Riwaya: Nitarudi Arusha

NITARUDI ARUSHA V
"Binti?" Niliuliza kusudi ili niipe akili yangu kufikiria zaidi.
" Ndiyo yule uliyemleta"
"Mhhh ....."
"Ndiyo nesi kuna tatizo lolote"Niliamua kukubali baada ya kufikiri kidogo kwani kukataa kungenifanya nitoe majibu ambayo yangeongeza maswali mengi zaidi ya kumtaka mume wa mama John ingawa jibu lile nalo lingeniweka kwenye wakati mgumu wa kuiibu maswali ambayo yangetaka majibu sahihi zaidi.
"Sawa , alikuwa ikihudhuria kliniki wapi?" Alijiuliza swali ambalo hata sikutegemea kuulizwa hivyo kunifanya nijute kudanganya.
''Nesi''Nilimwita nikimshika mkono na kumvutia upande ambao nilikuwa na hakika hakukuwa na mtu aliyetuona ilikuwa ni sehemu iliyozuiwa na nguzo nene za ukuta.
''We vipi mbona unanivuta hivyo kama mbuzi!'' Alishangaa yule nesi ambaye alionekana kunielewa nilichokuwa nikikihitaji wakati ule ambacho ni usiri.
''Sikiliza nesi mie ni msamalia tu nimekutana naye alfajiri hii nilikuwa naelekea mjini nimeamua kumleta hapa apate huduma''Nilijieleza nikimshikia noti kadhaa za shilingi elfu kumi ambazo sikujua hata zilikuwa ngapi.
''Hii ni kwa ajili ya huyu mama naomba msaidie apate huduma'' niliongea nikimkazia macho.
''Usijali nitalisimamia hilo''Alinijibu kwa kifupi akiweka zile hele kwenye mfuko wa vazi lake la kazi na kutaka kuondoka lakini nilimvuta tena mkono lakini alinikonyeza na kunieleza kwa macho kuna wauguzi wengine waliokuwa wakipita.
Nikamwelewa, nikasubiri wale watu wapite kisha akaniachia kadi iliyokuwa na mawasiliano yake.
''Nitafute ukihitaji kujua maendeleo yake''Akaondoka.
Nami nikarejea kule nje kuungana na akina Japhet ambao walikuwa na hofu sana na waliponiona wakanikimbilia na kunitupia swali.
''Anaendeleaje?''
''Anaendelea vizuri msijali ,atapona''Niliwajibu nikiwa nimewashika mikono huku na huku tukitoka na kwenda kukaa nje karibu na lango la kuingilia hospitalini.
Hapo nikakumbuka kuhusu ile picha iliyomfanya mama John kuangua baada ya kuiona, nikachukua simu yangu na kuangalia zile picha kwa umakini zaidi.Kuna kitu kilikuja akilini mwangu baada ya kuzitazama zile picha kwa umakini zaidi.
''Mbona huyu mtoto anafanana sana na John?'' Japhet aliniuliza akinionesha mtoto mmoja aliyekuwa akionekana kwenye zile picha, ni kweli ndicho hata akili yangu ililigundua hilo.
''Huyu ni mdogo wake rafiki yangu mmoja wa chuoni ila kwao ni huku Arusha''Nilieleza.
''Ila wanafanana sana na John mwone huyu mkubwa ,huenda ni ndugu zake na John hawa''
''Kwani mama John alisema ana ndugu zake hapa mjini?''
''Mie hajawahi kuniambia juu ya ndugu zake''Japhet alinijibu akiendelea kuziangalia zile picha lakini wakati huyo John alikuwa kimya sana hata nilipomtazama hakuonekna kuwa na habari na simu.
''Mama atapona John usiwaze sana''Nilimpooza.
''Ulimfanya nini mama yangu?''Aliongea machozi yakimtoka kana kwamba nilikuwa nimemtonesha kidonda na kumruhusu alie.
''Sijamfanya chochote mama , ila atapona''Niliongea nikimsogelea John nikitaka kumlaza miguuni mwangu lakini alisimama na kwenda hatua kama tatu.
''Utakuwa umemfanya kama wale wengine tuu! ona sasa umemuumiza mama yangu''
‘’Wengine wamefanyaje John?’’Nilimuuliza nikimfuata Joh ambaye alionekana kukasirika sana, lakini Japhet akanishika mkono na kunikalisha chini.
‘’Ni habari ndefu sana nitakueleza , naamini utaniaelewa kaka yangu’’Aliongea Japhet wakati nikiwa bado natafakari jambo hilo simu yangu inaita mpigaji ni Alice.
‘’Nipo Moshi mjini nakusubiri’’Ilisikika sauti ya Alice bila hata kunipa nafasi ya kuongea chochote simu ilikatwa.
‘’Nipo kwenye gari nakuja Arusha mpenzi’’Nikaamua kumtumia ujumbe.
‘’Arusha si mahali salama kwako tena mpenzi tafadhari niambie ulipo ili nije, tafadhari ‘’Ujumbe mpya kutoka kwa Alice ulisomeka na kunitesha kiasi cha kuhisi haja ndogo ilikuwa ikikaribia kutoka pengine ilitoka kabisa.
Hapo nikajikuta kwenye mtiohani mkubwa sana wa kuijua hatari iliyokuwa hapo Arusha , ni kuhusu ile simuya hatari niliyokuwa nimepigiwa na wale watu waliodai wangenifuata chuoni? Ni juu ya kifo cha Eric? Ni hatari ipi hiyo?
Sikuwa na jibu nikamtazama Japhet ambaye naye alidai kulikuwa na stori ndefu juu ya mama John ambaye naye alionekana kuwa hatarini kwani hali yake haikuwa nzurio na mwanaye anaamini kuwa mie ndiye sababu ya kuumwa kwake.John anye alikuwa kabaki amesimama machozi yakimtoka akinitazama kwa jicho la chuki.
‘’Ni stori gani hiyo ndugu yangu?’’Nilimuuliza Japhet ambaye alionekana kuwana na mawazo sana.
‘’Kwa kifupi dada (mama John) alikuwa akilala na wanaume wakati mwingine ili apate pesa ya kutulisha hivyo hata John anaamini hata wewe huenda ulikuwa ni mmoja wa waliokuwa wateja wake’’Alininong’oneza Japhet na kunifanya nizidi kuchanganywa na hali ile.
‘’Kwa hiyo hata ujauzito ule huenda asijuenani muhusika wake?’Niliendelea kunong’ona nikimwangalia kwa makini john asije kusikia.
‘’Kwa hiyo mama John ni mjamzito? Hawezi kujua ujauzito wa nani maana kuna wakati analala na wanaume watatu kwa siku, hatojua jamani Mungu kwa nini haya yanatupata?’’
‘’Ameacha lini hiyo tabia?’’ Niliuliza nikataka kujua kama baada ya kuanza kuwasaidia aliweza kuachana na tabia hiyo.
‘’Hajaacha, hata jana walikuja watu wawili wakamfanya walivyojua, tulikuwa tunasikia hivyo hata nilivyokuona nilijua na wewe ulikuwa miongoni mwa waliokuwa wamelala naye’’
‘’Mungu wangu kwa nini ameendelea licha ya kuwasaidia hela ya kutosha tuu?’’
‘’Hata sijui kuna wakati anatuambia kuwa hela huwa anaibiwa na wale watu wanaokuja na tunapomwambiawasije anatuambia bila wao kuja hawezi kuishi.
‘’Nini?’’
______
Meristella Josephat wengi walimwita Stella kama yeye alivyopenda, aliingia jijini Arusha kwa mara uya kwanza akiwa na umri wa miaka kumi na tano akitokea Manyara kipindi hicho ikiwa ni sehemu ya mkoa wa Arusha.Aliingia jijini akiwa na mwenyeji wake ambaye alimwambia angekuja kufanya kazi za ndani jambo ambalo kwake halikuwa ni mtihani kwake kwani aliokuwa ameshachoshwa na maisha ya kijijini, alitamaninaye kuwa mmoja kati ya watu wa mjini.Naam ni naaani angekataa kuja jijini, jiji ambalo lilisifika kama Geniva ya Afrika, jiji lililo na kila kinachotakiwa kuwa nacho ili liwe jiji la kitalii, jiji ambalo kama angekuwa na bahati angekuwa miongoni mwa waafrika wachache wanaojikuta wakioana na wazungu ambao wamezagaa kwa shughuli mbalimbali ukiwemo utalii.
Kuwepo jijini lilikuwa jambo moja lakini jambo lingine lilikuwa ni kupata fursa za jijini ambazo hata kama hata pata mzungu wa kumwoa basi ataolewa na mtu wa mjini ambaye atakuwa ni sehemu ya ukombozi wake, kwani alishawakataa wanaume uchwara ambao tangu akiwa shuleni walikuwa wakimsumbua, hakuwaona wakiwa na chochote cha maana, hawakuwa wasomi, hawakuwa matajiri hata wale walioonekana matajiri kwa kuwa na uwezekano wa kurithi ng’ombe na mifugo mingine ya wazazi wao hakuwaona wakimfaa kwani kama urembo na uzuri alikuwa nao.Aliamini uzuri wake na tabia njema ungemfanya amvutie yeyote huko mjini kutaka kumuoa.
Naam alifanikiwa kuingia jijini na kama alivyotegemea alikuwa kivutio cha kila aliyekuwa akimuona, hata pale nyumbani alipokuwa kifanya kazi za ndani alianza kuwasumbua wengi , vivulana uchwara navyo havikukoma kujipitisha alipokuwa kiishi mradi tuu vipate nafasi ya kumtakia neno la kumtaka lakini hali haikuwa rahisi kama walivyotegemea Stella alikuwa ni mtu aliyejiamini sana na hivyo walijikuta wakiahirisha kusema kila walipotaka kusema.
Mwezi mmoja baada ya Stela kuwa jijini Arusha akiwa na furaha ya maisha mapya alikuja mtu pale nyumbani, mtu ambaye ni kama aliutikisa moyo wake kwani alijikuta akimpenda mara tuu alipomuona.Huyu alikuwa ni mmoja wa watoto ambao wa familia ile, huyo alikuja likizo akitokea shuleni alikokuwa akisoma kidato cha pili.Zile ndoto za kupata mwanaume wa mjini zilianza kumsumbua tena, aliamini Yule alikuwa ni mwanaume wa maisha yake hakutaka kujiuliza kama alimtamani ama alimpenda kweli bali alijiaminisha kuwa alikuwa akimpenda sana.
Aliendelea na kazi zake huku akitamani yule kijana amwambie neno lolote la mapenzi ili aitulize nafsi yake lakini yule kijana hakuonesha kuwa alikuwa akimpenda.Hakukata tama aliamini kabisa ipo siku atauona uzuri wake na kumwambia kuwa anampenda, alijua kuwa huenda hakuonekana kumpenda kwa kuwa alijua alikuwa mfanyakazi wa ndani kutoka kijijini lakini ‘’mapenzi hayachangui’’ aliamini atakuja kupendwa tuu na yule kijana aliyekuwa akimpenda.
Wiki mbili baada ya yule kijana wa kwanza kuja pale nyumbani alipokuwa akifanya kazi alikuja kijana mwingine ambaye alionekana kuwa alikuwa ni mkubwa zaidi ya yule wa kwanza , huyu alikuwa akisoma chuo kikuu cha Dar es saaalam.Huyu licha ya kuwa alivutia zaidi lakini hakuushtua moyo wa Stella.Kwa kifupi Stella hakumpenda kijana huyu aliyeonekana kujiona sana mara nyingi alikuwa akiwa pamoja na baba yake wakienda huku na huko.Baba yake ambaye alikuwa Daktari katika hospitaliya Mount Meru alikuwa akijisia sana kuwa mwanaye alikuwa anaakili sana na alikuwa ni mwanaye aliyempenda zaidi kuliko wote jambo ambalo lilionekana kuwakera hata wanafamilia wengine.
Kijana huyo aliyekuja kufanya mafunzo kwa vitendo katika ofisi za Jumuhia ya Afrika ya mashariki alionekana kuwa ni mtu wa wasichana sana, mara kadhaa Stella aliwafuma wakigombezana na mama yake kwa tabia yake ile akimuona kuwa alikuwa hatarini kuparta magonjwa ya ajabu kwa tabia yake ya zoa zoa.Siku nyingia likuwa halali nyumbani na baba yake siku zote alikuwa akimtetea kuwa alikuwa mwanaume mtu mzima aliyekuwa akijua kutengenisha jema na baya hivyo hakuhitaji kuchungwa kama walivyotakiwa kuchungwa wadogo zake.
Baada ya likizo kuisha yule mdogo aliondoka , Stella alionekaa kukosa raha kwa kuondoka kwake bila kumwambia chochote kuhusu mapenzi lakini hakuwa na namna kwani alijua kwa mwanamke kuanza kumtamkia maneno ya mapenzi mwanaume ni kitu kisicho cha kawaida na hakuwahi kusikia kama kilikuwa ni sahihi hata kwenye zile filamu alizokuwa akiziangalia pale nyumbani mwanaume alikuwa ni mtu wa kusubiri kuanzwa.Aliona pia katika filamu hizo namna wanawake wanaowaanza wanaume wanavyochukuliwa na jamii husika na wanavyoteswa na hao wanaume.
Baada ya yule mdogo wake kuondoka yule kaka mkubwa akabadili tabia yake ya kupenda kutolala nyumbani na kuanza kulala nyumbani na wakati mwingi akiutumia kushinda pale nyumbani huku akijenga urafiki na Stella ambaye alijilazimisha kumzoea yule kaka ambaye alionekana kutokuwa na tabia njema.Katika kushinda nyumbani huko ndiko kulikomfanya Stella akuhisi alikuwa mawindoni kwani kuna nyakati alikuwa akirudi mara tuu baada ya kuondoka na wazazi wake kwenda kazini akijifanya kasahau kitu huku akimpa zawadi nyingi ambazo licha ya kuzipokea Stella hakuzifurahia hivyo alikuwa kizitunza tuu chumbani kwake.
Hali iliendelea hivyo hadi siku mbili kabla ya yule kaka kuondoka na kurudi chuoni .Siku hiyo walibaki wawili pale nyumbani baada ya wazazi kwenda mjini .Stella alikuwa akiafanya usafi mara akaona mtu akifunga milango ya nyumba, alipouliza kwa nini alikuwa akifunga milango hakujibiwa zaidi alimwona mtu huyo akimsogelea.
Hakufanikiwa kukimbia kwani alijikuta kwenye mikono imara , hakufanikiwa kupia kelele kwani alizibwa mdomo na kujikuta akilegea na kukosa nguvu hata ya kuinua hata kope.

Mweh!
 
NITARUDI ARUSHA
Hakufanikiwa kukimbia kwani alijikuta kwenye mikono imara, hakufanikiwa kupia kelele kwani alizibwa mdomo na kujikuta akilegea na kukosa nguvu hata ya kuinua hata kope.Mara akajikuta yupo kwenye ulimwengu mwingine, ulimwengu wa raha na hisia za hali ya juu.Alipojaribu kutamka neno alijikuta akipata kitetemeshi cha mdomo macho nayo yalikuwa ni kama yakiiangalia dari nadhifu iliyokuwa ikizunguka.
Alimwona yule kijana ambaye mwanzoni alihisi alikuwa na nia mbaya kwake kama mtu mpya ambaye amempeleka kwenye ulimwengu ambao hakuwahi hata kuuota.
‘’Ka….kaa’’ Aliongea kwa kitetemeshi kilichotokana na hisia nzuri alizokuwa anazo kwa wakati huo.
‘’Niambie Stella dada yangu, mambo ndo hayo siyo kila siku unanikwepa kama simba’’Alijibiwa na yule kijana ambaye alikuwa akitabathamu moyoni na usoni kwani alikuwa ametimiza lile alilokuwa akiliwaza siku zote.
‘’Yaani we aaacha tuu mbona umechelewa kuniambia haya mambo?’’ Stella aliongeaakijariu kumsogelea yule kijana kutaka kumkumbatia badala yake anajikuta akikutanisha mikono yake bila kushika chochote kwani alikuwa amekosea makadirio, mtu aliyetaka kumkumbatia alikuwa mbali na pale alipohisi kuwa yulo.Nusura aanguke lakini yule kijana anamuwahi na kumdaka na wanakumbatiana.
_____________
Baada ya kukosa kumgonga Joseph, Alice alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa wazazi wake akiwa haamini kama alikuwa ameweza kuikwepa ajali ambayo si tuu ingeweza kuutoa uhai wa mtu bali ingeutoa uhai wa mtu aliyekuwa akimpenda sana.Alihitaji utulivu wa nafsi na utulivu huo aliamini angeupata akiwa karibu na wazazi wake.Lakini tpfauti na alivyotegemea akwani alipofika nyumbani alibonyeza kengele ya mlangoni bila kujibiwa tofauti na ilivyokuwa kawaida.
Alichungulia ndani lakini hakumwona yeyote hata mlinzi wao, jambo ambalo lilimpa hofu kwani licha ya kuwa hakuwa amewasiliana na wazazi wake tangu walivyoachana kanisani lakini haikuwa kawaida yao kuondoka wote pale nyumbani.Akazunguka nyumba nzima kuchungulia lakini utulivu ulionekana kutawala mahali pale na kumfanya aogope sana.Akampigia simu baba yake simu yake haikupatikana alivyompigia mama yake iliita muda mrefu bila kupokelewa aliendelea kupiga hadi ilipopokelewa.Aliongea na mama yake aliyemwambia familia nzima ilikuwa imetoka kuelekeaziwa Duruti kwa ajili ya mapumziko, alipouliza kuhusu baba yake aliambiwa naye alikuwa huko lakini simu yake ilikuwa imeishiwa chaji.
Alipouliza uwezekano wa kuwafuata aliambiwa walikuwa wakikaribia kurudi wangemkuta nyumbani kwake kwani walisahau waliondoka na mlinzi na funguo walikuwa nazo.Alice alirudi kwenye gafri lake na kukaa huko akifikiri arudi kwake ama aende popote akapoteze muda lakini alipokumbuka namna alivyokumbuka namna alivyokosakosa kumgonga Joseph alijikuta akitetemeka mikono kwa hofu na kushidwa kuondoa gari.Akafikia uamuzi wa kuwasubiri wazazi wake pale akweka mziki laini kwa sauti ya chini na kurudi siti ya nyuma ya gari na kujilaza huko hadi usingizi ulipompitia.
Baada ya kama saa moja hivi alishtushwa na kelele za kugongewa kioo, alipoangalia mgongaji wa gari hiyo alikuwa ni mtu ambaye hakujua ni mtu gani lakini alikuwa akimtaka atoe gari kwani alikuwa amezuia njia ya kutokea kwenye geti la nyumba yao na kuna gari ambayo hakuifahamu ikitaka kutoka.Alishtuka lakini akajikaza na kutoonesha kushtuka kwake na kwa bahati tule mtu alikuwa amesharudi kwenye gari lile tayari kwa kuondoka.
Kwa umakini wa hali ya juu Alice alizikariri namba za gari lile wakati akilitoa gari na kulitoa kwenye njia, alikumbuka hakuwahi kuliona lile gari kabla na zilionekana si namba za hapa nchini.Hakutaka tena kuingia ndani licha ya mlinzi kuliacha geti wazi aigeuza gari na kuelekea kule lile gari alilolipisha bila kujua ni nini kilimtuma kufanya hivyo aliendelea kulifuata hadi pale liliposimama ambapo Alice alihisi kuwa walikuwa wamemuona hivyo akaamua kuchepuka na kuingia njia nyingine iliyokuwa ikiingia upande wa kushoto huku akitupia macho upande ule ilipokuwa ie gari.Alishuhudia yule mtu aliyemgongea kioo akishuka garini ka kwenda kung’oa namba za lile gari mbele na nyuma namba nyingine zikaonekana alifanikiwa kuzikariri pia.
Akapata hofu kuwa wale watu hawakuwa watu wema, akaamua kumpigia simu mama yake ambaye alimjibu kuwa walikuwa njiani kuelekea nyumbani jibu ambalo lilimchanganya kwani awali aliambiwa hata mlinzi alikuwa ametoka lakini alikuwa amemwona pale nyumbani.Alikata simu na kutafakari kidogo juu ya mambo yale ambayo yalizidi kumchanganya akili.Akaamua kwenda kituo cha polisi kulipoti juu ya lile tukio la gari kubadilisha namba kwani alihisi lilikuwa likihusiana na mambo mabaya.Alipofika kituoni alikuwana na kitu kilichomtisha na kumvunja moyo.Alikuwa ni yule mtu aliyemgongea kioo pale getini.Alimsalimu huku akiwa ameahirisha kufanya kile amabacho alikuwa amekusudia kukifanya kwani akili yake alimwambiankuwa kama si wazazi wake walikuwa wakichunguzwa na askari basi walikuwa wakishirikiana na yule askari kufanya mambo ambayo ni kinyume na sharia.Kwani kitendo cha wazazi wake kumdanganya kilimpa jibu kuwa kuna kitu alikuwa kifichwa.
‘’Ulichokiona kiache kama kilivyo, ukienda kinyume utapotea wewe hata wazazi wako’’Aliambiwa na yule Askari aliyeonekana kubalika kimavazi tuu lakini sura ikiwa ile ile aliyokuwa ameiona pale nyumbani kwa wazazi wake.
‘’Kivipi?’’ Alice aliuliza huku akijaribu kuificha ile hofu aliayokuwa nayo.
‘’Usijifanye mtoto, nilichokiongea kinaeleweka’’ Aliongea kwa sauti ndogo yule Askari ambaye aligeukia upande ambao kulikuwa na gari kadhaa za polisi zimeegeshwa, hapo alifanikiwa kuiona kumbe zile namba za pili alizokuwa ameziona na kuzikariri zilikuwa ni namba za magari ya polisi.
‘’Kwa hiyo mnashirikiana na wahalifu?’’Alijikuta ameropoka.
‘’Kwa hiyo unajua baba yako ni mhalifu?’’ Alijibiwa kwa swali.
‘’Hapana nyie mmeenda kuvamia kwetu?’’
‘’Na baba yako pia’’
‘’Sawa’’Alice alijibu na kutaka kuondoka lakini yule askari akamfuata.
‘’Funga mdomo wako kama hutaki kurudi mavumbini na usithubutu kumwambia baba yao atakuangamiza’’Aliongea yule askari kwa sauti ya chini nay a kutisha lakini kinywa chake kilionesha kilikuwa kikitoa harufu mbaya ya pombe na sigara.
Hapo Alice akahisi kuwa yule hakuwa askari kwa haraka akaangalia namba kwenye vazi la yule askari ambaye aliligundua hilo alimwoneha kitambulisho kabisa akiaangalie kisha akakipokonya na kuondoka.Alice aliduwaa pale kwa muda kabla ya kuondoa gari lake hukua akiwaza mengi sana juu ya siku ile tangu kukutana na Joseph kule mgahawani bila skutegemea, kunusurika kumgonga na gari, kudanganywa na wazazi wake na hili la Askari mlevi alieyeenda kwao.
Kwa kuwa giza lilikuwa limeshaanza kuingia aliamua kwenda nyumbani kwake kwani aliona akili yake ilikuwa kama imevurugwa.Alipofika nyumbani kwake akapitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake ambapo alijilaza kitandani akitafakari mambo yale yaliyokuwa yametokea kutwa.Alitamani ampigie Joseph amweleze ili ampe ushauri lakini aliona ni mapema sana kumweleeza mambo hayo aliyoyaona ya kifamilia.Aliona kabisa kwa kuujua upande hasi wa familia yake Joseph angeweza kupata uoga wa kuendelea kumpenda hivyo angemkosa kabisa au angeamua kufuata taratibu za kisheria jambao ambalo huenda lingeiaibisha familia yake ama lingemweka matatizoni kutokanna nguvu ya pesa ambayo baba yake alikuwa nayo.
Matukio ya siku ile yalimfanya aanze kuamini zile tetesi za kuwa wazazi wake wanafanya biashara haramu.Zile alizoziona kama tuhuma zilizotokana na wivu wa watu juu maendeleo ya wazazi wake zilianza kupata maana kichwani mwake na kuendea kumchanganya akili.Akiwa katikati ya lindi la mawazo hayo Alice alishtushwa na mlio wa kengele ambao ulionekana ulikuwa umeenza mud asana kusikika lakini kutokana na mawazo aliyokuwa nayo hakuusikia tangu mwanzo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom