Roma, Wakazi na Linex ni mfano wa watu waliopishana na vipaji vyao!

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
Awa ni watu walio kwenye muziki muda mrefu lakini kiuhalisia sio wasanii. Wanaupenda sana muziki lakini hawakuzaliwa kuwa wanamuziki.

1. Roma
Huyu jamaa ana kipaji chake ambacho uwa nikimsoma twitter nakiona. Mshikaji ni content creator wa level kubwa sana alafu ni ile natural sio wa darasani. Aina hii ya kipaji uwa kujipata ni ngumu kwa dunia ya tatu ila Roma ukimuweka nyumba yoyote ya ubunifu wa maudhui ni pesa. Muziki kiukweli mshikaji anafosi tu sio sehemu yake na watu walimpa sikio sababu ya content zake sio ile sanaa ya muziki. Akiweka uko nguvu ataiona pesa mara 10 ya muziki anaoukomalia.

2. Wakazi
Huyu ni msanii ambaye kama juhudi ndio njia ya kupata mafanikio basi angekuwa zaidi ya kina Rayvanny. Anapenda sana muziki especially hip-hop ila kipaji chake huko ni kidogo ni jambo ambalo amekuwa akili-deny lakini atakuja kubali baadae sana. Huyu ana talent ya kuanzisha mijadala, kufanya presentation na kuchimbua vitu visivyo zungumzika. Angekuwa anachukua ushauri wa wenye akili angeamia kwenye utangazaji haswa niche ya controverse ni ndani ya miezi mitatu atakuwa ni talk of the town. Ile attention wanampa twitter itaaamia mtaani.

3. Linex
Huyu dogo wa Kigoma angestaafu kuimba aamie kwenye kipaji chake halisi cha kuongea. Jamaa ni muongeaji mzuri na sehemu anayofiti zaidi ni mapenzi. Anaweza kuwa vyote mtangazaji wa vipindi vya mapenzi na mtoa mada kwenye events za mahusiano. Sijamfollow sehemu yoyote ila uwa nakutana na clip zake au screenshots akizungumzia mapenzi naona kabisa huyu anapishana na hela. Duniani hakuna niche inayouza kama mapenzi kuna hela za kutosha.

Nikipata time nitanzungumzia Vannila wa Ali Kiba pia.
Acha nirudi kwenye maokoto sasa.
 
Chukua hii toka kwangu "Mziki ni bidhaa ukiona wewe haikufai/haifai basi kuna watu inawafaa, fashion ngapi zinatoka na wewe hujapenda kununua?,au vingapi vimetoka pia wewe umependa na ukaamua kununua mfano hiyo simu yako hapo.

Ila Asante Kwa ujumbe wako watapita hapa na wataona kama itawafaa watakujibu ila binafsi nimekupa kutoka kwangu.
 
Na huyu je?👇
jamiiforums1267461471_387x387-jpg.2572374
 
Napingana/natofautiana na wewe kwa Roma, of course he is very natural when it comes to content creation lakini hip hop inahitaji sana watu wa aina hiyo na mashairi yake huwa yanadhihirisha hilo. He is a great story teller and hip hop is such an ideal platform for doing that.
 
Chukua hii toka kwangu "Mziki ni bidhaa ukiona wewe haikufai/haifai basi kuna watu inawafaa, fashion ngapi zinatoka na wewe hujapenda kununua?,au vingapi vimetoka pia wewe umependa na ukaamua kununua mfano hiyo simu yako hapo.

Ila Asante Kwa ujumbe wako watapita hapa na wataona kama itawafaa watakujibu ila binafsi nimekupa kutoka kwangu.
Hata wakipita, yule dada WAKAZI atabisha tu
 
Linex nakukatalia huyo jamaa anajua Sana. Ana uandishi fulani wa kipekee kwenye mapenzi anafanya vizuri Sana.
Linex ni kichwa kwenye utunzi na sauti yake ipo natural and soulful, habani pua na pia ni aina ya waimbaji ambao wana uwezo wa kuongea na hisia za mtu kiasi kwamba hata akiamua kuimba gospel atatoboa

Kuna soundtrack ya Juakali series inaitwa Kaa nami, ni wimbo uliopo katika tenzi za roho. Ukiacha undisputed version ya Angela chibalonza, ya Linex inafuatia kwa maoni yangu
 
Ndio wafanye kitu kitachowalipa. Hawana vipawa kwenye music ni wakawaida wanafosi.
Dah.. hivi Mkuu unajua mziki vizuri kweli? Huyo Wakazi sijawahi kumfuatilia, hata ukiniuliza kaimba wimbo gani sijui kwakweli, ila kwa hao wawili uliowataja.. hao ni Wanamziki parceee... sio wasanii, ni MUSICIAN...
 
Back
Top Bottom