Ron Paul: Marekani haiiwezi kivita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

MpigaKura

JF-Expert Member
Jan 25, 2007
384
101
Ron Paul: Marekani haiiwezi kivita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
ron-paul_republican.jpg
Ron Paul anayewania kuteuliwa na chama cha Republican cha Marekani kugombea urais nchini humo amesema kuwa, Washington haiiwezi kivita Tehran na haiwezi kugharamia vita kati yake na Iran.
Pia amewataka viongozi wa Marekani waache uadui wao dhidi ya Tehran na watafute njia za kidiplomasia kuamiliana na Iran.
Vile vile amevilaumu vyombo vyahabari vya Marekani kwa kuwatangazia habari za uongo wananchi wa nchi hiyo kuhusiana na lengo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran la kufunga Lango Bahari la Hormuz.
Amesema, vyombo vya habari vya Marekani havipaswi kupiga makelele ya kiuchaguzi dhidi ya Iran na kusema kuwa baadhi ya habari zinazotangazwa na vyombo hivyo kuhusu lengo la Iran la kuanzisha vita dhidi ya Marekani kupitia kufunga Lango Bahari la Hormuz, hazina ukweli.
Vile vile amekumbushia jinsi Marekani ilivyovamia Iraq kwa kutegemea taarifa za uongo za kuweko silaha za mauaji ya umati nchini humo na kuvitaka vyombo vya habari vya Marekani visiwapotoshe wananchi wa nchi hiyo.
Hivi karibuni pia Paul anayewania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican cha Marekani alisema kuwa Iran si tishio, tofauti na jinsi vyombo vya habari vya Magharibi vinavyojaribu kuwaonesha walimwengu.
 
Where is the source? Hata Obama naye alikuwa hapendi vita, ila waliomuweka madarakani ni wale wale wapenzi wa vita. Soko lao linapatikana kama kunatokea vita
 
ukiwa rais wa usa,swala la vita huwezi likwepa
huyu anazungumza kwa kuwa yupo nnje ya system
 
Kwa namna moja ama nyingine yuko sahihi,
Lakini je, Inawezekana kweli kutafuta suluhu ya kidiplomasia na Iran?
Manake uzoefu unaonesha kuwa Iran siyo tishio kwa Marekani bali kwa Israel,
Je Marekani atakubali kuona Rafiki yake mkuu Israel akiishi kwa wasiwasi kwa sababu ya Ki Iran?
 
Huyo amekosea, hawezi kupata kura kwa wamarekani. Anapoteza tu muda wake, na ninadhani mpaka sasa alishafahamu ndiyo muda wake wa kutoa pumba zake maana hakuna atakaye msikiliza hapo baadaye.
 
yaaani huyu kishashindwa uchaguzi rais gani muoga kama kafulila anakimbilia kupiga magoti
 
Jamaa anakosea kuifananisha kijeshi Iran na America! anatafuta kuungwa mkono no waislamu na waarabu lakini anasahau kwamba idadi yao still ni ndogo sana! Mwamuzi wa mwisho mpaka sasa ni Beijing, kama wakiiunga mkono USA, basi Tehran lazima ishuhudie kitimtim
 
Huyu babu mnamdharau uliza matokeo ya hivi karibuni masaa machache yaliyopita hapo New Hampshire kashika nafasi ya ngapi,babu ana msimamo mkala sana toka wamzo wa kampeni kuhusu uchokozi chokozi wa marekani,na anasema marekani iache kuidekeza israel na kuingilia ingilia kila ugomvi wa israel,iiache israel isimame yenyewe kwa kuwa ina uwezo na pia haifanyi biashara yeyote na israel so haoni sababu ya kujipendekeza kwao!

Ron Paul Educates Rick Santorum on Iran During Ames Iowa Debate - YouTube
 
Hivi wewe kweli unadhani huyu babu kwa miujiza awe rais wa Marekani unafikiria anaweza kuyafanya hayo anayoyasema majukwaani....Thubutu yake!.
 
Back
Top Bottom