Rushwa:Live mgambo akichukua chake mitaa ya katikati ya jiji

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
IMG_2816.JPG
Hapa Mgambo akimfukuza mpiga picha bia kujua kuwa wapiga picha walikuwa wawili mwingine alijificha , halafu mgambo ni hakika hajui mambo ya kuzoom

IMG_2818.JPG

Picha liliendelea kwa askari huyu wa Jiji la Dar es Salaam alipomkuta mama huyu amesimama pembezoni mwa jengo la IPS jijini Dar na kuanza kumfokea pindo alipomuomba kidogo dogo ili asimfikishe ofisini kwao.

IMG_2820.JPG
... Baada ya kumalizia mazungumzo alichukua kidogo dogo kwa staili ambayo si rahisi mtu kujua alichokuwa akifanya. Mambo kama haya ndiyo wanayoyafanya askari hawa wa jiji la Dar kwa kunyanyasa wananchi hasa akina mama pindi wanapowakuta wamepaki vibaya magari yao. Lakini jambo la kushangaza kwa nini magari hasa ya viongozi/serikali yakipaki hayasumbuliwi
IMG_2853.JPG

baada ya kuwa amekula kidogo dogo kutoka kwa mwanamama na kumuachia akaondoka, zilipita dakika 3 tu ndipo lilipokuja gari lililokuwa limeandikwa Wizara ya Kazi na Ajira (W KA), na kupaki ila hawakulifanya lolote
 
Mtakatifu unyanyasaji kwa hawa wanajiita watu wa parking au mgambo ni mkubwa sana
Ssidhani kama wamewekwa kuwanyanyasa watu au wamewekwa kuwasaidia watu
kuna maeneo hata vibao vya No parking havionekani ila ukipark tuu jamaa wanakuja kasi kama umeme wanaanza kukuambia uko kwenye wrong parking. inaumiza sana
 
hawa jamaaa sijui tuseme ni mtaji wa mtu au dili ..lakini tatizo ni wakubwa wanashindwa kufikiria system nzuri ambayoingeweza kuepusha kero zote hizi..tatizo kila mtu anawaza tumbo lake tu
 
Mkuu matumbo yanawafanya watu wanafanya vituko na mambo haya ndio yanayofanyika kwa watu ambao hawaelewi haki zao
 
Wacha mjomba nae apate cha kupelekea familia yake.Mshahara wenyewe wanaopewa mdogo sana.Tena na mlaani huyo jamaa aliye mpiga picha.Hamna mtu Tz asiye mlarushwaa sema fursa hajapata tu.
 
Wacha mjomba nae apate cha kupelekea familia yake.Mshahara wenyewe wanaopewa mdogo sana.Tena na mlaani huyo jamaa aliye mpiga picha.Hamna mtu Tz asiye mlarushwaa sema fursa hajapata tu.
REAL TANZANIAN...sishangai
 
ukiwa na katoroli kama hako ni lazima wakufanyie, nenda na gari ya maana uone nani atakuuliza
 
Mfumo huu ndugu yangu, jaribu kuuliza analipwa sh ngapi? japo malipo kidogo au makubwa hayahalalishi mtu kuchukua mapato ya kificho, akini kuna muktadha.............namhurumia kwa sababu wakiiona hii picha hana kazi na afya yake inaonekana kabisa ni mlalahoi...jamani...jamani...jamani
 
Sio gari la wizara bali WAZIRI sasa unadhani yeye mjinga apelekwe Nangurukuru badala ya kutesa mujini bana.
 
Back
Top Bottom