Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

kuna wakati niliweka uzi humu kuhusu shida ya maji rombo,lakini sikueleweka.kwa kweli kwa mfano kata za mmomwe,kiraen,un'goro,talaha,na nyingine nimezisahau majina kama sio mradi wa masister wa kiraeni parish basi wananchi wa maeneo hayo wangeathirika kupita kiasi.walio maeneo hayo ni mashahidi kuwa hawakumbuki siku mabomba ya maji ya kiliwater yalitoa maji.nilifikia kuhoji kama kuna serikali iliyohai w.rombo.sasa kwa hali hiyo kuna ubaya gani warombo wakihamia kenya ambapo huduma za nyanya,vitunguu,mboga za majani na matunda kwa sasa warombo hupata kutoka kenya.
 
Mkuu mimi nakubaliana na wewe....Kwanza tukubaliane kwamba Kama kweli hili tukio limefanyika basi ni Uhaini...
Pili Kuna njia nyingi amabazo ni halali kikatiba amabazo Mtanzania anaweza kuzipitia kufikisha Malalamiko(Maoni).....

Anaweza Kuandamana...anaweza Kufungua Kesi....na mengineyo.....

Lakini Huwezi kufikisha ujumbe kwa Kupandisha bendera ya nchi JIRANI....Huku ni kujidharau na kudharau Wa-Tanzania wengine ....

Nimewahi kuishi na Wakenya ...Ki ukweli Wakenya wana dharau ya Hali ya juu kwa wa-Tanzania,Lakini walikuwa wanakoma Na mimi....

Wa-Tanzania ambao Hawapati huduma za kijamii ni wengi sana.....Kila pande za nchi hii kuna watu wanataabika kuhusu Hospitali,Wajawazito wanakufa Barabarani ,watu hawapati maji ya kunywa ...watu hawana hela ya kununua dawa...shule hakuna...chakula cha Tabu.....

Je hawa wote wapandishe Bendera za Kenya ?
Mimi nimesikia Kuwa Huko kilimanjaro(Rombo) Kuna Maendeleo Kuliko Sehemu nyingi za Tanzania....
Je Wana-Rombo wana Haki zaidi ya Kupandisha Bendera ya Kenya Kuliko Wa-Tanzania wengine ?

Mimi Naunga Mkono harakati zote za Kujiletea Maendeleo...Lakini Siungi Mkono kupandisha Bendera ya nchi Nyengine
Especially Kenya ... angalu wangepandisha ya Rwanda ningeweza Kuvumilia..lakini Kenya...Hapana..Hapana

Mkuu Tangu Mwanzo nilisema siungi mkono kupandisha bendera ya Nchi nyingine

Pia serikali ikome kuwanyanyasa wananchi wa Rombo
 
Wa Rombo wapuuzi wakubwa.Wakenya wenyewe wanataka kuwa watanzania kukimbia njaa.Kwani lazima munywe chai,si nyinyi huwa munakunywa uji wa ndizi?.
Yaani kukosa sukari tu munakimbia nchi.si watu wa kuaminika hata kidogo.Ndio nyinyi munaobadili dini na vyama kwa kuhongwa vitu vidogo kama pombe na mitumba.Poleni sana warombo.

we huna tofauti na (SHIBUDA)
 
Ni jambo zuri kuwaua akina CCM kuliko kuhama nchi eti kwasababu ya huduma maana serikali bila wananchi haipo sasa Baba akimkimbia mtoto ujue huyo baba hatoshi kuwa baba maana baba anayestahili humchapa mtoto huyo mpaka atii sheria ndo humuacha sasa ninyi warombo mbona mnakimbia tatizo halafu mnakwenda kwenye matatizo zaidi?
 
Pengine watu hawajui kuwa kilimanjaro ilishwahi kuwa na rais wao, kma si Marealle kuvuruga mambo wachaga wangeweza strike deal na Nyerere na kuwa na muungano kama Zenj.Rais wao alibadilishwa kuwa waziri wa elimu.Sijui mnashangaa nini hapa?Alichoharibu Marealle kikamaliza power ya local authority ya Wachaga, na ndipo pakawa na mpango madhubuti wa kuwabana wachaga.Sikushagaa sana kauli za akina Rizwan na mwenyekiti wa Vijana wa CCM pwani kusema waliyoyasema.

Mwenye macho taona kwanini sera za dar zenye baraka za dodoma ni maalumu kuwamaliza wachaga.sasa si kuchelewesha maendeleo ya nchi.NImekuwa nikisema haya sana humu ndani watu wakaniona kuwa ni extremeist wa kichaga na mbaduzi mkubwa.
 
Lini Chadema mtatangaza rasmi taifa lenu la Kaskazini.
 
Lini Chadema mtatangaza rasmi taifa lenu la Kaskazini.

Acha uhuni wewe,CDM ingehitaji hilo ingefanya kama CUF au Chama cha Mzee wa mapesa kule kanda ya ziwa hana haja ya kupanua chama.CDM hawajawahi sema kam Maalimu Zanzibar Huru.
 
kuna njia mbalimbali kuonyesha watu wameichoka serikali yao. sehemu ambayo bendera huruhiwa kupandishwa mathalani ya mataifa mengine ni ktk balozi tu. ikitokea hapo inamaanisha tayari eneo hilo limetwaliwa na kenya kama yale yaliyotokea enzi za idd amin kule kagera.

Ushamba tu hao waliopandisha bendera
 
Wa Rombo wapuuzi wakubwa.Wakenya wenyewe wanataka kuwa watanzania kukimbia njaa.Kwani lazima munywe chai,si nyinyi huwa munakunywa uji wa ndizi?.
Yaani kukosa sukari tu munakimbia nchi.si watu wa kuaminika hata kidogo.Ndio nyinyi munaobadili dini na vyama kwa kuhongwa vitu vidogo kama pombe na mitumba.Poleni sana warombo.

Ahsante sana mkwe.re. Ila sisi si wapuuzi kama wewe na maanko zako. Tutake radhi.

Karibu sana Jamhuri ya watu wa Rombo.
 
dawayao ni kunyolewa na kuchomwa mikuki tu wasipoteze watu muda vibaraka hao

Kuna tofauti ya watu wanataka wawe huru kuleta maendeleo na watu wanaotaka kuwa huru ili wapewe bure zaidi au kutishia watu wazidi wapa bure.Tanzania inawachelewesha na kuwapa msoto warobo bure.Ni kama mtu nayemwaga mboga yako ikiwa jikoni, na kukufanya ulale njaa kama yeye ambaye hana chakula.
 
Acha uhuni wewe,CDM ingehitaji hilo ingefanya kama CUF au Chama cha Mzee wa mapesa kule kanda ya ziwa hana haja ya kupanua chama.CDM hawajawahi sema kam Maalimu Zanzibar Huru.

Mbona unapingana na Mbunge wenu Nassari alisema wataanzisha taifa la kaskazini unaogopa nini.
 
Poleni wana Rombo. Sitetei manyanyaaso na shida mnazozipata,lakini kulikimbia tatizo si utatuzi wa tatizo.Kenya kuna maeneo hawana unga kabisa,je nao wapandishe ya Tanzania?
 
Mbona unapingana na Mbunge wenu Nassari alisema wataanzisha taifa la kaskazini unaogopa nini.

Bahati mbaya unaongea desire za watu na si sera za au msingi wa CDM.Kwa mwenye kujua jinsi gani TANU na CCM ilivyorudisha mkoa makusudi nyuma, mipango ya siri ya kuwarudisha wachaga nyuma na kauli za wazi za wana CCM kuwa wachaga na wenzao wa Kaskazini hawastahili ongoza nchi.Hatosita kusupport au kufikiri kuwa na taifa la kaskazini ikibidi.Kilimanjaro iliwahi kuwa na rais aliyeishia fanywa waziri wa Elimu na Nyerere.Sasa Cha ajbu nini?Mbona unasupport Zenj?

Nchi sipobadilika hata mimi nitafurahi kuota hivyo,ila kwa sasa napigania utanzania.
 
Kuna tofauti ya watu wanataka wawe huru kuleta maendeleo na watu wanaotaka kuwa huru ili wapewe bure zaidi au kutishia watu wazidi wapa bure.Tanzania inawachelewesha na kuwapa msoto warobo bure.Ni kama mtu nayemwaga mboga yako ikiwa jikoni, na kukufanya ulale njaa kama yeye ambaye hana chakula.

uhuru wakupika gongo na mbege wakauze Kenya ???? ni bakola tu wakizidi jaziba wanakula mikuki
 
Rombo mnataka kutanganza uasi mnataka kuwa Wakikuyu, kaeni mkijua Jeshi letu JWTZ lipo kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi yetu msije mkalalamika kuwa Jeshi limetumia nguvu kubwa kuwasambaratisha wanarombo.
 
uhuru wakupika gongo na mbege wakauze Kenya ???? ni bakola tu wakizidi jaziba wanakula mikuki

Wewe usifananishe mbege na gongo wala pombe zenu huko.Jk akipewa offer ya kuchagua pombe ya kuwakilisha nchi atakimbilia mbege.Mbege inanyweka sehemu Kibuku haingii.

Sasa wa kuchapa bakora nani?waliogomea sensa au wanaotaka chukua jukumu la kujiletea mendeleo?Siasa mbaya na mipango ya hila ya CCM inawalazimisha walale njaa kama walalavyo wavivu,tena wavivu wanalishwa kwa vijiko.Warombo wanaweza nunu sukari popote na kuifikisha kwao,CCM wanaizuia,kama wanazuia isiende kenya si wangakaa mpakani?Uzembe za kufikiri wa waliokaa dar kwa uhalali wa ndiooo za dom ni mauaji nchini.

CCM imefikia mwisho wa kufikiri kilichobaki ni kuharibu tuu fikra.
 
dawayao ni kunyolewa na kuchomwa mikuki tu wasipoteze watu muda vibaraka hao

Wananchi wa Rombo ni watanzania.Huu ubaguzi wa kipuuzi mnaouonyesha hapa unaonyesha ni jinsi gani tuna watu wenye ufinyu wa mawazo

Rombo ni halmashauri inayojiongoza kwa ufanisi.Ni wapenda maendeleo ndiyo maana ni wapenda mabadiliko tofauti na wengine walioko mjini hawajui maana ya mabadiliko ni nini

Mwananchi wa Rombo siku zote yuko proud na anajiskia fahari kufanya kazi kwa bidii

Wanapenda haki zao na hawapendi kunyanyaswa.Ingawa siungi mkono kupandisha bendera lakini ninawapongeza kwa kuwa na msimamo thabiti katika kutetea haki zao na mabadiliko

Mramba alijinasibu amejenga barabara lakini kutokana na dharau zake na kutowathamini walimpiga chini.Ingekua ni majimbo mengine wangeweza kumtangaza mbunge wa kudumu
Rombo hatuna urafiki wa kudumu,tuna maslahi ya kudumu katika maendeleo

Nitoe wito kwa wananchi wote wa Rombo na hasa vijana,tuendelee kupambana na tusapoti maendeleo ya jimbo letu
 
Back
Top Bottom