Rukwa: Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) akatwa mkono

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
11025627_910737655613505_6323703960052205674_n.jpg
Mtoto Baraka Cosmas akiwa hospitali baada ya kukatwa kiganja cha mkono.

Habari wanaJF,

Wakati nafuatilia mechi ya Simba dhidi ya Yanga, wakati wa Mapumziko mtangazaji kutoka studio ametangaza kuwa Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) mwenye umri wa miaka sita amekatwa mkono wake.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.

Habari hii pia imethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa.-

Chanzo: Azam Tv


LICHA ya Serikali, jamii na jumuiya ya kimataifa kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bado kuna wanaoendelea kung'ang'ania mila potofu za kuamini kwamba bila ya ushirikina unaohusishwa na matumizi ya viungo vya albino, hawawezi kufanikiwa kimaisha, iwe katika kisiasa au kibiashara.

Hayo yanathibitishwa na kuendelea kuripotiwa kwa matukio ya ukatili dhidi ya albino, ambapo usiku wa kuamkia jana, watu wasiojulikana walimshambulia na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na kisha kutokomea nacho kusikojulikana.

Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32) na Prisca Shaaban.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda.

Alisema tukio hilo ni la saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo akiwa amelala na mama yake. Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo.

Akielezea zaidi, Kamanda Mwaruanda alisema usiku huo kikundi cha watu wasiojulikana walivamia nyumba alimolala Baraka na mama yake mzazi, Prisca wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo mapanga na fimbo na kuanza kumshambulia kwa kumcharaza viboko Prisca baada ya kukataa kuwapatia mtoto huyo, mwenye ulemavu wa ngozi.

"Baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo walimwamuru mama mzazi wa mtoto Baraka kuwakabidhi mtoto huyo, lakini alikaidi ndipo walipoanza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumjeruhi vibaya … "Waliingia ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia na kuondoka nacho kusikojuliakana," alibainisha.

Aliongeza kuwa wakati hayo yakitokea, baba mzazi wa mtoto huyo inadaiwa alikuwa amelala katika nyumba ya mkewe mdogo kijijini humo.

Kwa mujibu wa Mwaruanda, mtoto huyo amelazwa katika katika Kituo cha Afya cha Kamsamba wilayani Momba mkoani Mbeya kwa matibabu akiwa pamoja na mama yake mzazi.

"Watu watatu ambao majina yao yamehifadhiwa, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea ili kuwasaka wahusika na kiungo hicho cha kiganja cha mkono wa mtoto Baraka," alisisitiza Kamanda.

Chanzo: Habari Leo
 
Muda huu wakati wa matangazo ya match ya Simba wakicheza na vibonde wao Yanga mdebwedo, kuna taarifa Azam Tv kuwa mlemavu wa ngozi Albino kakatwa mkono huko mkoani Rukwa. Polisi kama kawaida wanaendelea na uchunguzi.
 
wakuu Niko naangalia azam TV wametoa breaking news kuwa kuna albino mwingine kakatwa mkono Leo mkoani rukwa pamoja na kampeni hii ya Imetosha sasa!

My God sijui hii ishu kama itaisha hasa kipindi hiki cha uchaguzi

source Azam TV
 
Pamoja na vitisho vikali Vya mkuu wa nchi ambae pia ni mkuu wa majeshi jana usiku mtoto wa miaka 6 amekatwa MKONO na Watu "wasiojulikana" . Source Azam tv na kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa.

Naona wazi HAKUNA nia njema kukomesha MAUAJI haya. Kelele zote na mikwara vipo Dsm Tu. Intelijensia uendeshaji mikoani sasa.
 
Nilishasema hili tatizo haliwezi kuondolewa kwa kuwavalisha watu nguo zisemazo SASA YATOSHA, hiyo ni slogan kama big results now, mkurabita, mkukuta, mkulachuma, hiyo kampeni ni watu wanatumia fulsa tu!! watu waliohukumiwa kifo wanyongwe tu. Kina masoud kipanya, zembwele eti ndio mabalozi wa kampeni hii.
 
Duh...... kila mkuu wa mkoa na wilaya wawe na jukumu la kuwalinda hawa watu, ifanyike survy maalum ya kujua idadi yao na shughuli zao, makazi yao n.k ili kuwalinda na kusaidia kuwatafuta wanapopotea.
 
Inasikitisha, kama vigogo wa serikali ndo wateja wakubwa, tatizo litaishaje? Na kama sio wateja wakubwa kwanini wanashindwa kumaliza tatizo hili? Na huu ni mwaka wa uchaguzi.
 
Kutangaza ni lazima cz tangu tukiwa wadogo tulikuwa tukidanganyana kuwa albino hawafi, ila wanapotea tu, kumbe masikini walikuwa wanauliwa kimya kimya, had miaka ya hii 2000 walipoanza kutangaza ndio wengine tumefunguka na kujua ukwel, na hii imetufanya wote kiwa macho ss wewe unapokuja leo na kusema wasitangaze, kwel hamnazo
 
Back
Top Bottom