Ruzuku kwa mwezi: CCM milioni 800/-, Chadema 200/-, CUF 117/-

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo:-

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi........

Chadema...................Tshs 200 Million kwa mwezi.......

Cuf...........................Tshs 110 kwa mwezi...............

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma.....

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ametangaza viwango vya mgawo wa ruzuku kwa vyama vilivyotimiza sifa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, huku kiwango cha mgawo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilichokuwa ikipata kila mwezi, kikiwa kimeshuka.

Licha ya CCM kuvipita vyama vingine katika viwango vya mgawo uliotangazwa jana na Tendwa, kiwango cha mgawo wake wa ruzuku, kimeshuka kutoka Shilingi bilioni moja ilizokuwa ikipata kila mwezi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kufikia Sh. milioni 800 inazopata hivi sasa.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, ruzuku hiyo hutolewa kwa chama kilichofikisha kuanzia asilimia tano ya kura za urais na kwa uwiano wa wabunge na madiwani, ambao chama ‘kilivuna' katika uchaguzi huo.

Mbali na CCM, vyama vingine, ambavyo vinapata ruzuku, baadhi vikilingana na vingine vikitofautiana sifa ya kupata ruzuku hiyo, ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP. Viwango vya mgawo wa ruzuku hiyo, vilitangazwa na Tendwa alipozungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ruzuku hiyo ilianza kutolewa na ofisi yake kwa vyama hivyo, kuanzia Novemba, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu na ule uliofanyika baadaye katika baadhi ya majimbo kukamilisha uchaguzi huo.

"CCM imeshuka kwa ruzuku. Huko nyuma ilikuwa inapata Shilingi bilioni moja, lakini sasa inapata Sh. milioni 818," alisema Tendwa.

Hata hivyo, alisema ruzuku kwa uwiano wa madiwani, haijaanza kutolewa kwa vile bado hawajapata takwimu za madiwani, ambao kila chama kilipata, katika uchaguzi huo. "Tunasubiri tuweze kuwa na data za madiwani. Hatuwezi kutoa ruzuku za madiwani bila kupata data. Kwa mfano CCM kuna madiwani wamejiuzulu. Kila mgawo (wa ubunge na madiwani) una fungu lake," alisema Tendwa.

Alisema CCM inapata kiwango hicho, kutokana na kupata asilimia 60.40 ya kura za urais katika uchaguzi huo, ambazo ni sawa na Sh. milioni 354 na asilimia 77 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 460) kwa mwezi.

Pia alisema licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kupata kura katika majimbo mengi ya uchaguzi, kimepata kiwango kidogo cha mgawo wa ruzuku kulinganisha na Chadema. Alisema hali hiyo inatokana na baadhi ya majimbo kiliyovuna wabunge, kama vile ya kisiwani Pemba kuwa na wapigakura wachache waliokiunga mkono katika uchaguzi huo.

"CUF ilipeleka nguvu kubwa Pemba, lakini huwezi kulinganisha na idadi ya wapigakura kama wa Dar es Salaam," alisema Tendwa.

Kutokana na hali hiyo, alisema CUF sasa inapata Sh. milioni 117.4, kutokana na kupata asilimia 9.80 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 57.9) na asilimia 10 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 56). Alisema katika mgawo huo, Chadema inapata Sh. milioni 203.6, kutokana na kupata asilimia 24 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 146) na asilimia 9.62 ya wabunge (sawa na Sh. milioni milioni 56).

Tendwa alisema vyama vya NCCR-Mageuzi, UDP na TLP havipati ruzuku ya urais kwa vile vilipata chini ya asilimia tano ya kura za urais.

Hata hivyo, alisema NCCR-Mageuzi inapata ruzuku ya Sh. milioni 10, kutokana na kupata asilimia 1.08 ya wabunge wakati UDP na TLP alisema vinapata ruzuku ya Sh. milioni 2.4 kutokana na kupata asilimia 0.42 ya kura za ubunge kila kimoja.

Alisema iwapo viwango vya mgawo wa ruzuku ya madiwani itaongezeka kwa chama husika, viwango hivyo navyo pia vitaongezeka.

Kuhusu fomu za gharama za uchaguzi, ambazo wagombea wanatakiwa kujaza, alisema tarehe ya mwisho, ambayo zinatakiwa ziwe zimerejeshwa ofisini kwake, ni Januari 30, mwakani na kwamba, yeyote atakayekiuka ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

"Wanatakiwa waeleze katika hizo fomu walitumia nini, kiasi gani na kutoka wapi. Wathibitishe kwa risiti," alisema Tendwa.

Akijibu swali kama kuna mgombea yeyote, ambaye hakujaza fomu, alisema hakuna, isipokuwa aliyekuwa mgombea ubunge kupitia TLP Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, Ndaka Wolfugang ndiye aliyechelewa kujaza fomu hiyo.

Kutokana na kasoro hiyo, alisema ofisi yake (Msajili) ilimwekea pingamizi Wolfugang, lakini akarudishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwania nafasi hiyo kwa maelezo kwamba, kuchelewa kwake kujaza fomu hiyo, kulitokana na kuwekewa pingamizi na aliyekuwa mgombea kupitia CCM, Bernard Membe, ambalo baadaye lilitupwa.

CHANZO: NIPASHE
 
thanks for the info..... i think we should pave for a way that all financial statements for the responsible political parties are open on quarterly basis... we can then measure developments within political parties against the money used..... its better to scrutinize each political party's coffer to make sure taxpayers money do not transact the wrong doings
 
Wana haki ya kugombana, namkumbuka Mrema na Marando, kila siku Mrema alikua anlia kuwa Marando kala milioni 104
 
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo...................................

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma......................

Ruzuku ya Chadema haitoshi.

Chadema ni zaidi ya CCM.
 
Naamini kuna chama fulani watauana kwa hizo. Maanake mhh hao jamaa kwa pesa! Mhh!!!
Kwanza watajiibia wenyewe!!
 
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo...................................

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma......................

I suggest chadema wangeweka open financial statements, at least every six months, hiyo ingekuwa njia nzuri sana ya uwazi, na CCM watashindwa kugeza, hiyo hela inaliwa tu....
Hopeful chadema wataweza kutujulisha sis wafuasi wao... jinsi gani 'Hela zetu" zinavyotumika
 
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo...................................

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma......................

Duh kumbe ndiyo maana akina Makamba wako tayari kufanya lolote ili mradi wapate kura, iwe kwa kuiba, vurugu, au hata uhuni wa moja kwa moja kama ule wa Karagwe.

Je hizi 800m wanatakiwa kutolea maelezo yake? Isije ikawa hizi ndizo hutumika kubaka demokrasia yetu kwa kuajiri na kuwalipa Green Guard
 
Gazeti la Nipashe la leo linatujulisha ya kuwa Msajili wa vyama vya siasa Bw. John tendwa ametangaza ruzuku kwa vyama vya siasa na mgawanyiko wake ni kama ifuatavyo...................................

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................

Jamani hizi pesa sasa zisiwe chanzo cha mifarakano ya ubinafsi na ufujaji wa mali ya umma......................

Hela yote ya kodi anayolipa mdanganyika inaishia kulipia dowans, viongozi wa serikali,baraza la mawaziri, na safari zao,posho, na hizo, 800,200,110 milioni kwa vyama vya siasa, halafu tunazungumzia maendeleo Tanzania, kumbe safari haija anza bado. Na umasikini kwa mtu wa kawaida unazidi.Mzigo huu anaubeba mlalahoi,plus kupanda bei ya vyakula,umeme,nauli..walalahoi tunakamuliwa kama ng'ombe!

Hivi kuna mtu anayejua deli la taifa lina ukubwa gani? Serikali inalipa milioni ngapi kila mwezi ku-service deni la Taifa, ikiwemo lile la Barclays la ununuzi wa rada?

Kwa hali hii maisha bora kwa kila mtanzania hayatowezekana. Ni bora tuambizane ukweli!

kanga, vitenge, t-sheti na kofia zitatutokea puani!

Tanzania oyeeeee!
 
za wengine poa, ila za cuf zinaniuma kwani si cuf si chama cha tz bali cha znz

Mkuu,

Punguza hamasa!

Nilifikiria chama cha siasa ili kupata usajili wa kudumu inapasa kiwe cha kitaifa. Hivi CUF hawana sifa hii? Nilisikia pia kuwa uchaguzi uliopita wamepata wabunge wawili wa kuchaguliwa majimboni huku Tanzania bara(Tanganyika), au???

Myonge mnyongeni ila mpeni haki yake, huo ndio ustaarabu.
 
Ruzuku ya Chadema haitoshi.

Chadema ni zaidi ya CCM.

Mkuu,
Katika Tanzania ya leo, hakuna chama cha siasa kilicho zaidi ya CCM.Ukweli huu ni mchungu,lakini ndio ukweli,mkuu. Vyama vya Upinzani vina safari ndefu bado.

Kumbuka kuwa walio-mastermind mfumo wa chama kupata ruzuku ni hao hao wanaopata 800milioni. Na hawakuwa wamekusudia kuwa CHADEMA,NCCR,CUF wapate zaidi ya wao!

Nafikiri pia hii ruzuku imekuwa designed ku-black mail vyama vya usindikizaji(upinzani), pia ni mechanism ya kuviparaganya vyama hivyo kwa viongozi wake kuchangamkia kumega sehemu ya huo mgao na kuweka mifukoni mwa.Inaitwa ulafi, uroho wa hela ya bure! Na hivyo ku-create migogoro ndani ya vyama hivyo.

Washauri CHADEMA wazitumie kukipeleka chama vijijini.
 
Ruzuku ya Chadema haitoshi.

Chadema ni zaidi ya CCM.

Haya ni matunda ya kukosa TUME huru ya uchaguzi na kura za Chadema ziliibiwa na matokeo yake hakuna kura za kuongeza mgawo wa ruzuku...................
 
CCM imeshuka kwa ruzuku, huko nyuma ilikuwa inapata Shilingi bilioni moja, lakini sasa inapata Sh. milioni 818.

CCM inapata kiwango hicho, kutokana na kupata asilimia 60.40 ya kura za urais katika uchaguzi huo, ambazo ni sawa na Sh. milioni 354 na asilimia 77 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 460) kwa mwezi.

Chama cha Wananchi (CUF) kimepata kiwango kidogo cha mgawo wa ruzuku kulinganisha na Chadema.

Chadema inapata Sh. milioni 203.6, kutokana na kupata asilimia 24 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 146) na asilimia 9.62 ya wabunge (sawa na Sh. milioni milioni 56).

Kutokana na hali hiyo, CUF sasa inapata Sh. milioni 117.4, kutokana na kupata asilimia 9.80 ya kura za urais (sawa na Sh. milioni 57.9) na asilimia 10 ya wabunge (sawa na Sh. milioni 56).
 
Hizo ni kwa mwezi au kwa mwaka??
 
Back
Top Bottom