Ruzuku ndiyo, lakini kwa mfumo upi?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Edmwanga.jpg

Maoni ya Katuni


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inakusudia kutafuta utaratibu wa kusaidia vyama vya siasa wakati wa kazi ya kupiga kura kwa kuwapa posho mawakala kwa nia ya kukuza demokrasia nchini, hatua hii pamoja na ile ya kutaka kuajiri watumishi wake wa kudumu ni miongoni mwa mambo ambayo inataka kuchukua kujiimarisha katika utendaji wake.

Kulingana na habari ambazo gazeti hili liliandika katika toleo lake la jana ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari ‘NEC yatafutia vyama ruzuku’, hatua hizo zinalenga kuvipa vyama vya siasa uwezo wa kushiriki chaguzi nchini, kwa kuwa imekuwa ni kawaida vyama kushindwa kutumia haki ya kushiriki uchaguzi kwa sababu ya uwezo wa kifedha.

Kwa maana hiyo, NEC inataka walau kusaidia posho kwa mawakala wa vyama ambavyo vitakuwa vimesimamisha wagombea katika chaguzi zinazoendeshwa nchini nia ikiwa ni kukuza demokrasia, lakini pia kuvipunguzia vyama mzigo huo ambao kwa hakika umekuwa ni mkubwa na mzito.

Tunasisitiza kwa nia ya kweli kwamba tunaelewa kuguswa kwa NEC na hali ya vyama vya siasa ilivyo, na kwa kweli tunaelewa kwamba ina kazi ya kuhakikisha kwamba chaguzi zinazofanyika nchini zinakuwa za kidemokrsia kweli kwa maana ya kuweka mazingira yaliyosawa kwa vyama vyote. Ni nia njema na tunaiunga mkono.

Wakati tukiunga mkono nia hiyo, hata hivyo, tungependa NEC pia isisahau historia ya vyama vya siasa nchini hasa baada ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi kuanzia mwaka 1992. Itakumbukwa kuwa kati ya mwaka 1992 na 1995 zilifanyika chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo yafuatayo, Kwahani, Zanzibar; Ileje, Mbeya; Tabora Kaskazini na Igunga, Tabora na Kigoma Mjini, Kigoma.

Katika chaguzi zote hizo vyama vyote vilivyosimamisha wagombea si tu ilitoa posho kwa ajili ya mawakala, ila ilitoa ruzuku kwa ajili ya kila mgombea kwa maana ya kuwajengea uwezo wa kufanya kampeni kwenye majimbo, kununua vifaa vya kampeni na kujikimu kwa mahitaji ya kibinadamu.
Hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 vyama vyote vilivyosimamisha wagombea wa ubunge na urais walipewa ruzuku na NEC. Hizi zilikuwa ni

fedha za kampeni. Mwaka huo vyama vinne vilisimamisha wagombea urais na vingi zaidi vilishiriki kwenye nafasi ya ubunge na udiwani.
Ni baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 ndipo serikali ilitunga sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa, ikielekeza kuwa kigezo ni kulingana na idadi ya wabunge, lakini pia kura za urais ambazo chama kilipata, kigezo kiliwekwa kuwa walau chama kipate asilimia tano ya kura za urais ndipo haki hiyo inapatikane.

Itakumbukwa kuwa sheria hii ilitungwa si kwa sababu ya kukomoa vyama, ila ni kutokana na historia halisi na ushahidi wa wazi kabisa kwamba baadhi ya wanasiasa walikuwa wanatumia fedha za ruzuku si kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Wapo wanasiasa hususan viongozi wakuu wa vyama vya siasa waliogeuza ruzuku kuwa ni mradi wa kuendesha maisha yao.

Fedha nyingi zilizotolewa kwa baadhi ya vyama kwa hakika hazikufika kwa walengwa, yaani wagombea, na zilikuwa ni mwanzo wa migogoro kwa baadhi ya vyama, kiasi cha kuvifanya vishindwe kufanya kazi ya kisiasa na kuishia ama kufukuzana au kufunguliana kesi mahakamani. Ruzuku ilileta balaa baadala ya neema kwa baadhi ya vyama vya siasa. Kwa hiyo sheria hiyo ililenga kupembua vyama jina na vyama makini katika kukuza demokrasia nchini.

Kwa hiyo, kama NEC sasa imeamua kurejea tena kwa mtindo wa zamani wa kutoa fedha kwa vyama vya siasa kwa sababu yoyote ile, ni vema ikajikumbusha juu ya historia ya utoaji wa ruzuku kabla ya kutungwa kwa sheria ya ruzuku baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995.

Tunasema haya kwa kuwa ruzuku ni kodi za wananchi, ni jasho la wananchi, si vizuri sana kuchukua fedha za umma na kuzigawa kama hakuna njia ya kuhakikisha zinaleta matunda tarajiwa; hatukatai NEC kuviwezesha vyama, lakini pia hatuungi mkono utaratibu wa watu kugeuza vyama vya siasa kuwa NGOs za kuendesha maisha yao; ruzuku ni lazima itolewe kwa kuangalia jinsi chama kinavyokubalika kwa wananchi na hii ni kwa kushiriki uchaguzi na kushinda nafasi mbalimbali kuanzia serikali za mitaa na vitongoji, halmashauri, ubunge na urais. Tuwe makini kabla ya kuamua.

CHANZO: NIPASHE

 
Edmwanga.jpg

Maoni ya Katuni

sasa hiyo sheria mbona imetulia vizuri tu. Hapa kuna namna na hawa NEC nao wanataka kuchakachua kwa kisisngizio chha kukuza demokrasia. Watanzania tushtuke haya nia matumizi mabaya ya fedha. Itakuwa wana vyama vyao vya kichinichini walivyovitega ili viwe vitega uchumi vyao. Sasa kila mtu ataanzisha chama ili apate RUZUKU. Tukiwa na vyama elfu moja visivyo na mwakilishi hata mmoja na vyote visimamishe wagombea urais Tanzania tuna uchumi wa ku accomodate mzigo huu? Mbona hatufikirii zaidi ya urefu wa pua zetu. Hii kitu HAPANA KUNA MCHONGO WA VIGOGO KAMA NJIA RAHISI YA KUVUNA JASHO LETU kwa mgongo wa demokrasia. Kama chama kiko serious wachangishane wenyewe mpaka watakapopa wawakilishi ndo wapewe ruzuku vinginevyo NOOOOOOOOOOOOO!
 
Back
Top Bottom