Roho nzuri inalipa, aliyetumiwa milioni 54 apewa laki 2 kama "ZAWADI NONO"

Mimi ningeziacha hizo hela mpaka pale watakapozitoa wao wenyewe. Na kama uwezekano wa kuzitoa haupo, basi hiyo ingekuwa ni halali yangu.

Kitendo alichokifanya huyo jamaa siyo cha kishujaa! Huo ni uzwazwa.
 
Angeajiriwa zimamoto, hana tofauti na Majaliwa aliyetoboa ndege kwa kasia, maji yaingie ndani ya ndege ili aokoe raia. Wote ni mashujaa....
 
Pesa kwakua haikuwa yake hiyo laki 2 ni sawa tu.hatujui mtumaji alikua anatuma wapi na kipato chake ni kipi.angezichukua ni wizi pia
 
Angejichanganya akosee kutuma kwangu,, yaan naenda kwa wakala natoa,, narudi home naacha kila ktu kuanzia smu, lain, vitambulisho vyangu vyote,, vyeti vyangu vyootee, nguo zangu zote,,,, kasoro nlizovaa. Natafuta nguo zlizochoka choka,, raf rafu nazivaa, chini napiga kandambili,, natafta kibeg cha mtumba chenye muonekano duni afu nazijaza zle hela,, napanda basi/lori natokomea kuskojulikana bush vijijini huko,, naenda ishi kwa jina lngne, nabadlisha mpaka muonekano kama nlikua nafuga ndevu basi nakua nakwangua zoteeeee!!
 
Unafungwa kwa makosa yapi?
elezea kisheria zaidi.

Pascal Mayalla ,, mfalme wa jukwaa la sheria
Mkuu ukikuta pesa imezidi au kupungua kwa account yako toa taarifa kwa mtoa huduma wako,unamkumbuka yule bwana aliyeenda kutoa pesa benki,nadhani ni Dar es salaam ,lengo la bwana yule lilikuwa kutoa laki mbili,lakini kwa bahati mbaya ATM ilikuwa mbovu ikaanza kutema pesa mfululizo hadi 11M naye kwa kujiona mjanja akazichukua,bwana yule alifungwa nadhani zaidi ya miaka miwili kwa kosa la wizi na kutokuwa mwaminifu!!.


Pesa iliyo katika mfumo wa kimtandao haipotei kizembe,kuwa mwaminifu mkuu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom