MpigaKura
JF-Expert Member
- Jan 25, 2007
- 384
- 101
Ron Paul: Marekani haiiwezi kivita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran |
Pia amewataka viongozi wa Marekani waache uadui wao dhidi ya Tehran na watafute njia za kidiplomasia kuamiliana na Iran. Vile vile amevilaumu vyombo vyahabari vya Marekani kwa kuwatangazia habari za uongo wananchi wa nchi hiyo kuhusiana na lengo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran la kufunga Lango Bahari la Hormuz. Amesema, vyombo vya habari vya Marekani havipaswi kupiga makelele ya kiuchaguzi dhidi ya Iran na kusema kuwa baadhi ya habari zinazotangazwa na vyombo hivyo kuhusu lengo la Iran la kuanzisha vita dhidi ya Marekani kupitia kufunga Lango Bahari la Hormuz, hazina ukweli. Vile vile amekumbushia jinsi Marekani ilivyovamia Iraq kwa kutegemea taarifa za uongo za kuweko silaha za mauaji ya umati nchini humo na kuvitaka vyombo vya habari vya Marekani visiwapotoshe wananchi wa nchi hiyo. Hivi karibuni pia Paul anayewania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican cha Marekani alisema kuwa Iran si tishio, tofauti na jinsi vyombo vya habari vya Magharibi vinavyojaribu kuwaonesha walimwengu. |