Ruge Mutahaba: Mr II aniombe msamaha

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159

Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (T.H.T) Bw. Ruge Mutahaba amemtaka Mkurugenzi wa Deiwaka Production Bw. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu amwombe msamaha dhidi ya tuhuma zilizotolewa juu yake kuhusiana na kampeni ya Malaria No More.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana Mikocheni jijini Dar,Ruge Mutahaba amesema kuwa amempa Mr II masaa 72 ili aweze kumuomba msamaha/radhi dhidi ya shutuma ambazo amezisambaza dhidi yake kuhusiana na sakata hilo la Malaria No More

"Kiukweli nimeamua kuwaita waandishi wa habari ili niweke sawa haya mambo, mimi nilipewa tenda na kampuni ya Roundtrip kusimamia upande wa wasanii, jukwaa pamoja na`kusimamia mambo mengine hilo ndiyo lilikuwa jukumu langu mimi kama mimi,haya mambo mengine yanazungumzwa juu yangu sijui yanatoka wapi,hivyo namuomba Mr II aniombe radhi/msamaha kwa vyombo vile vile vya habari alivyovitumia kunidhalilisha mimi na kunivunjia uaminifu kwa jamii ninayoiongoza"alisema Ruge Mutahaba.
 
Hivi ni vibweka sasa!
Mr II alisema anakwenda mahakamani huko America na akiomba msamaha ataonekana hakuwa na uhakika na alichodai.
 
Ruge, utapeli ni jadi yako.
Wewe uaminifu ni adui yake.
Hivi wale watoto wa t. H. T wananufaika vipi na sanaa wanayoifanya?
Wale waruka sarakasi umewakatia bima kweli au ndio bora punda afe mzigo ufike?
Ruge ulichokifanya unakijua, na ukome kuwafanya watanzania kuwa ni mazuzu wasio na akili.
Kwa muda mrefu tumekusoma na sasa tunakujua na kukuelewa ndani nje ndani.
 
Huu utamaduni wa kukimbilia media bado haujafanikiwa katika kutatua migogoro katika jamii, manake huwa mnaanzia katika media halafu mnaelekea mahakamani na kuishia katika visasi. Ruge mtafute Sugu mkae chini kama washkaji na kumaliza tofauti zenu mambo ya media waachieni wazee na wanasiasa.

Manake kwa umri wenu mtakuja kununuliana bastola mpasuane vichwa.
 
well said Mkuu............ushauri mzuri sana huu...........sina hakika na understanding kuhusu hii issue na wahusika wenyewe........if you know what I mean..........
 
Ruge, utapeli ni jadi yako.
Wewe uaminifu ni adui yake.
Hivi wale watoto wa t. H. T wananufaika vipi na sanaa wanayoifanya?
Wale waruka sarakasi umewakatia bima kweli au ndio bora punda afe mzigo ufike?
Ruge ulichokifanya unakijua, na ukome kuwafanya watanzania kuwa ni mazuzu wasio na akili.
Kwa muda mrefu tumekusoma na sasa tunakujua na kukuelewa ndani nje ndani.

Watu wa mjini wala hawakushangaa kwa maana ndo zake, anasubiri wenzie wapike ye anakuja kupakua tu. kaka noma!
 
Back
Top Bottom