Rwanda: Wakili wa Paul Rusesabagina afukuzwa nchini

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,265
4,716
Wakili wa Paul Rusesabagina, anayeelezwa kuwa shujaa katika filamu ya mwaka 2004 ya Hollywood ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda" na ambaye anatuhumiwa kwa "ugaidi", amefukuzwa na mamlaka ya Rwanda Jumamosi jioni kwa "kukiuka sheria ya uhamiaji", kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Uhamiaji.

1629620268184.png

Mamlaka ya Rwanda inamshutumu Vincent Lurquin, raia wa Ubelgiji, ambaye aliwasili nchini Rwanda Jumatatu kwa visa ya kitalii, kwa kuhudhuria kesi katika mahakama ya Kigali Ijumaa akiwa amevaa mavazi yake ya wakili, wakati "visa yake ilimruhusu kutembelea nchi hii (...) lakini sio kufanya kazi, ”Regis Gatarayiha, Mkuu wa idara ya Uhamiaji nchini Rwanda, ameliambia shirika la habari la AFP.
Uamuzi wa kesi ya Paul Rusesabagina utatolewa Septemba 20, kulingana na taarifa kutoka mahakama ya Kigali.

Mwaka mmoja uliopita, alikamatwa, na kutekwa nyara kulingana na familia yake, na kurudishwa Kigali ambako tangu wakati huo anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi. Hukumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ambayo ilipangwa kutolewa Alhamisi, Agosti 19, iliahirishwa hadi Septemba 20.

Hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa kwa mwezi mmoja kwa sababu ya ukubwa wa kesi hiyo, mahakama ya Rwanda ilisema. Uamuzi wa mahakama utacheleweshwa kwa mwezi mmoja kabla ya kujuwa hatima ya Paul Rusesabagina, ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha, na washtakiwa wenzake 20. Wote wanashukiwa kuwa katika kundi la FLN, kundi lenye silaha ambalo lilidai kuhusika katika mashambulio kusini mwa Rwanda mnamo 2018. Kundi hilo linachukuliwa kama tawi la kijeshi la MRCD, vuguvugu la upinzani la Paul Rusesabagina.

Tangu kuanza kwa kesi hii ya muda mrefu, familia ya Paul Rusesabagina inalaani kuingiliwa kwa mahakama na serikali na kutaka aachiliwe. Ubelgiji na Bunge la Ulaya pia wameelezea wasiwasi wao juu ya mazingira ya kukamatwa kwake na jinsi kesi hiyo inavyoshughulikiwa.

RFI
 
Aache dharau ajifunze kufuata sheria. Mtu hana working permit, hana leseni ya uwakili Rwanda na baada ya siku mbili tu kuingia nchini kwa visa ya visiting anataka kukaa mahakamani na kupractice kama lawyer suspect!!! Hell NO.
 
AAli
Aache dharau ajifunze kufuata sheria. Mtu hana working permit, hana leseni ya uwakili Rwanda na baada ya siku mbili tu kuingia nchini kwa visa ya visiting anataka kukaa mahakamani na kupractice kama lawyer suspect!!! Hell NO.
Alinyimwa viza sahihi
 
Ashukuru Mungu kwa hatua hizo vinginevyo yangekuwa kama yale ya Area D hapo dodoma

Huyu hata ndani hajawekwa afurahi kwa hilo,wakili mmoja mmarekani aliwekwa ndani siku 21 huko Kigali mpaka wakina Hillary Clinton wakapiga kelele sana ndio akaachiwa,mpaka leo hataki kupasikia huko.
 
PK yuko serious na mambo yake, hauwezi ukawa na tourist visa, halafu ufanye kazi za uwakili. ni kupiga punch kama za Kiduku tu!
Wakili alinyimwa proper Visa kwakuwa PAKA hataki victim atetewe
 
Ndiyo, mbona Lisu ana practice; mbona Fatuma Karume anatetea kule Scotland ❕❕❕❔❔
Hakuna kitu Kama hicho,Lissu ha practise mahakamani Ila anaweza akafanya consultation tu.

Rais wa Brussels Bar Association(Chama Cha wanasheria huko Belgium), Maurice Krings amesema mwenyewe only raia ubelgigi na Raia wa EU ndio wanaweza kupractise.Hakuna raia wa nchi nyingine nje ya hapo anaweza ku-practice as a full lawyer in Brussels.

The only exception is a "list B" of foreign lawyers, who can serve as "associate members" in their Brussels' law offices but can never represent clients before any judicial or administrative court of law in Brussels.

Unless uniambie Lissu siku hizi Ni raia wa Belgium au EU.
 
Back
Top Bottom