Rostam Aziz aachia ngazi CCM

- Well, saa imefika sasa wameanza kama ilivyosemwa, sasa wakishatoka wote liangaliwe suala la Sheria!

Willie @ NYC, USA.

Mkuu wakishatoka wote wangapi? Ni hao watatu au wale kumi na moja wa Dr. Slaa? Hizi siasa zitaigharimu CCM manake CCM imeanza kucheza ngoma ya CHADEMA. Sasa CHADEMA na watu wengine wenye mapenzi mema na nchi hii watauliza je mafisadi ndani ya CCM ni hao watatu tu na kama sio hao watatu tu (naamini ni zaidi ya watatu) wengine je? Matokeo yake CCM na Serikali vinaweza kumong'onyoka. Naona dalili za CHADEMA kukaa mkao wa kula kwani huenda uamuzi wa ngoja tukose wote ukaimaliza CCM!
 
Rostam Aziz ajiuzulu nafasi za uongozi katika chama (Sehemu ya gamba imevuka)

Habari hii imepamba kurasa za mbele za magazeti ya leo pamoja na mazungumzo ya watanzania katika mikusanyiko mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kwamba Rostam amechukua uamuzi huu katika mazingira yanayofahamika kwa watanzania wengi bila kujali ufafanuzi alioutoa Rostam katika hotuba yake kwa wapiga kura wake katika kutangaza hatua yake hiyo.

Kilichonifanya kuuliza swali hili ni hali iliyojitokeza katika baadhi ya makundi ya watu kutokana na jambo hili. Kuna baadhi ya watu wanashangilia na kufurahia hatua hii ya Rostam kwa kuonyesha kuwa . Pia kuna baadhi ya watu wanasikitika na wengine walifikia hatua ya kuzimia baada ya Rostam kutangaza hatua yake hiyo.

Kwa upande wa vyombo vya habari vipo ambavyo vimeelezea tukio hilo kwa ushabiki wa kufurahia na kuonyesha kuwa huu ni ushindi kwa chama fulani cha siasa katika hatua za kujisafisha.

Kwa jinsi ninavyoelewa hatua hii ya Rostam imetokana na juhudi ya baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa mstari wa mbele kufichua kashfa mbalimbali za rushwa na ufisadi ulioota mizizi tangu awamu ya pili ya uongozi wa nchi hii.

Swali langu hapa ni Je kujiuzulu kwa Rostam ni ushindi? na kama ni ushindi, ushindi huu ni wa nani?
 
Mapambano bado yanaendelea mpaka mwisho wa mchezo maana bado kuna mafisadi wengi tu wamebaki huko CCM. Wakishaondoka kwenye chama hatua za kisheria inabidi zifuate. Lazima warudishe hela zote walizopata kwa njia za ujanja ujanja.
 
Ushindi huu ni wa WATANZANIA WOTE,wenye kuitakia MEMA TANZANIA na WATU WAKE.Wenye kutaka kuiona Tanzania yenye USTAWI kama TAIFA na WATU wake wenye SIHA njema na wenye FURAHA kwa kumshukuru MUNGU wao,WAO NA VIZAZI vyao kwa KUZALIWA NDANI YA JAMHURI HII YA MUUNGANO WA TANZANIA.NA KUAPA KUILINDA DAIMA KWA FAIDA YA WOTE NA VIZAZI VIJAVYO.

Bali wenzetu waliotangulia kuweka maandishi kama kumbukumbu,yaani wazungu wanasema ''THERE ARE THREE KIND OF PEOPLE IN THE WORLD,THOSE WHO DONT KNOW WHAT HAPPEN,THOSE WHO WONDER WHAT HAPPEN AND THOSE WHO MAKE THINGS HAPPEN".

Kwa tafsiri yangu kibongo ningesema kuna aina tatu za watu hapa duniani "Wale wasiojua nini kimetokea.Wale wanaoshangaa kilichotokea na Wale wanaosababisha hayo yatokee".

Na daima kundi hilo la Mwisho yaani wale wanaosababisha hayo kutoke [those who make things happen] wako nyuma,kama ni kwenye harusi au dalasani basi wako safu za mwisho yaani Back Benchers.Na tabia mojawapo yao ni kutokutambulika daima ila utawatambua kama unajua kuwa kuna aina hizo tatu za watu duniani.
 
Igunga bila Rostam inaweza kuwa Imara zaidi. Hana mchango wowote bungeni. Siku zote yuko kimya. Aende na ashauri wenzake waharakishe kuvua magamba. Wakichelewa watatinduliwa.
 
Rostam kaamua kuachia ngazi baada ya kuuzwa kwa miambo ya Dowans kwa hiyo anajua hamtamshitaki kwa lolote kwani mitambo ile haimhusu tena.

Mimi nachosikitika ni kwa nini wahuni kama rostam wameichezea mali na akili ya watanzania kiasi hiki.
 
Kama rostam anataka kulinda heshima yake ya kijamii na kibiashara sasa ni wakati wake wa kumwaga mboga kwakuwa wenzie walishamwaga ugali kwa kuelezea ushiriki wake katika kuchota hela za kagoda na jinsi zilivyotumika wakati wa uchaguzi wa 2005 kuwasaidia magamba kupata ushindi wa kimbunga vinginevyo heshima yake itashuka na atadharaulika machoni pa watanzania na nje hailipi kujiuzulu vyeo pia arejeshe sehemu ya fedha za epa kwakuwa kuna kiasi alichukua mwenyewe.verry sorry kwa heading
 
Saaafiii
 
Mapambano bado yanaendelea mpaka mwisho wa mchezo maana bado kuna mafisadi wengi tu wamebaki huko CCM. Wakishaondoka kwenye chama hatua za kisheria inabidi zifuate. Lazima warudishe hela zote walizopata kwa njia za ujanja ujanja.
ni kweli mkuu, wa-TZ tuc jejisahau, mpira(wa miguu) ni dakika tisini, hapa tumefika dk kama ya kumi tu. kazi bado mbichi hii na kipute ndo kwanza kimetulizwa kunako dimba. Aluta continue mpaka mafisadi yote yafikishwe mahakamani na warudishe pesa zetu. Yaone kwanza haya mafisadi wahedi...!!! yanakula mavyakula yanayotuibia sisi mafukara, yanavimbiwa na yanajamba mpaka yanatapikia juu ya viatu vyetu sisi mafukara...pimbafu kweli haya!!!
 
Hotuba nzuri, but hii kitu' wazee wangu' amerudia sana ,imeniumiza kichwa next time kuwa muungwana Rostam tumia mara moj au mbili hivi
 
Je wajua siku bwana Rostam Aziz anajivua gamba muheshimiwa JK alikua wapi? basi kwa sisi tulioko kanda ya kaskazini mkoa wa Arusha mimi nilikua niko kwenye mbuga za wanyama Serengeti niko na watalii wangu tunaangalia chui pamoja na simba ndipo kwenye kuangalia kundi la simba na chui tulikua pamoja na muheshimiwa JK tukijivinjari huku bwana Rostam akiwa Igunga na wananchi wake waliompigia kura siku anajivua gamba, nahisi kujivua gamba kwa bwana Rostam Aziz sio kwamba JK alikua hajui ni nini kinaendele hapana hawa watu walishapanga mpango mzima wa kuwahadaa wananchi kwa bwana Rostam kujivua ubunge pamoja na nyadhifa zote CCM lakini eti atabaki kama mwanachama tu! Mimi nasema haitoshi kama kweli hapendi siasa uchwara basi arudishe na kadi ya uanachama hapo tutamuelewa. Nawasilisha.
 
Sasa wewe ulitaka aende msikitini kuombeleza? Topic uharooooooo
 
Mkuu huo ulikua ni mpango. rostam azizi kwa manemo yake mwenyewe kasema barua yake ya kujiuzuru kamkabidhi mwenyekiti wao wa chama!
 
Wewe binafsi ulitaka awe wapi wakati Rostam anjiuzulu? R ni Mtanzania kama Watanzania wengine, hivi kuna utaratibu gani wa kuwepo rais mahali fulani wakati mbunge ye yote anapojiuzulu?
Sio lazima ajiuzulu uanachama wa CCM kwa ajili ya siasa uchwara iliyopo Tanzania, siasa inahusu Watanzania wote hata kama sio mwanachama wa chama cho chote.
 
Back
Top Bottom