Riwaya ya Kijasusi: Mlio wa Risasi Harusini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,903
RIWAYA: MLIO WA RISASI HARUSINI
Mtunzi: Robert Heriel
WhatsApp 0693322300




>>>>>>>>>>>>>>>>>>> Episode 01 <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

Akajitazama kwenye kioo kikubwa cha kabati akiwa chumbani kwake. Kila alipojitazama hakuona kasoro yoyote katika mwili wake. Aligeuka huku na huku akiendelea kujitazama. Macho yake yalimuambia yeye ni mrembo mwenye mvuto wa viwango vya kimataifa, ni kweli wala macho yake hayakuwa yamemdanganya. Ismaiya alikuwa mwanamke aliyeumbwa akaumbika. naweza kusema alikuwa ni moja ya wanawake wazuri kuwahi kutokea katika dunia. Alikuwa na urefu wa futi sita kasoro. Mwenye umbo matata kama chungu cha kimakonde ambalo lililaza na kulewesha nyoyo za wanaume waliobahatika kumuona. Uso wake wenye macho makubwa kiasi yaliyolegea ulizidisha maradufu uzuri wake. Pua iliyochongoka huku chini yake ikipokelewa na midomo minene kiasi ilizidi kumpa kura muhimu katika urembo wake, hakuna ambaye hakutaka kumuona mwanamke kama Ismaiya akitabasamu kutokana na mpangilio mzuri wa meno yake meupe pee yenye mwanya wa kichokozi. Kichwani alikuwa na nywele fupi zilizokatwa kwa ustadi mkubwa huku masikioni kukiwa na hereni za duara. Kifua chake laini kilibeba maziwa madogo kiasi huku kiuno chake chembamba kikishikilia makalio makubwa yenye nyonga nene zilizotesa nguo aliyokuwa ameivaa. Mapaja yake laini yalimeta meta mithili ya bilauri ya dhahabu. Huyo ndiye Ismaiya binti Ndossi. Mwanamke mwenye uzuri usiyosemeka. Rangi yake ya kahawia alimaarufu kama maji ya kunde.

Pamoja na uzuri wote huo lakini Ismaiya aliuona si chochote wala si lolote. Uzuri ulikuwa na faida gani ikiwa kiberenge tuu kilimshinda. Hakuamini kabisa kwamba rafiki yake Adele angeweza kumnyang'anya mchumba wake. Sasa aliuona uzuri wake siyo kitu tena. Alijilinganisha na Adele ambaye hakumfikia kwa lolote lile. Siyo kwa sura wala kwa umbo. Siyo kwa kimo wala kwa rangi. Alimzidi karibu kila kitu. Sasa iweje Adele amnyamng’anye mchumba wake. Kwa kipi hasa. Kwa lipi hilo lililompiku mpaka Adele ampindue katika penzi lake.

"Kile kinyago cha mpabure kinanizidi kwa lipi. Msichana hana mvuto wa kumvutia mwanaume yeyote. Mtu mwembamba kama mlingoti wa kupandishia bendera. Embu cheki! Tazama mzigo huu. Embu ona " akaongea mwenyewe akijitazama kwenye kioo huku akitingisha makalio yake yaliyoshiba haswa.

’Nimetimiza vigezo na masharti ya kuitwa mwanamke mrembo, wapo wanaonifananisha na malaika, wapo wanaoniona malkia wa sheba wa kizazi hiki. Lakini iweje! Iweje Yule ngedere anipiku! Au yule kiberenge kanizidi mambo ya chumbani. Mmmh!’’ akaongea kwa sauti ya upole huku uso wake ukionyesha kukata tamaa baada ya kuwaza jambo hilo. Ni akama alikaribia ukweli.

Basi kama kuna jambo ambalo Adele alibobea ni suala la kummudu mwanaume kitandani. Adele alikuwa fundi msanifu wa masuala ya kitandani. Alijua ni vipi ammiliki mwanaume yeyote yule. Adele alikuwa na kipaji cha kukata mauno katika mkao wowote ule jambo ambalo wanawake wengi linawashinda. Kama hiyo haitoshi Adele alifuzu mafunzo ya kumdumaza mwanaume akili kwa kumpa mahaba na kumdekeza. Wapi alijifunza mambo hayo siyo mimi wala wewe, hakuna aliyekuwa anajua. Mtoto Adele alikuwa kisanga kwenye shuka na godoro. Alikuwa mwepesi kushuka katika mabonde na mito bila kudondoka.

Ismaiya akajibwaga katika kitanda kama mzigo. Alikuwa amechoka. Katika chumba cha Ismaiya kulikuwa na kabati kubwa lenye kioo. Karibu na kitanda kulikuwa na dressing table iliyosheheni vipodozi na mafuta ya kila namna. Chini lilikuwepo zulia la manyoya. Kilikuwa chumba kilichobeba choo na bafu ambacho kilisheheni vitu vilivyomtosha mtoto mrembo kama alivyo yeye. Ismaiya aliiangalia saa ya ukutani iliyoonyesha ni saa mbili kasoro, asubuhi. Kisha akachukua kadi iliyokuwa kwenye dressing table. Akaitazama kama mtu ambaye haamini. Akasoma majina yaliyokuwa kwenye ile kadi. Majina yalikuwa ni Adele kisena na Robert Gabriel. Aliposoma jina la Robert alijikuta akitoa machozi. Alikuwa akimpenda sana; Robert alikuwa mwanaume ambaye aliuteka moyo wake kikamilifu. Hakuwahi kufikiri kuwa siku moja wataachana . Hata hicho kifo chenyewe aliahidi kupigana nacho kama kingekuja kuwatenganisha. Kama alikuwa tayari kupambana na kifo sembuse mwendawazimu mmoja aitwaye Adele. Alitaka kumuonyesha Adele kuwa yeye siyo mwanamke wa kuchezewa. Alitaka kumfunza Adele kama mfano kwa wanawake wengine wenye tabia za kuiba waume au wachumba za watu.

Akanyanyuka na kuvaa nguo zake. Akashika simu yake na kubonyeza bonyeza kisha akaiweka sikioni.
"hello! Ndio natoka nyumbani" Ismaiya aliongea na mtu aliyeupande wa pili kisha akakata simu. Kama kawaida yake alikuwa amependeza mno. Alivalia suruali nyekundu iliyochora umbo lake kikamilifu. Juu alivalia blauzi ya maua ua iliyoachia sehemu kubwa ya kifua chake ambapo kulikuwepo na mkufu wa dhahabu aliouvaa shingoni. Huyo ndiye Ismaiya bhana. Binti ambaye kama angegombea umiss wa dunia angeshinda bila kupingwa.



*************************************************​



Msafara wa magari ya harusi uliowabeba Adele na Robert ulikuwa upo njiani ukiwa umefunga barabara kuelekea ukumbi wa harusi. Ulikuwa msafara wa aina yake kutokana na uwepo wa magari mengi ya gharama. Magari hayo yaliongozwa na Polisi wa barabarani.

"pipipi..pipipipi..pipipi.pipipipi.!" Ilikuwa ni honi ya magari yaliyotoa mlio uliopokelewa na ngoma na matarumbeta. Wapita njia walisimama kushangaa msafara huo wa aina yake. Baadhi ya watu waliacha shughuli zao ili waangalie msafara wa harusi ya aina yake ambao ulikuwa nadra sana kwa jiji la Dar es salaam . Baadhi ya watu wengine walikuwa wapo madirishani wakichungulia tukio hilo lililoibua msisimuko mkubwa kwa kila mtaa ulipokuwa ukipita. Adele akafarajika sana kuona mpango wake wa kuolewa na Robert umekamilika. Akachungulia dirishani akiwa ndani ya gari akaona jinsi watu walivyokuwa wakiutazama msafara wa magari ya harusi yake. Akaachia tabasamu jepesi huku akijisifu na kuona fahari kwa siku ile. Aliwaona watoto wakizuiwa na wazazi wao wasiufuate msafara wa harusi yake ili wasije kupotea. Adele muda wote alikuwa anatabasamu kwa kila alichokuwa anakiona. Hata hivyo ilikuwa ni haki yake kutabasamu. Hiyo ilikuwa ni siku yake kufurahi sasa kwa nini anune.

Alimkumbuka rafiki yake Ismaiya. Alikumbuka siku ya kwanza walipokutana chuoni wakiwa mwaka wa kwanza. Akakumbuka siku Ismaiya alivyokuja kwa mara ya kwanza akiwa na Robert ambapo alipomuona Robert moyo wake ulimpasuka. Adele alikumbuka jinsi alivyomuonea wivu rafiki yake Ismaiya kisa yupo na Robert . Bado aliendelea kukumbuka mambo mengi ambayo mengine yalimfanya atabasamu mengine yaliusononesha moyo wake. Mawazo ya Adele yalikatishwa baada ya mlango wa gari alilokuwa amepanda kufunguliwa. Tayari walikuwa wamefika ukumbini. Alijiweka sawa akisubiri maelekezo ya namna atakavyotoka. Ukumbi ulikuwa umepambwa ukapambika. Watu walikuwa wamefurika wakiwa wamependeza sana. Mbele alisimama mshehereshaji ambapo kushoto kwake alikuwepo Dj aliyekuwa akiweka muziki kuhakikisha tukio lile linavutia zaidi. Maputo yaliranda randa na mapovu yenye rangi za kupendeza ya shampoo yalikuwa hewani. Watu walikuwa wametulia tuli wakisubiri maharusi waingie ili sherehe ianze. Muziki mwororo uliendelea kupiga ukizibembeleza nyoyo za wazazi, ndugu, jamaa na wageni waalikwa waliokuwamo ukumbini. Upande wa kulia mbele kabisa karibu na jukwaa walipoandaliwa maharusi, walikuwa wameketi wazazi na ndugu wa Adele Kisena. Mama na baba yake Adele pamoja na kaka zake walikuwa wamevaa sare zilizokuwa zimewapendeza sana. Upande wa kushoto mbele waliketi wazazi wa Robert Gabriel wakiwa na ndugu na rafiki zake. Nao walikuwa wamevaa sare nzuri za kuvutia zilizokuwa tofauti na wazazi wa Adele.

Punde mshehereshaji akaagiza dj aweke muziki wa kuwaingiza maharusi ukumbuni. Kwa sauti yenye bashasha na ucheshi uliojawa na utani mshehereshaji aliwahamasisha watu wote waliokuwa ukumbini kushangilia. Hapo ukumbi wote ulitikisika na kurindima.
Bibi harusi aliingia akiwa na bwana harusi kwenye lango kuu. Macho yote yaligeuka nyuma kuwatazama. Waooh! Walikuwa wamependeza sana. Walipendeza kupita kiasi mithili ya malaika. Kila mtu alitamani aseme neno kuwasifia lakini midomo ya ikawa mizito. Maharusi wakaendelea kutembea kuelekea mbele walipokuwa wamewekewa siti zao. Adele akainua uso wake uliokuwa ndani ya shela akatazama mbele kabisa lilipojukwaa. Moyo wake ukalipuka kwa shangwe. Alijawa na kiwewe cha furaha. Aliona picha kubwa ikimuonyesha yeye akiwa kakumbatiwa na Robert . Aliikumbuka picha hiyo walipiga studio jana yake. Chini ya ile picha yaliandikwa majina yao, Robert na Adele. Ilikuwa picha iliyovuta hisia zake. Polepole akageuza macho yake kumtazama Robert ambaye naye alikuwa anaitazama ile picha iliyokuwa mbele kabisa jukwaani huku wakicheza polepole wakisonga mbele. Hapo Robert akageuka wakatazamana. Wote kwa pamoja wakatabasamu wakiendelea kucheza taratibu kufuatana na ala ya muziki huku ukumbi ukiendelea kupiga vigelegele.

Wakafika, wakapokelewa na washenga wao. Hatimaye walifika katika sehemu zao walizokuwa wameandaliwa. Ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe na chereko wakiwapongeza. Wakati wengine wakiwapongeza, washenga walikuwa na kazi ya kuwahudumia. Mshenga wa Adele alikuwa na kazi ya kulishika na kuliweka sawa shela alilokuwa amelivaa Adele ili lisijemtega akaanguka. Hivyo kila mara alikuwa akilibeba na kumfuta uso wake uliokuwa umerembwa ukarembeka.Maharusi walikaa kwenye viti vyao. Adele akamuuliza mshenga wake.

" Usalama upo Ramla?"

"Kila kitu kipo sawa kama tulivyopanga"
Ramla ambaye ndiye mshenga wa Adele akajibu huku akimfuta jasho usoni.

"Vizuri.. Yule malaya sijui huko yupo katika hali gani?" Adele aliongea kwa sauti ya chini huku akifutwa jasho na Ramla.

Hata hivyo Ramla hakumjibu. Harusi iliendelea lakini jambo ambalo Adele hakulitegemea lilijitokeza. Adele moyo wake ulilipuka kwa hofu. Akapoteza utulivu. Ni kama hakuwa na uhakika na kile alichokuwa amekiona. Alishangaa kumuona mshenga wake akiwa kavaa saa ya Ismaiya. Iweje Ramla avae saa ya Ismaiya. Aliitazama kwa umakini akajiridhisha kabisa ilikuwa ni ileile saa ya Ismaiya waliyonunua wote pale mlimani city. Adele akili ikamzunguka. Hofu ikamkumbatia. Alihisi kuna mchezo hauelewi. Akamtazama Ramla ambaye alikuwa hana hili wa lile akiwatazama watu waliomo ukumbini uso wake ukiwa kama mtu anayewaza jambo fulani. Punde Ramla akamgeukia Adele hali iliyomfanya ashtuke. Kilichomshtua ni kukutana na macho ya Adele yenye wasiwasi mwingi. Wote wakatabasamu, Ramla akachukua kitambaa akamfuta Adele usoni. Wakatabasamu tena lakini Adele alishtuka sana, Kitendo cha Ramla kutabsamu kilimtia hofu. Adele aligundua jambo ambalo liliipindua akili yake. Aliona mwanya kwenye kinywa cha Ramla, “hakuwa na mwanya”. Adele alikuwa akiwaza. Marafiki zake wote hawana mwanya isipokuwa rafiki mmoja tuu, Ismaiya! Iweje leo hii Ramla awe na mwanya wakati siku zote hana. Au ameenda kuchonga meno. Mbona ni jana tuu tuliongea naye hakuwa hivi. Huu mwanya umetoka wapi. Adele aliwaza mwenyewe akiwa haelewi, wasiwasi ukamuingia kuwa yule hakuwa Ramla bali alikuwa Ismaiya. Hakuamini kuwa jambo lile lingeweza kutokea. Alianza kumuogopa Ismaiya. Akajiuliza ni kwa kivipi Ismaiya acheze mchezo mgumu kama ule. Hata hivyo akajiuliza kama huyu siyo Ramla. Je Ramla yupo wapi. Akiwaza na kuwazua huku moyo wake ukipoteza utulivu alishtuka kumuona Ramla halisi akiingia mlangoni akiwa kavaa nguo zake kawaida. Moyo ulimlipuka. Alihisi kijasho kikimtoka. Ni kama presha ilimpanda. Akamtazama Ramla akiwa kule mlangoni akiingia, wote walitazamana. Adele akagundua jambo kwenye uso wa Ramla, macho yalikuwa mekundu kama mtu aliyekuwa analia. Hapo wasiwasi ukaongezeka. Akili yake ilichanganyikiwa. Akageuka kumtazama mshenga wake ambaye hapo mwanzo alijua ni Ramla kumbe siye. Ismaiya akatabasamu.

"Unashangaa! Mchezo ndio umeanza bi. harusi muiba waume za watu" Ismaiya aliongea kwa sauti ya chini akimtazama Adele.

Adele bado alikuwa ametekewa akiwa amekodoa macho akiwa haamini. Sasa ilikuwa ni dhahiri aliyekuwa ameketi pale alikuwa ni Ismaiya. Adele aliliona shela zito alitamani alivue ili apate ahueni. Alihisi joto huku kijasho kikimtoka. Ismaiya bado aliendelea na kazi yake ya ushenga. Adele alikwepesha uso wake huku akijitahidi kuwafanya watu ukumbini wasielewe kilichokuwa kinachoendelea.

Kitendo cha Ismaiya kumfuta Adele jasho kilimuumiza sana moyo wake. Aliumia kugeuka mshenga wa bibi harusi aliyemuibia mchumba wake. Hasira zilimpanda. Roho yake ilichafuka. Alitamani ampige Adele muda uleule lakini alikumbuka kuwa yupo mbele za watu. Jambo lolote angelifanya lingemponza na kumharibia mipango yake. Ismaiya alijua kuwa anahitaji uvumilivu kutimiza mipango yake. Ismaiya akamtazama Robert ambaye mara kwa mara alikuwa akimshika mkono na kumpiga mabusu Adele. Roho yake ilimuuma alihisi uvumilivu kumshinda. Alijikaza kuzuia machozi yasidondoke lakini lilikuwa ni zoezi gumu sana. Machozi yalishalamba mashavu yake laini ambayo hayakustahili dhuluma ile.

Ismaiya akakumbuka miaka minne nyuma alipokutana na Robert . Ilikuwa siku ya maonyesho ya sabasaba katika viwanja vya sabasaba pale temeke. Ni siku hiyo ya sabasaba iliyobadilisha muelekeo wa moyo wake. Siku ambayo kamwe hawezi kuisahau. Siku aliyokutana na mwanaume aliyempenda kwa dhati yote. Ismaiya pia alikumbuka siku walipoenda Zanzibar wakiwa na Robert kuosha macho. Ilikuwa ni kumbukumbu iliyomfanya azidi kutoa machozi.
"Maiya nitakupenda siku zote za maisha yangu" Ismaiya alikumbuka maneno ya Robert walipokuwa Zanzibar. Robert alizoea kumuita maiya kama kifupi cha Ismaiya. Huku ndiko kunipenda. Huku ndiko kunipenda Robert . Ismaiya alilalama kimoyo moyo huku akimtazama Robert kwa macho ya uchungu. Robert alishangaa kumuona Ramla akilia. Alijiuliza nini kinamfanya Ramla alie. Masikini, laiti angejua kuwa yule hakuwa Ramla bali ni Ismaiya wala asingejiuliza maswali hayo ya kipuuzi. Angejua majibu ya kinachomfanya binti huyo kulia. Angejua kuwa yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha machozi ya Ismaiya ambaye muda huo alijua ni Ramla. Basi ndio hivyo hakuwa anajua. Walitazamana kwa kitambo kisichozidi sekunde kumi. Robert alimsogelea Adele na kumuuliza kwa sauti ya chini kuwa mbona Ramla alikuwa analia. Adele alimjibu kuwa wala hakuwa analia bali ni matatizo ya macho yaliyokuwa yakimsumbua.

"Pole shemeji Ramla. Sikujua kuwa unamatatizo ya macho" Robert akasema. Maneno ya Robert yaliongeza hasira kwa Ismaiya. Donge zito la hasira lilimkaba kooni. Leo Robert ni wakuniita mimi shemeji. Leo mimi nina matatizo ya macho. Ismaiya alilalama peke yake kimoyo moyo. Huku akimtazama Robert. Adele akaanza kufikiria namna ya kumkabili mshenga wake. Ilikuwa vita baridi baina ya bibi harusi na mshenga wake. Kitendo cha Ismaiya kumkaribia Adele mpaka kuwa mshenga kilimpa Adele hofu kubwa. Akili yake ikamuambia anapaswa afanye jambo la haraka kumkabili Ismaiya. Adele alimnong'oneza Robert jambo fulani. Kisha Robert naye akalifuata sikio la mshenga wake ambaye ni Onesmo Kitoi akamdokeza jambo fulani. Onesmo ni mme wa Ramla. Punde mshehereshaji alitoa taarifa fupi kuwa kutakuwa na mapumziko ya dakika kumi. Kisha harusi itaendelea. Mc aliita band ya muziki kutumbuiza wakati huo bibi harusi Adele na bwana harusi Robert wakitoka kuelekea maliwatoni. Ismaiya akagundua kuwa Adele anataka kumfanyia ujanja ili amtoroke. Hakutaka kumuachia Adele hata sentimita moja. Alijua kufanya hivyo anaweza akampoteza adui yake. Akili yake ikafanya kazi haraka kujua afanye nini. Akataka kumsindikiza bibi harusi lakini yeye na mshenga wa kiume waliambiwa wabaki palepale. Hapo alijua tayari Adele amemkimbia. Na kama ishu ikibumbuluka inaweza hatarisha usalama wake. Adele alitoka kwenda msalani akiwa kashikwa mkono na mume wake, Robert . Watu walishangalia sana jinsi walivyokuwa wakitoka huku band ya muziki ikiimba mubashara. Adele aliyainua macho yake kuangalia kule alipomuona Ramla akiingia lakini hakumuona. Akaangalia pande zote, Robert akamvuta kutokana na kupunguza mwendo.

"Unashangaa nini. Twende. Tunadakika kumi tuu" Robert akasema. Adele hakumjibu zaidi ya kuongeza hatua huku mkono mwingine ukishika shela lisiburuzike lisije likamtega akaanguka. Akaingia chooni. Huko alijiuliza maswali ambayo hakupata majibu yake. Ramla aliyemuona ameingia kaenda wapi. Alijihisi kama amechanganyikiwa.

" ninaota? Lakini hapana! Nimemuona kwa macho yangu kabisa" Adele aliwaza. Alihisi kama anaota. Lakini hakutaka kupuuzia. Alitoka chooni akamkuta mume wake akimsubiri. Kwa jinsi alivyomkuta ni kama alikuwa akimlinda. Unaweza sema alikuwa bodyguard wa Rais. Ilikuwa zamu ya Robert kuingia chooni. Robert alimkabidhi simu Adele ili isijeikaanguka chooni. Robert alipoingia chooni Adele alibinya binya kwenye ile simu kisha akaweka sikioni.

"Mambo yameharibika, Maiya… Ndiye mshenga mpigeni risasi nitakaporudi... Wee usibishe wewe mpige risasi mshenga.." Adele akakata simu baada ya kuona kitasa cha chooni kimetekenywa na Robert kutokea. Robert alisikia kwa mbali maneno “risasi mshenga”

"Nani anataka kumpiga risasi mshenga?" Robert akauliza akichomekea vizuri shati lake kwenye suruali.
"Mume wangu jamani, umesikia vibaya. Au ndio unawaza leo usiku!nitakupa vitu mpaka leo upagawe " Adele aliongea kwa sauti ya kike haswa akiilegeza sauti yake. Kama ni ulaghai Adele alikuwa amesomea. Adele alifanana kabisa na Delila wa Samson. Robert akajikuta akilipotezea swali hilo baada ya Adele kumpelekea mdomo. Wakanyonyana ndimi kwa kitambo kisha wakarudi ukumbini. Ukumbini walimkuta Ramla na Onesmo ambao ni washenga wakipiga stori. Adele alijua dakika fupi zijazo Ismaiya ambaye mle ukumbini watu wanajua ni Ramla atakuwa amekufa kwa kupigwa risasi na watu aliokuwa amewapanga. Adele akarudi sehemu yake akaketi. Muda huu alikuwa na ahueni kutokana na kujua kuwa mwisho wa Ismaiya unakaribia. Alipoangaza kule nyuma ya ukumbi alimuona yule mtu aliyefanana na Ramla. Akamtazama kwa udadisi alafu akashtuka. Sasa waligongana macho. Yule mwanamke ambaye Adele aliamini ndiye Ramla halisi akatabasamu. Moyo wa Adele ulichanganyikiwa baada ya kumuona anamwanya. Akageuka kumuangalia mshenga wake lakini kabla hajafanya lolote ghafla mshenga akadondoka sakafuni huku damu ikitambaa kwenye sakafu. Mshenga alikuwa amepigwa risasi kama Adele alivyoagiza. Adele alihisi kuchanganyikiwa kutokana na kuhisi kuwa aliyepigwa risasi ni Ramla halisi wala siyo Ismaiya. Ukumbi ulishikwa na taharuki kubwa kutokana na tukio la mshenga kudondoka kwa kupigwa risasi. Adele aliamka nakumfuata Ramla aliyekuwa amelala sakafuni

"Ramla! Ramla! Amka Ramla! Ramlaaaaa!" Adele akaita kwa kupagawa huku ukumbi mzima ukiwa tuli umetulia watu wakimtazama kwa macho ya taharuki. Onesmo alibaki amepigwa na butwaa. Aliishiwa nguvu mwishowe akapoteza fahamu. Harusi iligeuka sinema ya kikatili na kutisha. Adele akainua uso wake uliojawa na machozi akamtazama Ismaiya ambaye alikuwa amevaa kinyago chenye sura ya Ramla. Ismaiya akatabasamu kisha akaongea maneno bila kutoa sauti lakini Adele aliyaelewa sawia.

Itaendelea........

Riwaya ya Mlio wa Risasi harusini softcopy Tsh 3,000/= Hardcopy Tsh 10,000/=
Piga simu 0693322300
 
1647088782223.png


MLIO WA RISASI HARUSINI
Mtunzi Robert Heriel
WhatsApp 0693322300



>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> Episode 02 <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

ILIPOISHIA
Onesmo alibaki amepigwa na butwaa. Aliishiwa nguvu mwishowe akapoteza fahamu. Harusi iligeuka sinema ya kikatili na kutisha. Adele akainua uso wake uliojawa na machozi akamtazama Ismaiya ambaye alikuwa amevaa kinyago chenye sura ya Ramla. Ismaiya akatabasamu kisha akaongea maneno bila kutoa sauti lakini Adele aliyaelewa sawia.

ENDELEA

Licha ya MC kutangaza watu wasitoke lakini watu hawakumsikiliza, mule ndani ilikuwa vurugu kila mmoja akijaribu kukimbia kuokoa roho yake. Hata hivyo jitihada za walinzi waliosimama pale nje zilifanikiwa kuwatuliza waliokuwa wakikimbia hovyo.

Wengine wakahisi ile risasi ilipangwa imlenge bibi harusi lakini kwa bahati mbaya ikampiga mshenga. Ukweli ni kuwa ile risasi ilikusudiwa impige aliyelala sakafuni. Ijapokuwa anayejua kuwa risasi ile imepigwa kimakosa alikuwa ni Adele na Ismaiya. Hawa ndio walijua fika kuwa risasi ile mlengwa wake alikuwa nani. Risasi ile ilikusudiwa ipite katika kichwa cha Ismaiya na kutawanya ubongo wake. Adele akapata wazo. Wakati watu wakiendelea kushughulika na Ramla, yeye akachukua simu ya mume wake kwenye koti la suti na kupiga simu. Aliongea kwa sauti ya chini akiwa kainama. Alipomaliza aliangaza kule alipokuwa Ismaiya. Alishtuka. Hakumuona Ismaiya. Ismaiya alikuwa keshaondoka. Hakujua ni kwa kivipi Ismaiya aliyeyuka kama moshi wa sigara. Mara akatabasamu alipokumbuka kuwa tayari. ameshawapa watu wake taarifa kuhusiana na kosa lililojitokeza. Kumbe Adele alikuwa ameweka walinzi waliobobea katika fani ya ukomando na upelelezi kwenye kila kona ya ukumbi kuhakikisha hakuna hatari itakayokwamisha mipango yake. Wapo aliowaweka nje ya ukumbi yalipo magari. Hawa aliwapa kila mmoja picha yenye taswira ya Ismaiya kusudi kama angetokea wamzuie nje kabla hajaingia ukumbini. Lakini Ismaiya mtoto mwenye akili za ajabu alilitambua jambo hilo. Alijua kama angefika na sura yake halisi asingefanikisha mipango yake.

Kwa upande wa ndani aliwapanga makomando kila pembe. Hawa walikuwa wakiangalia kila kilichokuwa kinaendelea ukumbini. Labda niseme, kwa jinsi Adele alivyokuwaa amewapanga watu wake ingekuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kupangua na kuharibu tukio lile. Alikuwa amejipanga vilivyo, hata hivyo kitendo cha Ismaiya kujipenyeza mpaka walipokuwa maharusi ilikuwa kama muujiza. Kwa upande nje, Kijana mmoja mrefu mweusi mwenye mwili uliojengeka vizuri kama wanyanyua vyuma alichukua uelekeo wa vilipo vyoo vya nje katika eneo la ukumbi. Akiwa na miwani yake nyeusi usoni alitembea kwa tahadhari kana kwamba alikuwa anamvizia adui hatari. Alipokaribia mlango wa chooni akajipapasa kiunoni kisha akatoa bastola. Alichezwa na machale. Kwa uzoefu wake ukimya ule ulimuambia yakuwa eneo lile kulikuwa na mtu. Na mtu huyo ndiye waliyekuwa wakimtafuta. Akashika kitasa cha mlango wa kwanza akakitekenya mlango ukafunguka. Akaufungua taratibu lakini hakukuta mtu wala hapakuwa na dalili ya Ismaiya kupita eneo lile. Aliendea choo cha pili ambacho hiki kilikuwa wazi. Nacho hakikuwa na mtu isipokuwa ndoo ndogo iliyokuwa na maji nusu. Akapiga hatua nyingine za tahadhari huku akiongeza utulivu kuelekea kilipo choo cha tatu. Alipofika kwenye mlango wa choo hiki akahisi jambo. Moyo wake uliingia upepo wa mashaka. Ngozi ikamsisimka. Hakujua ni kwa nini alihisi jambo la hatari. Akasimama kisha akatulia kwa umakini kuyapa masikio yake nafasi ya kusikia lolote kutoka mle ndani. Akasogelea kitasa na kukitekenya kwa taratibu bila kutoa sauti. Lakini aligundua kuwa ule mlango umefungwa kwa ndani. Sasa alijihakikishia kuwa mule ndani kulikuwa na mtu. Akafikiri kidogo kisha akarudi nyuma na kuupiga teke moja la nguvu mlango ukavunjika. Alifanya hivyo kwa wepesi huku bastola yake ikiwa mkononi tayari kwa kushambulia. Alishangaa kuona choo kikiwa tupu bila kuwa na mtu. Akasonya huku akipiga hatua kuingia ndani. Mule chooni aligundua kuwa dakika chake zilizopita kulikuwa na mtu. Macho yake yalihamahama kuangalia huku na huku. Ghafla alishtuka kuona gloves ya mikono kwenye karo ya kuoshea mikono iliyomo mule chooni. Mbele ya karo ile ukutani kulikuwa na kioo. Sasa aliishika bastola yake vizuri akijua anasogelea hatari. Akashtuka alipofika karibu ya ile karo. Macho yake yalipokelewa na kinyago chenye sura ya Ramla. Moja kwa moja akajua kuwa Ismaiya ndiye aliyeivua na kuiacha pale chooni. Akatazama juu ya paa ambapo aliona kipande kidogo cha silling board kikiwa kimetolewa. Akili yake ikamuambia kuwa pale ndipo alipopitia Ismaiya.


"Ismaiya ni komando! Mwanamke gani apande sehemu kama hii?" aliongea kwa sauti ya chini lakini kabla hajamaliza kuongea akasikia sauti ya mtu anayenyata kuja kule alipokuwa. Akaishika bastola yake vyema tayari kwa kushambulia. Alijibanza kwenye mlango uliobaki nusu kutokana na yeye kuuvunja. Hapo akatulia kimya huku mikono yake yenye misuli ikizidi kuikumbatia bastola yake. Yule mtu aliyekuwa akinyata kivuli chake kilijitokeza jambo ambalo liliongeza hofu kwa yule kijana aliyejibanza nyuma ya mlango. Akajua muda wa mapambano umefika. Akavuta pumzi nzito tayari kurukia windo lake Lakini kabla hajafanya hivyo alishusha pumzi nzito kama mtu aliyemaliza mbio ndefu.

"kumbe ni wewe Chuma" yule kijana aliongea baada ya kuona taswira ya chuma ikijitokeza kwenye kile kioo kilichopo ukutani juu ya karo ya kunawia.



*************************************************​

Magari matatu ya Polisi yaliingia kwenye geti la ukumbi. Polisi wenye sare walishuka wakiwa wamebeba bunduki aina ya SMG. Waliingia ukumbini hali iliyofanya ukumbi mzima kunyamaza. Tukio la Polisi kuingia ukumbini lilimfanya Adele achukie. Hakutaka Polisi wafike mapema. Polisi wengine walikuwa nje wakikagua na kulinda usalama. Upande wa ndani Adele alikuwa akipiga akili kuhusu jambo fulani alilolijua yeye mwenyewe.

Adele alikuwa ni mwanamke ajuaye kucheza na akili za watu. Mwanamke anayejua kupika njama na kuhakikisha inafanikiwa. Lengo la Adele kutaka Polisi wale wachelewe ni kuwa alitaka mchungaji afungishe ndoa haraka. Alifikiri kuwa endapo ndoa itafungwa basi mpango wake utakuwa umekamilika. Kufunga ndoa na Robert alihesabu kama mafanikio makubwa katika maisha yake. Hakujali njia mbaya alizotumia. Alichojali yeye ni kufunga ndoa na Robert, mwanaume pekee aliyeuteka moyo wake. Ukumbini watu waliobakia walitulia kuona mwisho wa sinema ile huku wasiwasi ukiwazingira lakini walitamani kujua mwisho wa mambo yale.

Mchungaji akasimama kisha akawaomba watu watulie kusudi ndoa ifungwe kwani asingechukua hata dakika kumi.

"Kwa tulipofikia hatuwezi kughairi. Tunashukuru ndugu zetu Polisi wamewahi kulinda usalama wa kila aliyeko humu ndani" Mchungaji akakohoa kidogo kisha akaendelea.
"wote tunasikitika kwa tukio la kupigwa risasi kwa mshenga wetu lakini tunaimani atapona yeye na mume wake bwana Onesmo. Tuzidi kuwaombea" Mchungaji akaongea akiwapa moyo waliokuwa ukumbini. Polisi mmoja alimfuata mchungaji na kuomba kipaza sauti.
"Ndoa haitaweza kufungwa kufuatia tukio hili lililotokea. Tunaomba radhi na kutoa pole kwa haya yaliyotokea. Tunaomba utulivu wakati tukiendelea kuangalia namna ya kuwatoa humu salama" Polisi aliongea huku akijaribu kuwasihi kwa unyenyekevu kama mtu aliyeguswa na madhila yale. Maneno hayo ya Polisi yaliuchoma moyo wa Adele ambaye alikuwa ameshikana mkono na Robert . Akamtazama Robert aliyekuwa ameduwaa kama mtu aliyewekewa limbwata. Akajikuta machozi yakimtoka. Alikiangalia kidole chake cha pete ya ndoa ambacho aliamini siku hiyo kingekuwa kinameremeta kwa kuvalishwa pete ya dhahabu. Lakini haikuwa hivyo.
Punde akaingia Polisi mmoja kwa kasi akitokea lilipo lango la kutokea. Jambo hili lilimfanya Adele ahisi kitu. Adele akatumia ishara kwa walinzi wake waliokaa nyuma. Kisha akachukua simu akabonyeza harakaharaka ujumbe fulani. Yule Polisi alikuwa amefika na kutoa agizo kuwa Adele na Robert wapelekwe kituo cha Polisi. Adele alishtuka kusikia maneno hayo. Yalikuwa ni maneno ya karaha ambayo yalimchefua. Yeye alipanga siku hiyo akitoka ukumbini wangeelekea moja kwa moja kwenye hotel kubwa waliyoikodi kwa ajili ya kula fungate na mume wake, Robert. Leo hotel imegeuka kituo cha Polisi. Thubutu! Adele hakutaka hilo litokee.

Akaomba aende chooni wakamruhusu lakini kabla hajapotea kwenye kona. Milio ya risasi ikasikika. Tayari Polisi wawili walikuwa wamelala sakafuni baada ya kupigwa risasi. Mmoja alipigwa ya kifuani huku mwingine kichwa chake kikiwa kimepasuliwa vibaya na risasi. Taharuki na mikikimikiki ikazuka. Watu ukumbini wakaanza kukimbiakimbia mtihili ya nyumbu huku wengine wakilala chini ya mabenchi. Polisi mmoja akamshika Robert na kumuweka kama ngao. Huku wengine wakijificha wakishambuliana na wale walinzi wa Adele. Ilikuwa piga nikupige. Chapa ni kuchape. Rusha nikurushe! Huko nje napo milio ya risasi ilisikika jambo ambalo liliwafanya waalikwa wa harusi waliokuwa wakikimbia kwenda nje wasijue waende nje au warudi ndani. Kote palichafuka. Mapigano ya risasi yalidumu kwa takribani dakika kumi mpaka Polisi walipopata upenyo wa kutoka nje ya ukumbi wakiwa wamembeba Robert ambaye alikuwa haelewi, alijiona kama yupo kwenye ndoto ya kutisha ya usiku wa manane lakini haikuwa ndoto. Wakamuingiza Robert ndani ya gari aina ya Murano nyeusi na kwa kasi kubwa gari likaondoka likiacha vumbi eneo lote la nje la ukumbi.
Mule ndani alipotupwa Robert ndio kulikuwa na kizaazaa. Robert alishtuka akipopokelewa na uso wa Ismaiya ambao ulikuwa nyuma ya miwani kubwa nyeusi. Moyo wa Robert ulidunda sana. Alihisi pumzi ikimuacha. Hakuamini kama Ismaiya angemkuta mule ndani. Lilikuwa ni tukio lililomshtua kuliko matukio yote aliyowahi kuyaona. Lilikuwa ni tukio la aina yake lililofanya moyo wake kufa ganzi. Mapigo yaliukimbia moyo wake akajikuta ameduwaa asijue yupo ama hayupo. Ismaiya alitoa machozi huku akimtazama Robert, mdomo wake ulitetemeka huku mwili ukitingishwa na kwikwi. Kila alipotaka kunyanyua mdomo wake alishindwa kutokana na kuzidiwa na kwikwi.

Bado gari aina ya Murano lenye vioo vyeusi walilokuwamo Ismaiya na Robert lilikuwa likikata mitaa kwa kasi iliyowashangaza watu wengi. Tayari lilishafika Morogoro road maeneno ya shekilango likachukua uelekeo wa sinza kwenye barabara ya shekilango.



*************************************************​



Adele alikasirika kwa kitendo cha Robert kutoroshwa.

"Mmeshindwaje kumlinda Robert? Hee! Nyie ni wanaume gani? Ehhe! Sinaongea na ninyi"
Adele alikuwa akiwafokea walinzi wake aliowaweka kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Watu walikuwa wamekimbia wote kutoka ukumbini. Ukumbi ulikuwa na miili minne ya Polisi na walinzi sita waliouawa kutokana na majibizano makali ya risasi yaliyokuwa yakiendelea. Adele aliingia tena ukumbini. Akaanza kukagua mwili mmoja baada ya mwingine ya wale Polisi.

Polisi wa kwanza alikuwa na bastola tuu. Huyu alipigwa risasi nyingi za kifua na moja ya bega. Alimsogelea Polisi wa pili, huyu alikuwa amelala juu ya benchi. Adele akamkagua mifukoni hakukuta kitu cha maana. Huyu alipigwa vibaya kwenye jicho lake la kulia. Alitisha sana.
Mwili wa tatu ulikuwa ni wa Polisi aliyechomwa kisu tumboni huku mikono yake ikiwa imeshika kile kisu kikiwa tumboni. Kwenye mifuko yake kulikuwepo simu iliyokuwa inachungulia. Jambo hili lilimfanya Adele aso gelee na kuichukua ile simu. Adele akashtuka baada ya kusoma kwenye kioo cha simu aliyoichukua kwa yule Polisi aliyeuawa pale chini. Aliona ujumbe uliosomeka

"Make sure she does not runaway" Moyo wa Adele ulipiga paa! Akaiangalia namba iliyotuma ujumbe huo. Moja kwa moja aliitambua. Ilikuwa namba ya Ismaiya. Adele alikuwa ameikariri namba ya simu ya Ismaiya kama table ya tano. Moyo wake ulichanganyikiwa. Aliona Ismaiya ameshamzidi kete. ”Kumbe wale hawakuwa Polisi! walikuwa ni watu wa Ismaiya”. Adele akapigapiga miguu yake chini kwa hasira huku akisonya. Hasira alizokuwa nazo ni kama mbogo aliyejeruhiwa.

"Nitakuua Ismaiya. Umejitafutia kifo chako" aliongea kwa sauti ya juu hali iliyofanya sauti yake kujirudia kutokana na ukumbi ule kuwa mtupu bila watu. Akachukua ile simu na kutoka nje ya ukumbi akitembea kama komando Nemes Nebula. Vijana wake walipomuona waliiona sura ambayo hawakuwahi kuiona tokea wamjue Adele. Walitambua kuwa Adele amechukizwa kwa kitendo chao cha kushindwa kumlinda Robert.

"tumechezewa mchezo. Wale siyo Polisi" Adele akasema huku akifungua mlango wa gari aina ya cruzer mayai nyeupe.

"Hahahahaaa!" moja ya wale vijana aliachia kicheko. Adele akiwa na vazi lake la harusi akachukua bastola iliyokuwa mule ndani ya gari akampiga risasi ya kichwa yule kijana. Huo ndio ukawa mwisho wa yule kijana aliyejichekesha. Haukuwa muda wa mchezo hata kidogo. Yaani unacheka wakati Adele amepokonywa mpenzi wake. Adele aliona cheko lile kama dhihaka na dharau kwake. Watu wa namna hiyo yeye hakuona shida kuondoa shingo zao. Ndivyo alivyomfanya yule kijana. Waliingia ndani ya gari akiwa yeye na wale makomando watatu wakawa wanne ndani ya ile cruzer mayai. Akachukua simu yake alafu akaiweka sikioni. Wakati huo gari lilikuwa linatoka getini kwa kasi ya ajabu likitimua vumbi kwa nyuma.

"Hello Justin" Adele alikuwa akiongea na mtu kwenye simu.

"Helow Adele mpenzi. Nambie" Justin alijibu akileta utani kidogo.

"Justin, Please…! naomba nichekie namba zifuatazo......" akamtajia kisha anaendelea kuongea.
"Nijulishe zinasoma mnara wa wapi. Sasa hivi justin" Adele aliongea mwisho akakata simu. Kisha akamtumia laki tano justin kama njia ya kumhamasisha afanyekazi kwa haraka. Adele alitoa namba za Ismaiya na kuchukua namba alizozishuku kutoka kwenye ile simu ya yule mtu aliyejifanya Polisi aliyeuawa ukumbini. Justin hakuchukua muda mrefu akamtumia Adele uelekeo wa gari alilopanda Ismaiya na Robert ambalo muda huo lilikuwa linakatiza maeneo ya tegeta nyuki likielekea Bunju.
"ongeza mwendo. Tuelekee Bunju"Adele akaongea kwa sauti ya amri ambayo haikuwa na dalili ya mzaha. Ndani ya gari kulikuwa kimya. Adele alikuwa akitafakari namna siku yake ilivyoharibika. Muda huo alipanga tayari wangekuwa wametoka ukumbini yeye na Robert na kuelekea kupiga picha katika maeneo mbalimbali yenye vivutio. Lakini Ismaiya kavuruga mipango yake. Badala ya muda huo awe katika maeneo ya kupiga picha lakini haikuwa hivyo. Amejikuta akikimbizana kumsaka kipenzi chake. Moyoni akaapa siku atakayompata Ismaiya mikononi basi huo ndio utakuwa mwisho wake.”Nitamuua kwa mikono yangu mwenyewe” Adele akawaza. Gari lilikuwa linaenda kwa kasi sana. Dereva alionyesha kuijua vyema kazi yake. Pia alijitahidi kukata vichochoro hatimaye walikuwa wamefikia makutano ya mwenge. Hapo walikutana na foleni kidogo. Adele aliona foleni kama inamchelewesha akamuamuru dereva aiote gari na kuliingiza kwenye upande ambao siyo sahihi. Dereva akafanya kama alivyoagizwa. Aliitia moto gari na kuanza kwenda kwa kasi kuvuka makutano ya barabara za mwenge. Hii ilizua taharuki kubwa miongoni mwa watu. Gari yao ilikoswakoswa kugongwa na magari yaliyokuwa yanayotokea ubungo yaelekeayo kawe na makumbusho.

Walifanikiwa kupita; Wakaipita kambi ya Lugalo na sasa waliiona Tegeta hii hapa. Kabla hawajafika Tegeta kwa ndevu walikutana na kizuizi cha Trafiki waliozingira barabara kuwazuia wasipite.Adele alichanganyikiwa, akamuagiza dereva apunguze mwendo. Dereva akapunguza mwendo kisha wakasimama. Askari wa kike aliyevalia kofia nyeupe na nyeusi. Shati safi jeupe na sketi ya Dark bluu. Huku chini akiwa amevaa viatu vyeusi na soksi nyeusi. Alilisogelea gari lao. Dereva akashusha kioo.

"habari afande
"

"Salama. Mbona mnakimbiza gari namna hii. Hamuoni mtasababisha ajali? Na mmepita pale mwenge kwa kuvunja sheria?"Trafiki akasema huku akichungulia ndani kuwakagua waliokuwa mule ndani ya gari.

"Kuna mgonjwa tunamuwahi hapo Bunju. Tusamehe afande" dereva alikasema huku akitabasamu kwa unyenyekevu na kumshikisha Trafiki kibunda cha pesa.Yule Trafiki kuona bunda la pesa akatabasamu na kuwapa ishara ya kuendelea na safari.

"kazi njema afande" Dereva alimuaga afande kwa lugha ya urafiki. Sasa walifika Bunju A wasijue walipoelekea kina Ismaiya. Adele akachukua tena simu na kumpigia justin.

"Justin nimefika Bunju A. Sijui nielekee wapi"

"Mnara unaosoma yupo Bunju b. Nendeni mpaka Bunju b"
Justin akajibu na simu ikakatika.
Adele alishusha pumzi kwa kuchoka lakini hakuwa tayari kuchoka kwa sababu ya mpenzi wake, Robert . Iliwachukua dakika chache kufika Bunju b. Hapo hawakuwa na muelekeo. Adele akampigia tena Justin kuomba awape muelekeo. Lakini justin aliwaambia kuwa wapo hapohapo Bunju b. Kuhusu ni nyumba gani hapo alishindwa kuwasaidia. Adele alimshukuru Justin kwa msaada aliompatia. Adele akafikiri kidogo akawaambia walinzi wake warudi mjini ila yeye wamuache pale Bunju b. Wakabishana kidogo lakini baadaye walimkubalia. Gari ikaondoka na kumuacha Adele akiwa mwenyewe Bunju b. Tayari ilikuwa mida ya saa kumi na mbili jioni bado Adele hakuona dalili ya kumpata Robert, akiwa na shela lake la harusi; Aliamua kuchukua lodge nzuri kwa ajili ya kupumzika kwa usiku ule. Akachukua chumba kizuri ambacho ni self-contained. Akaenda kuoga. Akiwa bafuni hakuamini usiku ule unaingia akiwa hajamuona Robert. Akatazama gauni lake la harusi alilokuwa amelivaa. Moyo ulimuuma sana. Usiku ule ndio ulikuwa usiku wa fungate yao kwa siku ya kwanza yeye na Robert . Sasa yupo pekee yake. Hisia mbaya zikamjia na kuhisi huenda muda huo Robert alikuwa amelala kitanda kimoja na Ismaiya wakati yeye akiwa na shela lake. Alijikuta akipiga ukuta wa bafu huku akitukana. Akajifuta na taulo kisha akatoka bafuni kuelekea chumbani. Alijiandaa kisha akatoka nje, mbele kidogo ya ile lodge kulikuwa na duka la nguo. Alienda akiwa kavaa shela lake. Watu walimshangaa lakini hakujali. Alinunua nguo za kawaida kisha akarudi kwenye lodge kubadili nguo. Sasa alikuwa katika mwonekano mpya. Alivaa pensi na blauzi kisha akatoka kwenda kutafuta sehemu wanapouza chakula cha usiku. Akafika kwenye mgahawa mmoja uliochangamka kisha akatafuta sehemu iliyojificha ambapo asingeonekana kwa urahisi. Akakaa huku akiwatazama waliokuwa pale mgahawani. Mhudumu akaja akamuagiza nyama choma na savanah mbili. Haikupita muda mhudumu alimletea savanah lakini akamuomba asubiri kidogo ataletewa nyama. Akiwa mgahawani hapo akaanza kuchora mienendo ya watu waliokuwa wakiingia na kutoka. Hata hivyo hakuona tashwishwi yoyote. Kitambo kidogo mhudumu alisimama mbele yake akiwa na sahani kubwa iliyofunikwa na nyama choma. Adele akashukuru kisha mhudumu akaondoka. Akiwa anakunywa alishtuka kuona mtu mmoja akiingia. Alipomtazama vizuri alimkumbuka. Alikuwa ni yule askari aliyezuia harusi isiendelee kule ukumbini. Alikumbuka mpaka maneno yake. Muda huu hakuwa amevaa sare za kipolisi. Alikuwa amevaa tisheti nyeusi na suruali ya jeans. Mdomoni mwake ilikuwepo sigara iliyokuwa ikitoa moshi. Aliongozana na mwanamke mmoja mwembamba kiasi ambapo walienda kukaa kwenye kona yenye gizagiza. Adele alivuta pumzi nzito baada ya kuwa na uhakika kuwa yule aliyemuona akiingia ndio yuleyule Polisi aliyezuia ndoa yake isifungwe. Sasa macho yote yalikuwa makini kuangalia kila alichokuwa akikifanya yule Polisi. Hakutaka tena kuzembea. Aliongeza umakini huku akitafakari namna atakavyomkabili yule Polisi, ili amuambie ni wapi Ismaiya na Robert walipo. Masaa matatu yalipita wakati Adele akitongozwa na usingizi akimsubiri yule Polisi aliyekuwa bado anajivinjari na mwanamke aliyeingia naye pale mgahawani. Ilikuwa ni saa tano ya usiku. Adele alishtuka baada ya kumuona yule Polisi akiamka na yule mwanamke wakiondoka. Sasa alijua muda wa kujua alipo Robert mpenzi wake umefika.

Akiwa nyuma Adele akashtuka kumuona Polisi na yule mwanamke wakielekea kwenye ileile lodge aliyochukua chumba. Akajibanza kwenye mti wa muarobaini huku akiwachungulia walipokuwa wameingia mapokezi. Hapo aliwaona wakiandikisha majina yao kwenye kitabu cha wageni walichopewa na dada wa mapokezi. Kisha wakaingia ndani na kuchukua chumba namba 24 kilichoongozana na chumba chake ambacho ni chumba namba 23. Adele akaingia chumbani kwake akiwa na wasiwasi mwingi. Alijiuliza afanye nini kusudi amkabili yule Polisi ili amuambie mahali alipokuwa Ismaiya na Robert . Akaenda kitandani alipoliweka shela lake la harusi na kuichukua bastola. Akaishika huku akiigonga gonga kwenye mapaja yake. Ni kama alikuwa anatafakari jambo fulani. Punde alisikia kwa nje ilipokuwa korido mlango wa pili ukifunguliwa. Akasimama haraka kuelekea ulipo mlango wa chumba chake. Alipofika mlangoni mwake alisikia sauti ya viatu ikitembea usawa wa mlango wake. Kutokana na mlio aliousikia moja kwa moja alitambua ni viatu vya kike na huo ni mwendo wa kike. Ni mtu mwenye uzoefu pekee ndio angeweza kutambua jambo hilo. Adele akafungua mlango kwa haraka na kupokelewa na mgongo wa mwanamke aliyekuwa anatembea kwenye zile korido. Akamuacha mpaka akapotea kwenye kona ya korido. Akasogea kwenye kile chumba namba 24.
Akafungua kitasa polepole bila kutoa sauti alafu akaingia na kukuta chumba ni kitupu huku kitanda kikiwa na suruali ya jeansi, Pembeni kulikuwa na tisheti nyeusi. Akasikia maji yakimwagika upande wa kushoto ambapo aligundua lilikuwa ni bafu. Hivyo akajua yule Polisi ndiye aliyekuwa anaoga. Akaanza kuipekua ile suruali ya Polisi ambapo alikuta kadi mbili moja ya benki na nyingine ilikuwa kadi ya mpiga kura iliyokuwa na picha ya yule Polisi.
Pia aligundua kuwa yule Polisi alikuwa anaitwa Hamza Kimweri. Akaendelea kupekua katika mifuko mingine lakini hakuona kitu kingine. Ghafla alishtushwa na sauti ya simu ambayo hakujua ipo wapi. Akaanza kufuatilia mlio wa ile simu.

"Julieth…! Julieth!" Hamza aliyekuwa bafuni aliita. Kitendo cha Adele kusikia sauti ya Hamza kutoka bafuni kilimsisimua na kumfanya aingiwe na hofu. Akaikamata bastola yake vizuri kukabiliana na hatari endapo ingejitokeza.

Aliikuta simu chini ya mto ikiendelea kuita. Akaiangalia kwenye kioo cha simu akaliona jina la Bosslady. Alijiuliza bosslady ndio nani. Lakini alipoiangalia vizuri ile namba moyo wake ulikosa utulivu. Ilikuwa ni namba ya Ismaiya. Alitaka kupokea lakini kabla hajafanya hivyo simu ikakatika. Hapo akaanza kuipekuapekua. Akafungua sehemu ya meseji lakini alihitajika aweke nywila ili aweze kusoma meseji. Alisonya kwa sauti ya chini. Akiwa katika kujaribu nywila ili kufungua sehemu ya meseji punde akasikia kitasa cha mlango wa bafuni kikicheza. Akajiweka tayari kukabiliana na Hamza, kwa upesi akajibanza pembeni mwa mlango wa bafuni. Hamza alitoka akiwa kavaa taulo bila kutazama kulia wala kushoto. Alipiga hatua kuelekea kitandani. Alishtuka kuona simu ipo sehemu ambayo hakuiweka. Nani kaitoa. Macho yake yaliona vitambulisho vyake vikiwa vimetolewa kwenye mifuko ya suruali. hisia hatari zikagonga hodi. Lakini kabla hisia zake hazijaenda mbali alihisi ubaridi katika shingo yake ikifuatiwa na sauti ya kike.


"Mikono kichwani. Ukileta ujanja ubongo wako utamwagika" Adele akasema huku kidole chake kikiwa kipo kwenye kilimi cha bastola. Hamza aliifahamu sauti aliyoisikia. Aliijua vyema sauti ya Adele. "Where is my Robert ?". Aliongea kisha akampiga kwa nguvu teke la mgongo hali iliyomfanya Hamza aangukie kitandani na taulo likiachia mwili wake, akabaki uchi kama alivyozaliwa. "Sema haraka nitakipasua hicho kichwa" Adele alibweka huku sura yake ikimaanisha. Uso wa Adele ulitisha sana. Ulionyesha chuki na hasira alizokuwa nazo. Ulionyesha ukatili aliokuwa ameuhifadhi kwa muda mrefu. Hamza alitaka kujaribu kujinasua mbele ya Adele. Akamrushia taulo kwa upesi lakini kumbe Adele alikuwa kashamuona. Alilipiga teke lile taulo kama Van dame na kuachia risasi mbili zilizokuta paja la Hamza.
Hamza aligugumia kwa maumivu makali. Hakuamini kama Adele angetambua hila yake.
"Naona unataka kufa. Si ndio wee mbweha!" Adele alibweka huku akiachia risasi nyingine iliyopasua goti la mguu wa kulia. Hamza akapiga yowe la uchungu lakini Adele alimuonya kwa kumkemea anyamaze huku bastola ikiwa juu ya kichwa chake. Hamza akatulia huku akitetemeka kwa maumivu na hofu. Hakutaka aiache familia yake iliyokuwa inamtegemea. Lakini atafanya nini mbele ya Adele ambaye muda huo alikuwa na hasira kali ambayo alikuwa tayari hata kuua.

"Nasema! Usiniue Adele. Nitakuambia" "haya sema kabla sijapasua utosi wako" Adele akasema akizidi kuikaza sauti yake ili kumtisha Hamza. Punde simu iliita tena. Wakatazamana mithili ya majogoo yanayopigana.

"Pokea, unamuangalia nani wewe mbwa" Adele alimfokea Hamza.

"Ongeza sauti na mimi nisikie" Adele akaamrisha.

"hellow Hamza upo wapi?" Sauti ya kike ambayo Adele aliitambua kuwa ni Ismaiya iliongea.

"..ni..nipo hapa Bunju bosslady" Hamza aliongea kwa kusitasita lakini kutokana na kunyooshewa bastola ilimbidi aongee tuu.

"usichelewe si unajua kesho tuna safari" Ismaiya alisema akiwa kwenye simu.

"sawa bosslady. Sitachelewa" Hamza akasema na wakaagana.

"kesho mnaenda wapi" kimya bila Hamza kujibu.

"si nakuuliza, kesho mnaenda wapi na Robert yupo wapi?"Adele alimchapa kofi la nguvu lililofanya Hamza ajisikie maumivu makali sana. Hamza hakutegemea kuwa mwanamke mrembo kama Adele angeweza kumchapa kofi la namna ile. Adele alionekana ni mrembo na laini sana ambapo mtu angedhani kuwa hawezi hata kuvunja biskuti. Lakini haikuwa hivyo. Adele alikuwa mwanamke hatari sana. Akampiga risasi nyingine ya goti la mguu wa kushoto. Hali iliyomfanya Hamza apige yowe la kukata tamaa. "Nyumba namba 019. Yenye geti jekundu na paa la kijani" Hamza alibwatuka akiwa kashika mguu wake uliokuwa umepigwa risasi. "Kesho wanaenda wapi?"Adele alimuuliza baada ya kuridhishwa na jibu la kwanza. "Kesho tunampango wa kuelekea nairobi kule kenya" Adele alitoka haraka baada ya kujibiwa hivyo.

Akiwa anatoka mlangoni alipishana na yule mwanamke ambaye ni Julieth. Julieth alikuwa kabeba chupa kubwa mbili za wine. Alishangaa kumuona mwanamke akitoka kwenye chumba alichokuwepo Hamza. Alimsindikiza kwa macho Adele mpaka alipomalizika kwenye korido. Adele alichukua bodaboda na kumuambia dereva ampeleke nyumba namba 019. Walipatana bei kisha Adele akapanda. Safari ilianza na ndani ya dakika tano walisimama mbele ya geti jekundu lenye paa la kijani. Akampa bodaboda hela yake akaondoka. Adele alitazama uzio wa ile nyumba ambao kwa juu uliwekwa nyaya za umeme. Akafungua Geti na funguo malaya alizokuwa nazo na taratibu akazama ndani ya geti. Alimkuta mlinzi amepitiwa na usingizi ikiwa ni saa saba za usiku. Alinyata kama paka na kujikuta yupo kwenye mlango wa sebule. Akaufungua pia kwa aina ile ile ya funguo malaya. Akaingia ndani ya sebule kubwa yenye samani za kisasa. Hakutaka kuwasha taa. Alinyata chumba mpaka chumba. Akisikiliza kwenye milango bila kuifungua. Akafika kwenye mlango wa mwisho ambapo alisikia miguno ya watu wakifanya mapenzi. Donge zito la wivu likamkaba kooni. Hasira zilimpanda. Alijua Ismaiya na Robert ndio waliokuwa wakifanya huo uchafu. Aliamini yeye ndiye aliyekuwa na uhalali wa siku hiyo kulala na Robert .Sasa iweje Ismaiya ndio alale na kipenzi chake huku yeye akihangaika usiku kucha na bastola kama jambazi. Miguno bado iliendelea kutesa hisia za Adele aliyekuwa akilia mlangoni. Alihisi uchungu kuliko ule wa kuzaa. Wivu wa mapenzi ulimvaa kama kanzu. Akaamua kuufungua mlango kusudi awamalize wote. Akaufungua mlango polepole na funguo malaya. Alifanikiwa. Lakini kulikuwa na giza nene huku kitanda kikichezacheza na sauti ya miguno ikiendelea.
Aliwasha taa. Duuh! Walishtuka.

Kitendo cha Adele kuwasha taa ya kile chumba kiliwashtua sana waliokuwa wakifanya mapenzi.
Adele hakuamini kile macho yake yalichokuwa yanakiona.

ITAENDELEA

Jipatie Softcopy kwa Tsh 3,000/= Kitabu Tsh 10,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
MLIO WA RISASI HARUSINI (Episode 03)
Mtunzi: Robert Heriel
WhatsApp 0693322300

>>>>>>>>>> Episode 03 <<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

ILIPOISHIA

Miguno bado iliendelea kutesa hisia za Adele aliyekuwa akilia mlangoni. Alihisi uchungu kuliko ule wa kuzaa. Wivu wa mapenzi ulimvaa kama kanzu. Akaamua kuufungua mlango kusudi awamalize wote. Akaufungua mlango polepole na funguo malaya. Alifanikiwa. Lakini kulikuwa na giza nene huku kitanda kikichezacheza na sauti ya miguno ikiendelea.
Aliwasha taa. Duuh! Walishtuka.
Kitendo cha Adele kuwasha taa ya kile chumba kiliwashtua sana waliokuwa wakifanya mapenzi. Adele hakuamini kile macho yake yalichokuwa yanakiona.


ENDELEA

Kitendo cha Adele kuwasha taa ya kile chumba kiliwashtua sana waliokuwa wakifanya mapenzi.
Adele hakuamini kile macho yake yalichokuwa yanakiona. Hakuwa Ismaiya wala Robert bali alimuona baba wa makamo na mke wake waliokuwa wameshikwa na butwaa kutokana na uwepo wa ghafla wa Adele mule ndani kama mzimu uliokatisha starehe yao. Adele aliishiwa nguvu. Tayari aligundua kuwa alikuwa amedanganywa na Hamza. Alijilaumu kwa kumuamini Hamza.
"Sijui ni shetani gani alinipitia mpaka nikamuamini yule mbwa" Adele aliwaza. Huku akiwa amewanyoshea bastola wawili wale waliokuwa wakifanya mapenzi kitandani ambao muda huo walikuwa wamejawa na hofu iliyochanganyika na aibu; jasho likiwatoka. Adele akatoa kikaratasi ambacho ndani yake kulikuwamo na ungaunga kisha akawapulizia. Sekunde kumi tuu zilitosha kubeba fahamu zao. Akatoka kwa tahadhari huku akisikiliza mawimbi ya hewa yaliyokuwa mule ndani.



*************************************************​


Ilikuwa ni sebule kubwa ambapo upande wa mashariki wa sebule kulikuwa na kabati kubwa lenye luninga ya kisasa na sabufa kutoka Japan. Upande wa magharibi lilikuwepo sofa la watu wa nne ambapo mbele yake kulikuwa na meza ya kioo iliyokuwa juu ya zulia la manyoya. Upande wa kaskazini lilikuwepo dirisha lililofunikwa na pazia kubwa lenye rangi ya dhahabu. Mlango wa kuingia ulikuwepo upande wa kusini. Juu ya ukuta ilikuwepo picha iliyomuonyesha mwanamke na mwanaume waliokuwa wamekumbatiana. Picha hiyo ndiyo iliyomfanya Robert asimame mbele akiitazama kwa umakini huku akikumbuka kumbukumbu iliyoibua hisia za huzuni moyoni mwake. Robert alikumbuka siku aliyopiga picha hiyo akiwa na Ismaiya. Ilikuwa ni siku ambayo chuoni alipokuwa akisoma Ismaiya, kulikuwa na shindano la kumtafuta Mrembo wa chuo hicho. Ni siku hiyo ambayo Ismaiya aliibuka na ushindi mnono akiwabwaga walimbwende wengi waliokuwa wakisoma katika chuo hicho. Ismaiya alikuwa akimtazama Robert aliyekuwa akiitazama picha yao iliyokuwa ukutani. Machozi yaliteleza kwenye mashavu yake. Hakuamini kama angeweza kufanikiwa kupangua ndoa haramu ya Adele aliyetaka kumuibia mchumba wake. "Robert mpenzi wangu kwa nini umenisaliti? Kwa nini?" Ismaiya akamuuliza Robert huku akimtingisha kwenye bega lake.

Hali hiyo ikamfanya Robert aache kuangalia picha iliyokuwa ukutani kisha akamtazama Ismaiya aliyekuwa akilia. "Hukuona wanawake wengine mpaka umchukue Adele, rafiki yangu?" Ismaiya akalia kwa uchungu. "Nisamehe maiya mpenzi wangu, niliambiwa umekufa" Robert alimjibu huku sauti yake ikitoka kwa kukwaruza kama mtu aliyekula uketo. Jibu hilo likamfanya Ismaiya ahamaki. Hakuamini kama alikuwa amesikia vizuri.

“Robert Unasemaje? " Ismaiya akauliza.

"Mimi najua umekufa"

"Robert!!” “umechanganyikiwa" Ismaiya akasema kwa sauti ya kutetemeka
"Adele aliporudi kutoka Japan alisema kuwa, nawe ulikuwa miongoni mwa abiria wa ndege ya malaysia. Alinihakikishia kuwa umekufa" Maneno ya Robert yalimfanya Ismaiya awe kama mtu aliyepagawa. Hakuamini kama Adele angetunga uongo kama ule ili tuu amuibie mchumba wake.

“Nawe wewe ukamuamini yule chiz wako sio?”

“ Haikuwa rahisi! Niliumia sana Maiya, Nilihisi kifua change kupasuka, niliumwa nikakonda kwa ajili ya taarifa ya msiba wako. Nilitamani ningeenda hata kwenu kutoa pole lakini kama unavyojua, sio mimi wala wewe hakuna ajuaye kwa wazazi wetu. Mbaya zaidi sikuwa kujua hata ndugu yako mmoja”
Robert akasema huku akilia kama mtoto mdogo.

Ismaiya akagundua kuwa Adele hakuwa amedisco chuo bali alitoroka ili aje aolewe na Robert. Alikumbuka siku Adele alivyomdanganya kuwa amedisko hivyo anarudi Tanzania. Akakumbuka jinsi alivyoumia kusikia habari ya kufeli kwa rafiki yake wa damu. Kumbe hakuwa amefeli wala nini. Ismaiya pia akakumbuka siku aliyomsindikiza Adele uwanja wa ndege wa Kansai uliopo mji wa Osaka kurudi Tanzania. Akakumbuka alimpa zawadi nyingi ili amletee Robert. Akazigeuza zile zawadi kuwa zake na kumkabidhi Robert. Yote hayo yalimfanya Ismaiya azidi kumchukia Adele na kumuona kama adui namba moja katika maisha yake.

"Ati nimekufa kwenye ajali ya ndege ya malaysia" Ismaiya alijisemea kwa sauti ndogo.

"Robert Mpenzi wangu. Mimi sikufa. Wala sikuwepo kwenye hiyo ndege. Kama nilivyokueleza hapo" Ismaiya akasema kisha wakakumbatiana. Robert alihisi kama akili imemkimbia. Alikiri kuwa Adele amemuingiza mjini na ndevu. Akamuona Adele kama mwanamke aliyebobea katika fani ya ulaghai. Ati Ismaiya amepotea na ndege ya malaysia. Yaani Adele hajambo kwa uongo. Robert alikuwa akitafakari akiwa amekumbatiana na Ismaiya. Ismaiya akamuomba Robert akaoge. Kitambo kidogo kilipita Ismaiya akatoka bafuni akiwa kavaa kiguo laini cha kulalia. Robert akashangazwa na uzuri wa Ismaiya kwa jinsi ulivyofunikwa na kiguo kile. Aliyaona makalio makubwa ya Ismaiya jinsi yalivyokuwa yanatetemeka kwa deko. Ni kama Ismaiya alikuwa akifanya makusudi kumchombeza. Ismaiya alijua fika kuwa umbo lake lilikuwa linamzuzua Robert. Akayalegeza macho yake huku akiachia tabasamu jepesi la peponi. Hapa Robert hakuwa na ujanja tena. Hisia zake zilianza kuchemka na kupanda kama maziwa Fresh yanapochemshwa. Akamrukia kama mpira wa penati akamdaka kiunoni alafu akamvutia kitandani. Ilikuwa ni siku yenye furaha kwa wawili hawa baada ya kuachana kwa miaka miwili bila kukutana kimwili. Kila mmoja alikuwa na kiu na mwenzake. Wakati nyota zikimulika huko nje. Huku ndani chumba kilijawa na sauti za miguno ya mahaba. Kukurukakara za kuparurana zikadumu kila mmoja akimkamia mwenzake na kuonyesha ufundi, zilikuwa dakika za utamu, kila sekunde iliyokuwa ikiyoyoma ilikuwa na ladha ya kipekee kwao. Kitambo kidogo kila mmoja alikuwa ametosheka. Wote walikuwa wamelowa kwa jasho kutokana na kazi kubwa iliyokuwa imefanyika. Wakapongezana. Punde wakiwa wanapeana shukrani simu ya Ismaiya ikaita.

"Bosslady... Bosslady.. Njoo hapa Starwine lodge. Adele kanipiga risasi" ilikuwa ni sauti ya Hamza aliyekuwa akiongea kwenye simu. Kabla Ismaiya hajaongea chochote simu ilikatika. Akajaribu kuipigia lakini haikuwa inapatikana.Wasiwasi uliuzingira moyo wa Ismaiya. Alijua kama Adele kamfikia Hamza ni wazi kuwa hayupo mbali kumfikia yeye jambo ambalo hakutaka litokee kwa usiku ule. Usiku ule alitaka kupumzika na kufaidi mapenzi ya mpenzi wake, Robert.

"Adele anatufatilia. Hayupo mbali atakuwa hapa" Ismaiya akamuambia Robert.

"Yupo wapi huyo nguruwe. Mwanamke shetani, nitakuua Adele, acha kufuatilia maisha yangu" Robert akabweka. Maneno hayo yakamfanya Ismaiya aachie tabasamu. ."Twende Starwine lodge tukamchukue Hamza. Kisha tuondoke eneo hili" Ismaiya akaongea huku akichukua mkoba wake.

Wakakumbatiana na kupeana mabusu. Kisha wakatoka na gari. Punde wakasimama nje ya starwine lodge. Walipiga simu bado ilikuwa haipatikani. Eneo lote la ile lodge lilikuwa kimya. Giza lilifunika barabara hali iliyofanya pawe panatisha. Ismaiya hakutaka kushuka kwanza alijua huenda Adele katega mtego ili amnase. Akafikiri huenda Hamza alitekwa na Adele na kumrishwa awapigie simu ili Ismaiya naye aje kukamatwa. Jambo hili Ismaiya alijua fika kuwa linaweza kutokea. Punde wakaona watu wawili wakitoka ilipomiti mingi iliyokuwa upande wa pili wa lodge. Alikuwa ni Juliet aliyekuwa anamkokota Hamza. Ismaiya alishtuka kumuona Hamza akiwa katika hali ile. Akataka kushuka lakini akili yake ilimuonya.

“Ngoja nishuke mimi. Najua Adele hawezi kunidhuru kama yupo eneo hili’’ Robert akaongea akimtazama Adele aliyekuwa na wasiwasi mwingi. Robert akashuka kumsaidia Juliet kumbeba Hamza na kumuingiza ndani ya gari. Ismaiya akatia moto gari na safari ikaanza. Wakafika Bunju b Stand ilipo barabara ya bagamoyo. Wakachukua uelekeo wa bagamoyo. Gari ilikuwa inaenda kwa kasi sana yapata saa nane unusu usiku. Kabla hawajafika Mapinga wakaona mwanga ukiwamulika kutokea nyuma ya gari lao. Ismaiya akaongeza mwendo zaidi. Robert alishangaa kuona jinsi Ismaiya alivyokuwa analimudu gari. Hakuwahi kudhani kuwa mrembo kama Ismaiya anaweza kuendesha gari kwa kasi ile tena bila hofu yoyote licha ya barabara waliyokuwa wakiipitia kuwa na mashimo na virakaraka vya lami. Gari ya nyuma iliyokuwa ikiwafukuza nayo ikazidisha kasi. Kitambo kidogo ikawafikia. Milio ya risasi kutok anyuma yao ikasikika. Risasi ikaipapasa gari yakina Ismaiya na kupasua kioo cha nyuma. Ismaiya akaanza kuendesha kwa kukwepesha kwepesha gari ili lisipatwe na risasi. Robert alihisi anatazama filamu ya kivita. Lakini ile haikuwa filamu bali lilikuwa tukio halisi lenye kusisimua. Ismaiya akatoa bastola akampa Robert akamuambia awapige kwa tahadhari. Dooh! Robert hakuwahi kutumia bastola iweje ajifunzie kwenye vita. Ismaiya kuona Robert anazubaa akamnyang'anya bastola na kuanza kuwashambulia kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukishika usukani. Hakika Ismaiya alikuwa mwanamke komando. Gari la nyuma likaongeza kasi zaidi likafika usawa na gari la kina Ismaiya. Madirisha ya magari yakawa sambamba. Ismaiya akalipiga kikumbo kidogo cha ubavu hali iliyofanya gari lililokuwa likiwafukuza kuyumba kidogo na kutoka nje ya barabara. Punde mkono ulioshikilia bastola ulichungulia katika lile gari na kuachia risasi mbili zilizopasua tairi la mbele la gari la kina Ismaiya. Gari likayumba na kwenda swegemnege kisha likapinduka likaviringika umbali mrefu huku litimua vumbi nje ya barabara ambapo kulikuwa na vichaka. Lile gari lililokuwa likiwafukuzia kwa nyuma likaenda kusimama mbele kidogo. Kisha milango ya mbele ikafunguka. Upande wa kulia alipokuwa dereva akashuka mwanaume mmoja mrefu wa miraba minne. Upande wa kushoto akashuka mwanamke aliyevalia suruali iliyomshika vyema huku akiwa kavaa kofia. Hakuwa mwanamke mwingine bali alikuwa ni Adele.



*************************************************​



“Amebarikika ambaye mkononi mwake umo ufalme naye juu ya kila kitu ni muweza. Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Naye ni mwenye enzi ya nguvu asiyeshindika, mwingi wa kughufuria .” (qur-aan 67: 1-2)

Sheikh aliendelea kutoa mawaidha kuwausia waliohudhuria katika mazishi ya Ramla. Ilikuwa siku ya majonzi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Ramla. Hakuna ambaye hakuguswa na msiba wake. Ramla alikuwa mwanamke aliyefahamika kwa upole na mwenye heshima. Alikuwa ni mwanamke mwenye kupenda dini bila kujali uzuri wake na elimu yake tofauti na wanawake wengi wenye uzuri na elimu kama yake. Onesmo aliyekuwa mume wake ambaye alivalia kanzu ya rangi ya shaba huku kichwani akiwa kavaa kofia aina ya barakashee. Aliugulia maumivu makali moyoni mwake. Uso wake ulizingirwa na huzuni huku macho yake yakiwa mekundu jambo ambalo mtu yeyote aliyemtazama angegundua kuwa ametoka kulia tena kilio cha uchungu sana. Alilitazama kaburi la marehemu mke wake akiwa haamini kuwa ndio hatomuona tena. Sheikh akaendelea kutoa mawaidha kuwafariji na kuwakumbusha wale waliobakia kuwa mauti ni safari ya kila mmoja. Hivyo kila mtu ajiandae.

"Allaah anasema; kila nafsi itaonja mauti! …” (qur-aan 21: 35). Hivyo ndugu zangu waislam na wote mliofika katika mazishi haya ya mpendwa wetu, binti yetu tuliyempenda Ramla ambaye leo hatukonaye tena. Tunapaswa kumcha mola" Sheikh akamaliza na kupokelewa na sauti za nyimbo kutoka kwa umati uliokuwa umekusanyika. Zilikuwa ni nyimbo maarufu za kiislam zitumikazo kwenye mazishi. Watu walitawanyika huku minong'ono ikiendelea kufuatia tukio la kifo cha Ramla.

Tayari habari hiyo ilifika katika kituo cha Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kujua ni kina nani waliomuua Ramla. Kina nani waliovamia harusi ya Adele na Robert . Ni kina nani waliomteka Robert . Jacob Warioba ambaye ni sajini wa Polisi (SGT) alitaka kupeleleza tukio hili la kutisha lililoondoka na roho za watu. Jacob Warioba mbali na kuwa Polisi pia ni mwanasheria kitaaluma. Alichukua shahada ya kwanza ya sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Alipohitimu aliamua kuomba kujiunga na chuo cha Polisi (CCP) kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Kisha baadae alienda Monduli kwenye mafunzo maalumu ya uanajeshi na ukomando. Ni kutokana na tabia ya Sajenti Warioba kupenda haki na kuipigania ndio maana aliamua kusomea sheria. Lakini pia alipenda fani ya upelelezi na uchunguzi ili kujua haki ipo wapi na ili aweze kuisimamia. Aliamini kuwa huwezijua haki ipo wapi bila kuwa na elimu ya upelelezi na uchunguzi. Hapo ndipo akaona kujiunga na Polisi ni kete muhimu katika kutimiza ndoto yake. Lakini pia, upelelezi unachangamoto zake na hatari kwenye usalama, ndio maana akajiunga na mafunzo maalumu ya kijeshi na ukomando, kwa ajili ya kujilinda. Alitoka ofisini kwake akiwa na gari yake aina ya Toyota Harrier toleo jipya alimaarufu kama tako la nyani yenye rangi nyeusi na vioo vya tinted. Moja kwa moja akaelekea ulipo ukumbi wa Double x uliotumika katika harusi ya Adele na Robert. Alipofika alikuta geti likiwa limevunjwa vibaya. Akaingiza gari polepole kwa tahadhari. Ilikuwa mida ya jioni kama saa kumi na mbili kasoro. Tayari alikuwa ndani ya eneo la ukumbi. Akasimamisha gari lake na kutulia kwa dakika moja huku akiangaza macho yake huku na huko kuona kama kuna mtu. Lakini hakuona dalili ya mtu. Akafungua mlango wa gari akashuka chini. Akaangaza huku na huku ambapo aliona miili mitatu ya watu waliokufa kwa kupigwa risasi. Akaitazama akaona mwili mmoja ukiwa umepigwa risasi ya shingo. Mwingine alikuwa amepigwa risasi ya kichwa.

Huyu ni yule aliyepigwa na Adele kwa kosa la kucheka. Maiti ya tatu haikuwa na jeraha lolote. Ni kama mtu aliyekuwa amelala. Mwili huu wa tatu ulimvutia Sajenti Warioba. Akausogelea kisha akachomoa gloves za mikono na kuanza kumkagua. Akatoa kifaa kiitwacho fingerprint sensor (fs) kwa ajili ya kuona kama angeona alama yoyote ya vidole kwenye ule mwili. Akaukagua maeneo ya shingoni akagundua kuna alama za vidole. Akazi-scan kwa kutumia kile kifaa kisha akaondoka pale nje; akaelekea ndani ya ukumbi. Ndani aliona maputo yaliyoisha hewa yakining'inia kwenye kamba. Akaiona miili saba ikiwa imelala sakafuni. Miili mitatu ilikuwa imevaa sare ya Polisi ambapo ni wale watu waliojifanya Polisi wakamteka Robert kumbe ni watu wa Ismaiya. Akakagua miili yote lakini hakuona jambo lolote ambalo lingemsaidia katika uchunguzi wake. Akaenda lilipokuwa jukwaa walipokaa maharusi ambapo aliona damu zilizoganda kwenye sakafu. Hizo zilikuwa ni damu za marehemu Ramla aliyepigwa risasi ya kichwa masaa matatu yaliyopita. Alikaa kwenye kiti kimoja cha maharusi akijaribu kuvuta picha jinsi Ramla alivyokuwa amepigwa risasi. Kisha akaangalia zile damu zilizokuwa zimeganda pale sakafuni. Akagundua kuwa mpigaji wa risasi alikuwa upande wa kulia wa ukumbi. Akatazama upande wa kulia ambapo aliona viti na dirisha. Akasogea mpaka lilipo lile dirisha hapo akasimama. Akajaribu kuangalia uwezekano wa uwepo wa shambulizi lakini hakuona uwezekano wa mshambuliaji kuwa alikuwa eneo lile. Akatazama nje ya lile dirisha napo hakuona dalili. Akataka kuondoka lakini kabla hajafanya hivyo macho yake yaliona jambo la shaka. Nje ya uzio wa ukumbi ambao ulikuwa uzio wa ukuta wa futi kama tano kulikuwa na jengo la ghorofa tatu. Akili yake ikaenda mbio kidogo. Alihisi huenda mshambuliaji alikuwa kwenye lile jengo la ghorofa lililokuwa nje ya uzio wa ukumbi. Akatoka mbiombio nje ya ukumbi akatoka getini akiacha gari lake akaelekea kwenye ile ghorofa. Ilikuwa ni hotel.

Akaingia mapokezi akajitambulisha kama askari. Wahudumu wakashtuka kwa ujio wa askari katika hotel yao. Baada ya salamu Sajenti akaomba kupelekwa kwenye kile chumba alichohisi kuwa mlenga shabaha ndipo alipokuwa amejificha na kutenda uhalifu. Wahudumu wa hotel hawakuwa na ubishi. Wakampeleka. Kilikuwa chumba kilichokuwa ghorofa ya kwanza chumba namba 17. Akaingia akakagua huku mhudumu akimuangalia kwa makini. Akaenda kwenye dirisha la kile chumba akatizama ulipo ukumbi. Akagundua kuwa muuaji alikuwa kwenye kile chumba kutokana na kuwa moja kwa moja alikuwa akiona eneo walilokaa maharusi. Hii ni kumaanisha mlenga shabaha alichukua chumba pale kisha akatekeleza mauaji yale ya kikatili. Akakagua chooni lakini hakukuta kitu cha maana. Akaenda kwenye karo la kunawia mikono ambapo alijua kuwa ni lazima muuaji angefika pale na kushika bomba ili anawe mikono au uso. Akatoa kile kifaa cha fingerprint sensor lakini hakuona alama zozote za vidole. Hapo akajua kuwa muuaji alikuwa kavaa gloves za mikono. Hii ikamfanya aone muuaji alikuwa makini na anaujuzi wa kufanya uhalifu wa namna ile. Akamuuliza mhudumu wa ile hotel kuwa kuna yeyote aliyeingia baada ya huyo mtu kuchukua chumba hiki. Mhudumu akamjibu hakuna kwani alisema angerudi usiku.

Sajenti akashtuka kidogo. Ni kama aliona jambo fulani. Akapiga hatua taratibu mpaka kwenye kioo kikubwa kilichokuwepo ukutani. Akahisi muuaji lazima alijiangalia kwenye kioo. Akagundua muuaji ni mwanaume mrefu wa futi sita hivi kutokana na kuona alama ya mvuke kwenye kioo.

"Humu ndani hakuna kamera?" Sajenti Warioba akauliza.

"Hakuna labda za nje" mhudumu akajibu.

"Twende ukanionyeshe" Sajenti Warioba akaongea huku akitoka na mhudumu.

Mhudumu akamfungulia kamera na kumuonyesha mtu aliyechukua chumba namba 17. Akamuona mwanaume mrefu wa futi sita hivi kama alivyokadiria. Mweusi kama Mnubi wa sudani mwenye mwili mwembamba kiasi. Ajabu ni kuwa mtu yule pamoja na kamera kumchukua lakini uso wake haukuonekana vizuri kutokana na yeye kuvaa kofia. Jambo hili lilimfanya Sajenti Warioba kusonya huku hasira zikimtekenya. Alihisi mtu aliyefanya tukio lile alikuwa anaakili zisizo za kawaida ambazo hakutaka kukubali kama muuaji huyo amemzidi ujanja. Alimuona muuaji kama mtu aliyehitimu mafunzo ya hali ya juu sana. Akamuuliza mhudumu mahali alipojiandikisha mtu yule. Mhudumu akachukua kitabu na kumfungulia ambapo aliona jina lililoandikwa BinaMungu Albert. Mahali alipotoka ni morogoro. Mbele kulikuwa na namba ya simu. Akaichukua ile namba ya simu akapiga lakini ikawa haipatikani. Hata hivyo alijua watu wengi hutoa taarifa za uongo waingiapo nyumba za wageni. Akaamua kuzipuuza. Akagundua pia kuwa Mtu Yule alichukua chumba siku moja kabla ya harusi.

Akatoka na kurudi ukumbini akiwa amechanganyikiwa lakini angalau alishukuru kwa kupata moja mbili tatu kuhusiana na kilichotokea. Akachukua simu akawapigia Polisi waje kuchukua ile miili ya maiti pale ukumbini. Kisha Akaingia ndani ya gari yake aina ya Toyota Harrier na kuondoka. Akiwa ndani ya gari mawazo yalimjia. Alifikiri ugumu wa kesi ile. Pamoja na uzoefu wake wa kesi za namna hiyo lakini hakuwahi kukutana ugumu kama wa kesi ile. Alihisi kama kesi ile ndio inaweza kuwa kesi ya kwanza kushindwa. Akiwa kwenye foleni ya Ubungo mataa akiwa anaelekea nyumbani akaona jambo lililoshtua hisia zake. Akaona gari moja aliloliona kwenye kamera za ile hoteli. Ilikuwa subaru yenye rangi nyekundu. Alipoangalia ndani yake; moyo wake ulipasuka. Alimuona mwanaume mweusi lakini hakuwa amevaa kofia. Yule mtu aligeuka wakagongana macho. Wote wakashtuka. Ni kama walikuwa wameshtuana. Sajenti Warioba akazuga kwa kutoa tabasamu la kirafiki huku akimpungia mkono. Yule mtu naye aliitikia kwa ishara ya kupunga mkono huku akiikunjua sura yake ngumu iliyoficha kila aina ya hila.

Yule mtu alikatisha gari upande wa kushoto wa barabara ya Nelson Mandela na kuacha mataa ya ubungo. Sajenti Warioba naye akaifungia mkia gari ya yule mtu akiwa ameiacha kwa umbali wa mita mia kama uwanja wa mpira ili yule mtu asije akamshutukia. Wakapita Buguruni sheli wakafika makutano ya Tazara kilipo kiwanda cha Bakhresa. Wakapita chini ya Daraja la mfugale wakinyooka kufuata barabara hiyohiyo ya Nelson Mandela. Yule mtu bado hakujua kuwa nyuma yake alikuwa akifuatiliwa na Sajenti Warioba mtu aliyebobea katika fani ya ushushushu. Sajenti Warioba alikuwa na uwezo wa kipekee wa kumchunguza mtu bila ya mtu mwenyewe kujua. Akiwa ndani ya gari alikumbuka sura ya yule mtu aliyemuona kwenye kamera za ile hotel. Alikumbuka pia subaru nyekundu aliyoiona kule kwenye kamera za ile hotel. Hii ikamfanya awe na uhakika kuwa mtu yule ndiye aliyesababisha mauaji ya Ramla, “ Sababu ni nini mpaka amuue Dada wa watu, aharibu harusi ya watu, kwa mujibu wa maneno ya watu; Ramla alikuwa mtu mwema sana, iweje apatwe na ukatili wa namna ile. Lazima ipo sababu lakini shetani wakati mwingine huumiza na kuua watu hata pasipo sababu, furaha ya watu kama hawa ni kuwaona watu wakipata shida” Sajenti akawaza.

Giza tayari lilikuwa limeingia na mwanga wa mchana ulikuwa ukiaga uso wa dunia. Walikuwa wameshafika ulipo uwanja wa mpira wa uhuru ambapo umekaribiana na uwanja wa mpira wa taifa. Mataa ya uwanja wa taifa wa mpira yaliangaza kwa namna ya kupendeza hali iliyofanya eneo lile litawaliwe na nuru. Uwanja wa mpira wa taifa ulijengwa na kukamilika mwaka 2007 ukigharimu zaidi ya dola milioni 53 na nusu kwa msaada wa taifa la China. Unaouwezo wa kuingiza watu elfu sitini. Pia unafahamika kama Benjamin Mkapa National Stadium. Sajenti Warioba akautazama akajihisi fahari na kujivunia nchi yake kuwa na uwanja mkubwa kama ule. Akashangaa kuona ile gari aina ya subaru nyekundu ikikata mkono wa kulia kuifuata Kilwa road. Ilikuwa ni barabara ielekeayo Mbagala. Walipita mtoni mtongani bado yule mtu hakujua kama alikuwa akifuatiliwa. Wakapita Mbagala sasa walikuwa wakiitafuta Kongowe. Sajenti Warioba bado alikuwa makini kuhakikisha windo lake halimshtukii. Sasa waliingia Kongowe. Yule mtu alikata kushoto barabara ielekeayo kigamboni kupitia Twangoma. Sajenti Warioba hakumuachia nafasi yule mtu mweusi kama msudani amkimbie wala amshtukie. Wakafika sehemu iitwayo Mwembe mtengu. Hapo lile gari aina ya subaru likakata kulia likiwa limepunguza mwendo kidogo. Hii iliashiria kuwa muda siyo mrefu safari ingefikia tamati. Kama alivyowaza Sajenti Warioba ndivyo ilivyokuwa. Ile subaru nyekundu ikasimama mbele ya geti kubwa la kisasa ambalo ndani yake kulikuwa na jumba kubwa la kifahari. Sajenti Warioba naye akasimamisha gari lake umbali wa mita thelasini akimtazama yule mtu aliyekuwa akimfukuzia. Punde geti lilifunguka likiwa linateleza kwa ndani taswira ya jumba kubwa la ghorofa ikijitokeza. Yule mtu akaliingiza gari ndani huku geti likijifunga.

Sajenti Warioba akashuka kwenye gari lake, akasogea lakini ghafla akasimama. Alikumbuka kuwa kama atasogea karibu kabisa na geti huenda geti lile lilikuwa na kamera au vifaa maalumu vinavyoweza kuwapa taarifa watu waliomo ndani ya jumba lile. Akiwa mbali kama mita kumi akalikagua kwa macho geti lile akaona kamera pamoja na kifaa maalumu kinacho detect uwepo wa mtu atakayesogelea. Akazunguka upande wa pili ambapo kulikuwa na ukuta mrefu wa futi sita ambapo juu yake kulikuwa na waya za umeme pakiwa na kibao kilichoandikwa hatari na alama ya fuvu la mtu. Akatoa mkasi maalumu wa kukatia zile nyaya. Akaangalia huku na huko akaona hakuna mtu. Kisha akapanda kama paka aupandavyo mti. Ukuta ule haukumpa shida yoyote. Alikata nyaya kisha akapata nafasi ya kukaa. Alichungulia upande wa ndani ambapo aliona bwawa la kuogelea kubwa lililokuwa mbele kidogo ya lile jumba. Aliona magari matatu likiwepo na ile subaru nyekundu aliyokuwa anaifukuzia. Hakuona mtu ingawaje taa zilikuwa zikiwaka kwa ndani. Aligundua kuwa ile nyumba ilikuwa na vyumba sita na sebule, na ghorofa kwa juu. Ilikuwa nyumba kubwa na ndefu kwenda juu. Alishuka taratibu bila kutoa sauti kama nyoka atelezavyo kwenye nyasi. Akalisogelea dirisha la chumba kilichokuwa kinawaka taa. Dirisha lilikuwa limefungwa na kioo alafu ndani kulikuwa na pazi kubwa ambalo halikumruhusu aone jambo lolote. Akasogelea chumba kingine ambacho hiki pazia lake lilikuwa limekunjwa hali iliyomfanya aone kwa ndani kitanda kikubwa cha thamani na sofa moja huku mbele ya sofa kukiwa na kiti mfano wa stuli ambapo juu yake kulikuwa na gazeti. Akiwa anachungulia mara alishtuka kuona mlango wa kile chumba unafunguliwa. Akamuona mtoto wa kiume mwenye umri kama miaka kumi na nne hivi akiingia akiwa ameshika chupa ya konyagi. Kabla yule kijana hajakaa kwenye lile sofa; mlango ukafunguliwa tena na punde aliingia Mama mmoja wa makamo mwenye umri kati ya miaka arobaini na tano hivi. Sajent Warioba akatulia kuona ni nini kinaendelea. Akamuona yule Mama akisogea kwenye lile sofa ambalo alikuwa amekaa yule mtoto. Yule Mama akaivua ile kanga aliyokuwa ameivaa akabakiwa na chupi. Mapigo ya moyo wa Sajenti yakaenda mbio.

Ni kama alikuwa haamini wala haelewi yule Mama anataka kufanya nini. Yule Mama akamsogelea yule kijana akakaa juu yake kama mtu aliyepakatwa. "wewe Mama utamuua mtoto wa watu!" Sajenti Warioba akawaza

Alitamani amkemee lakini nafsi yake ikamuonya asijaribu kufanya hivyo. Sajenti Warioba akaitazama sura ya yule kijana. Masikini ya Mungu. Kijana wa watu alikuwa anatia huruma. Uso wake ulionyesha dhahiri kuwa hapendezwi na jambo lile. Alimuona yule Mama kama Mama yake mzazi. Iweje leo amfunulie utupu wake. Lakini atafanya nini. Hakuwa na jinsi zaidi ya kufuata maagizo ya yule Mama.

"Mpenzi jamani bado hujazoea tuu?" yule Mama aliongea huku akishika kidevu laini kisicho hata na ndevu cha yule kijana mdogo. "Atazoea vipi wakati wewe ni kama Mama yake. Hivi huoni huyo ni mtoto jamani?" Sajenti Warioba alikuwa akiwaza kama mtu anayemjibu yule Mama. Kama kuna watu waliomchukiza Sajenti Warioba basi ni yule Mama. Alimuona ni shetani mbaya asiye na huruma. Yule mtoto wa watu alikuwa kanyamaza kama kondoo anayesubiri kukatwa mkia. Mwili wa Sajent Warioba ulimsisimka na kufa ganzi alipomuona yule Mama akivua ile chupi na brazia akabaki kama alivyozaliwa. Akamuona yule mtoto akishindwa kuungalia mwili wa yule Mama. Kweli dunia imeisha. Akafikiri. Punde, Sajenti akasikia kitu kigumu kikimpiga kichwani na hapo hapo giza likavamia macho yake na ukungu ukazisonga fahamu zake. Akadondoka chini akapiga kichwa dirisha kutokana na kupigwa na kitu kizito. Jambo hilo lilimshtua yule Mama na mtoto waliokuwa mule ndani. Yule Mama akalisogelea dirisha na kufunga pazia.


*************************************************
ITAENDELEA

Jipatie Softcopy kwa Tsh 3,000/= Kitabu Tsh 10,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
Sawa mpendwa..story nzuri mnooo..


Unaweza endelea na hii

 
MLIO WA RISASI HARUSINI ( Episode 04)
Mtunzi: Robert Heriel
WhatsApp 0693322300

>>>>>>>>>>>>>>> EPISODE 04 <<<<<<<<<<<

ILIPOISHIA.
Yule mtoto wa watu alikuwa kanyamaza kama kondoo anayesubiri kukatwa mkia. Mwili wa Sajent Warioba ulimsisimka na kufa ganzi alipomuona yule Mama akivua ile
chupi na brazia akabaki kama alivyozaliwa. Akamuona yule mtoto akishindwa kuungalia mwili wa yule Mama. Kweli dunia imeisha. Akafikiri. Punde, Sajenti akasikia kitu kigumu kikimpiga kichwani na hapo hapo giza likavamia macho yake na ukungu ukazisonga fahamu zake. Akadondoka chini akapiga kichwa dirisha kutokana na kupigwa na kitu kizito. Jambo hilo lilimshtua yule Mama na mtoto waliokuwa mule ndani. Yule Mama akalisogelea dirisha na kufunga pazia.


ENDELEA....


Fahamu zikamrudia. Alishangaa kujikuta kalala kitandani ndani ya chandarua akiwa katundikiwa dripu kwenye mkono wa kulia. Mwanga hafifu wa bluu uliangaza katika chumba kile. Akajigeuza kwa tabu akashindwa. Alisikia maumivu makali kwenye kichwa. Akaangalia pembeni kidogo akaona meza kubwa yenye makopo na maboksi yenye madawa. Akagundua muda ule ulikuwa usiku lakini hakujua ni usiku wa saa ngapi. Akajaribu kukumbuka yaliyotokea. Alikumbuka alikuwa ndani ya gari akiwa na Ismaiya ambaye alikuwa ndiye dereva. Sasa akajua kuwa walikuwa wamepata ajali. “Hapa ni wapi? Ismaiya wangu yuko wapi?” akawaza. Lakini alijikuta akikata tamaa ya uwezekano wa Ismaiya kupona kutokana na kuwa aliyekuwa akiwafuatilia ni Adele. Robert akafikiri kuwa kama Ismaiya angekuwa amepona basi Adele alikuja akammalizia kwa kumpiga risasi. Alifikiri hivyo akiona katika mawazo yake; akamuona Adele akilisogelea gari lililopinduka akamkuta Ismaiya akiwa ameumia vibaya akiwa hoi taabani. Adele hakumuonea huruma Ismaiya. Akampiga risasi. Robert alishtuka! Kumbe yalikuwa ni mawazo yake mabaya na wala halikuwa tukio halisi. Usingizi ulimchukua tena mpaka asubuhi. Akazinduka. Muda huu chandarua ilikuwa imeondolewa na ile taa ya bluu ilikuwa imezimwa. Akaangalia kwenye ile meza akamuona mtu aliyemgeuzia mgongo akiwa anafanya jambo ambalo hakuwa analiona. Robert alitamani mtu yule ageuke ili amuone. Mtu yule alikuwa kavaa koti jeupe kama daktari. Punde mlango ulifunguliwa na sura ya Adele ilijitokeza. Robert akashtuka kumuona Adele ingawaje kwa upande wa Adele haikuwa hivyo. Yeye alitabasamu. Yule mtu aliyevalia koti jeupe akasalimia, Adele akamjibu kwa ufupi huku akienda kitandani alipolala Robert .

"Mume wangu Robert nilikuwa nakuombea upone" Adele akasema.

Adele akafurahi kumuona Robert akiwa yupo hai baada ya kuzimia kwa zaidi ya masaa thelasini. Aliomba usiku na mchana ili Robert aweze kupona. Sijui alimuomba Mungu yupi ilhali kaiba mchumba wa mwenzake. Sijui alimuomba Mungu yupi ikiwa yeye ndiye chanzo cha kifo cha Ramla. Labda mungu wa sangoma. Hivyo ndivyo alivyokuwa akiwaza Robert baada ya kumsikia Adele aliposema alikuwa akimuombea kwa Mungu. Punde mlango ulifunguliwa. Robert alishtuka kumuona mtu aliyekuwa akiingia. Mapigo ya moyo yakakimbia kwa hofu. Hakutaka jambo lile litokee. Lakini ndio basi tena lilikuwa limetokea. Mbele yake alisimama Mama yake akiwa analia. Macho yake yalilowa tepetepe kwa machozi. Uso wake ulikuwa mwekundu kwa kulia. Robert akamtazama Mama yake kisha akamtazama na Adele aliyekuwa akimbembeleza Mama mkwe wake asilie. Adele alijua kwa kufanya hivi angeuteka moyo wa Mama yake Robert. Aliamini kuwa kama akiuteka moyo wa Mama mkwe basi pasingekuwa na pingamizi lolote kwa Robert. Mama Robert akamsogelea Robert kitandani. "Mwanangu, dunia umeikosea nini? Umeikosea nini dunia?" aliongea kwa kigugumizi kutokana na kusumbuliwa na kwikwi.

"Baba yako walimuua. Wanataka kukuua tena na wewe?" Mama aliongea kwa uchungu sana.
Mama Robert aliona maisha ya mtoto wake yanaingia katika shimo refu lenye giza. Akakumbuka siku ya harusi yake jinsi wale watu wa Ismaiya walivyokuja kumteka Robert. Alikumbuka siku ya harusi ya mtoto wake jinsi alivyomuona Ramla akidondoka chini kwa kupigwa risasi. Akahuzunika kuona siku ya harusi ya pekee kwa mwanaye ikigeuka kutoka siku ya furaha kwenda siku ya kilio.

*************************************************​




Ilikuwa ni siku yake ya kwanza tokea alipopata ajali kupata nguvu ya kuweza kuamka kitandani. Hiyo ni baada ya kulala kitandani kwa miezi sita. Leo alijisikia nguvu kidogo ya kuweza kuamka na kutembea katika kile chumba. Akaamka akatembeatembea pale chumbani akiwa pekee yake. Akaenda mlangoni akakitekenya kitasa lakini mlango ulikuwa umefungwa. Akatembea kidogo kuelekea lilipo dirisha akachungulia kwa nje. Akagundua kuwa kile chumba alichokuwepo kilikuwa kipo ghorofa ya tatu. Akatupa macho yake akaona nyumba nyingi za aina mbalimbali. Hakujua kuwa ulikuwa mji gani lakini hakutaka kuamini kuwa pale ni Dar es salaam kutokana na kuwa mandhari ya eneo lile lilikuwa na miinuko miinuko ya hapa na pale. Alijua kuwa jiji la Dar es salaam kwa sehemu kubwa ni tambarare na kama ni miinuko ipo sehemu chache hasa maeneo yaelekeayo Goba. Chini kabisa alimuona Adele akiwa amepumzika pamoja na mtu mmoja ambaye hakuwa anamfahamu. Walikuwa wakinywa juisi ya chungwa kwa mrija. Aliwaona wakiongea na mara kadhaa walikuwa wakicheka. Akafikiri ni namna gani ataweza kutoroka mule ndani. Robert hakutaka hata mara moja aendelee kukaa mule ndani kama mfungwa. Alitaka atoroke akamtafute Ismaiya mwanamke aliyekuwa akimpenda kuliko kitu chochote kile. Lakini donge lilimshuka kooni baada ya kufikiri kuwa upo uwezekano mkubwa kuwa Ismaiya alikuwa amekufa. Akiwa anafikiri hivyo punde mlango ulifunguliwa na Adele akaingia ndani akiwa amebeba juisi ya kopo. Akamsogelea Robert na kutaka kumkumbatia lakini Robert akamzuia kwa mkono. "Usinikumbatie. Nambie Ismaiya yupo wapi?" Robert akasema akimsukuma Adele hali iliyofanya Adele aangushe lile kopo la juisi.

"Wee shetani haunisikii..! Mke wangu yupo wapi?" Robert akafoka kwa sauti hali iliyofanya kile chumba kiwe na uhai.

"Honey. Calm down. Wewe bado unaumwa" Adele aliongea kwa sauti ya mtu mwenye kujali.
"nani honey wako eeh! Nani? Siwezi kuwa na shetani kama wewe" Maneno hayo ya Robert yalimchoma sana Adele. Aliumia kusikia mtu ampendaye akimuita shetani. Lakini lawama zote akampelekea Ismaiya. Aliamini Ismaiya ndiye chanzo cha mambo yote yale. Adele aliamini kuwa huenda Robert alikuwa amelogwa na Ismaiya. Adele aliwahi kusikia kuwa mwanaume akipewa limbwata akili yake yote inakuwa imevurugwa. Muda wote anakuwa anamuwaza mtu mmoja. Hivyo ndivyo alivyokuwa anaamini Adele.

"Sikiliza Robert . Hata kama hunipendi mimi nakupenda" Adele akasema huku akimtazama Robert kwa macho ya kumaanisha.

"Mimi sioni tabu kupigana kufa kupona kwa ajili yako. Robert mimi nitakufa kwa ajili yako" akameza fumba la mate kisha akaendelea.

"Maisha yangu nimeamua kuyahatarisha kwa ajili yako . Nakupe...eenda Robert " Adele aliongea kwa sauti iliyochanganyika na kilio huku akipiga magoti kumbembeleza Robert . Magoti yake yalikanyaga juisi iliyokuwa imemwagika kutoka katika lille kopo hata hivyo hakujali. Alichojali ni kuuteka moyo wa Robert.

Robert akabaki ameduwaa akimtazama Adele. Unajua nini. Adele ni mwanamke aliyebarikiwa lugha na sauti yenye kushawishi. Alikuwa ni mwanamke mwenye uwezo wa kuigiza onyesho lolote ambalo angepewa na muongoza filamu. Sembuse onyesho hilo la mapenzi yake kwa mtu ampendaye. “Robert naomba unisamehe. Nimegundua bila wewe maisha yangu hayawezekani. Wewe ni kama pumzi yangu. Ndio maana na kuvuta uingie ndani yangu na sitaki nikutoe. Wewe ndiye roho yangu. Ndio maana nakupigania ili mtu mwingine asikuchukue. Tafadhali Robert ..." Adele akaendelea kulalama akiwa amepiga magoti akiishika mikono ya Robert . Akakumbuka jambo. Akasimama mbele ya uso wa Robert wakawa wanatazamana.

"Njoo huku" akasema huku akigeuka kuelekea mlangoni. Alipofika mlangoni akageuka tena kuona kama Robert alikuwa akimfuata. Lakini haikuwa hivyo. Robert alikuwa amesimama akimtazama tuu.

"Honey twende basi" akasisitiza. Robert akapiga hatua polepole kumfuata Adele pale mlangoni. Wakapita kwenye korido ndefu kisha wakaingia kwenye chumba cha lifti. Adele alibonyeza kitufe kilichoandikwa G yaani ground. Dakika moja walikuwa wamefika chini kabisa. Adele akataka kumshika mkono Robert lakini Robert alikwepesha mkono. Wakatembea bila kuongea mpaka waliposimama mbele ya mlango ambapo Adele alichukua funguo na kufungua ule mlango. Ilikuwa ni sebule kubwa yenye samani za kisasa kutoka uturuki. Masofa yalizunguka kijimeza cha kioo ambacho ndani yake kulikuwa na samaki wa urembo waliokuwa wakiogelea. Pia kulikuwa na luninga kubwa ya kisasa ya lg ikiwa imebandikwa ukutani. Juu ya luninga kulikuwa na saa kubwa ya ukutani iliyokuwa ikionyesha ni saa tisa mchana. Pia kulikuwa na midoli midoli iliyofanya sebule ile izidi kuvutia. Adele alimkaribisha Robert ambaye alikuwa amesimama akishangaa mandhari ya sebule ile. Hakutaka kukaa alibaki amesimama akimtazama Adele aliyeenda kuwasha luninga. Punde luninga ikaonyesha msafara wa watu waliobeba jeneza wakiwa wanaimba nyimbo za mazishi. Akagundua kuwa ule ulikuwa ni msiba wa kikristo kutokana na kuwaona wanawake wakiongozana na wanaume kwenda makaburini kuzika. Punde akamuona Mama yake Ismaiya akiwa analia. Alishtuka sana. Akili ilimkimbia na hisia za huzuni zikamzunguka. Hakutaka kujiongopea kuwa ule ulikuwa ni msiba wa Ismaiya mpenzi wake. Angewezaje kujiongopea ikiwa alimuona Mama yake Ismaiya akilia kama mtoto mdogo. Kilio kile kilimuambia jambo moja tuu kuwa kinachomfanya mtu alie vile ni tukio la kuondokewa na mtu ampendaye. Asingejiongopea tena alipomuona baba yake Ismaiya akiwa kavaa suti nyeusi na miwani nyeusi huku uso wake ukiwa na dalili zote za kuomboleza. Moyo wake ulikufa ganzi na kupondeka pondeka alipomuona mdogo wake Ismaiya aitwaye Evelyne akiwa amebeba msalaba ulioandikwa jina la mpenzi wake Ismaiya. akatazama mahali palipoandikwa siku aliyozaliwa na siku aliyokufa akagundua kuwa ilikuwa imepita miezi sita tokea Ismaiya afariki. Walimfikisha makaburini ambapo tayari kaburi lilikuwa limeshachimbwa. Mchungaji aliendesha mazishi na muda wa kuliingiza jeneza ndani ya kaburi ulikuwa umewadia.

"Tafadhali msimzike jamani. Msimzike! Subirini nyie watu" Robert akasema kama mtu aliyechanganyikiwa, muda wote machozi yalikuwa yanatoka. Robert akahisi uchungu mkali moyoni mwake ukipita kama kichomi. Wakati huo Adele alikuwa akimtazama kama mtu asemaye kuwa umeshajua alipo Ismaiya.

"Wewe ndiye uliyemuua Ismaiya. Wewe ni muuaji" Robert akamgeukia Ismaiya akimtazama kwa chuki. "Sikuwa na lengo la kumuua Ismaiya. Nilikuwa na lengo la kukupata wewe. Bahati mbaya rafiki yangu Adele aliumia sana siku ile. Alijeruhika vibaya sana. Hali iliyopelekea kupoteza maisha siku ileile" Adele akasema. Machozi laini yalilamba mashavu yake huku mdomo wake ukianza kutetemeka. Jambo hili lilimfanya Robert amuonee huruma. Maneno ya Adele yalimuingia akilini. Akawaza huenda ni kweli Adele hakuwa na lengo la kumuua Ismaiya kama alivyosema bali ilitokea tu bahati mbaya. Akakumbuka jinsi Adele na Ismaiya walivyokuwa marafiki walioshibana ungesema ni ndugu wa damu. Walikula pamoja. Walilala pamoja. Walikuwa wakivaa nguo zinazofanana mithili ya wachezaji wa mpira. Walivaliana viatu kutokana na miguu yao kulingana. Walitamani kuvaliana nguo lakini hilo halikuwezekana kutokana na kuwa Ismaiya alikuwa na makalio makubwa kumzidi Adele.

"Siwezi kumuamini shetani. Siwezi nasema" Robert akabwatuka huku akimsogelea Adele aliyekuwa ameangalia chini. "Umemuua Ismaiya kwa ufedhuli wako. Alafu unasema bahati mbaya. Unataka kuniletea uongo wako wa kipuuzi! Unafikiri nitakuamini eeh!" Robert akasema kwa sauti ya juu mdomo wake ukiwa umeukaribia uso wa Adele aliyekuwa bado ametazama chini kwa aibu.

"Ramla naye utasema bahati mbaya eeehe! Alafu ati unaongea upuuzi wako. Ati unanipenda..." Robert akasema kwa sauti ya chini huku akimzunguka Adele ambaye alikuwa kasimama palepale akiwa ameangalia chini. Alifika nyuma ya mgongo wa Adele akasogelea sikio lake. Kisha akaanza kuongea kwa sauti ya kunong'ona kwenye sikio la Adele.

"Adele umeutonesha moyo wangu. Umeusagasaga umekuwa kama unga. Umemuua mpenzi wangu. Adele kwa hili sitokusamehe. Umevuka mipaka ya uvumilivu wangu. Nitakuua kifo cha maumivu makali kwa mkono wangu" akavuta pumzi kidogo na kumeva fumba la mate.

"Adele sitokusamehe" hapa akapayuka kwa sauti hali iliyomshtua Adele kutokana na sikio lake kushindwa kuhimili mawimbi ya sauti iliyotolewa na Robert.





*************************************************​



Kilikuwa ni chumba chenye giza totoro. Punde taa ya chemli ikawashwa hali iliyopelekea giza kukimbia. Aliyekuwa ameiwasha ile taa alikuwa ni mtu mweusi tii kama mkaa. Alikuwa ameshika ndoo ya maji ya baridi yenye barafu ndogondogo. Akamtazama Sajenti Warioba aliyekuwa bado hajazinduka akiwa amefungwa kwenye nguzo akiwa ananing'inia. Akammwagia yale maji ya baridi pwaaaah! Hali iliyofanya akili za Sajenti Warioba kumrudia. Sajenti Warioba alipumua harakaharaka kama mbwa panya aliyekoswa na mtego. Yale maji ya baridi ndio yaliyomfanya apumue hivyo. Alihisi baridi ikiingia mwili kwake. Yule mtu mweusi akamsogelea Sajenti Warioba akiwa kashika mjeledi. Akamchapa tumboni kwa nguvu. Sajenti Warioba akasikia uchungu sana lakini alijikaza. Yule mtu mweusi kama msudani akakunja uso wake kidogo kisha akaanza kumcharaza mijeledi hovyohovyo Sajenti Warioba. Sajenti alitoa sauti za uchungu akilia kama mtoto mdogo. Maumivu aliyokuwa anayasikia yalikuwa makali mno. Ndani ya dakika tano Sajenti Warioba alikuwa yupo hoi akiwa kachakaa. Mwili wake ulivuja damu kutokana na mikwaju mikali aliyoipata. Alihisi maumivu makali sana. Donge kubwa la uchungu lilipita kooni mwake likasababisha koo kukauka. Akahisi kiu ya maji. Lakini asingethubutu kumuomba yule mtu mweusi katili aliyekuwa akifurahi maumivu yake.

"Wewe ni nani. unatoka wapi?" yule mtu mweusi tii akamuuliza Sajenti Warioba huku akijifuta jasho usoni mwake. Usijiulize jasho linatokana na nini. Unafikri kazi aliyoifanya ya kumcharaza mijeledi Sajenti ilikuwa ni ndogo. Alimchapa haswa mpaka akachakaa. "Wee mbuzi si ninakuuliza… Wewe ni nani?" yule mtu mweusi mwenye roho mbaya akamuuliza huku akimpiga ngumi ya uso iliyochana mdomo wa Sajenti. Kama ni ngumi basi Sajenti Warioba alikiri ile ilikuwa ngumi. Uchungu wake hakuweza kuufananisha. Akalamba mdomo wake uliokuwa ukivuja damu.

"Nitakuua wewe kenge. Unajifanya mgumu ehhe! Hahahaha! Hapa utasema tuu" yule mtu mweusi aliongea kwa majigambo huku akicheka kwa dharau. Yule mtu mweusi asiye na jina akaondoka kwenye kile chumba akarudishia mlango. Sajenti Warioba akaona afadhali. Aliona ni muda wa kupumua baada ya kipigo kikali. Kumbe alikuwa anajidanganya. Alishangaa kumuona yule mtu akifungua mlango na kuingia ndani akiwa kabeba kikopo kikubwa kama kikopo cha mafuta ya kimbo. Yule mtu mweusi akasogea pale alipokuwa Sajenti Warioba. "Wewe si unajifanya mbishi! Hapa utasema" aliongea hivyo huku akifungua kile kikopo. Mule ndani ya kikopo kulikuwa na siafu wengi mno. Siafu wale walikuwa na hasira kama wamevutishwa bangi. Yule mtu akawamwaga kwenye kichwa cha Sajenti. "Mamaaa! Ooooh! Watoe! Watoe! Nitasema yote. Watoe niseme" Sajenti Warioba alipiga mayowe kama mbwa koko aliyepigwa jiwe na wahuni. Wale siafu walimshambulia usoni. Wengi waling'ang'ania puani. Wengine masikioni, wengine walitaka kuingia ndani ya matundu ya pua na masikio.siafu wawili walishikilia kipande cha mdomo kilichopasuka kutokana na kupigwa ngumi kali na lile jitu jeusi lisilo na huruma. Sajenti Warioba ilibidi afunge mdomo ili siafu wasiingie mdomoni. Hata hivyo wapo siafu wachache ambao aliwafungia ndani ya mdomo. Walimng'ata ulimi na fizi. Pia aliyafumba macho yake ili wale siafu wasimdhuru machoni. Hata hivyo wale siafu walikuwa ni wajeuri na wakatili kama yule mtu mweusi mwenye roho mbaya kama shetani. Sajenti Warioba hakuwahi kupata maumivu makali kama yale. Awali aliwahi kung'atwa na nyuki lakini maumivu yake hayakuzidi maumivu ya kung’atwa na siafu. Hata hivyo aling’atwa nyuki mmoja na leo ni kundi la siafu wakatili wenye sumu kali wa yule bwana mweusi kama jinamizi. Akatamani kuwaondoa na mkono lakini mikono yake ilikuwa imefungwa. Akalia sana wakati yule mtu mweusi akiwa amewasha sigara yake na kuanza kuvuta. Alikuwa akivuta alafu ule moshi akawa anampulizia Sajenti usoni. Jambo hilo lilikuwa linawakera wale siafu. Ni kama ndio alikuwa akiwaambia muumeni zaidi na zaidi. Nao walifanya kama yalivyo mawazo yake. Sajenti Warioba alihisi uvumilivu ukimshinda. Akahisi kamba za uvumilivu wake zikilegea. Alikumbuka kuwa moja ya kazi ya askari Polisi tena mpelelezi kama yeye ni kulinda siri hata ikibidi kufa. Lakini leo siafu walimdhibiti vilivyo. Tayari siafu wengine walikuwa wametoboa mlango wa jicho karibu na kope. Mmmh! Sajenti Warioba alipoona hivi akajua asipofanya kitu macho yake yatafikiwa na kutobolewa na wale siafu wabaya wa mtu yule asiye na jina. "Wewe mtu! Watoe niseme" Sajenti Warioba akasema kwa kupagawa kutokana na siafu wengine kuingia mdomoni baada ya kuachia mdomo wake wazi.

"Hahaha! Nilikuambia utasema tuu. Sasa sema hivyo hivyo. Wewe si unajifanya nunda" yule mtu akasema huku moshi wa sigara ukitoka puani. "Naitwa Aidan Kaaya. Ni ndugu yake na yule mtoto niliyekuwa namchungulia pale dirishani" Sajenti Warioba akasema akimdanganya yule mtu mweusi. Sajenti Warioba aliamua kutumia jina hilo kutokana na alivyomuona yule kijana. Alivyomuona alifanana na watu wa arusha kama sio kilimanjaro. Lafudhi yake pia aliisikia na kuifananisha na watu wa arusha au wachaga. Hivyo kutumia jina la ukoo wa kaaya alijua siyo rahisi kuwa mbali na ukweli. Maneno hayo yakamfubaza kwa upesi yule mtu mweusi. Kutokana na ukweli kuwa yule kijana aliyekuwa na lile jimama chumbani, alikuwa akitokea arusha. Ingawaje ukoo wake haukuwa ni kaaya bali ni Laizer.

"Anaitwa nani huyo kijana" yule mtu mweusi aliuliza huku akimpulizia moshi wa sigara Sajenti Warioba kuwashtua siafu waliokuwa kama wamelegeza midomo yao. Jambo hilo likaamsha mchecheto kwa wale siafu. Wakamng'ata kwa ukali zaidi. Swali hilo alijua ni mtego, Akikosea jina la yule kijana ni wazi angeonekana muongo. Akatafuta koo maarufu za arusha akalipata jina la Laizer. "Anaitwa Nickson Laizar na mimi ni mjomba wake" Sajenti Warioba alimjibu huku akijitahidi kutingisha kichwa chake akijaribu kuwadondosha wale siafu waliokuwa wakimng’ata lakini hakufanikiwa. Jibu hilo likamfanya yule mtu mweusi kuamini kidogo maneno ya Sajenti Warioba ingawaje yule kijana hakuwa akiitwa nickson bali alikuwa akiitwa Joseph Laizer. Alijua huenda yule kijana alibadili jina siku ile walipomteka. Yule mtu mweusi akatoka mule chumbani. Hali iliyomfanya Sajenti Warioba kupiga kelele akimuita aje amtoe wale siafu. Hata hivyo yule mtu mweusi alikuwa kama kaziba masikio kwa pamba. Alitoka na kupotea. Punde mlango ulifunguka. Yule mtu mweusi akaingia akiwa na yule Mama wa makamo aliyekuwa amevua nguo mbele ya kijana Joseph. Nyuma yao alikuwepo Joseph Laizer. Moyo wa Sajenti Warioba ukaingiwa na upepo wa hofu. Akahisi anaenda kuumbuka. Akajua kama yule kijana akiulizwa na akasema hamjui basi huo ndio utakuwa mwisho wa maisha yake.

"Dogo Joseph, unamjua huyu mtu hapa" yule mtu mweusi mwenye sura mbaya aliongea akimnyooshea mkono Sajenti Warioba. Joseph akamtazama kwa kitambo. Pia Sajenti Warioba alikuwa akimtazama Joseph kwa huruma. Alijua muda ule Joseph ndiye alikuwa ameshikilia hatma ya maisha yake. Kimoyomoyo alikuwa akimuambia Joseph. " wewe Joseph, sema unanifahamu. Nakuomba. Nitakutoa humu. Sema unanijua tafadhali" yalikuwa ni mawazo ya Sajenti Warioba aliyekuwa akitazamana na Joseph. Joseph akanyanyua mdomo lakini kabla hajafanya hivyo Sajenti Warioba akaropoka.

"Wewe Mama hivi huoni aibu kumuwekea mtoto mdogo kono lako kwenye bega lake. Embu toa huo mkono" Kitendo cha Sajenti Warioba kuongea hivyo kiliamsha hasira za yule mtu mweusi na lile jimama. Wakamsogelea na kuanza kumpiga. Yule mtu alimpiga ngumi nyingi za tumbo hali iliyomfanya Sajenti Warioba kutapika damu. Jambo hilo likamfanya Joseph amuonee huruma. Sajenti Warioba alifanya hivyo makusudi kutokana na kuona kuwa Joseph alitaka kusema hamjui. Hii ilikuwa nafasi ya kuweza kumpa ishara Joseph kuwa aseme anamjua. Joseph akamtazama Sajenti jinsi alivyokuwa akitoa udenda wa damu mdomoni. Aliyatazama yale makovu mabichi ya mijeledi aliyochapwa Sajenti. Akawatazama wale siafu wabaya waliokuwa wakiushambulia uso wake. Huruma ilimuingia. Alijua kuwa Sajenti Warioba hakuwa na kosa lolote. Kimya kidogo kikatokea huku jibu la Joseph likisubiriwa kama filimbi ya mwisho katika mpira.

"Kohoo! Kohoo!" Joseph akakohoa kama mtu anayesafisha koo lake. Kitendo cha Joseph kukohoa kilimshtua sana sajent. Akajua sasa muda umefika wa yeye kusomewa hukumu yake. Alimtazama Joseph kwa huruma zote. Joseph alikuwa ameangalia chini tayari kwa kutoa maamuzi.
"Namfahamu" Joseph akajibu akiinua uso wake kumtazama yule mtu mweusi katili asiye na huruma. Jibu hilo lilimfanya sajent Warioba kushusha pumzi nzito mithili ya bata dume. Yule mtu mweusi akachukua ule mjeledi akaanza kumchapa nao tena Sajenti Warioba. Muda huu alimchapa mpaka akapoteza fahamu.



SURA YA PILI


Ilikuwa ni mtaa wa gizaasali uliopo mbezi beach ambapo Adelle alikuwa ameikodisha. Wakiwa ndani ya nyumba hiyo ya kisasa Adele akaagiza bodaboda amletee chakula. Ndani ya dakika kumi na tano bodaboda alikuwa getini akiwa kabeba chakula. Adele akaandaa chakula mezani akiwa kavalia nguo nyepesi iliyoonyesha nguo yake ya ndani. Alivaa makusudi nguo hiyo ili aitege akili ya Robert aliyekuwa amelala kwenye sofa. Adele alikuwa akimkata kijicho upembe Robert kuona kama anamuangalia. Alimshuhudia Robert akiyakodolea macho mapaja yake kwa hamu kubwa. Jambo hili lilimfurahisha sana Adele. Alijua kuwa Robert ni mwanaume asingeweza kuruka mitego yake. Adele akaanza kuimba nyimbo za kwao huko tanga.

"ooh mimi ni wako. Ooh kila kitu changu chako. Miguu mpaka kichwa vyote vyako. Siyo upaja wala macho mpenzi pakua kwa lako jiko"Adele kwa nyimbo na misemo alishindikana miaka mingi iliyopita. Aliimudu vyema sanaa ya ushairi na semi. Aliimba wimbo huo kwa sauti nyororo ya kumlaza simba mwendapole ambaye alikuwa akimtazama. Wakati akiimba pia alikuwa akinengua akikichezesha kiuno chake laini kilichoshikiliwa na shanga za kidigo. Looh! Kama ni mtego huyu alikuwa fundi wa mitego. Hakuna mwanaume ambaye angetegwa na Adele asiingie kingi. Robert aliduwaa alipoona kiuno cha Adele kikizungushwa kwa madeko na madaha. akamtazama Adele ambaye alikuwa anamuangalia macho yakiwa yamelegea huku ameung'ata mdomo wake kidogo. Adele jamani! Adele wewe. Adele kiboko ya wanaume. Siyo kwa madaha hayo. Ungedhani ni mlimbwende wa kimataifa anayetumbuiza jukwaani. Robert akahisi mwili ukipata hisia za mapenzi. Mapigo ya moyo yalibadilisha miondoko yake. Yalikuwa yakikimbia lakini kila yalipojaribu kukimbia ndivyo mitego ya Adele ilivyokuwa inayafukuzia. Adele alikuwa amesimama mbele ya Robert akiwa kashika sahani yenye vipande vya nyama ya kuku. Akamsogezea Robert mdomoni ili amlishe. Masikini Robert wa watu alikuwa kaduwaa. Akashtuka kipande cha nyama kikigusa mdomo wake. Akashusha pumzi kama mtu aliyemaliza mbio ndefu.

"Acha! Nitakula mwenyewe" Robert akaongea akikwepesha mdomo wake. Adele akatabasamu kisha akamkabidhi Robert ile sahani yenye vipande vya nyama ya kuku. Hakuwa na wasiwasi. Moyoni alisema; kuku wangu manati ya nini. Haha! Labda siyo mimi Adele mtoto wa kidigo. Akaenda kuwasha luninga kubwa ya bapa. Aliiwasha kisha akaenda chumbani. Akarudi akiwa kashika flash mkononi. Akaichomeka na punde muziki ulianza kuimba. Akamtazama Robert kisha akatabasamu kama ilivyokawaida yake. Robert alikuwa akila nyama kama mtu ambaye hajala muda mrefu. Ni kweli kabisa. Ni zaidi ya miezi saba imepita nyama haijaingia katika mdomo wa Robert . Hii ni kutokana alikuwa amelazwa kwa muda mrefu akiwa hoi kitandani. Jambo hili ndilo lililomfanya Robert azishambulie zile nyama. Adele akaenda kwenye jokofu akatoa chupa mbili za redwine akammiminia kwenye glass na kumpelekea. Hapa alijua kuwa tayari alikuwa amemaliza kazi. Akasimama mbele karibu na luninga jambo hili alilifanya makusudi kumziba Robert aliyekuwa akitazama muziki uliokuwa unaendelea. Kisha akaanza kucheza kidogokidogo kufuatana na mdundo wa muziki. Robert sasa aliacha kuiangalia luninga akawa anamuangalia Adele. Adele alijua kucheza buana. Aliwashinda hata wale waliokuwa kwenye luninga. Hii ndio ilimfanya Robert amuangalie. Punde uliingia muziki kutoka kabila la warazamo. Hapa ndipo kasheshe lilipokuwa. Adele alikata mauno duniani haijawahi kutokea. Robert akakiri moyoni kuwa hakuwahi muona mcheza ngoma kama Adele. Kumbukumbu zake hazikumuonyesha kama aliwahi kuona mtu achezaye kama Adele.

Ilikuwa ngoma ya kizaramo alimaarufu kama gombesugu. Ilikuwa ngoma haswa inayohitaji mchezaji ajue kukata mauno. Adele hilo alilimudu kwa asilimia zote. Adele akajibinua makalio yake na kuyatikisa tikitikitikitiki... Mama weee! Robert akapumbazika akawa amebaki ameshika kipande cha nyama mdomoni asijue akipeleke mdomoni au akirudishe kwenye sahani. Alinata mithili ya sanamu la michelini. Mdomo wake ulibaki wazi huku macho akiwa kayatoa nje. Alishangaa jinsi makalio ya Adele yalivyokuwa yakitikisika huku shanga kiunoni zikicheza ukutiukuti. Huyo ndiye Adele mtoto wa kidigo. Mwanamke aliyeshindikana sokoni kwa mkopo na kwa pesa mkononi. Muda wa kulala ulifika. Hata hivyo pamoja na mbwembwe zote za Adele lakini Robert hakutaka kulala naye. Angeweza vipi kulala na mwanamke aliyesababisha kifo cha mtu ampendaye. Angeweza vipi kulala na mwanamke aliyesababisha yeye kupata ajali nusura apoteze maisha. Hilo aliliona ni jambo ambalo kamwe lisingewezekana.

"Honey tulale wote kwa leo. Hatutafanya chochote" Adele akasema.

"Hilo haliwezekani Adele. Nielewe" kimya kidogo kilitokea wakati Adele anamtazama Robert bila kuongea lolote.

"Mimi naondoka. Naenda kulala kwangu".
"Haa! Unaenda wapi usiku huu. Muda umeenda sana mume wangu"

"Mimi siyo mume wako. Nimekuambia usiniite hivyo"

"Jamani kwani ni kosa kukuita hivyo, Anyway tuachane na hayo. Basi utalala chumba kile. Nami nitalala hiki. Sawa!"
Adele akasema akimuonyesha Robert vyumba vya kulalia. Robert akaondoka kwenda kwenye chumba alichoonyeshwa na Adele. Adele alimfuata nyuma nyuma kama bata na watoto wake. Alipofika chumbani Robert alishangaa kumuona Adele nyuma yake.

"Adele nimechoka. Nahitaji kupumzika"

"nimekuja kukuaga mpenzi. Mwaaah"
Adele akasema kisha akamkumbatia kwa nguvu na kumbusu Robert katika shavu lake kwa lazima. Robert akamsukuma hali iliyofanya Adele apepesuke. Adele akatabasamu kisha akasema. "Nakupenda mume wangu. Ulale salama" Maneno hayo aliyatoa akidengua kisha akaondoka. Robert akaenda kufunga mlango na funguo ili kukwepa kero za Adele. Aliingia bafuni kuoga kisha akatoka. Akajilaza kitandani. Mawazo mengi yakamjia. Aliwaza juu ya yote yaliyokuwa yametokea. Alikumbuka siku ile ya harusi ilivyokuwa imependeza lakini baadaye ikageuka kilio. Alimkumbuka Ramla aliyekuwa mshenga wa Adele jinsi alivyopigwa risasi. Kumbukumbu hii ilimtia uchungu sana. Moyoni alijisemea; nisamehe Ramla hukuwa na hatia yoyote. Akamkumbuka Ismaiya mwanamke aliyekuwa anampenda kuliko jambo lolote lile duniani. Alikumbuka alivyodanganywa na Adele kuwa Ismaiya alikufa kwenye ajali ya ndege ya malaysia. Punde uso wake ulikunjuka kwa tabasamu. Ni kutokana na kumbukumbu ya walivyokuwa wakifanya mapenzi na Ismaiya mara ya mwisho wakiwa maeneo ya Bunju. Akakumbuka jinsi walivyofurahiana. Kila mmoja alimchezea mwenzake kwa kadiri alivyoona inampendeza. Lakini tabasamu liliyeyuka alipoikumbuka ajali iliyosababishwa na Adele aliyerusha risasi kwenye gari lao likapinduka. Mwisho machozi yalimtoka alipoona jeneza la Ismaiya likibebwa kwenda makaburini.. Hiyo yote ilikuwa kumbukumbu. Akamuona Ismaiya akiwa anachuma maua kwenye bustani iliyokuwa kwenye uwanda wa tambarare akiwa kavaa dera na mtandio. Moyo ulilipuka. Akaogopa sana. Robert akapiga hatua kumsogelea huku akimuita.

"Ismaiya! Ismaiya!" Ismaiya akageuka na alipomuona Robert akatabasamu.

"Ismaiya mpenzi. Nilidhani umekufa kumbe upo hai mpenzi?" Robert akasema huku akipiga hatua kumfuata Ismaiya aliyekuwa umbali wa mita kumi.

"Mimi sijafa. Penzi letu ndio limekufa" Ismaiya akajibu akiwa ameshika ua zuri lenye rangi ya njano ya papai. Punde Adele akatokea kwa nyuma na kumchoma Ismaiya kisu cha mgongo. Robert akashtuka. Kumbe alikuwa akiota. Robert alijikuta yupo kitandani jasho likiwa linamtoka huku akipumua kwa pupa. Ni ndoto hiyo mbaya iliyomfanya ashtuke usingizini. Hata hivyo tayari kulikuwa kumekucha miale ya jua ilikuwa ikirandaranda katika chumba kile. Ndege walikuwa wakiimba nyimbo za sifa kuikaribisha siku nyingine mpya.

Robert akaenda kuoga. Akiwa bafuni alimsikia Adele akibisha hodi.

‘'Nipo bafuni. Nakuja adele" Robert akasema. Akamaliza kujiandaa akaelekea sebuleni ambapo alimkuta Adele akiwa kajilaza kwenye sofa akiangalia luninga. Adele alipomuona Robert akaamka na kumkumbatia kwa nguvu sana. Akamlazimisha denda mpaka akafanikiwa kubadilishana ndimi na Robert . Jambo hili likaibua hisia kali za mapenzi kwa Robert . Adele alijua ile ndio nafasi pekee ya kuonyesha ufundi wake. Alijua kama ataipoteza ile nafasi basi asingepata nafasi ingine. akamshika Robert kwenye maeneo yake nyeti kwa ustadi wa hali ya juu huku wakiendelea kupeana asali ya mdomoni. Hali ya Robert ikazidi kuwa mbaya. Hamu ya mapenzi zikamzidi nguvu. Akajikuta akimuachia nafasi Adele ambaye alionekana kukamia. Adele akamsukuma Robert kwenye sofa na kwa haraka aliwahi ilipo zipu ya suruali akaifungua na kupeleka suruali chini. Sasa Robert alibakiwa tuu na pensi ya ndani. Ulikuwa wakati mzuri wa Adele kuchota asali katika mzinga. Robert alikuwa amepagawa mno. Mbaya zaidi ni kuwa Adele hakuwa amevaa kitu chochote ndani isipokuwa kanga nyepesi. Jambo hili lilizidisha uhondo kwa Robert.

"Mimi sijafa ila mapenzi yetu ndio yamekufa" Robert alikumbuka maneno ya Ismaiya aliyoyaota usiku wa jana. Maneno hayo yalimrudisha kwenye akili yake. Akamsukuma Adele kwa nguvu chini, kanga aliyoivaa Adele ikachomoka kiunoni akabaki uchi kama alivyozaliwa. Adele hakuamini kama hatua aliyofikia; Robert angeweza kufanya vile. Kwa hatua ile alijua tayari mtego wake umefanikiwa lakini haikuwa hivyo, Robert alikuwa ni mtu makini na mwenye msimamo thabiti linapokuja suala la mapenzi. "Hutanidanganya kama kipindi kile Adele" Robert alimuambia Adele huku akimbetulia mdomo kwa dharau. Adele bado alikuwa pale chini akiwa amejishika kiuno kama mtu aliyeumia. "Ulinidanganya Ismaiya alikufa kwenye ndege ya malaysia. Leo hutanidanganya"

Robert akasema huku akiamka kwenye sofa. Akavaa suruali yake iliyovuliwa na Adele.

"Nikudanganye kipi. Kwamba Ismaiya hajafa? Nitakupeleka kwenye kaburi lake ili uamini" Adele akasema kwa hasira akiwa bado palepale chini. "Kumbe hakufa kwenye ndege si ndio wee kenge? Hivi wewe mwanamke huyo shetani uliyenaye anakulipa nini mpaka ufanye mambo yote haya?" Robert akadakia kabla Adele hajamaliza kuongea. Maneno hayo Adele hakuwa na lakujibu. Akabaki amemtazama tuu Robert. "Twende kwenye kaburi la Ismaiya. Usije ukawa hata hili umenidanganya. Amka twende" Robert akasema huku akienda ulipo mlango wa kutokea.

"Sasa kama Ismaiya hajafa tunaenda kwenye kaburi la nani? Si umesema mimi ni muongo. Basi hakuna haja ya kwenda” Adele alipoona Robert amemkata jicho la hasira akasema; “Sawa subiri nikavae nguo ili twende maana unavyoniangalia”

"Kavae unasubiri nini hapo chini?"
. Adele akaamka pale chini na kujifunga kanga yake iliyochomoka baada ya kusukumwa. "Basi kunywa chai nikienda kujiandaa" Adele alimuomba Robert aliyekuwa akimtazama kwa hasira. Maneno hayo yalimpoza kidogo Robert lakini hayakumshawishi.

"Sina haja na chai. Namtaka Ismaiya wangu" Robert alibwatuka kama mlevi. Kisha akaendelea. "Nakupa dakika tano. Hujamaliza naondoka"

"Yamekuwa hayo tena. Sawa nakuja"
Adele alijibu huku akienda chumbani kujiandaa.

Wakafika kwenye makaburi ya kinondoni na moja kwa moja Adele alimpeleka lilipokaburi la Ismaiya.

"Hapa ndipo alipopumzishwa rafiki yangu kipenzi Ismaiya" Adele akasema huku akipiga magoti kwenye kaburi la Ismaiya. Akasujudu akachota mchanga kwenye mikono yake akalia. "Maiya kipenzi changu. Nisamehe kwa niliyokufanyia rafiki yangu. Nimekukumbuka sana"
Adele akasema huku akilia kwa sauti ya kwikwi. Akiwa kavaa baibui jeusi lenye vishikizo kwa mbele. Kichwani amevaa lemba na miwani ya rangi nyeusi. Huku masikioni akiwa amevaa hereni za mduara zenye rangi ya dhahabu. Robert akasimama mbele ya msalaba wa kaburi la Ismaiya ambapo akaona jina la Ismaiya na umri aliozaliwa na tarehe aliyofariki. Aligundua kuwa Ismaiya ni kweli alikufa siku ileile waliyopata ajali. Robert akajikuta akitoa machozi bila kujua. Akalia sana. Alijiona yeye ndiye chanzo cha kifo cha Ismaiya. Alijua bila yeye Ismaiya leo hii angekuwa hai. Mbaya zaidi Ismaiya alikufa kwenye tukio la kutetea penzi lao. Alikufa akirusha risasi kuwashambulia watu waliotaka kumtenganisha na yeye. Alikuwa akikimbiza gari akikiwakimbia watu wanaotaka kumtenga naye. Yote hayo Robert alikuwa akiyawaza. Lakini alishindwa kukikimbia kifo ambacho kimemtenganisha naye daima.

"Kifo njoo hapa nikupige. Njoo hapa. Kama wewe ni kidume. Njoo....." Robert akapayuka kwa sauti huku akivuta ule msalaba kama anayetaka kuung'oa.

"Kama ungekuwa na nguvu si ungenichukua mimi eeh...! Mbona ukamchukua msichana wa watu. Kifo njoo hapa" akasema huku akiuangalia msalaba kana kwamba msalaba ndio hicho kifo alichokuwa akikiita. Kuna muda alikuwa anaunyooshea ule msalaba kidole. Adele aliona jinsi Robert alivyokuwa anauchungu na kuchanganyikiwa. Akajuta kwa tukio alilokuwa amelifanya, lililoondoa uhai wa rafiki yake kipenzi. Lakini majuto siku zote ni mjukuu. Kaburi la Ismaiya bado lilikuwa halijajengewa. Lilikuwa na maua machache. Robert hakuona ua lake katika kaburi la mpenzi wake. "Ona! Ona! Ona sasa. Kaburi la mtu ninayempenda halina hata ua langu. Maiya.. Maiya mama yangu...eee" Akaanza kulia tena huku akishika maua yaliyowekwa juu ya kaburi la Ismaiya. Akatoa ua moja baada ya ua jingine huku akilia kwa uchungu. Punde akanyanyua ua moja na jambo lisilotarajiwa likajitokeza. Kilianguka kipande kidogo cha karatasi lilichokunjwa vizuri. Adele naye alikiona. Adele alitaka kukiokota lakini Robert alikuwa mwepesi zaidi yake. Akawahi. Kisha akakifungua. Ile karatasi ilikuwa inamandishi ya wino mweusi yenye hati ya Ismaiya. Wino mweusi uliashiria huzuni na maombolezo. Robert akaanza kusoma wakati Adele akimsogelea karibu na bega lake kwa nyuma.

"Kwako Robert mpenzi. Nimeondoka sitorudi tena. Nimeondoka bila kuagana na wewe kipenzi changu. Nimeenda mahali usikofika. Mapenzi yangu yataisha kwako siku jua likiacha kuangaza. Nitakupenda hata kama sikuoni tena. Nilijitahidi kupigania penzi langu. Ilikuwa haki yangu kukupigania. Lakini... Lakini.. Laki..ni mwenzangu amenishinda. Roobert. Kifo kilimsaidia. Kifo hiko mume wangu kilimsaidia" Robert aliweka kituo akaanza kulia. Yalikuwa maneno makali aliyoyasoma kwenye ile karatasi ambayo aliamini yalikuwa yametoka kwa Ismaiya. Kisha akaendelea kusoma; "Mimi nimekimbia bila kupenda. Mwenzangu alisaidiwa na kifo. Mimi sikuwa na wakunisaidia. Baki salama mume wangu kipenzi. Tutaonana baadaye. Eu te amo ternamente mimi Ismaiya"

"Nakupenda pia mke wangu"
Robert aliyajibu maneno yaliyokuwa yameandikwa Eu te amo ternamente ambayo ni lugha ya kireno yakimaanisha nakupenda sana. Robert alimkamata Adele na kumpiga vichwa vitatu mfululizo. Hali iliyomfanya Adele apige kelele.

"Unaniua! Unaniua Robert " Robert hakujali akaendelea kumpiga akichanganya ngumi na mateke. Adele akaongeza mayowe akiomba msaada.

"Nakuua leo Adele. Nenda ukamlete Ismaiya" Robert akafoka huku akimpiga ngwala Adele ambaye alidondoka chini kama gunia la chumvi. Alimpiga mateke ya tumbo mpaka Adele akaanza kutoa damu za mdomoni huku sauti ikianza kupungua. Punde kundi kubwa la watu lilikuwa likija huku likimrushia mawe Robert.

Robert alipoona watu wanakuja akajua anaweza kuuawa na watu wale. Akamuacha pale chini Adele na kuanza kukimbia. Mawe yalikuwa yakimkosakosa huku akisikia wakiimba mwizi! Mwizi! Kamata mwizi huyo. Robert akaongeza kasi lakini wale watu nao walikamia. Walimfukuza kama paka shume jizi lililoiba nyama ya mabaharia. Bahati haikuwa yake. Alipigwa jiwe la kichwa akadondoka chini. Aliona kizungu zungu na kichwa kilikuwa kizito sana. Akili yake ikamuambia; walimuua Ismaiya na wewe sasa wanakuua. Kimbia Robert . Alijikaza akaamka na kuendelea kukimbia huku akipepesuka. Damu zilimtoka kichwani zikalowesha shati alilokuwa amelivaa. Akaingia kwenye uchochoro mmoja wa mitaa ya kinondoni iliyozunguka yale makaburi. Lakini bado alisikia wale watu waliobeba mawe wakisema mwizi! Mwizi wakija huku wakitupa mawe. Robert akahisi nguvu zikiwa zinamuisha baada ya damu nyingi kuvuja. Masikini Robert akapigwa jiwe jingine la mgongo lililompeleka chini. Hata hivyo alijikaza akaamka. Alijua kama atajilegeza siku ile ndio ingekuwa mwisho wa maisha yake. Akakaza mbio lakini za kujikokota. Alipiga kona akaona nyumba ambayo mlango upo wazi. Akatoma ndani moja kwa moja akaingia chumbani bila hodi mpaka uvunguni.

Kule uvunguni alisikia vishindo vya wale watu waliokuwa wakimkimbiza wakipita huko nje. Moyo wake ulikuwa unadunda sana. Alimuomba Mungu amuepushe na watu wale ambao walitaka kumpiga kwa mawe. Ghafla akasikia wale watu wakimuuliza mwanamke mmoja huko nje.

"Habari za asubuhi Mama. Hujaona mtu yeyote aliyejeruhiwa akikimbia?"

"Mtu akikimbia! Mimi sijaona mtu njia hii" Yule Mama alijibu huku akiwa ameshtushwa na maswali ya wale watu. Robert akiwa chini ya uvungu aliendelea kuomba Mungu wale watu waondoke pale nje. Mungu siyo Athumani wala siyo selemani. Aliwasikia wale watu wakiondoka. Akashusha pumzi nzito mithili ya kobe mzee. Ni kama alikuwa amebeba mzigo mzito. Punde alisikia maji yakimwagwa kwenye pipa lililokuwa sebuleni alipokuwa yule mwanamke. Hapo akajua kuwa yule Mama alikuwa ametoka kuchota maji. Akahisi kichwa kikimzunguka. Macho yakaingiwa na giza zito. Hatimaye alipoteza fahamu.

ITAENDELEA

Jipatie simulizi yote ya MLIO WA RISASI HARUSINI Softcopy kwa Tsh 3,000/= Kitabu Tsh 10,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
Back
Top Bottom