Mrao keryo
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,611
- 2,169
Watu 13 wamepoteza maisha na majeruhi kadhaa baada ya Fuso walilokuwa wanasafiria kutoka mnadani kutumbukia mtoni. Watu hao walitoka kijiji cha Nambendo wilaya ya Namtumbo kurudi Songea walikokwenda kuuza vitu mbalimbali jana siku ya Pasaka! Miili ya marehemu ipo hospitali ya mkoa wa Ruvuma. Pole kwa wote waliokumbwa na maafa hayo.
---------------- -------------
==================
Updates
Ajali hiyo imetokea wakati gari aina ya Mistubishi Fuso (T.800 BXB) lililokuwa limewabeba watu kutoka Ndongosi Mnadani kutumbukia mtoni wakati walipokuwa wakielekea Namatui, Aprili 9, 2023.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema majeruhi wawili wamelazwa katika Kituo cha Afya Mpitimbi na miili ya marehemu ipo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni ubovu wa barabara na utelezi kutokana na mvua.