Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

Zed

JF-Expert Member
Mar 28, 2009
435
257
Baada ya kunyanyaswa na vizuizi vya polisi vilivyomo mji mdogo wa Himo, viliosababsha upungufu mkubwa wa sukari na bidhaa nyingine za chakula, kiasa cha Rombo jimbo linaloongozwa na CDM, na linalopakana na nchi ya Kenya, kujisiakia wageni nchini mwao Tanzania, wamechukizwa na kitendo cha serikali yao ya Tanzania kuwanyanyapaa na wameamua kupandisha bendera ya Kenya! Source ITV
 
Hata kama viongozi wa nchi hii watafanya upuuzi kiasi gani, nitapoteza fahari yote lakini sio utaifa wangu

Kuna haja ya kuusoma waraka wa Lema kwa umakini na kuutendea kazi....KURUDI KWENYE MISINGI YA UTU NA UTAIFA WETU
 
Baada ya kunyanyaswa na vizuizi vya polisi vilivyomo mji mdogo wa Himo, viliosababsha upungufu mkubwa wa sukari na bidhaa nyingine za chakula, kiasa cha Rombo jimbo linaloongozwa na CDM, na linalopakana na nchi ya Kenya, kujisiakia wageni nchini mwao Tanzania, wamechukizwa na kitendo cha serikali yao ya Tanzania kuwanyanyapaa na wameamua kupandisha bendera ya Kenya! Source ITV
mbunge wa rombo ****** matupu
 
ehe safi kabisa je serikalli inasemaje katika hili, i love the confidence and the daring that some Tanzanians have.
 
kuna njia mbalimbali kuonyesha watu wameichoka serikali yao. sehemu ambayo bendera huruhiwa kupandishwa mathalani ya mataifa mengine ni ktk balozi tu. ikitokea hapo inamaanisha tayari eneo hilo limetwaliwa na kenya kama yale yaliyotokea enzi za idd amin kule kagera.
 
Hiyo bendera itasaidia kupata sukari.

Usiwe unaaandika kwa kukurupuka wewe Kibaraka wa CCM!! Unajua taabu ya sukari kule Rombo wewe.

Unajua kilo moja ya sukari sasa hivi kule Ni shilingi Ngapi. Jaribu kufuatilia mambo ndio uandike Upupu.

Yaani wewe kwasababu ni mwana CCM hutaki kusikia mwananchi akilalamika Matatizo yake.

Jaribu Kutumia Kichwa angalau.

Kwa kupandisha hiyo Bendera serikali yenu sasa itatambua the seriousness of the situation.

Sishabikii kupandishwa Bendera ya Kenya. Ila nafurahia kuwa Hii serikali ya CCM itaona kule kule kuna tatizo.

Tafuta Sehemu nyingine ya kuwatetea magamba. lakini sio katika matatizo yetu.

sawa wewe unayejiita Mzee asiye na hekima?
 
Hata kama viongozi wa nchi hii watafanya upuuzi kiasi gani, nitapoteza fahari yote lakini sio utaifa wangu

Kuna haja ya kuusoma waraka wa Lema kwa umakini na kuutendea kazi....KURUDI KWENYE MISINGI YA UTU NA UTAIFA WETU

Kweli mkuu hilo ni muhimu sana hasa viongozi wetu
 
Conspiracy za ccm dhidi ya wat wake. Kwa nini kiwekwe kizuizi Himo?? Kwani himo ni mpakani? Wangeweka kule tarakea na holili. Hawa watu nashindwa kuwaelewa, Hivi wana akili hizi za kawaida za binadamu au ni za kuku. Logically ukizuia sukari himo watu wa rombao wanakosa hiyo bidhaa. Ahh hawa watu watakuwa wametoka sayari ya Jupiter
 
Ingawa siungi mkono kitendo cha kupandisha bendera ya nchi nyingine,lakini serikali ya Tanzania ndiyo imewafanya wananchi wakafikia huko.Sukari imezuiliwa Himo bila kujali kuna Eneo lingine la Tanzania mbele ya Himo linaloitwa Rombo.

Rombo inastahili haki zote kama wananchi wa maeneo mengine.Kwa muda mrefu rombo imekuwa ikikandamizwa na kudharauliwa na watawala wetu,sijui ni kwa nini hasa.

Mkuu wa mkoa ameshindwa kuweka mkakati wa kutosha kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hii wakati huo huo akidhibiti magendo.Ni kwa nini maeneo mengine yaliyopakana na nchi jirani wameweza kudhibiti hali hii bila kubughudhi wananchi ndani ya territory yake halafu mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ashindwe.Madiwani wa CCM ndiyo wanaoongoza halmashauri hivi kweli wanashindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kuweka ukaguzi katika usambazaji wa sukari kuanzia Himo,Mwika,Mamsera,Mkuu,Mashati,Useri na Tarakea? ni kwanini tusiweke logistics katika level yenye uwajibikaji wa kisiasa kama kata kisha nadharia ya monitoring and evaluation ikatumika?

Wananchi wa Rombo hata katika ugawaji wa Mahindi ya misaada madiwani wa CCM na wenyeviti wa vitongoji walitaka watu waonyeshe vitambulisho kwanza yaani kadi za CCM ndiyo wagawiwe.Nina ushahidi wa majina ya watu wasiojiweza kabisa hawakupewa mahindi,na pia hujuma iliyotumika kudhulumu watu waliostahili kupewa mahindi hawakupewa.Nimeorodhesha malalamiko na ushahidi wote ukajadiliwe kwenye vikao vya baraza la madiwani walifanyie kazi watoe ripoti kwa wananchi wa Rombo

Wananchi wa rombo wanatia huruma kwa jinsi wanavyobambikiwa kesi na watendaji wa serikali,ni ukandamizaji uliopitiliza.Kulikuwa hakuna vituo vya polisi na hata vilivyopatikana vinatumika kama tools za kutisha raia na kujipatia hela.Mojawapo ni kesi iliyomuhusu mwananchi mmoja anaitwa Aristariki Kimaryo aliyewekwa mahabusu na mtoto wake pamoja na mkwe wake kituo cha polisi Mashati kisa hawajatoa hongo ya kumnusuru mtoto wake,hivyo polisi wakaamua kuwasweka mahabusu.Tulipowahoji polisi sababu ni nini wakaishia kutoa vitisho hadi tulipotishia kutumia nguvu ndipo walipowaachia

Tembo wanaotoka nchi jirani wamekuwa wakivamia mashamba ya wananchi,wakiharibu na hata kuuwa watu lakini hakuna fidia ya maana iliyofanyika.Wanachi wa Rombo sasa inabidi kwa ruthless,wanyama wanaoingia kwenye mashamba inabidi wauwa na hakuna kutoa taarifa kwa idara ya maliasili,wauawe na pembe ziuzwe hela iingizwe kwenye akaunti maalumu ya kufidia walioathiriwa na wanyama hao

Leo hii watu wanawalaumu watu wa Rombo kwa kujiskia sehemu ya kenya bila kufikiria saikolojia iliyowaathiri ya muda mrefu.Huduma za kijamii na kiuchumi zimekuwa attached na wakenya.Hata Radio ya Taifa TBC haifiki kule badala yake KBC ndiyo inasikika sijui kama watu walioko Tunduma,Songea na kigoma wanasikiliza redio za Zambia,malawi,msumbiji au DRC kuliko TBC au ni Rombo peke yake?

Sasa serikali itende haki,mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,madiwani pamoja na Mbunge wa Rombo simamieni maslahi ya wananchi wa Rombo.Serikali iache vitisho,iache kuwatisha wananchi wa Rombo.

 
Wananchi wa Rombo wamechoshwa na minyororo ya utumwa nchini mwao sasa wanachokifanya nikujitambua na ni haki yao kuchagua kuwa wananchi wa Kenya kwani hiyo mipaka aliyeiweka sini mkoloni ata bila ya kuwashirikisha warombo.Mtasikia siku chache na sisi tunapandisha ya nani
 
Hata kama viongozi wa nchi hii watafanya upuuzi kiasi gani, nitapoteza fahari yote lakini sio utaifa wangu

Kuna haja ya kuusoma waraka wa Lema kwa umakini na kuutendea kazi....KURUDI KWENYE MISINGI YA UTU NA UTAIFA WETU

na kweli..tuwe wazalendo jamani..
 
Naunga hoja mkono! Acha wapandishe tena ingewezekana na wafanye mchakato ya kwmb huduma zote ya kuanzia za afya wapate huko.
 
Hongera wamethubutu na wemeweza waendelee mkono wa heri upo mikononi mwao
 
mbunge wa rombo ****** matupu

Tatizo siyo Mbunge, tatizo ni JK na serikali yake. wameamua kuwanyanyasa wananchi waliowachagua wabunge wa chadema, na rombo ni mojawapo.
Arusha ni moja ya majimbo yanayonyanyaswa na serikali ya Vasco da Gama
 
Back
Top Bottom