatelekeza wazazi wako hapa kijijini halali?. Rudi huku mazazi wako ombaomba sasa hivi, kwanza tulikukuwa hutujui uko wapi asante kwa kufahamisha kuna siku tutawaleta wazazi wako Dar.

Kama mtu hadi aliweza kutamka kuwa kifo ni Mkosi kwa hivyo mnavyomtetea sidhani kama mko sawa siku zote mkae mkijua MUNGU ni fundi na ufundisha kwa wale wenye dharau kama huyu Komba

Last edited by a moderator:
Ebu naomba na wewe ututajie sababu ambayo kila mtu wa itikadi tofauti ataikubali, ni kwa nini na wewe ukifa watu tuje tukuzike?

Acha fikra mgando na kujionesha hadharani ulimbukeni wako. Hata mimi pia kiitikadi nipo tofauti kabisa na marehemu, lakini sio hivyo

Unataka kwenda kumzika unamjua?? ............................... hiyo ndiyo tofauti yake na Komba. Komba alikuwa ni kiongozi na alibeba dhamana na alijitolea kulitumikia taifa. Haya ni matokeo ya jinsi gani hakufanikiwa ................... hunda ndiyo sababu ya yeye kuanza kuwaza kwenda mstuni. Ila huyu mwingine unayemsema yeye kaamua kuwa anonymous kwa hiyo hana madhara kwa taifa!!
 
Haya hatozikwa kwa ufanisi kwakuwa wewe hujafika, acheni upuzi,acheni sifa CDM,CCM,CUF, Nivyama tu
 
We unawazimu unachojaribu kufanya unajiridhisha tu tangu lini kanisa katoliki likatambua mitala?
Pamoja na hayo ni kweli kanisa halitambui mitala na kwa sababu hiyo ukishaingia mitala unakuwa umejitenga na kanisa.
Sheria taratibu na kanuni za kanisa zinafuatwa kama zilivyo hazihojiwi ni aidha uzifuate uendelee kuwa muumini au uzikatae ujitenge na kanisa,bila kujali cheo au wadhifa wa muumini.
Kwa maana hiyo hakuna swala lakujiridhisha hapa.
Hivi kwenye hili kuna haja yakutukanana na kutoleana mapovu kwa udhaifu wa Komba,kinachotakiwa hapa ni hoja si viroja.
 
Back
Top Bottom