Roho mbaya ya korosho isikie tu. Hadi jeshi limeshindwa

Naogopa sana kukomenti kwenye mambo ya jeshi. Mnamkumbuka yule mwandishi alieandika kuhusu kifaru cha jeshi?
 
Mwenyewe si anajiita mwanamahesabu, sasa alishindwaje kupiga hesabu za haraka kutambua gari 75 za jeshi zinazobeba Tan 30 kila moja zitamaliza kwa muda gani kusomba Tani laki 2.. Hapo tuna consider other things should remain constant..

Uhalisia ni wakati wa msimu, zinahitajika Lori zaidi ya mia 4 kumaliza kusomba korosho ndani ya muda tarajiwa kabla mvua havijaanza kunyesha. Sasa Mvua ndio zinaanza kuchanganya, miundombinu ya huko vijijini barabara zitashindwa kupitika na korosho kuharibikia kwenye maghala ya vyama vya msingi. Mpaka sasa tayari kuna korosho zimeshaanza kuota, hivyo hazibanguliki tena..

Wakati mwingine ni vizuri kushirikisha wadau na si kujiamria eti sababu tu we ni muhimili uliojichimbia chini zaidi. Serikali kuamua kununua korosho hata waziri mkuu hakuwa anajua, alishtukizwa tu. Na inawezekana alijiamlia tu kimuhemko na vile hapendi kuwa challenged hakuna aliyethubutu kumbishia. Yetu macho...
 
Baada kuwang'oa akina Charles wawili ( waziri wa kilimo na yule wa viwanda). Naona korosho ina mpango wa kuondoka na mkuu wa operesheni korosho.

Maana haingii akilini jeshi limpe taarifa za uongo amiri jeshi mkuu kwamba wanaweza kusomba korosho zote na kuzibangua hata kwa meno, halafu wiki 2 baadaye wanaomba poo.

Hapa kichwa cha mkuu wa operesheni kinatafutwa na roho mbaya ya korosho.

Hivi kweli jeshi mlishindwa kufanya tathimini ya kina na kisha kumpa amiri jeshi mkuu mrejesho sahihi ya kwamba kazi ya kusomba korosho ni ngumu na itawashinda?

Sasa angalia fedheha hii. Kesho itaandikwa kwenye magazeti yote kwamba "Jeshi lashindwa kukusanya korosho na kuzibangua!"
Siasa ni mtego wa kuangamiza uchumi wa mwafrika,
Anaejidai siyo mwanasiasa anafanya mambo kisiasa zaidi hata ya wanasiasa wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom