Rukwa: Chongolo akiona cha moto, wananchi wampekekea maji machafu ili anywe

Ni kwanini Serikali ya CCM isizirejeshe zile fedha za Plea Bargain zilizofichwa kwenye Akaunti ya China ili zije zichimbe Visima pamoja na kuviwekea Filters

Halafu Vizinduliwa na Biswalo Mganga.
 
IMG_4147.jpg
 
Katibu Mkuu wa CCM , chama ambacho kimeasisi kila dhiki unayoiona Nchini Tanzania , Ndugu Chongolo , amegonga mwamba huko Rukwa , pale alipotembelea Jimbo la Kwela (ngome ya Chadema)

Mbwembwe zote za Chongolo zilisha zenyewe baada ya wananchi kumletea maji machafu wanayoyatumia , hata baada ya zaidi ya miaka 60 tangu nchi hii kupata Uhuru.
---

Tatizo la maji katika Kijiji cha Mwela, Jimbo la Kwela, wilayani Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, umewafanya wananchi wa eneo hilo kuusimamisha msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ili kufikisha kilio chao.

Msafara huo ulikuwa unatoka Kata ya Muze kwenda Mto Wisa leo Jumanne Oktoba 10, 2023, kuendelea na ziara yake, ndipo wananchi walipojipanga barabara wakiwa na ndoo zenye maji machafu.

Kutokana na hilo, Chongolo amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi na mwenyekiti wao Chrispin Bernaba na papo hapo, akatoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Ally Nyakia na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa).
Ndo dawa. vile hakuna jinsi ya kubeba giza hili tuwapelekee wajua umeme hakuna
 
Yaani hii ndio dawa yao, hadi AKILI ziwakae sawa..haiwezekani nchi yenye RASILIMALI nyingi hivi tulale gizani kama mende na tunywe maji machafu kama vyura
 
Katibu Mkuu wa CCM , chama ambacho kimeasisi kila dhiki unayoiona Nchini Tanzania , Ndugu Chongolo , amegonga mwamba huko Rukwa , pale alipotembelea Jimbo la Kwela (ngome ya Chadema)

Mbwembwe zote za Chongolo zilisha zenyewe baada ya wananchi kumletea maji machafu wanayoyatumia , hata baada ya zaidi ya miaka 60 tangu nchi hii kupata Uhuru.
---

Tatizo la maji katika Kijiji cha Mwela, Jimbo la Kwela, wilayani Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, umewafanya wananchi wa eneo hilo kuusimamisha msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ili kufikisha kilio chao.

Msafara huo ulikuwa unatoka Kata ya Muze kwenda Mto Wisa leo Jumanne Oktoba 10, 2023, kuendelea na ziara yake, ndipo wananchi walipojipanga barabara wakiwa na ndoo zenye maji machafu.

Kutokana na hilo, Chongolo amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi na mwenyekiti wao Chrispin Bernaba na papo hapo, akatoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Ally Nyakia na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa).

Mzee wa mastory bora amekutana na reality show. Hawa wanaotembelea Ma VX huwa wanajisahau kuwa katika watu milion 60, takribani asilimia kubwa wanaishi maisha magumu sana. Lazima kimkakati, maendeleo yaanze kusogezwa mpaka vijijini. Miundombinu na huduma nyingine muhimu ili viwe chachu ya maendeleo
 
Back
Top Bottom