Kibukuasili
JF-Expert Member
- May 15, 2010
- 1,050
- 605
Kuna matatizo sehemu nyingi hapa.
Hata wazazi tuna matatizo pia.
Hata wazazi tuna matatizo pia.
- Inakuaje mzazi unakaa 12 km kutoka shuleni kwa mtoto tena umepanga? kwa nini usipange karibu na shule ya watoto wako unaamua kupanga karibu na kazini kwako?
- Kwa nini mzazi usimtafutie mtoto shule karibu na nyumbani. Kama kwa radius ya 5km na hapo unapokaa hakuna shule nzuri, basi umekosea mahali pa kupanga/kujenga.
- Si lazima masomo yaanze saa 1 asubuhi kila shule. Ni kukariri tu. Shule zinaweza kuwa na masaa tofauti ya kuanza masomo.
- Shule zibanwe ziwe na mabasi mengi ili route zisiwe za kuzunguka sana. Hii itasaidia kupunguza muda wa watoto kuwa njiani. Wenye shule wasipobanwa kwenye eneo hili hawawezi kujali maana ni mahali wanapobana matumizi.
- kama kwenye eneo moja kuna watoto wa shule moja wengi wazazi wanaweza ku opt kutolipia basi la shule wakatafuta usafiri wao wenyewe. Kuna mahali wazazi wamekodi noah inachukua watoto asubuhi na kuwarudisha jioni, badala ya basi la shule. Wanatumia pesa nyingi zaidi lakini kwa manufaa ya watoto wao