Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo, na vingine vya kutafutia masoko

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko.



Leo nitatoa sababu chahche kwanini biashara yako inahitaji hivyo vyote ili ifanikiwe kibiashara. Ukiviangalia vyote kwa juu juu unaweza kuviona sio vya muhimu sana Mfano: Kampuni kuwa na logo wakati hakuna mtu anaekuja kuulizia logo wala hakuna mtu anaekuja kununua logo hivyo ni kitu ambacho unatengeneza kwa gharama na kinaendelea kuwa chako.
Nimepokea maswali mengi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vitu kama Nembo, Flaya,Tovuti,Broshua na vingine vingi


Vivyo hivyo kwa vingine unatengeneza broshua kwa gharama kubwa lakini unasambaza bure kwa watu na unaweza kumpa mtu hapo hapo akakitupa ,ukiangalia kwa macho ya fedha zangu nimeziweka hapa kipewe heshima hauwezi kuona ninachokimaanisha.


Kila biashara inahitaji kuonekana na pia inahitaji kukua bila kukua na kuonekana haiwezi kufanikiwa hivyo kutengeneza Nembo yako ni kujipa muonekano katika soko na kutengeneza vitu kama Flaya,Broshua,Poster hiyo ni kukuza biashara hivyo ili biashara yako ikue ni lazima ufanye vyote malipo au faida za kufanya hivyo hazionekani kwa muda huo huo lakini zinaweza kuonekana muda wowote kuanzia ulipo anza kuzitoa, marejesho yake sio ya papo kwa hapo lakini yana faida ya muda mrefu Mfano: unapotengeneza logo itatumika kwenye kila sehemu inayokutambulisha kwa muda wote wa biashara yako na ukitengeneza flaya itasomwa na wengi kwa muda mfupi au mrefu ambapo tayari utakuwa umewafikia watu wengi bila wewe mwenyewe kwenda kuonana nao mmoja mmoja, hapa chini zifuatazo ni sababu kwanini biashara yako inahitaji vitu hivyo.


1.Kuonekana mkubwa na uliojengeka

Unapotengeneza vitu hivyo vinapokutambulisha sokoni hukuonyesha wewe ni mkubwa na umejengeka ndio maana hata umeweza kutengeneza vitu hivyo, biashara isiyokuwa na nembo ikienda sehemu moja na biashara yenye nembo biashara itakayopata kipaumbele ni yenye nembo ambayo imeonyesha uthubutu hata kwa kujijenga yenyewe.


2.Kuongeza nafasi ya biashara yako kwenye soko.

Ukitengeneza na vitu vyako vikaonekana sokoni tayari umeipandisha nafasi yako na hadhi katika soko, ambapo kwa kuwa na vitu hivyo ni rahisi kwa soko kukutambua na kukupa nafasi. Mfano umetengeneza flaya za huduma yako na kisha ukzisambaza zikasomwa na watu wengi hao watu ndio watakao kupa nafasi kwenye soko kwa kukutafuta watakapo kua na shida na hata kama hatakutafuta atakuwa amekuoneza kwenye listi ya biashara anazozijua zinafanya shughuli hiyo.


3.Kuvutia wateja wengi

Sababu kubwa ya kutengeneza vitu hivyo ni wateja na unapotengeneza flaya au broshua ni lazima utaweka dizaini nzuri na maneno ya kuvutia hivyo ni njia rahisi ya kumvutia mteja kwa kile anachohitaji kutoka katika biashara yako.


4.Kujitengenezea Chapa( Brand) yako.

Brand ni kitu kikubwa sana lakini pia unapojitangaza na kujipa muonekano ni sehemu ya kujibrand na unapotoka nje ya ofisi yako ukiwa na vitu vya kuwapa watu nje ya walioko ofisini hapo ni unaitoa chapa yako ndani ya ofisi na unaenda kuwapa watu wengine nje hivyo unaitengenezea brand yako muonekano.


5.Kuonyesha unaijali biashara yako

Mara zote mteja huhitaji kufanya kazi kwa mtu anaejielewa na anaejijali hivyo kufanya hivyo ni kumpa uhakika mteja na biashara yako kuonyesha unaijali na unaweza kufanya kitu kwa ajili ya biashara yako mwenyewe hivyo ni rahisi kwa mteja kupata ile hamasa ya kuamini unaijali biashara yako hivyo hautaweza kumharibia kazi yake.


6.Kuwapa wateja hali ya uaminifu

Katika soko kumekuwa na makanjanja wengi hivyo kwa kuingia gharama na kufanya hivyo unampa mteja hali ya kukuamini na kuona uthubutu sababu kwenye flaya au broshua kunakuwepo na mawasiliano ya wazi na pia kunakuwa na anwani ya sehemu ofisi inapatikana ambapo nirahisi kwake kuja kujiaminisha kama kweli hata kabla hajakupa kazi.


7.Kukumbukwa

Unapojitangaza na kuijenga brand yako ni kuingiza brand yako ndani ya vichwa vya watakaoona na pia kusoma hivyo brand yako itakuwa inakumbukwa kwa vile tayari iko kwenye vichwa vya wengi.


muendelezo fuatilia katika blogu Elisha Chuma


Bado mnakaribishwa kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko lazima.

 
Karibu mkuu kwa machapisho mengine ya nyuma unaweza kupitia blogu utapata mengi ya kushibisha nyama ya uelewa karibu@Unwanted
 
Asante sana, somo zuri, logo/ni sura ya biashara, kuwa na jina bila logo ni sawa na mtu kuitwa Masawe lakini hana sura au haonekani. NAME WITHOUT A FACE.
 
Mchango was ziada:
Pindi ukishaipata nembo yk hakikisha unaidhibiti kisheria kwa kuisajili Brela. Hii itakulinda kisheria dhidi ya mafisadi watakaoweza kuitumia nembo yk kukidhi matakwa yao binafsi
 
Wish ningesoma hii mapema kuna sehem nimeshalipia Label designing ya product yangu fulani! Ntakuja whatsapp for more details
 
Jipatie elimu zaidi inayohusu masuala mbalimbali ya ujasiliamali uikuze zaidi biashara/mradi wako. Aidha utanufaika na ushauri wa kitaalam kutoka kwa mtaalamu aliyebobea ktk masuala ya biashara, ujasiliamali na branding. Kufanya kazi kwa mazoea hakutoshi. Jenga utamaduni wa kujisomea ili kujikuza kimaendeleo zaidi.

Tafadhali tembelea blog ifuatayo unufaike:

Elisha Chuma
 
Back
Top Bottom