Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni
Na Mwandishi Maalum,
Taifa Letu
April 3, 2009
Yule mfanyabiashara mwenye maadili yenye utata, Bw Rostam Aziz wiki hii amekuwa akifanya vikao kadhaa vya faragha na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Vikao hivyo ambavyo vinasadikiwa vinahusiana na sakata la kukwama kwa mara nyingine kwa jaribio la kutaka kuiuzia Tanesco mitambo chakavu ya Richmond, vimekuwa vilifanyika ofisini kwa Lowassa, Alpha Cleaners iliyoko eneo la viwanda Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba vikao hivyo vilimshirikisha pia Bw Yusuf Makamba.
Baadhi ya mashuhuda wameliambia gazeti hili kwamba vikao vya mikutano kati ya wakubwa hao vimeongezeka mno hasa kwa wiki hii ambapo baada ya gazeti hili kutonywa walipo vigogo hao lilivamia katika ofisi za Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kumshuhudia Bwana Rostam Aziz akiingia sehemu hiyo ba gari la kifahari lenye namba za usajili T 347 AJL.
Uchunguzi wetu umebaini kwamba kikao cha kwanza baina ya Lowassa na Rostam kilifanyika Alhamisi wiki iliyopita lakini hapoakuwa na uhakika kama Bw Makamba alikuwepo.
Hata hivyo katika kikao ambacho kimefanyika juzi Jumatatu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tano na dakika 45, makachero wa gazeti hili walimshuhudia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akijumuika na Bw Rostam Aziz pamoja na Wziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa
- Vyote vyafanyika ofisini kwa bw Edward Lowassa
- Katibu Mkuu CCM, Makamba abainika alikuwepo
- Vilifanyika Alhamisi wiki hii na vingine Jumatatu wiki hii kuanzia saa 4.00 asubuhi