Rose Manfere, Mshindi wa taji la Miss Tanzania 2020

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,881
1,850
Mashindano ya taji la Miss Tanzania kwa mwaka 2020 yamefika tamati leo tarehe 5/12/2020 na Mshindi wake kutangazwa kutokana na maoni ya majaji na wapiga kura. Jina lake anaitwa Rose Manfere na namba yake ya ushiriki ilikuwa ni namba 14. Huyu ndiye ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Miss world huko Brazil. Kwenye historia ya mataji ya Miss Tanzania, Ukitoa lile la Miss Tanganyika aliloshinda mzungu mmoja wa kikoloni, huyu anakuwa ni Miss wa 24 tangu mwaka 1964. Baadhi ya picha zake.

1607223251118.png
1607223108536.png
1607223280109.png
rosey_manfere_20201206_1.jpg
rosey_manfere_20201206_2.jpg

Orodha ya Mamiss waliomtangulia huku ikiambatana na mwaka waliochukua mataji:
JinaMwaka
Theresa Shayo1967
Aina Maeda1994

Emily Adolf​

1995
Shose Sinare1996
Saida Kessy1997
Basila Mwanukuzi1998
Hoyce Temu1999
Jacqueline Ntuyabaliwe2000
Happiness Magese2001
Sylvia Bahame2003
Faraja Kotta2004
Nancy Sumari2005
Wema Sepetu2006
Richa Adhia2007
Nasrin Karim2009
Miriam Gerald2009
Genevieve Emmanuel2010
Salha Israel2011
Brigitee Alfred2012
Happiness Watimanywa2013
Lilian Kamazima2014
Diana Edward2016
Queen Elizabeth Makune2018
Rose Manfere2020

Video inayoonesha Rose akitangazwa ushindi wa Taji la Miss Tanzania 2020.

 
Hivi hili shindano bado lipo?
Mbona halisikiki?
Sikuwaza kabisa kama kuna hilo shindano mpaka nilipoona hii thread hapa JF.
Kuna kitu hakipo sawa.
 
Niko Tingetinge nataka kirikuu nielekee upande upi maana naona nazurura sipati kitu
 
Back
Top Bottom