Rostam, Lowassa wafumwa kikaoni

Story ya thread hii si kamili. Nimelitafuta gazeti hilo na kuisoma story yote. Inavyoelekea makachero wa gazeti hilo walikuwa wanafuatilia ingia-toka ya ofisi hiyo ya EL hapo Alpha DryCleaners ambayo haiko mbali sana na ofisi za IPP, wachapishaji wa gazeti hilo la Taifa Letu.

Hizi ingia-toka za vigogo hawa ziliongezeka maradufu baada tu ya mpango wa tanesco kununua mitambo chakavu ya Dowans kukamwa na vikao hivyo vinaonekana ni crisis talks. Si kazi kubwa sana kuspeculate walikuwa wanaongea nini.

Mnadhani walikuwa wanaongea namna ya kuwapiga vita mafisadi?

mimi nafikiria RA,EL NA YM walikua wanafanya mpango wa kuwapiga vita mafisadi....
kwi kwi......
 
Majambazi sugu yanayofahamika mtaani yakikutana faragha watu wote mnakaa kwa tahadhari kubwa siku hiyo,hilo halina mjadala.
Hofu inaongezeka maradufu mkiona faragha hiyo hata mwenyekiti wa mtaa wenu naye naye alikuwa mjumbe na hatoi taarifa kuwa kikao hicho kilihusu nini na watuhumiwa hao.
Tunajiuliza Makamba kama Katibu Mkuu wa CCM alikuwa anaongea nini nahao washukiwa wa ufisadi kwa siri? Au ni maandalizi ya CC ya CCM maana wote ni wajumbe?
 
unajuwa kitu cha kushangaza ni kuwa, dhidi ya tuhuma zote mnazotowa kwa ra, hao wengine sijui, sijaona hata mmoja humu jf aliesema sasa nakwenda mahakamani kumfungulia mashtaka ra, mpaka nikatowa wazo humu, kwa mwenye nia na mwenye kuweza, atangaze jf apatiwe ushahidi au apatiwe ushauri wa vipi aanze kumfungulia kesi ra. Hivi maneno, kejeli, vijembe, matusi bila ya kutenda (action) inasaidia kweli? Sidhani, kinacho washinda ni nini kufanya hivyo? Au mnaogopa kuwa haya ni maneno tu na porojo za kijiweni na hamna ushahidi wa kosa lolote alilofanya na mkifanya action itawageukia?

Ra kimyaaa, kapowa, anafanya vitu vyake taratibu na wala humsikii kusema sema hovyo, mie nasema siku zote, mtikila alileta ngebe akaonyeshwa action ndogo tu, akaufyata.

Chuki na kero zenu zina agenda fulani, mimi naiita agenda ya siri. Lakini kwa ukweli ni kwamba, hamna hoja kabisa bali ni chuki binafsi za kibaguzi, ama kwa rangi yake au kwa dini yake au kwa fedha yake.

mtoto wa mjini(dar es salaam) unalipwa bei gani, kwa utetezi kama huu?????, NINAISI UJAAJIRIWA BALI UNAJILIPA MWENYEWE (RA). HAMNA AJA YA KUTUMIA KIVULI CHA DAR UNGEWEKA TU RA? AU CONFIDENCE ZERO?
 
Last edited:
Hawa jamaa wana njama gani?
Tatizo sio kuwa wao kufanya vikao! wala kufanya kwao vikao si tatizo lolote kwetu, kwani hawa jamaa ni maswahiba wa siku nyingi walioshibana wakafikia hata hatua ya kuihujumu nchi kwa kuhusika kwao kwenye deal ya kitapeli ya Richmond iliyoingiza nchi kwenye Hasara kubwa.

Tatizo ni hawa jamaa kukutana nchi ikiwa kwenye hali Tete kwa sasa ikikaniliwa na malumbano ambayo misngi wake ukiangalia kwa kina wao wanahusika moja kwa moja kwa namna moja au nyingie. Kwa nini usifikirie vibaya kama Iliandokwa na gazeti moja lenye kuandika habari za kiuchunguzi ambazo ziko makini kuwa Lowasa amzunguka JK halafu usikie vikao vinafanywa halafu mhusika ndio mwenye ofisi na vikao vimefanyika ofisini kwake!

kwa nini tusipate hofu ya kikao anachohudhuria Rostam wakati anatuhuma nyingi za kifisadi alizoshindwa kukanusha mpaka sasa la Kagoda likiwa mojawapo!? kwa nini usujiulize kikao ni cha nini baina ya maswahiba hawa wawili ikiwa ni juzi tu alikuwa kwenye malumbano na Mwakiembye tena imebainika kuwa tuhuma hizo anagombea eneo la kuanzisha kampuni ambayo wananchi wana lalamikia kulazimishwa kuhama kwenye eneo hilo bila hata kujua taratibu za fidia zikoje?!

Vikao vyao kutokana na haiba yao wawili hawa wala sioni kama vina nia njema kwa wakati huu! hawa inawekena kuna jungu wanalipika na likiiva watalipakua na wakukulilia watapatikana.

Ni hayo tu.
 
Hivi kitu gani kifanyike ili hawa jamaa RA na Lowassa wafikishwe mahakamani? Kama ni ushahidi wa kuwatia hatiani, nani anakusanya ushahidi huo na amefikia wapi hadi hii leo? kama ushahidi umepatikana, ila amri ya kuwapeleka mahakamani haijatoka, nani anapaswa kutoa hiyo amri? Au amri imeshatoka ila hakuna wa kuwakamata?
 
Watanzania tunasikitisha; yaani watu hawawezi hata kuunganisha dot zilizoko mbele yao wanabakia kuulizana kama doti hii ni kubwa au ndogo, ina rangi kama ile, mbona doti hazionekani vizuri!

Hivi nilipowaambia kuhusu mkutano wa Dubai.. mnajua nani mwingine alikuweko? Tukiwaambia mtasema walikuwa wameenda kufanya shopping! Waacheni watawale wapendavyo!
 
Jamani naomba kujua Jana mchana Rostam amekula nini?

Saa sita mchana jana Lowassa alikuwa amevaa nguo gani?

Makamba Mzee, katibu wa CCM jana saa kumi alikuwa anaongea na nani?

Ni hayo tu.

Wabongo bwana!

Tutake radhi tafadhali!! How fair can u play?
 
TUlishatahadharishwa lakini leo nimeona wazi kuwa tumeingiliwa na makuwadi na wafuasi na wapambe....
Tuachane nao tuendelee kukata ishus: mi naona kuna sababu ya kushangaa kuwa RA na EL wanakutana Alpha Cleaners. Just few weeks ago RA alikuwa hadharani Kempinski pale Zanzi Bar maana siku hizi ameona anachoreka sana Movenpick. Kwa hiyo , kama wangetaka wangeweza kuonana kule na wakaongea masuala ya Yanga na AlAhly na vitu vingine visivyo na uzito. Kukutana kwao ofisini ni ishara ya kuwa:
- hawakutaka kuonekana pamoja hadharani
- hawakutaka mtu asikie wanachokiongea yaani ni mazungmzo ya faragha

Sasa hebu tu-factor in issue ya baba January - sasa katibu mkuu mzima kwenda kuonana na watu katika Dry Cleaners office inaleta picha tofauti sana kwani kama ni urafiki wangeonana sehemu ya kurelax na time zisizo rasmi.
Hivyo ni dhahiri mazungumzo yao hayakuwa ya pwagu na pwaguzi.
Ni kweli hatuwezi kujua walichokiongea na maybe hata si muhimu sana lakini ni vyema kupata confirmation kuwa RA na wenzake wamekwama na pia shughuli zote za RA amefanya kwa niaba ya chama. Hivyo ndiyo maana he is untouchable. It is also good to know kwamba EL bado yuko in picture na anamtumia RA na baba January kufanikisha mipango yake.
Tulikuwa tunahisi na kusikia minongono lakini sasa tumepata confirmation. And now they have been marked ... :)
 
Mi investment aliyokuwa nayo Tanzania na nchi nyingi duniani inatosha kabisa kumnyima usingizi, na hizi za JF hata sijui kama ana time ya kuziona.

Acha kumpigia pande jamaa yako, Nafikiri na kuamini kuwa hizo investment nje/duniani ni za Habibu na sio yeye na hana hata share moja except Caspian Tanzania
 
Watanzania tunasikitisha; yaani watu hawawezi hata kuunganisha dot zilizoko mbele yao wanabakia kuulizana kama doti hii ni kubwa au ndogo, ina rangi kama ile, mbona doti hazionekani vizuri!

Hivi nilipowaambia kuhusu mkutano wa Dubai.. mnajua nani mwingine alikuweko? Tukiwaambia mtasema walikuwa wameenda kufanya shopping! Waacheni watawale wapendavyo!

MKJJ uwe unamaliziaga na wewe! uachage hizo nusunusu zako zinatunyima raha
 
mtoto wa mjini(dar es salaam) unalipwa bei gani, kwa utetezi kama huu?????, NINAISI UJAAJIRIWA BALI UNAJILIPA MWENYEWE (RA). HAMNA AJA YA KUTUMIA KIVULI CHA DAR UNGEWEKA TU RA? AU CONFIDENCE ZERO?

Ingekuwa hivyo ningekuwa na time ya kubishana humu? na isingekuwa Dar... ingekuwa Igunga au Tabora.

Hapana sitetei, nnachojaribu kufanya ni kuhamasisha, sioni sababu ya kumsakama mtu kwa labda Rangi yake, labda Kabila lake, labda Utajiri wake, labda Dini yake, kweli kabisa, sijaona mpaka leo data za kumhusisha na ufisadi unaosemwa, ikiwa Richmond, wenyewe tumeshawajuwa, ikiwa Dowans hali kadhalika sijaona jina la RA, au nyie mmeshaliona? kama mna ushahidi wa kutosha si mumshatkai mahakamani mnangoja nini?

Sasa, nawapa wazo lingine, kama mnaogopa kumshitaki na ushahidi mnao, basi mimi najitolea, nikusanyieni ushahidi wote, wanasheria humu ndani wasaidiane kuuchambuwa ushahidi, si wapo wengi tu, wakiona unafaa kumpeleka mahakamani na kuna uwezekano wa kushinda, basi mimi ntakwenda kushtaki mahakamani kwa niaba ya JF, tufunguwe account mchangie gharama za mahakama na usumbufu wangu, mnasemaje kwa hilo? tufanye action ya uhakika sio kulalama tu.
 
Watanzania tunasikitisha; yaani watu hawawezi hata kuunganisha dot zilizoko mbele yao wanabakia kuulizana kama doti hii ni kubwa au ndogo, ina rangi kama ile, mbona doti hazionekani vizuri!

Hivi nilipowaambia kuhusu mkutano wa Dubai.. mnajua nani mwingine alikuweko? Tukiwaambia mtasema walikuwa wameenda kufanya shopping! Waacheni watawale wapendavyo!

Mwanakijiji dont give up! hawalali kwa raha hawa watu (kila siku wanahamisha mali na wengine hadi familia haziishi bongo) coz of people like you na magazeti mengi tuu yanayowachoma..kwa sasa nchi yao but time shall be the judge..everything has an end and not necessarily a happy one. There is only so much we can do here at JF the rest is left to the average tanzanian, If the average tanzanian does not see anything wrong with him or her not gettin their essential needs we should not expect the leaders to act any different.
 
Mnajua maana ya parti pris?
Kama mnajua basi mnafanaya makosa kuendeleza malumbano na mtu anayejiita hivo.
 
Sioni hoja hapa, waache wakutane. Kwani wewe unapokutana na wenzako kijiweni ni lazima muwe mnapanga maovu? Kwani uhuru wa kukutana umeishaondolewa? Nimesoma hoja zote mlizoleta sebuleni sikuona la maana mnalopigia kelele zaidi tu ya hisia. Si afadhali wanakutana mchana kweupe, je wangekuwa wanakutana usiku si ndiyo ingekuwa balaa, mnasema lakini sijaona hoja kabisa.

Mzee DSM nakuunga mkono 100% kama kuna mtu mwenye ujasiri ajitokeze basi tumsaidie kumpeleka RA mahakamani kuliko kelele za chura zisizo mzuia tembo kunywa maji. Mimi siupendi kabisa UFISADI lakini napenda kuchukua hatua pale ninapoona ukweli upo. Leteni ukweli tushughulike.

Mzee K umenena.
Jamaa alieanzisha thread pamoja na gazeti lililoripoti vimekaa ki u-daku. sijaona logic ya kusema eti .wafumwa kikaoni. Na watu mnaanza kujadili. Jamani how low! we are now? this is completely udaku.

Acheni hizoooo...kama kuna issue serious za kuziongea zungumzeni lakini habari za majungu acheni. Very dis appointed.

Ila nadhani Rostam must be genious if at all he is. Nchi nzima inatikisika and no one can come vividly to implicate him with anything direct..tutaishia tu oh! fisadi... then so what.

Rostam endelea na hamsini zako so long as no one has dare to proove how bad you are.

Kingwele.
 
Iwe iwevyo. Kama walikutana kweli kwa malengo yale yale ya siku zote ama kwa mipango ya sherehe za harusi, EL na RA si watu wazuri hata kidogo.Tuliwapuuza awali wakati wanapanga mikakati ya kushinda uchaguzi leo hii nchi nzima inaimba wimbo kuhusu ufisadi. Hivi tunadhani kama RA na EL wasingekuwepo leo hii tungekuwa hapa? Kwa nchi za wenzetu wanaojua madhara ya ufisadi hawa viumbe wangekuwa wameshaning'inia kwenye vitanzi siku nyingi.
Haitoshi kuwafuatilia tu inabidi sasa kufanya jitihada za makusudi kabisa kuvunja nguvu zao maana aina hii ya watu hawana tofauti na Osama kitabia. Wataanza kuandaa vizazi vya kuwarithi baadae pindi wakiwa hawapo kitu ambacho ni hatari.
Nyerere aliona mbali sana, EL ana bahati tu kipindi kile Mwalimu alikuwa hana dola maana sidhani kama angeweza kumwacha mtu kama huyu kuendelea kuivuruga nchi kwa tamaa zake.
 
Jamani naomba kujua Jana mchana Rostam amekula nini?

Saa sita mchana jana Lowassa alikuwa amevaa nguo gani?

Makamba Mzee, katibu wa CCM jana saa kumi alikuwa anaongea na nani?

Ni hayo tu.

Wabongo bwana!
Acha mawazo mgando wewe unadhani Ze Komedi hii? hata Komedi wanazungumza ya maana siku hizi pamoja na kuburudisha. Hao ndio wanaopanga matumizi ya kodi yako. Wakisema watanzania hakuna umeme maana yake hakuna. Wakisema hela ya kununulia dawa hospitali wanafanyia sherehe za harusi za watoto wao hakuna wa kuhoji.

Hawa si watu wa kuwadhihaki hata kidogo.
 
Iwe iwevyo. Kama walikutana kweli kwa malengo yale yale ya siku zote ama kwa mipango ya sherehe za harusi, EL na RA si watu wazuri hata kidogo.Tuliwapuuza awali wakati wanapanga mikakati ya kushinda uchaguzi leo hii nchi nzima inaimba wimbo kuhusu ufisadi. Hivi tunadhani kama RA na EL wasingekuwepo leo hii tungekuwa hapa? Kwa nchi za wenzetu wanaojua madhara ya ufisadi hawa viumbe wangekuwa wameshaning'inia kwenye vitanzi siku nyingi.
Haitoshi kuwafuatilia tu inabidi sasa kufanya jitihada za makusudi kabisa kuvunja nguvu zao maana aina hii ya watu hawana tofauti na Osama kitabia. Wataanza kuandaa vizazi vya kuwarithi baadae pindi wakiwa hawapo kitu ambacho ni hatari.
Nyerere aliona mbali sana, EL ana bahati tu kipindi kile Mwalimu alikuwa hana dola maana sidhani kama angeweza kumwacha mtu kama huyu kuendelea kuivuruga nchi kwa tamaa zake.

Mwanakwetu unazidi kuninyon'gonyeza na hoja zako. Very dis appointing kwani ni lemavu mno na hazina mashiko yoyote.

unapoongea kama EL na Rostam ndo waliotufikisha hapa. It is absolutely out of touch! yaani umasikini huu tuliokuwa nao leo chanzo ni ni EL na RA? Hii nayo kali. EL? kawa Mbunge, Waziri na hatimaye Waziri Mkuu kuanzia lini..na lini hali yetu imeanza kuwa dhouful hali?

Chanzo kikuu ni sera zetu za uchumi baada ya kuchukua nchi..mambo haya ya ujamaa na kujitegemea na azimio la arusha na vita ndo hasa chanzo cha umasikini lakini sio EL wala RA kaka.

Sababu ya mwalimu kumkataa EL, umeiona ni ya msingi sana na kuihusisha na umasikini..hii nayo kali Je Mkapa ambaye mwalimu mwenyewe alimfanyia kampeni..Mbona sasa hae pia ameingizwa kwenye ufisadi.

Honestly mie nadhani one day..tutakuja kutambua mchango wa EL kama kweli ni waumini wazuri. His influence kwenye ujenzi wa shule za sekondari haukuwa na mfano. Shule hizi mnazozicheka na kuziita majinia kibao..mtakuja kuona faida yake very soon.

EL mnyonge mnyongeni lakini unastahiki sifa, utakumbukwa kwa uimara wako na uongozi wako..kweli uliogopwa na maelekezo yako yalifuatwa...ushahidi ni matunda ya kazi yako.

Kingwele.
 
Ingekuwa hivyo ningekuwa na time ya kubishana humu? na isingekuwa Dar... ingekuwa Igunga au Tabora.

Hapana sitetei, nnachojaribu kufanya ni kuhamasisha, sioni sababu ya kumsakama mtu kwa labda Rangi yake, labda Kabila lake, labda Utajiri wake, labda Dini yake, kweli kabisa, sijaona mpaka leo data za kumhusisha na ufisadi unaosemwa, ikiwa Richmond, wenyewe tumeshawajuwa, ikiwa Dowans hali kadhalika sijaona jina la RA, au nyie mmeshaliona? kama mna ushahidi wa kutosha si mumshatkai mahakamani mnangoja nini?

Sasa, nawapa wazo lingine, kama mnaogopa kumshitaki na ushahidi mnao, basi mimi najitolea, nikusanyieni ushahidi wote, wanasheria humu ndani wasaidiane kuuchambuwa ushahidi, si wapo wengi tu, wakiona unafaa kumpeleka mahakamani na kuna uwezekano wa kushinda, basi mimi ntakwenda kushtaki mahakamani kwa niaba ya JF, tufunguwe account mchangie gharama za mahakama na usumbufu wangu, mnasemaje kwa hilo? tufanye action ya uhakika sio kulalama tu.

tatizo sio ushahidi , tatizo ni mahakama, serikali na security organs ambazo zipo kwenye payroll yako na ndio zinazokupa kiburi cha kusema neno ushahidi

those who protects you, how long are they going to be in their positions?

I can see you are trying to recruit one for the future?

for how long are you gonna maintain the status quo????

We dont just hate you, we will get rid of you.
 
Yangu tena, duhh!
 
Back
Top Bottom