Riwaya: Nitarudi Arusha

Oct 12, 2016
38
17
MWANDISHI;Moringe Jonasy
Sehemu ya Kwanza


Hali ya hewa ya jiji la Arusha jioni hii ilikuwa ya ubaridi kama kawaida yake huku upepo ukisogeza wingu dogo la mvua kuelekea upande wa kasikazini magharibi na kuzuia mvua iliyotaka kuleta karaha kwa wananchi na wafanyabiashara ambao mvua ilikuwa kero kwao licha ya kuwa wengi wao kwa wakati huo walikuwa wakifunga biashara zao.Taratibu nilijisogeza kwenye kituo kikubwa cha mabasi baada ya kuagana na rafiki yangu mpya ambaye nilikuja kuonana naye baada ya kufahamiana naye kwenye mtandao mmoja maarufu wa kijamii.
Hii ilikuwa safari yangu ya kwanza si kufika jijini Arusha , bali kusafiri kwa zaidi ya saa moja kwenda kuonana na rafiki wa kike ambaye ilikuwa imepita miezi nane tangu tuanze kuwasiliana kwenye mitandao wa kijamii kabla ya kupeana namba za simu na kupigiana simu.
Japokuwa mwanzoni nilimtaka rafiki huyu aje Moshi ambako ndiko nilikokuwa nikisoma,lakini kwa msimamao wake wa kutomuamini mtu moja kwa moja nilijikuta nikikosa sababu za kutomfuata huko Arusha hasa baada ya kudai kuwa nilikuwa nimeshaanza kumpenda na kumwomba awe mpenzi wangu.
Kwangu ilikuwa ni mara ya kwanza pia kupata mpenzi ambaye alikuwa akitoka kwenye familia ya kitajiri sana , kwani kabla ya hapa wengi nilikuwa nikilingana nao uwezo wakati mwingine hata kuwazidi lakini kwa huyu niliyekuwa nimemfuata Arusha alikuwa amenizidi kila kitu kuanzia umri, kiwango cha elimu na hata kipato chake na cha wazazi wake.
Kwa uzuri wa asili naye hakuwa nyuma alijaaliwa rangi nyeusi isiyokolezwa ama kupunguzwa na kemikali yoyote huku nywele zake alizokuwa amezikata kwa mtindo wa kuziacha kidogo juu na kuzipunguza sana pembeni zikimfanya aonekane ni miongoni mwa vijana wa kisasa.Macho yake ya wastani yalikuwa kama yakinikonyeza kila aliponiangalia huku miguu yake ikionekana sehemu ndogo sana kwani ilikuwa imefunikwa na pensi jeupe chini akiwa na viatu vyepesi vya rangi nyeupe pia.
Midomo yake mikubwa haikurembwa na chochote zaidi ya kulainishwa na mate ambayo kila baada ya dakika kama kumi hivi yalifikishwa hapo na ulimi ambao ni kama alikuwa na kilema cha kuutafuna muda wote, kiasi kwamba nilifikiria kuwa kama angekuwa akiuremba mdomo wake basi urembo wote ungeishia kinywani kwa kupelekwa na ulimi wake ambao haukupenda kutulia.
Kwa kifupi kila sekunde iliyokuwa ikienda wakati nimekaa na huyo rafiki mpya basi nilikuwa nikigundua kitu kimoja kizuri alichokuwa amejaaliwa na mwenye kuumba vilivyo na visivyo na uhai.Alikuwa na uzuri ambao hata kuueleza nahisi sitoweza kwani nitakuwa ninasahau baadhi ya vitu vya kipekee vya dada huyo ambaye tofauti na ilivyozoeleka alinipeleka nyumbani kwake ambao alikaa na mdogo wake kabla ya kwenda nyumbani kwa wazazi wake ambako nako nilipokelewa kama rafiki mwema wa familia.
Mwanzoni nilipata shaka kufika kwa wazazi wake lakini alinitoa hofu kwa kunieleza kuwa alikuwa amewapa taarifa juu ya ujio wangu na hawakuwa na mawazo hasi juu ya urafiki wetu kwani wao ni miongoni mwa familia ambazo utandawazi kwao hauna athari nyingi hasi kiasi kwamba washindwe kujua nini maana ya urafiki.
Alidai pia sikuwa rafiki wa kwanza kwenda kwao kwani kuanzia alipokuwa shule ya msingi hadi alipopata shahada ya uhasibu alikuwa akipata na kupoteza marafiki wengi hivyo alijivunia sana kupata rafiki mpya.Safari na mizunguko yote hiyo tuliifanya kwa gari ambalo si kwa kunieleza bali kwa kuchunguza tuu nilihisi kuwa lilikuwa lake.
Jioni hiyo ilinikuta nikiwa miongoni mwa wasafiri wengi walikuwa wakiwahi magari ya kuwafikisha waendako huku wafanyabiashara licha ya wingu lile dogo kuhamishwa na upepo bado walikuwa na hofu ya mvua kunyesha hivyo walifungafunga na kuweka bidhaa zao vizuri hasa zile ambazo waliziweka nje ya vibanda na ofisi zao za biashara.Baada ya kuhakikisha kuwa nimepanda gari rafiki yangu huyo niliyemjua kwa majina ya Alice Josephat Temu alirudi garini na kunipungia mkono kisha aliondoka eneo lile akiogopa kusababisha foleni kwani haikuwa ni sehemu rasmi ya kuegesha magari madogo.
Baada ya dakika kama thelathini hivi taratibu gari nililopanda lilitoka nje ya kituo baada ya kuunguruma na kusogezwa kisha kurejeshwa kwa muda mrefu sana huku wapiga debe wakiumiza viganja vyao kwa kulibamiza makofi kwa muda mrefu sana.Baada ya kutoka kituoni gari lilingia kwenye njia kuu ya kutoka jijini lakini tulikuta foleni kubwa sana iliyokuwa imenitia hofu ya kuchelewa magari ya kunitoa Moshi mjini kunifikisha nilikokuwa nikiishi ambako ni nje ya mji huo uliokuwa ukisifika kwa usafi kwa kipindi fulani kilichopita.
Foleni iliifanya gari kusimama huku ikiunguruma, hapo ndipo nilipogundua kuwa aliyetutoa kituoni na kutufikisha pale hakuwa dereva bali kondakta wa lile gari kwani wakati tupo kwenye foleni nilishuhudia dereva akiingia garini na yule aliyekuwa akiiendesha gari alirudi upande ambao tulikaa abiria.
Naye baada ya kushilia usukani alijaribu kupita pembeni mwa barabara kukwepa ile foleni huku akipitisha gari sehemu ambazo zilikuwa zikitumiwa na waenda kwa miguu ,mara mbili nilishudhudia akisimamisha gari kwa ghafla akiwakosa kosa waendesha baiskeli ambao kwa jioni ile waliamua kutumia njia za waenda kwa miguu.Baadaye aliamua kusimamisha gari baada ya kuona askari wa usalama wa barabarani wakija upande wake , ambapo licha ya kusimama walimpa onyo kali.
Tukiwa kwenye foleni hiyo alipita kijana mmoja aliyekuwa akiomba fedha ya chakula kutoka kwa abiria waliokuwa kwenye magari, alikuwa akitembea kwa kuchechemea huku mwili wake ukionekana kuegemea upande mmoja kana kwamba alikuwa akiumia upande mmoja wa mwili wake hivyo kupunguza maumivu alikuwa akiupunguzia mzigo upande uliokuwa ukimuuma.Hakuwa mchafu kama wengi wa kundi lake walivyokuwa alionekana nadhifu sana baada ya kupigwa na mwanga wa magari yaliyokuwa kwenye foleni , shati lake la bluu bahari na suruali yake nyeusi ya kitambaa ambayo kwa haraka haraka licha ya kuwa ilikuwa safi yeyote angejua kuwa ilikuwa haijaonja pasi tangu ilipotolewa dukani.
Licha ya kuwa kulikuwa na ubaridi ambao hata kwa mtu aliyekuwa garini alikuwa akiuhisi ukigusa mifupa lakini yule kijana alikwa akitembea kana kwamba hakuihisi ile baridi huku shati lake likipepea na kuubana mwili wake ambao haukuwa na nguo nyingine chini ya lile shati.Nilikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wakimfuatilia kwa macho yule kijana kwani hata alipolifikia gari letu wengi tuligeukia upande aliokuwa akianzia kuomba.
Nilimshuhudia kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa mbele yangu akiwa amejifunika shuka la kimasai na msichana ambaye kwa harakaharaka nilihisi kuwa walikuwa wapenzi akimpa noti ya mia tano kutoka kwenye burungutu la pesa ambalo aliisaka sana hiyo mia tano, huku yule mwombaji akishukuru sana baada ya kupewa ile hela kabla ya kuhamia dirisha nililokuwa nimekaa ambapo kama kawaida aliomba hela ya chakula.
Hapo nilimwona kwa ukaribu na uzuri zaidi ,kumbe kabla sikuona kovu lililokuwa mdomoni mwake na kumfanya ongee kwa shinda kwani liliufanya mdomo wake ukae vibaya kidogo lakini aliponyanyua mdomo wake nilijua kuwa hakuwa na meno ya mbele, sikutaka kumwangalia zaidi kwani si tuu alinifanya nimwonee sana huruma bali alinifanya nimwogope kwani nilihisi natazamana na kiumbe fulani cha kutisha ambacho kilifanana sana na binadamu, kwa haraka haraka nikatoa noti ya shilingi elfu moja na kumpa.
Wakati nampatia hiyo noti nilikuja kugundua pia hakuwa na vidole vyote kwani mkono wake wa kushoto ulikuwa una kidole kimoja na mkono wake wa kulia ulikuwa umebaki kiganja tuu bila vidole.Nilijikuta nikisimka mwili wangu nikikwepesha macho kwake lakini nilijikuta nikimgeukia hata alipohamia kwenye dirisha la nyuma na nilipokaa.
Alizunguka karibu madirisha yote ya upande wetu na kuhamia upande mwingine akianzia nyuma ya lile gari ambapo alikutana na mzee mmoja ambaye kwa mwonekano wake nilimchukulia kama siyo mkurugenzi wa kampuni fulani basi alikuwa ni mwanasiasa ambaye alikuwa ameamua kutumia usafiri wa umma ajue kero zake akiiacha gari yake ama ya kampuni ipumzike.
‘’Nikusaidie ukale we mwanangu?’’Alipaza sauti na kuwafanya abiria wengine waungane na wachache tuliokuwa tukimfuatilia kwa macho yule kijana wa ajabu.
‘’Hapana baba naomba tuu nikapate chakula sijala tangu jana ndugu yangu’’Aliongea kwa taabu yule kijana.
‘’Hahaaaa , hivi wewe ni mtanzania kweli, maana nimekuuliza kwa Kiswahili sanifu kuwa wewe ni mwanangu bado unaniita baba yako, kama mama yako kakudanganya kuwa baba yako yupo kwenye hili gari basi kanifananisha tuu, nina watoto watatu tuu ambao nimewazaa ndani ya ndoa takatifu ambayo Nilifungishwa na Padre Karugendo mwaka themanini na saba sasa we mwanangu wa wapi? Haaaahahahaa watanzania bwana kwa mbinu za maisha ’’Alimalizia kwa kicheko yule mzee ambaye niliamua kumpa jina la Mwanasiasa.
Nilimwona yule kijana akilengwa na machozi baada ya pikipiki moja iliyokuwa ikitokea mbele yake kumumulika usoni, taratibu aliondoka na kusogea pembeni kuipisha ile pikipiki iliyommulika ipite.
‘’We mpumbavu nenda kaanzishe shamba la mchicha kijijini huko uje utuuzie tujenge afya si kuja kutunukia meno yako hapa, haya shika mtaji huo’’Aliongea yule Mwanasiasa akimtupia noti kadhaa za shilingi elfu kumi lakini kitu cha ajabu yule kijana ni kama alikuwa ameganda hakuongea wala kujongea hadi vijana kadhaa wa mjini wakiwemo makondakta wa magari yaliyokuwa kwenye foleni walianza kuzigombania zile noti.
Nilishuhudia Yule kijana akitoka eneo lile taratibu akionekana kuguswa na kitu fulani kilichokua kimemuumiza hadi alipopotea kwenye upeo wa mboni zangu.Nilijikuta nikimhurumia sana yule kijana ambaye niliamini kuwa alikuwa akiumia sana kwa maneno yale si tuu kutoka kwa yule Mwanasiasa bali yalitoka kwenye vinywa vya watu wengi wenye roho na akili kama ya Mwanasiasa kila siku alipokuwa kwenye harakati zake za kutafuta mlo.
Niliona kabisa hali yake kwa nje kuwa haikumruhusu kufanya kazi yoyote ngumu kutokana na umbo lake, nilihisi kuwa alikuwa akiteseka sana kutokana na hali yake ,hasa alipoambiwa kuwa alikuwa akinuka meno, ni kweli nilisikia harufu mbaya alipokuwa amesimama dirishani pangu lakini haikuwa ni harufu iliyotoka kinywani bali ni harufu ya kuoza sehemu ya mwili.
Nilijaribu kubashiri sababu ya kukutana na adha ile lakini kila nilipobashiri niliona kama angekutana na madhira niliyombashiria basi angekuwa mfu ama asingekuwa kwenye hali mbaya kama ile.Nilijikuta nikizama mawazoni peke yangu licha ya maongezi ya hapa na pale kumhusu yule kijana kuendelea garini.Kuna waliokuwa wakiungana na msimamo wa yule Mwanasiasa ambao walikuwa wengi na wachache sana walimpinga tena kwa kuaamua kukaa kimya huku wakijitambulisha kwa miguno na nyuso zao za huzuni.Wengi waliamua kutotoa msimamo wao kinyume na yule Mwanasiasa kwani kila aliyejaribu kunyanyua kinywa kupingana naye alikataliwa na wa upande wake ama yeye mwenyewe huku wakitoa mifano kadhaa.
Alianza yule kaka aliyekuwa amekaa mbele yangu huku akiwa amejifunika shuka la kimasai na ambaye nilihisi kuwa alikuwa ni mpenzi wake;
‘’Mie hao nawafahamu, kuna mama alikuwa akija pale UDSM yaani ye kila lecture alikuwa akiingia class na kuanza kupitisha daftari kuomba msaada akidai kuwa alikuwa mjane na alikuwa akisome…’’Hakumaliza yule kijana ambaye niliamua kupachika jina la Msomi wa Mlimani alikatishwa na sauti nyingine kutoka siti za nyuma.
‘’He! bado yupo hadi leo yule mama mie nakumbuka mwaka 2009 nilimwacha akiendelea kukusanya pesa nasikia anamiliki hoteli nyingi sana yule mama licha ya kuwa mjane kweli lakini anasaidiwa sana na watoto wake ambao wengi wana uwezo na wapo nje ya nchi’’ Aliongeza huyu mwingine ambaye niliamua kumpa jina la Mwana UDSM.
‘’Mmeona hawa ni wezi tuu , katumia ulemavu wake kaongezea na uchafu anakusanya hela zenu bila jasho, mtaishia kuwaita wanasiasa wezi wakati hela zenu mnaibiana wenyewe tena bila kodi’’Aliongea yule Mwanasiasa kwa madaha wakati huo gari ilikuwa imeshatoka kwenye foleni.
‘’We kweli mwanasiasa na unatetea wezi wenzako kwa kuwatumia hawa watu unataka kutuaminisha hawa ni wezi wakubwa kuliko walioiba kwenye RICHMOND au ESCROW? acheni hizo bwana’’Ilisikika sauti ya dada mmoja aliyekuwa jirani tuu na yule Mwanasiasa ambaye niliamua kumpa jina la UKAWA.
‘’Mnadanganywa na hao CHADEMA wenu muwaone wanasiasa ni wezi bila kujua kuwa hata hao chadema ni wanasiasa maadui wenu ni wengi sana wakiwa pamoja na hao wezi eti mtu anajaza daftari zima na kukusana pesa za wanachuo kila siku huku akimiliki hoteli mwisho wasiku wanachuo hao hao wanaandamana kudai kuongezewa hela na hao Chadema wanawaunga mkono bila kujua matumizi yenu mabaya, lakini mie wala siyo mwanasiasa na hata siipendi hiyo siasa mie ni mtaalamu bwana nawatibu watu’’Aliongea yule Mwanasiasa kwa madaha huku akiukana uanasiasa kwa kujitambulisha kuwa alikuwa tabibu.
‘’Kwani wewe kuwa tabibu ndo kunakuzuia kuwa mwanasiasa nakujua sana wewe nakuona pale KCMC nasikia ulikuwa umeshiriki sana kwenye mgomo wa madaktari waliokuwa wakidai pesa zao na kusababisha vifo vya mamia ya Watanzania nyie ni zaidi na hawa omba omba ambao hawamuumizi yeyote’’Aliongea dereva la gari akigeuka geuka kisha kurudisha umakini kwenye usukani.
‘’We dereva endesha gari na wewe unataka utuue hapa kisa siasa , ndio maana siwapendi wanasiasa ‘’Aliongea kwa unyonge yule Mwanasiasa wangu ambaye maneno ya dereva yalionekana kumchoma.
‘’Nyie mnasema omba omba hawamjeruhi mtu, mnadhani wanakula wapi wasipopewa wanachoomba?’’ Aliuliza yule niliyempachika jina la Mwana UDSM na kusababisha ukimya kwani hakuna aliyekuwa amenyanyua kinywa kwa dakika nzima, kisha akaendelea.
‘’Hao wakikosa pesa ya kula kwa kuomba huhamia kwenye kazi nyingine isiyo rasmi itegemeayo nguvu na kuanza kuwapora watu…’’Alifafanua Mwana UDSM, lakini alikatishwa na sauti ya binti mmoja aliyekuwa akibishana na kondakta kwenye siti za nyuma.
‘’Mie nimeuliza kwa kondakta nimeambiwa elfu mbili mia tano hadi Moshi sa hiyo elfu tatu inatoka wapi?’’ Aliongea yule binti akipaza sauti.
‘’Kondakta gani aliyekuambia hiyo bei usiku huu ?’’ Aliuliza yule kondakta kwa sauti iliyojaa kebehi na ya kumuaibisha yule binti ambaye wakati huo alikuwa amesimama , amefura kwa hasira.
‘’Si yule aliyetuleta kwenye gari , yenu isitoshe mchana nimekuja Arusha kwa elfu mbili mia tano kwa hiyo hiyo mia tano imeongezwa leo mchana?’’ Alihoji yule dada na kuwafanya watu waendelee kumtazama kwa mshangao kwani alionekana kutojua utaratibu usio rasmi na wa kibabe ambao umekuwa ukitumiwa na makondakta wa magari ya kutoka na kwenda Arusha kuongeza nauli kila ilipofika iliyoitwa jioni.
‘’We umeibiwa pale jijini umepelekwa na wahuni kwenye gari halafu unaniletea u much know hapa’’Aliendelea kujigamba yule kondakta na kuondoka akikusanya nauli kutoka kwa abiria wengine ambao wengi waliokuwa wageni walionekana kushangazwa na utaratibu huo kuna ambao hawakuwa na hela ya ziada waliamua kumbembeleza kondakta kwa kudai kutojua na alipokea pesa zao baada ya kuwakashifu sana kitu ambacho kilinikera lakini sikuwa na cha kuongea kwani bado nilikuwa nikirejewa na taswira na kijana omba omba ambaye bila kujua nilijikuta jina la MTU-JITU likiwa kama jina lake kutokana na kuwa kiumbe aliyetisha sana kwa mwonekano lakini alikwa akiishi miongoni mwa binadamu wengine.
Nilikuwa na uhakika kuwa kulikuwa na jambo kubwa baya lilimpata maishani mwake na hapo nikajikuta kilijiapiza kuwa NITARUDI ARUSHA bila kujua nilikuwa nimetamka maneno hayo kwa sauti iliyowafanya wengi kunigeukia.
‘’Unarudi kwa sababu nimeongeza nauli ama? Na wewe dada nikirudi nikute umeniandalia Buku tatu yangu na jero ya usumbufu’’Aliongea yule kondakta na kuwafanya watu waangue kicheko.
Baadaye yule dada alitoa shilingi elfu tatu na kumkabidhi kondakta huku akitokwa na maneno.
‘’Ikutajirishe na siku uwe na gari yako hiyo mia tano, huo ni utapeli tuu kama wanaodai ombaomba wanaufanya na sipandi gari yenu tena’’Aliongea yule dada kwa hasira na kutoa simu yake akibonyeza namba kadhaa na kupiga.
‘’We ndo hujielewi eti nitajirike niwe na gari yangu halafu hupandi gari yetu tena nishatajirika ndo maana ninamiliki hili gari’’Aliongea akiwafanya abiria kuangua kicheko.
‘’Tajiri anakuwa kondakta? Huna hata haya’’aliongea yule binti akionekana bado kuwa na hasira japokuwa alikuwa akijitahidi kuficha hasira zake lakini zilijidhihirisha kwenye sauti yake , sikupata hata jina lililomfaa yule binti zaidi ya jina SIKUJUA.
Basi baada ya ubishi kati ya Sikujua na yule kondakta ukimya ulichukua nafasi hadi pale mazungumzo ya watu wawili yalipokuja kusikika gari zima na kuvuta wengi waliokuwa wakisikia mazungumzo yao. Alikuwa Mwana USDM akiongea na kijana aliyekuwa jirani yake huku wakisimuliana visa mbali mbali vya omba omba.
Mwana UDSM alisimulia kisa cha yule mama ambaye alikuwa akiomba chuoni UDSM huku akijfanya bubu pale alipokutana naye kwenye chuo kimoja mkoani Iringa na alipomshtua kwa ishara kuwa je , ni yeye wa mlimani alimtuliza kwa kumwekea kidole mdomoni kuwa asizungumze chochote. Alichokifanya ni kuondoka huku akijutia elfu tano zake kadhaa alizowahi kumpa huyo mama aliyeamua kuwaibia wanafunzi mchana kweupe bila kutumia nguvu kubwa.
Yule mwenzake alimsimulia kisa cha mzee mmoja ambaye hana ulemavu wala ugonjwa wowote lakini yupo mjini Moshi na asubuhi huamka na kutembea mwenyewe hadi maeneo ya posta ambapo hukunja mguu wake na kuanza kuomba kana kwamba ni mlemavu na wengi wamegundua na wageni ndio hujikuta wakiingia mkenge kumpa chochote mzee huyo mwenye nguvu ya kufanya shughuli nyingine.
‘’Mie huyo ndiye aliyenifanya niwachukie hao watu maana nilimpa sana pesa kila nilipoenda posta nilipokuja kusimuliwa hilo nilichukia sana na bahati mbaya nilimwona kwa macho yangu akitembea vizuri kabla ya kuangaza huku na huko na kukaa chini kama vile mlemavu wa mguu na mkono mmoja’’Alidakia yule Mwanasiasa ambaye mada ile kama ilimvutia kuliko wote akitetea alichomfanyia yule kijana kule Arusha.
Msomi wa mlimani naye akadakia na kuongeza lake wakati huo akifunua hata shuka alilokuwa amejifunika na yule msichana ambaye alionekana kuzama kwenye kusikiliza muziki uliokuwa ukisikika kwa mbali kutoka kwenye ear phones alizokuwa amevaa.
‘’Mwenyewe kuna omba omba mmoja kule Dar nilishuhudia akiomba hela na baada ya dakika kama kumi nilikutana naye akinywa kiroba. Siku nyingine si akaniomba pesa nikamuuliza nikupe pesa ama nikakununulie kiroba? Mbona alipotea kama upepo hawa wezi sana’’
‘’Wengine huwatumia wazee wao ama watoto wao kuomba omba na hata kujibadika vidonda bandia ili waombe pesa’’Aliongeza mama mwingine aliyekuwa kimya tangu mwanzo wa safari lakini aliamua kutoa la moyoni mwake huku wengi wakionekana kuwalaumu omba omba na kunifanya nijiulize maswali mengi juu ya kundi hilo la watu ambalo si tuu Afrika bali hata kwenye nchi nyingine zilizoendela ambapo visa vya akina Balotelli vilithibitisha uwepo wa omba omba hata kwenye nchi hizo.
Lakini mwisho wa mawazo yangu nilijikuta nikijiuliza , ni kipi kilimpata Yule MTU-JITU wa Arusha? Sikuwa na jibu zaidi ya kuamua kwa mara nyingine tena kuwa NITARUDI ARUSHA safari hii sikutamka kama awali.
Hatimaye tulifika Moshi mjini na hapo nilishuka na haraka haraka nikaelekea kwenye magari yaliyokuwa yakielekea chuo cha maliasili cha MWEKA ambako nilikuwa nikisoma hapo.Baaada ya saa moja ya kubanana kwenye daladala nilifika chuoni na moja kwa moja nilielekea Hosteli ambako nilioga na kulala hadi siku ya pili ambayo ilikuwa ni siku ya jumapili.
Siku hiyo sikuenda kanisani kama ambavyo wenzangu wengi walifanya wakisema uchovu kama sababu ya wao kutoenda kanisani tukiungana na wanachuo wengine ambao jumapili haikuwa siku ya ibada.
Nilikumbuka kuwa nilijipa kazi ya kurudi Arusha, hivyo niliandaa tena kwa safari ya kwenda Arusha bila kumwambia mtu yeyote kwani niliamua kuifanya safari ile kuwa safari ya siri.Sikuwa na sababu nyingi za kuifanya safari ile kuwa siri zaidi ya kutotaka yeyote ajue kilichokuwa kikinirudisha Arusha kwani nilijua wengi wangeniona mtu wa ajabu sana kufuatilia kitu ambacho wangeamini kuwa kilikuwa hakinihusu.
Saa nne na nusu ilinikuta nikiwa kwenye gari la abiria lililokuwa likielekea Arusha huku kichwa changu kikiwa na mawazo mengi sana, nilikaa kimya hadi pale niliposhtushwa na sauti ya kondakta aliyenitania na kufanya watu wacheke na kunigeukie.
‘’Kumbe sikukuelewa ile jana uliposema ungerudi Arusha kumbe ulifurahia huduma zetu?’’ Aliongea kondakta ambaye baada ya kumtazama niligundua kuwa nilikuwa nimepanda tena kwenye gari nililokuwa nimepanda jana yake.
‘’Umeona sasa, wengine waliapa kutopanda gari yetu lakini wewe umeamua kupanda tena , karibu sana leo nakupunguzia mia tano kwenye nauli utatoa elfu mbili tuu’’Aliongea yule kondakta na kuwafanya watu wacheke sana nami nikatabasamu kisha nikainama.
Nilipompa nauli yule kondakta alinirudishia shilingi mia tano huku akinikumbusha kuwa alikuwa amenipunguzia nauli na angenilipia yeye , napo sikusema kitu zaidi ya kutabasamu na kumshukuru.
Nilipofika eneo ambalo nilikuwa nimemwona yule omba omba jana yake niliamua kushuka na kutembea kwa miguu nikiangaza macho huku na huko nikiwa na kibegi changu kidogo mgongoni.
Nilitembea kwa dakika kama kumi na tano hivi bila kumwona MTU –JITU niliyekuwa nimemfuata nikiwa na zawadi zake kadhaa kama vile dawa ya meno, mswaki, nguo mafuta ya kupaka na kiasi kidogo cha fedha nikiwa na matumaini ya kutaka kujua kilichomfanya akawa kwenye hali ya UMTU-JITU.
Baada ya kuzunguka sana nikaamua kujipumzisha kwenye mgahawa mmoja kwani jua lilikuwa likichoma sana siku ile nikishangaa hali ya jiji lile lilivyo kwani jana yake kulionekana na tishio la mvua lakini siku ile palikuwa na jua kali sana.
Nikiwa pale mgahawani ambapo nilikuwa nikinywa maji ya baridi niliyokuwa nimenunua ili kupooza joto la mwili wangu nilikiona kitu ambacho kinipa matumaini na kufanikisha kilichokuwa kimenirudisha Arusha.
Alikuwa mtoto mmoja wa umri wa miaka kati ya tisa na kumi na moja akipita kwenye meza za wateja akiomba chochote.Wengi walionekana kukereka sana na usumbufu aliokuwa akiwaletea kutokana na mwonekano wake ambapo asilimia tisini na sita ya mwili wake ilikuwa imetawaliwa na uchafu na asilimia nne tuu ambayo ni mboni zake na viganya vyake vilionekana vikiwa salama.
Wateja wengi ambao walikuwa wazungu walionekana kukereka sana na kumwita mhudumu ambaye alikuja kumtimua akimwita kwa jina la John .
‘’Kumbe anajulikana?’’Alihoji mteja mwingine wakati huo John alihamia upande mwingine wa mgahawa ule ambao ulikuwa ni wa hadhi ya juu nako alifukuzwa na kuamua kutoka akipita karibu na meza niliyokuwa nimekaa kutoka nje.
Kwa haraka haraka nilimwita mhudumu na kumlipa hela yake kisha nikatoka nje nikiangaza macho huku na huko nikimtafuta John.Niliita jina lake baada ya kumwona amejificha nyuma ya pipa la takataka lililokuwa nyuma ya ule mgahawa , ajabu licha ya kuwa alikuwa jirani yangu hakuitika hadi nilipomsogelea akataka kukimbia kwa haraka nikamdaka mkono.
‘’Naomba niachie sirudii tena kuomba kaka’’ Alijitetea John.
‘’Mie sikupeleki popote nataka nikuulize kitu John nitakupa zawadi’’ Niliongea kwa sauti ya upole.
‘’Nisamehe kaka wala sitorudia’’Alizidi kujitetea yule mtoto akijitahidi kujinasua mikononi mwangu, hapo nikamweka John kwenye kundi la omba omba ambao wameamua kujiingiza huko kutokana na uvivu wa wakubwa wao.
‘’Shika hii, nataka unielekeze sehemu’’ Nilimkabidhi noti ya elfu tano na kumwona John akiniamini na kuwa mpole, lakini licha ya kuwa mpole niliendelea kumshikilia safari hii nilikuwa sijamkamata kwa nguvu sana japokuwa nilikuwa makini sana.
‘’Kuna mtu mmoja hivi anachechemea hivi, halafu anakovu moja mdomoni anafanya,,,,,’’Sikufanikiwa kumalizia maelezo yangu nilijibiwa na yule mtoto.
‘’Nani kaka Japhet? Kama umenipa hela kuniulizia habari zake basi shika tuu hela yako’’ Aliongea yule mtoto akinishikisha ile hela niliyokuwa nimempa na akitaka kujinasua mkononi mwangu.
‘’Kumbe unamfahamu , niambie basi yupo wapi ni ndugu yangu yule nahitaji kumsaidia’’ Niliamua kujieleza.
‘’Ndugu yako, ndo humfahamu hata jina? Mhh sikuamini nenda tuu kaka’’ Aliuliza yule mtoto akitaka kukimbia.
‘’Ni ndugu yangu namfahamu kuwa anaitwa Japhet nilikuwa nakueleezea alivyo ili iwe rahisi wewe kumtambua namhitaji sana ndugu yangu nataka akapate matibabu’’ Niliongea kwa kirefu.
‘’Tunavyojua Japhety hana ndugu hivyo najua wewe ni wale wale siwezi kukutajia alipo’’ Aliendelea yule mtoto huku akihangaika kujinasua lakini nilizidi kumshika mkono wake mwembamba na hata waliokuwa wakipita njia walijua nilikuwa nimemkamata akitaka kuniiba maana nilisikia sauti ya mama mmoja akisema kutokea upande wa pili wa barabara.
‘’Kamezidi wizi hako kapeleke tuu polisi’’ Lakini si hivyo tuu pia niligundua kuwa MTU-JITU au Japhet kama nilivyomfahamu hapo hakuwa na ndugu hivyo na kufanya safari yangu ya kurudi Arusha kuwa na maana ingawa kauli ya kuwa ‘’wale wale’’ na kukataa pesa yangu ingawa alikuwa akiomba pesa mgahawani iliniachia maswali mengi bila majibu juu ya huyo mtu aliyeitwa Japhet.
Kwa mbali niliiona gari niliyokuwa nikiifahamu ikiwa imewasha taa ya kuonesha kuwa ilikuwa ikitaka kuchepuka upande niliokuwa nimesimama na John na nilipoangalia njia ya kwanza kuchepukia upande ule ilikuwa ni pale mgahawani.Nilichokifanya ni kutoa noti mbili za shilingi elfu kumi nikimpa John nikimtaka noti moja aifikishe kwa Japhet.
‘’Nimwambie amempa nani?’’ aliuliza John.
‘’Joseph,’’ nilimwambia na kumwachia wakati huo ile gari iliingia upande wa mgahwani na kuegeshwa na aliyeshuka alikuwa ni mtu niliyemtegemea ingawa nilikuwa nikijifanya kutokuwa na habari na uwepo wa gari ile mahali pale.
‘’Mambo Joseph’’ alinisalimia Alice huku wenzake wakiingia mgahawani walikuwa jumla wanne, nilijifanya kutosikia salamu ile na kama niliisikia basi aliyeitoa lazima ajue kuwa sikujua kama ndiye niliyelengwa na ile salamu.
‘’We Josee unawaza nini ?’’ Aliuliza Alice akinishika begani nami nikajifanya kushtuka.
‘’Ha! Kumbe wewe nilikuwa mbali sana kimawazo’’ Nilimjibu baada ya kumwona Alice, rafiki yangu ambaye jana yake alinifanya niende Arusha.
‘’Mbona upo hapa?’’ Aliuliza.
‘’Tulikuja na mkuu wa chuo akaniacha hapa akiniahidi kunipitia baada ya nusu saa lakini saa la pili hili linaisha hajanipitia , namba yake ya simu sina nimepiga chuoni nimesikia kuwa ameshafika chuoni hapa nashindwa kuelewa kwa nini na hapa nina mia tano tuu mfukoni’’ nilidanganya.
‘’Sa kwa nini hukunipigia?’’ Aliuliza akionekana kukerwa na kitendo cha kutomtaarifu kuwa nilikuwa Arusha na hata baada ya matatizo.
‘’Kwanza nilijua ulikuwa kanisani, halafu mkuu alinitaka kutoendekeza mambo binafsi wakati nimekuja kwa safari ya kiofisi’’ Niliendelea kujitetea.
‘’Kiofisi ndo kuachana kwenye mataa?’’ Aliuliza kwa kejeli lakini akiwa kama mwenye hasira.
‘’Basi tuu kwenye hii nchi watu wa daraja la mwisho tunateseka sana’’niliongea nikionesha unyonge wangu na kumfanya anihurumie , akanitaka niingie mgahawani akanitambulishe kwa rafiki zake nami bila kusita nikaingia ndani akanitambulisha na baada ya dakika kama tano hivi nilipigiwa simu na haraka haraka nikapata akili nikaikata ile simu na kuweka sikioni kisha nikainuka nikiongea.
Niliporejea nilikuja na taarifa ya kuwaaga na kudai kuwa kulikuwa na gari ambalo nilitakiwa nipande ili linifikishe Moshi, licha ya kupingwa sana na Alice baadaye nilikubaliwa kwa shingo upande baada ya madai kuwa ilikuwa ni safari ya kiofisi zaidi hivyo nilitakiwa kufuata maelezo ya wakuu wangu.Nilisindikizwa na Alice hadi nje ya mgahawa ambapo alinikamatisha noti kadhaa ambazo alidai zingenisaidia mbele ya safari.Nilishukuru na kuaga .
Nilienda moja kwa moja hadi upande wa pili wa barabara ambapo nilipotupa jicho langu ng’ambo bado niliona macho ya Alice yakiwa kwangu , nilimpungia mkono kabla ya kupanda pikipiki iliyokuwa jirani yangu na kutoa maelezo ya kupelekwa kituo kikuu cha magari.
Njiani nilimuuliza yule mwendesha pikipiki kuhusu mtu aliyekuwa na wasifu wa Japhet bila kutaja jina lake naye bila kusita alinijuza kuwa alikuwa ameshawahi kumwona yule mtu lakini hakujua chochote kumuhusu kwani hakuwa mwenyeji sana na lile jiji.
Nilipofika kituo kikuu cha mabasi nilimlipa yule jamaa wa pikipiki kisha nikaanza kuzunguka zunguka nikimtafuta Japhet ambaye ndiye aliyenirudisha Arusha.Nilitumia zaidi ya nusu saa bila mafanikio yoyote hadi nikaanza kukata tama.Nikaona nitumie tena njia ya kuwauliza omba omba waliokuwa maeneo yale ajabu kila niliyekuwa nikimuulizia kuhusu Japhet alionekana kumfahamu lakini akikataa kuongeza chochote kumhusu jambo ambalo lilinifanya nihisi kuwa kulikuwa na kitu kilichokuwa kimejificha kwenye maisha yake.
‘’Kiukweli ninavyomfahamu huyo mtu ni hivyo nilivyokueleza, hakuna kingine ninachokifahamu hata ukanipa mamilioni ili niachane na huku kuomba siwezi kukuambia kingine maana sijui’’Aliongea mzee mmoja omba omba akitetemeka na kunifanya nianze kupata uoga kufuatilia maisha ya Japhet ambaye baadaye nilikuja kugundua kuwa halikuwa jina lake halisi kwani katika watu kumi niliowauliza walinitajia majina mengine matano tofauti.
Nilichoka. Lakini kitu cha ajabu ni kuwa kadri ugumu wa lile jambo lililokuwa limenirudisha Arusha ulivyoongezeka ndivyo hamu ya kutaka kujua zaidi juu ya Japhet ilivyoongezeka mara dufu.Niakaamua kupita kwenye kituo cha magari madogo ya usafiri maarufu kama vifodi ili kuendeleza utafiti wangu usio rasmi.
Wakati naelekea huko nikikaribia kufikia barabara ingiayo kwenye kituo cha Vifodi nilimwona John na Japhet wakitokea nilikokuwa nikielekea na kwa maana hiyo tungekutana baada ya mimi kuvuka barabara iliyokuwa ikielekea mjini.Waliponiona walionekana kuelekezana kitu na hapo nilimwona Japhet akiniangalia sana kana kwamba aliwahi kuniona sehemu.
Kwa haraka bila umakini nikaingia barabarani nikikimbia kuelekea ng’ambo ya barabara kuwafuata akina Japhet, nilikuja kushtuka nikiwa nimebakiza hatua mbili ili niwe ng’ambo ya barabara baada ya kusikia kelele za watu na matairi ya gari yakilalamika.Nilipoinua uso wangu kuangalia kushoto kwangu nilikutana na macho makali ya mtu akiwa garini akiwa haamini kama alikuwa amenikosa kunikanyaga na gari yake.
‘’We Joseph utanipa kesi bure’’ Aliongea Alice ambaye nilikuwa nimeachana naye mgahawani, kwa kuwa akili yangu ilikuwa ni kuonana na Japhet nilijikuta nikigeuzia uso wangu pale nilipokuwa nimewaona Japhet na John lakini sikuwaona zaidi nilikutana na kundi kubwa la watu wakishangaa ile ajari ambayo ilitaka kutokea lakini ilisababaisha msongamano mwingine.
Nilirudisha uso wangu kwa Alice wakati huo nikiwa pale pale barabarani nikiwa nimepiga magoti mikono nikiwa nimeishikilia ardhi kana kwamba nilikuwa nikiizuia kupanda juu zaidi.
Nikajikuta nikipata cha kutamka.
‘’Nimechelewa gari tena’’
‘’Nitakupigia’’Alinijibu na kuondoa gari yake kuzuia kutokea kwa msongamano zaidi wa magari.
Niliinuka na kujichanganya kwenye kundi la watu kwani askari wa usalama wa barabarani walikuwa wakiwasili eneo lile hivyo niliona hatari ya kujiingiza kwenye matatizo mengine.
Nilipita kwenye njia kadhaa na kujikuta nipo kituo kikuuu cha magari ambapo nilidandia gari moja iliyokuwa ikitoka kituoni kuelekea Moshi mjini hakukuwa na siti iliyokuwa wazi hivyo nilisimama nikisubiri kupata siti baada ya abiria wengine kushuka.
Simu yangu iliita na mpigaji alikuwa Alice , nilipokea na kumweleza kuwa nilikuwa garini kuelekea Moshi na aliponitaka nimweleze kilichotokea hadi nikachelewa gari nika mjibu kwa kifupi, ‘’Usijali Nitarudi Arusha ‘’ nikakakata simu na kuiweka mfukoni.
Njiani nilipata mawazo mengi juu ya maisha Japhet ambaye awali nilimwona kama MTU-JITU kutokana na mwonekano wake, nilihisi kuna kitu kilichomfanya akawa MTU-JITU na kitu hicho si kidogo kutokana na hofu waliyokuwa nayo niliokuwa nimewauliza juu yake hapo nikajikuta nikijiapiza akilini kuwa NITARUDI ARUSHA.

Je nitarudi kweli Arusha?
Huyu mtu jitu ni nani?


Tuwe pamoja hadi mwishoView attachment 417515
 

Attachments

  • IMG_1476371096.186073.jpg
    IMG_1476371096.186073.jpg
    31.9 KB · Views: 196
NITARUDI ARUSHA...II
Mtoto John alivyoponyoka mikononi mwa Joseph alienda moja kwa moja hadi kwa Japhet ambaye kwake haikuwa taabu kumpata kwani alikuwa si tuu kaka yake bali kama mlinzi wake akifuatilia nyendo za wale ambao aliwaona kama maadui zake.
‘’Kaka uliniambia huna ndugu mbona leo kuna ndugu yako amekuulizia?’’ Aliongea John baada ya kukaa chini , walikuwa kando kando ya mto ambao ulikuwa katikati ya mji wa Arusha mita chache magharibi mwa Ofisi za Jumuhiya ya Afrika ya Mashariki mahali ambapo daima walikuwa wakikutana na kujadili mambo yo hasa wanapokuwa na jambo ambalo wanaona ni hatari kwa usalama wao.
‘’Kaka kumbe hukuniambia kuwa una ndugu yako? Amekuulizia leo’’Alianza John baada ya kimya kifupi.
‘’Ndugu yangu, anaitwa nani?’’ Aliuliza Japhet ambaye mara nyingi alikuwa akijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kwa watu kwa ajili ya kuwakwepa watu aliohisi kuwa walikuwa ni maadui wake.
‘’Anaitwaa ,,,, Joseph’’Alikumbuka.
‘’Joseph, mhhh ulimtajia jina langu?’’ Aliuliza akijaribu kukumbuka hilo jina lakini akahitimisha akilini kuwa huenda ni wale wale waliokuwa wakimsaka siku zote.
‘’Hapana sikumtajia nila alieleza sifa zako na kudai kuwa ni ndugu yako na amesema nikupe hela hii’’ Jonh alidanganya akitoa noti moja ya elfu kumi huku akijilaumu kumtajia jina halisi la Japhet , hakujua kitu kilichomsukuma kumtajia jina lake halisi.
‘’Yukoje?’’
‘’Ni mrefu hivi halafu mweupe halafu macho yake kama anapepesa muda wote’’John alijaribu kumwelezea.
‘’Hujawahi kumwona kabla ya leo?’’
‘’Mhhh kiukweli kwangu ni sura mpya’’
‘’Sawa ngoja twende tukale siku nyingine ukimwona nitafute haraka’’Alifunga kikao chao kisicho rasmi na kuanza kupanda kuelekea katikati ya jiji kwa lengo la kujipatia chakula.
Wakati wanarudi tena bondeni ndipo John alipofanikiwa kumwona Joseph na kumwonesha Japhet mtu ambaye alijitambulisha kama ndugu yake.Ingawa hakuwa akimfahamu yule mtu Japhet alijikuta akisukumwa na nafsi yake kutaka kuonana na yule mtu ili ajue lengo la kujitambulisha kama ndugu yake pia akijua kama alikuwa na jema kwake basi amshukuru kwa pesa aliyokuwa amempa kupitia John.
Hakumfahamu yule mtu lakini akili yake ilimwambia kuwa aliwahi kumwona ila hakujua ni lini na wapi.Wakiwa wakisubiri ujio wa Joseph pale ng’ambo ya barabara ndipo waliposhuhudia mtu waliyekuwa wakimsubiri akikoswa koswa na gari la mtu ambaye kwa Japhet alikuwa ni kama adui yake na hakupenda kabisa kumwona kwani kila alipomwona alijikuta akipata uchungu mkubwa na kitendo cha mwenye hilo gari kumwita kwa jina Joseph kuonesha walikuwa wakifahamiana kilimfanya ahisi kuwa naye hakuwa mtu mwema bali wale wale ambao siku zote walikuwa wakiisaka roho yake hivyo aliamua kuondoka.
___________
Nilipofika Chuoni akili yangu ilikuwa ikirudiwa na matukio ya Arusha kama filamu fulani hivi ambayo nilikuwa nimeiangalia nusu na nusu yake nilikuwa sijaimaliza hivyo nikajikuta nikitamani sana kurudi Arusha.Saa nililiona mwaka siku nikaona muongo na hata juma nililiona kama karne.Baada ya wiki mbili za kusoma huku nikitamani kujua kilichokuwa kimejificha nyuma ya maisha ya Japhet ziliisha hatimaye Jumamosi moja niliamua kurudi Arusha kumalizia filamu ambayo nilikuwa nimeiona huko bila kujua mwisho wa matukio yaliyokuwa yamewakuta wahusika wake huku nikijaribu kubashiri visa mbali mbali ambavyo niliona vinanipa mwisho mbaya kabisa usiovutia.
Niliamua kuwa na mwonekano tofauti na siku zote nikivaa shati la kahawia na suruali nyeusi na viatu vyeupe.Juu ya shati nilivaa sweta la rangi ya udongo huku kichwa changu kikiwa kimefunikwa na kofia nyeusi iliyokaa vyema na miwani ndogo ikawa vazi la macho yangu kwa kifupi yalikuwa ni mavazi ambayo hayakumwonesha Joseph aliyezoeleka machoni pa wengi kiasi kwamba hata nilipotoka nje ya chuo hata yule mama ambaye alikuwa na mgahawa hapo ambaye ni kama alikuwa ana kipaji cha kukariri majina ya wanafunzi na kuwita kila walipopita hakunitambua wala kushughulika nami na kibegi changu cha mgongoni nilikuwa nikibeba nilibadilisha nilibeba ambacho kilikuwa kigeni kwa wengi na kuonekana kama mtalii, hivi aliyetoka nje ya nchi.Kwa kuwa palikuwa na baridi viganja vyangu navyo nilivifunika kwa gloves nyeusi.
Saa nne juu ya alama nilikuwa katikati ya jiji ambalo azimio la ujama na kujitegemea liliasissiwa miongo kadhaa iliyopita nikirandaranda mitaani nikijaribu kumtafuta Japhet njiani nilikuwa nimepishana na gari la Alice kama mara tatu hivi lakini kwa mwonekano nilikuwa nao hakunigundua kwani hakujishughulisha nami.
Baada ya kuzunguka kwa karibu saa tatu nilijikuta nimechoka na kuamua kutalii tuu jijini nikitamani kukutana hata na John ili nimuulize chochote kumhusu Japhet, nilimua kushuka mtoni ili nipumzike.Nilitoa kofia na miwani na kuziweka kwenye kibegi changu , hapo nilishangaa nikiitwa jina langu.Mwanzoni nilifikiri huenda alikuwa Alice lakini haikuwa sauti ya mwanamke bali ilikuwa ya mtoto lakini zaidi alitanguliza jina kaka.
Niligeukia upande sauti ilipotoka nilishangaa kuwaona watu ambao kwa saa tatu nilizunguka kuwatafuta pale jijini wakija upande niliokuwa nimesimama.
‘’Habari zenu jamani’’Niliwasalimia kwa wahka.
‘’Salama habari zako bwana, Joseph’’Alijibu Japhet.
‘’Shikamoo kaka’’John naye alisamilia.
‘’Salama, marhaba John habari za siku kadhaa’’Niliwajibu.
‘’Salama ‘’Walijibu kwa pamoja.
‘’Samahani tunaweza kuongea kidogo?’’Niongea nikimgeukia Japhet.
‘’Hakuna shida twende tukakae pale’’Alinijibu akionesha mbele ya tuliposimama chini ya daraja ambapo palikuwa pamejificha sana, japokuwa nilisita kwa kukumbuka ile kauli kwamba omba omba huweza kugeuka vibaka wakosapo baada ya kuomba lakini kwa ile roho ya kutaka kujua maisha ya Japhet nilijikuta nikijongea bila shaka na kukaa kwenye mawe yaliyokuwa pale chini ya daraja.Japokuwa kulikuwa na harufu kali ya taka zilizokuwa zimetupwa hapo na kuoza lakini nilivumilia sana.
‘’Samahani naitwa Joseph ni mwanafunzi wa chuo cha MWEKA huko Moshi mwenzangu waitwa nani?’’Nilianzisha mazungumzo na Yule MTU-JITU ambaye nilimfahamu kwa majina mengi huku jina la Joseph likiwa limenikaa sana kichwani licha ya kutajiwa majina yake mengine kama matanO hivi na watu niliokuwa nikiwaulizia juu yake.
‘’Mimi naitwa Joseph , si ulisema mie ni ndugu yako hunifahamu hata jina we ndugu wa wapi?’’Aliongea na kucheka huku akijitahidi kuficha mapengo yake.
‘’Hapana ndugu yangu, si unajua sisi sote ni ndugu hapa duniani , mie ni ndugu yako kwa wazazi wetu Adam na Hawa lakini nilikuona mara ya kwaza siku moja kule mjini ukitafuta riziki nilikusaidia kiasi kidogo sana cha fedha lakini nilishuhudia ukitukanwa na mzee mmoja hivi hapo ndipo nilipopata hamu ya kutaka kujua kilichokufanya ukawa hivyo leo hii mara ya pili narudi Arusha kwa ajili ya hilo mara ya kwanza sikufanikiwa baada ya ile ajali iliyonikosa sikukuona tena’’Nilijaribu kujieleza kwa kifupi.
‘’Ohhh nimekukumbuka ndugu yangu asante sana kwa msaada wako ulionipa, habari za siku nyingi’’Aliongea kwa furaha na sauti kubwa kidogo huku akishindwa kuzuia mate kutoka kinywani mwake kupitia pengo lake kubwa , lakini nafanikiwa kuyafuta kwenye paji langu la uso.
‘’Samahani sana ndugu’’Aliongea akinifuta mate kwa kiganja chake kilichokosa vidole, hapo huruma inaniingia sana.
‘’Unaweza kunieleza kilichokufanya ukaingia kwenye haya mateso?’’Niliuliza huku nikiwa na huzuni sana.
‘’Usijali ndugu yangu ngoja nikueleze kisa changu kwa kifupi maana ni historia ndefu sana’’Alinijibu na kuanza.
‘’Naitwa Japhet Jackson Kaaya mtoto wa tatu kuzaliwa kwenye familia iliyokuwa na watoto watatu , maana yake nilikuwa mtoto wa mwisho.Nilikuwa nimetanguliwa na kaka yangu mmoja na dada yangu akimfuatia.
Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kuwa ningekuja kuishi kwenye maisha haya bali ndoto zangu zilikuwa kuja kuwa mwanasheria mkubwa nchini hata kuja kuwa mwanasheria wa serikali.Kazi ambayo wazazi wangu walidai ningekuja kuifanya kama ningetia bidii kwenye masomo lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa hata kufika darasa la sita kwani nikiwa darasa la tano kila kitu kilipotea na kuzima kama mshumaa’’Hapo alitulia na kuniangalia kisha akamwangalia John ambaye niligundua pia alikuwa mgeni wa simulizi hiyo.
‘’Sikuwahi kumsimulia yeyote lakini najikuta nakusimulia kwani nafsi yangu imenisukuma kufanya hivyo tangu niliposikia habari zako kutoka kwa John, na siku zote tangu uondoke nimejikuta nikiahirisha hata kuomba omba nikikutafuta nijue adhma yako huku nafsi ikiniambia ulikuwa mtu mwema.Hata leo hii tumekufuatilia kwa takribani saa tatu tangu uliposhuka garini hadi ulipofika hapa ndipo tukakufuata’’Alitulia na kuniangalia usoni kisha akaendelea.
‘’Ndoto zangu zilikufa nikiwa darasa la tano mwezi wa kumi na mbili ambapo tulikuwa tukisafiri kuelekea Manyara tulipokuwa tukienda kutalii baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye mitihani yetu ya muhula wa pili kuanzia dada yetu na kaka.Tulikuwa na watoto wa mama mdogo na binamu zetu ambao nao walikuja likizo pale nyumbani.Kwa kifupi ilikuwa ni siku ya furaha sana huku mama akitusimulia hadithi mbali mbali si unajua tena utoto lazima mtalazimisha hadithi hata kama za uongo.
Baba naye hata wafanya kazi wetu hawakuwa nyuma kupiga soga na kuifanya safari yetu ikapendeza lakini tukiwa tukianza kuliona ziwa kwa mbali ghafla kilitokea kitu cha kutisha sana kwani gari iliacha njia na kugonga mti kabla ya kupinduka na kilifuata baada ya hapo sikukijua hadi baada ya siku kadhaa nilipojikuta Mount Meru hospitali.Sikuwa kwenye hali nzuri na nilipouliza kuhusu ndugu zangu sikujibiwa chochote hadi baada ya siku kadhaa nilipoeleza ukweli kuwa sikuwa na wazazi na ndugu zangu duniani kwani wao walipoteza maisha katika ajali ile tena walikufa kwenye eneo la ajali na nilikuwa nimenusurika huku nikiwa kwenye hali niliyonayo, ilikuwa miaka kumi iliyopita ila kwangu naona kama juzi ‘’.Aliongea kwa masikitiko iliyofuatiwa na machozi.
‘’Pole sana kaka’’Nilimpooza.
‘’Basi nilipopata nafuu nilipelekwa makaburini ambako hapo ndipo niliamini kuwa ndugu zangu walikuwa wameniacha peke yangu, nilitamani hata tungekufa wote kwani matuta zaidi saba yaliyokuwa yamewameza wazazi , ndugu zangu dereva na wafanyakazi wetu yanilifanya niumie sana ikizingatiwa walikuwa wameniacha kwenye umri ambao nilikuwa nikiwahitaji sana.Wajomba zangu walinipooza kwa kuniambia kuwa walikuwa wameenda mahali pazuri zaidi ya hapa duniani na ipo siku ambayo tungewafuata na kuonana nao.Moyoni nilikuwa nikitamani niende hapo pazuri ili nicheze na kufurahi na ndugu zangu hivyo nililaumu sana kwa kitendo chao cha kuniacha nao kwenda mahali pazuri peke yao.
Niliendelea kupata matibabu madogo madogo hata nilipotolewa nyuzi nilizokuwa nimeshonwa, huku wajomba zangu wakiwa ni wazazi wangu wapya wakishinda nami pale hosipitalini hasi siku moja kabla ya kuruhusiwa ambapo nilijikuta peke yangu.Niliporuhusiwa nilitoka nikitembea kwa kuchechemea hadi nyumbani ambapo nilishangaa kuwaona watu wengine ambao sikuwafahamu kabisa wakidai nyumba ile ilikuwa imeuzwa.
Nilijikuta nikikosa kwa kulala hapo nilichanganyikiwa kwanza kuwakosa wajomba zangu ambao waliahidi kunichukua hospitalini siku moja kabla ya kuruhusiwa wakapotea kabisa. Niliamua kurudi tena hospitalini nikiwasubiri wajomba zangu ambao walikuwa wadogo zake mama kwani baba alikuwa amezaliwa peke yake kwenye familia yake hivyo ndugu zetu wengi tuliokuwa tukiwafahamu ni wale waliokuwa ndugu zake mama na kwa kuwa walikuwa wenyeji wa Arusha walikuwa wakija sana nyumbani kwetu.
Siku ile ilipita bila kumwona mjomba mkuwa wala mdogo na sikuwa pa kwenda hadi pale jirani yetu ambaye ndiye mama yake John aliponiona pale hospitalini na kunichukua kama mtoto wake na nikalala walikuokuwa wamelala wajawazito kipindi hicho alikuwa amemmbeba John.
Nilijikuta nipo chini ya himaya yake kwaa kipindi chote na hata nilipotaka kwenda nyumbani alinizuia akidai kuwa tungeenda wote.Hata alipojifungua nilirudi naye nyumbani kwake ambapo alikuwa maepanga chumba jirani na tulipokuwa tunakaa nilijaribu kwenda hapo nyumbani lakini nilizuiwa na mlinzi ambaye nilikuwa nikimfahamu kwani alikuwa mlinzi wetu kumbe waliokuwa wameuziwa ile nyumba walikuwa wameuziwa hadi mlinzi.
Ilikuwa ngumu sana kukubaliana na hali hiyo ikizingatiwa umri wangu mdogo ambapo nilikuwa nikihitaji zaidi mwongozo wa wazazi lakini haikuwa hivyo sikumwona mjomba wala nani zaidi ya mama John ambaye nilimwita mama ambaye nilijikuta nikimsaidia kumlea John naye akihangaika kututafutia chakula akiuza matunda kwa kutembeza.
Nilijitahidi kuwatafuta ndugu zangu nikisaidiwa na mama John lakini tulipofanikiwa kuwaona nilikataliwa na kupigwa sana.Nikawa mtu wa kulifuatilia gari alilokuwa akilitumia binamu yangu hadi lilipoishia na aliposhuka alinichalaza bakora na nikajikuta nikirudi kwa mama John ambapo alihamishwa kwa nguvu kupisha ujenzi wa Hoteli kubwa ya Manyara Hotel.Pale ilipojengwa ile hoteli palikuwa na nyumba yetu na nyumba nyingine ambazo ziliuzwa kupisha ujenzi wa ile hoteli kubwa ambayo nasikia mjomba ni mmoja wa wamiliki.
Inasikitisha sana lakini sina jinsi , manyanyaso na kichapo kutoka kwa binamu zangu na watu waliokuwa wakiwatuma zikanifanya niachane nao na kuungana na mama John kuuza matunda ,nikiwa na miaka kumi na tatu nilimwomba mama John pesa na kwenda huko vijijini nilikokodi shamba na kuanza kulima nyanya wazo ambalo nililipata siku moja nikiwa ndotoni ambapo niliwaona wazazi wangu wakinishauri kufanya hivyo.
Kweli mradi huo ulikuwa na matokeo mazuri na msimu wa mavuno ulikuwa mwema kwangu na nikakodi gari lililoleta nyanya mjini ambapo niliuza kwa faida kubwa na siku ya pili nikiwa njiani kurudi kijijini ili nikamalizie nyanya zilizobaki tulivamiwa na watu ambao nilikuja kujua baadaye kuwa walitumwa na mjomba waliniteka na kunipiga sana wakipa vitisho vingi na wakinituhumu kutaka kumshtaki mjomba wangu kwa kuuza nyumba niliyodai yetu bila kujua kuwa wazazi wangu walipewa wakae kwa muda lakini ninavyoamini kuwa ile nyumba ilikuwa yetu kwani tulihamia pale muda mfupi baada ya kukamilika ujenzi wake ambao wakati ukiendelea baba alitupeleka na kudai nyumba ilikuwa yetu.
Nipigwa sana na kuumizwa ubavu kabla ya kutupwa huko porini wakiamini kuwa nilikuwa mfu kitu cha ajabu hakuna cha dereva wala mtu mwingine aliyepigwa zaidi yangu.Kwa bahati walipita watu waliokuwa na wakichunga ng’ombe dakika chache baada ya tukio ambao waliniokota na kunipeleka walipoweka kambi wakikitibu kwa miti shamba na baada ya kama wiki hivi nilipata nafuu na kuniruhusu kuondoka kwani wao walikuwa wakihama na kuelekea sehemu nyingine na kwa kuwa hali yangu haikuwa nzuri waliniacha barabarani na nikapanda gari kuja mjini na kuanza kuomba omba nikiwakwepa binamu zangu na watu wake ambao kila waliponiona wamekuwa wakituma watu wao kuja kunipiga sana.
Leo hii mbavu zangu zinaoza taratibu na siku yoyote nawafuata ndugu zangu huko mbinguni waliko namshukuru mama John ambaye licha ya kuwa na maisha magumu ameamua kuwa nami bega kwa bega na amemruhusu John kila siku zisizo za masomo kuniangalia tukiomba hapa na pale.
Nilipogundua kuwa unafahamiana na binamu yangu aliyetaka kukugonga nilipata mashaka kuwa huenda na wewe ni wale wale watu wao ambao hakuna wanachotamani kama kifo changu ama nakuwa kichaa kama ninavyowaigizia ili waishi kwa raha mustarehe.
‘’Kwa hiyo binamu yako ni yule mwanamke?’’Niliuliza nikiwa siamini kama mwanamke niliyekuuwa nikimpenda ni mmoja wa wasababishaji wa maumivu yake.
‘’Ndiyo yeye na kaka zake pamoja na wazazi wake wanapenda nife’’Aliongea Japhet akilia.
‘’Pole sana ndugu yangu, kwa yaliyokukuta nilipoona umetukwanwa niliumia sana leo hii sina cha kukupa zaidi ya hiki kidogo nilicho nacho, pesa hii utaitumia kwa matibabu na twende hadi kwa mama John ili tukaongee zaidi kuhusu matibabu yako’’Niliongea nikimkabidhi kibegi changu.
‘’Asante sana ndugu yangu, Mungu akubariki’’. aliongea akiwa haamini kabisa.
Tulitoka pale chini ya daraja na kukodi teksi iliyotupekeleka kwa mama John kwa maelezo yao na tulipofika alikuwa hajarudi hivyo tulisubiri hadi jioni ambapo alirejea na kukutana na ugeni akiwa na sinia lake la matunda ambalo lilijaa kuonesha kuwa hakuwa ameuza matunda mengi.
Baada ya salamu nilitambulishwa kwake na Japhet kabla ya kumpa kiasi kikubwa cha pesa ambazo nilikuwa nimetumiwa na Alice niliyemdanganya kuwa nilikuwa nimepata tatizo chuoni hivyo kilihitajika kiasi hicho ili nitatue tatizo lake.Furaha ilirejea kwenye familia ile wakinishukuru na kuniahidi kumpeleka Japhet Hospitali.Nikawaachia mawasiliano yangu na kuondoka wakinisindikiza hadi kituo cha magari nilipanda gari na kuondoka.Nilijiona nimetua mzigo mkubwa na hata nilipofika chuoni nilijikuta ni mtu mwenye furaha baaada ya kumsaidia mtu aliyekuwa akiteseka sana.
Niliendelea kumnyenyekea na kujifanya kumpenda Alice akinipa pesa ambazo nilikuwa nikigawa na kuwatumia akina Japhet kupitia mhudumu wa afya kwenye hospitali aliyokuwa akitibiwa Japhet.Nilitumiwa picha nyingi kupitia Whatsap zikimwonesha Japhet akiwa na tabasamu kuonesha matumaini kuwa amepona.
Siku moja nikiwa nimepumzika uwanjani nikiwaangalia wanamichezo wakicheza michezo mbalimbali nilipigiwa simu na yule muuguzi ambaye aliniambia kuwa Japhet alikuwa akitaka kuonge nami, nilinuka na kuelekea chumbani nikiongea naye.
‘’Kaka Joseph asante sana kwa sasa naelekea kupona’’Ilisikika sauti ya Japhet.
‘’Pole sana sijaja hata kukuona ndugu yangu’’Nilimjibu.
‘’Usijali kaka msaada wako ni mkubwa sana wenye nguvu ya fedha walipania kuniua’’Sauti yake ilipata udhaifu na kunifanya nimuhurumie sana.
‘’Mungu yupo atawaadhibu kaka wala usijali NITARUDI ARUSHA kukujulia hali’’Nilimjibu nikijaribu kumpooza.
‘’Karibu sana karibu tena Arusha ulipotangazwa ujamaa lakini hakuna kitu’’Alijibu akicheka.
‘’Hahahaaaa! na wewe umo kwenye siasa kumbe?’’Nilimtania.
‘’Hahahaaa! tunakariri tuu ya wanasiasa kaka’’
‘’Sawa sawa ndugu yangu tutaongea zaidi NIKIRUDI ARUSHA’’
‘’Karibu sana John anakusalimu sana alikuja kuniangalia mchana’’Alijibu na simu ilikatika, nilipopiga tena haikupatikana.Niliweka simu mfukoni nikijiapiza KURUDI ARUSHA.


Nitarudi kwelinArusha?
Twende pamoja
 
NITARUDI ARUSHA...III
Niliendelea na ratiba ya masomo huku nikiwa na hamu ya kumwona Japhet akiwa katika hali nzuri baada ya matibabu.Kwa kuwa ratiba ya masomo ilikuwa ngumu kwangu nilijikuta nikishindwa hata kutumia mwisho wa wiki kwenda Arusha kwani nilikuwa nikitumia hata siku hizo kufanya kazi za shuleni huku nikiendelea kuwasiliana na Japhet , John na mama yake kwa kutumia simu.Japhet aliniona ndugu na mkombozi wake , hilo alilionesha kila alipokuwa akinipigia simu kwani alionesha furaha yake na shukrani kwangu akiniahidi kuzidi kuniombea kwa Mungu ili nifanikiwe kwenye mipango yangu mema.
Siku moja nikiwa kwenye maandalizi ya mitihani ya kumaliza muhula nilipigiwa simu na namba ya mpigaji ilikuwa ngeni, nilipoipokea nilikutana na sauti ya kiume iliyonisalimu na kuniuliza jina.
‘’Naitwa Mathew , mwenzangu nani?’’ Nilidanganya jina.
‘’Mie Alfred , upo wapi Mathew?’’ aliuliza huku nikijaribu kuifananisha ile sauti kama niliwahi kuisikia mahali pengine.
‘’Mhh ndugu Alfred wa wapi jamani hata sikufahamu mbona maswali yako mengi sana’’Niliongea kwa kulalamika.
‘’Ndugu si hata wewe unafanya ambacho hukipendi we unaniuliza swali ambalo hutaki kulijibu sawa bwana huenda una ndugu yako yupo kwenye matatizo’’Alinijibu kwa kulalama yule mtu simuni.
‘’Okey nipo Lindi mwenzangu upo wapi?’’Niliendelea kudanganya.
‘’Sawa nipo Kilimanjaro kuna mtu alikuwa amekwama hapa kanipa namba yako kadai wewe ni ndugu yake nikamsaidia akadai nikupigie upo Moshi Mjini utanirejeshea hela niliyomsaidia’’Alipotaja Moshi moyo ulinilipuka kwani nilijua yule mtu ananifahamu kwani nilitegemea kama Lindi badi angenitajia Morogoro ,Mtwara ,Tunduru ama hata Dar es saalamu sasa kunitajia maeneo ambayo si mbali na nilipokuwepo nikaona ni hatari kubwa sana.
‘’Ndugu yangu kama umemsaidia huyo mtu nashukuru ila kiukweli huko moshi unakosema nakusikia tuu sijawahi fika na ndugu zangu ninaowafahamu wengi wanaishi huku kusini’’Nilisema kwa kujiamini sikujua kilichonifanya nimdanganye yule mtu.
‘’Sawa kama huyu mtu kanidanganya na kuamua kunidhurumu Mungu atalipa hapa hapa duniani huenda hatasaidiwa tena ama akadhurumiwa huko mbele’’Alilalamika yule mtu simuni.
‘’Pole ndugu yangu hii ndio Tanzania mtu hatumii nguvu kuiba’’Niliamua kumtania.
‘’We unaona mchezo unadhani kanidhurumu shilingi ngapi?’’Aliniuliza kwa ghadhabu.
‘’Sijui ndugu samahani huenda alikuwa amekosea kuandika namba’’Niliamua kurejesha umakini na kuacha utani.
‘’Poa bwana’’Aliongea kinyonge.
‘’Sawa siku njema ndugu’’Niliamua kuaga.
‘’Sawa’’Nilisiia sauti lakini nilijikuta nikiendelea kuweka simu sikioni bila kuikata kwa sekunde kama saba hivi nikasikia kitu kilichoufanya mwili wangu usisimke kwa woga.
‘’Tutamfuata huko huko chuoni kwake anajifanya bingwa’’Ilisikika sauti kisha simu ikakatwa sijui kwa kuishiwa salio ama kwa kukusudiwa.
Haraka haraka ule uoga wa mitihani ukatoka sasa uoga wa mtu kama si watu ambao nao kwa malengo na mipango ya Mungu aliamua kututofautisha na Simba ama Chui wa porini na kutufanya viumbe wa utofauti sana.
‘’Ina maana wanajua kuwa nipo chuoni?’’
‘’Wapo wangapi?’’
‘’Nimewakosea nini?’’
‘’Wanafanya wakifanyacho kwa faida ya nani?’’
‘’Kwa nini wanipigie kwanza badala ya kunivamia tuu chuoni na kufanya walichopanga kunifanyia?’’
Maswali hayo yalipita kichwani kwangu haraka haraka na kukosa majibu na kunifanya nichukue uamuzi wa kuzima simu yangu kisha kwenda nje ya darasa ambalo tungefanyia mtihani nikijiunga na moja ya vikundi vingi vya wanafunzi waliokuwa wakijisomea dakika za mwisho mwisho.Sikutaka kusoma tena maana akili yangu ni kama ilivurugika kwani nilikuwa nikijaribu kukumbuka kama kulikuwa na watu wowote niliokuwa nimewakosea.
Sikumkumbuka yoyote tangu utotoni nilipompiga jiwe mtoto wa mwalimu Eddy mwalimu aliyekuwa mkali sana shuleni baada ya kunipiga fimbo za begani na kusababisha jipu lililonifanya nitembee kwa kuinama na kunisababishia kilema ambacho ninacho hadi leo hii.Naye alikuwa ameniadhibu badaya tukio lile japokuwa mwanaye aliyeitwa Inocent aliahidi kulipa hata baada ya miaka mingapi kupita.
‘’Je, Inocent ama Inno kama alivyopenda kuitwa alikuwa na hasira za miaka zaidi ya kumi tano?’’
‘’Alijuaje kama nilikuwa Chuoni wakati ule wakati baba yake alihamishiwa Mbeya kutoka kwetu Lindi miaka mingi iliyopita ?’’
Nilijiuliza maswali hayo lakini nikaona si rahisi kwa Inno kuamua kulipa kisasi kile wakati ule kwani hayo yote yalifanyika tukiwa watoto.Nilimfikiria mwingine ambaye niliwahi kugombana naye nikapata majina mawili, la kwanza liliuwa Jose ambaye naye alikuwa mtoto wa mwalimu niligombana naye sana tukiwa darasa la saba baada ya kumtania kuwa alikuwa bubu kila alipokutana na msichana aliyekuwa akimpenda sana shuleni na kushindwa kumwambia ukweli lakini licha ya kugombana sana kipindi kile tukaja kuwa marafiki na bahati nzuri tulisoma wote sekondari Malangali mkoani Iringa akinikumbusha visa na ugomvi wetu wa nyuma na kuwa sehemu ya kufurahi kwetu pale ugenini Iringa na kujiona marafiki tuliotoka mbali.
Jina la pili likuwa jina la Eric Joseph ambaye nilisoma naye kidato cha tano pale Ifunda sekondari kabla ya kuhama na sababu ya kuhama ilikuwa ni ugomvi wetu.Nilisikia alihamia shule ya Ufundi Moshi ingawa sikujua ipo upande upi mjini Moshi.
Nilikumbuka kabisa chanzo cha ugomvi wetu ambacho kilikuwa ni Msichana Aneth Swai ambaye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya wasichana Iringa.Msichana ambaye alikuwa na sifa zote ambazo kwa wakati huo niliziona ama niseme wengi tuliziona ni sifa za msichana mzuri.Aneth alikuja shuleni na wanafunzi wenzake kwenye ziara ya shule yao.
Nilikumbuka tukio lililotugombanisha na kugundua kuwa inawezekana kabisa tukio lile kuwa na uhusiano na simu niliyokuwa nimetoka kuipokea dakika kadhaa zilizopita.
____
Nikiwa nawaza hayo nilishtushwa na kelele za wanafunzi waliokuwa wakigombania kuingia kwenye chumba cha mtihani na kunifanya niungane nao lakini nikiwa sina haraka kwani wengi walifanya hivyo wakienda kutengeneza kile tulichokiita ‘pattern’ ama ‘’Vijiji’ kwenye chumba cha mtihani wakikaa kwa makundi ya watu waliokuwa wakijisomea pamoja ili wasaidiane darasani.Kwangu hilo halikuwa na nafasi kwani nilikuwa nikipenda kukaa mbele kabisa ya chumba cha mtihani kwani moja ya vitu vilivyokuwa vigumu kwangu kuweka umakini kwenye mtihani ni pamoja matukio mbali kama mtu kukamatwa na simu , akisaidia na mwenzake na wakati mwingine akiwa na karatasi yenye majibu yangeniharibia umakini wangu.Niliingia kwenye chumba cha mtihani na kuinamia dawati nikuomba mwongozo wa Mungu kama wengi walivyofanya lakini kwa bahati mbaya mawazo yangu yalirudi kwa Eric Joseph.
Niliamua kukatisha sara yangu ambayo hata mwenyewe sikuilewa na kusikiliza maelezo ya mwalimu kisha nikafanya mtihani huku nikiwa na hofu sana.Sikujua kingine kilichoniogopesha.
Wakati nikifanya swali la mwisho kwenye ule mtihani ili nitoke nilipata wazo ambalo niliona lingenipa mwanga juu ya ile simu.Nilipanga kwenda kumuuliza mwanafunzi yeyote ambaye alisoma kwenye shule aliyokuwa akisoma Eric juu ya wapi alikuwa Eric kwa wakati ule.Nilimalizia lile swali haraka haraka na kumkabidhi mwalimu ambaye alidai muda wa kutoka ilikuwa hadi nusu saa iishe nami nilikuwa nimetumia dakika zisizozidi ishiri nikamdanganya kuwa nilikuwa najisikia vibaya sana yaani nilikuwa nikiumwa tumbo la kuhara hapo akanielewa kwani hata uso wangu ulisadifu nilichokuwa nikiongea ingawa uso ulibanwa na hofu na uoga juu ya ile simu niliyopigiwa.
Nilipotoka nje ya chumba cha mtihani ambako nilonekana kumshangaza kila mtu hasa baada ya kumpa msimamaizi karatasi yangu.Nilienda hadi hostel ambako nilikutana na wanafunzi waliokuwa hawana mtihani mda ule wakiwa wametingwa na kujisomea kwani wengi walikuwa na mtihani mchana wa siku ile.
‘’Naona mapema kama kawaida yako’’nilipokelewa na maneno ya mwanafunzi wenzangu.
‘’Hapana sijisikii vizuri’’nilijibu na kupanda kitandani.
‘’Pole bwana ‘’
‘’Asante hivi Ludovick si alisoma Shule ya ufudi Moshi?’’ Nilimuuliza yule mwanafunzi mwenzangu.
‘’Ndiyo , kuna nini ama unataka ukafundishe pale, maana hamueleweki unasomea uji unaenda kufanya kazi ya chai’’Alinitania yule mwenzangu ambaye tulikuwa tumezoeana sana licha ya ukimya wangu chuoni.
‘’Ndo hivyo na Ludo mwenye yule nimwite?’’ Aliniuliza , nikaitikia kwa kichwa naye akamwita kupitia dirishani kwani alikuwa amelala kitanda cha juu.
‘’Sema Ludo’’niimsalimu baada ya Ludovick kuingia mle ndani.
‘’Fresh za pepa?’’
‘’Safi, samahani pale Ufundi uliingia ukiwa kidato cha tano?’’Nilimuuliza baada ya Ludovick kukaa kwenye kiti kimoja kilichokuwa mle ndani.
‘’Na wewe maswali yako kama mpelelezi ehhe pana nini?”’ Alinijibu kwa swali.
‘’Unamfahamu Erick?’’ Nilimuuliza nikimwangalia usoni, nilimwona akigwaya na kujiweka kwenye hali ya kawaida lakini ilishindikaana .
‘’Eric Joseph aliyetokea Ifunda Sekondari?’’ Aliniuliza huku akionekana kukumbuka kitu ambacho ni kama alikuwa hataki akikumbuke.
‘’Huyo huyo yupo wapi kwa sasa?’’ Nilimuuliza Ludovick ambaye ni kama alikuwa ameganda.
‘’Eric alifariki wiki moja tuu baada ya kuhamia pale shuleni na kwa bahati mbaya nilikuwa nimempokea kitandani kwangu baada ya kukosa kitanda na siku aliyofariki ndiyo siku aliyopewa kitanda ‘’Aliongea kwa hisia Ludovic .
‘’Eric alifariki! nini kilimuua?’’Niliuliza nikiwa kama nimepigwa na shoti ya umeme, ingawa nilikuwa chanzo cha Eric kuhama nilijikuta najijutia kutopata nafasi ya kupatana naye lakini upande mwingine wa akili yangu ukijiuliza kama angefariki kule Ifunda basi nami ningeonekna kama sababu ya kifo chake.
‘’Asee hata sipendi kukumbuka kifo chake kilivyokuwa kwani kiliniweka matatani sana na kunifanya nionje mahabusu’’Aliendelea Ludovick kwa uchungu mkubwa na kunifanya nizidi kupata wahka.
‘’Mahabusu! Kwani alijiua?’’ Nililizidi kuchanganywa na maelezo juu ya kifo cha Eric.
‘’Bwana we acha tuu kifo cha Eric kilinitesa sana’’Aliongea Ludovick na kuniongezea maswali mengi bila majibu.
‘’Yule jamaa alikuja pale shuleni akiwa na mawazo sana , kitu cha ajabu mawazo yenyewe yalikuwa ni kuhusu mapenzi ‘’Aliposema mapenzi moyo wangu ni kama ulikuwa ukitaka kutoka na kuniacha.
‘’Mapenzi?’’ Niliuliza kana kwamba sijui lakini mikono yangu ilikuwa ikitetemeka kwa hofu ingawa nilijitahidi kuficha kutetemeka huko kwa kutikisa miguu yangu.
‘’Erick aliondoka Ifunda baada ya kukorofisha na rafiki yake ambaye walikuwa wakimtaka msichana mmoja wa shule ya jirani.Kwa maelezo yake ni kuwa huyo rafiki yake alikuwa ameingilia penzi lake kwa kutumia uongozi wake uliomfanya awe na nafasi ya kuwa kwenye safari za kwenda mjini alikokutana na msichana huyo aliyemfuata kwa madhumuni ya kumpa barua ifike kwa Eric lakini binadamu hawana jema huyo rafiki yake akamjaza uongo huyo binti akimtuhumu Eric kuwa miongoni mwa wanafunzi wenye tabia mbaya na walikuwa kwenye hatari ya kufukuzwa shule kutokana na tuhuma za kuwabaka wanakijiji wanaopita kwenye msitu wa shule kuokota kuni’’Ingawa aliongeza chumvi lakini maneno yake yalikuwa na ukweli kiasi kikubwa ila suala la kumpakazia tabia mbaya sikuzisema ila nilijua lazima alieelezwa hivyo na yule binti kabla ya kuchukua uamzi wa kuhama kwani siku aliyokuja pale shule na kunigombeza alikuwa ametoka kuonana na yule binti mjini, akili yangu ilikuwa ni kivipi alifariki kutokana na mapenzi.
‘’Alijinyonga?’’ Hilo sikulijua nikasubiri Ludovick aendelee.
‘’Basi alipokutana na yule msichana mjini Eric alichukua uamuzi wa kuhama kwani yule binti alikuwa amemdhalilisha sana mbele ya wanafunzi wenzake wa kike na wanafunzi wenzake na Eric hivyo kurudi shuleni na kubaki Iringa aliona ni suala ambalo lingemuumiza na kumwaibisha sana’’.
‘’Kweliii....’’Niliitikia kwa masikitiko.

Dah! makubwa
 
NITARUDI ARUSHA ...IV
‘’Basi alipofika pale Ufundi akaanza ulevi kwa kile alichokiita kupoteza mawazo na hayo yote alinisimulia usiku tukiwa tumelala baada ya yeye kutoka mjini alikokuwa akinywa pombe hadi saa sita za usiku akitumia nafasi ya kulala na mimi na ugeni kutoonekana mtoro kwani kila kitanda namba moja jambo ambalo baadaye likuja kuniiumiza sana lakini sikumia sana kwani yale matatizo yalinifanya nifahamine na ndugu zake na hadi ninavyoongea na wewe Eric angekuwa mzima basi angekuwa shemeji yangu kwani nimemuoa dada yake mdogo ambaye baada ya kumweleza hiki kisa baada ya kutoka mahabusu alijikuta akinihurumia na kuwa karibu nami mwishowe tukawa wachumba na tumepata mtoto mmoja’’.
‘’Kwa hiyo Eric alikufa kutokana pombe?’’ Nilimuuliza kwani nilimwona akitoka kwenye kile nilichotaka kukijua.
‘’Hapana kwani wewe unamfahamu?’’Ludovick aliniuliza swali ambalo sikulipenda.
‘’Simfahamu ila niliambiwa na jamaa yangu mmoja alikuwa amemfundisha pale Ifunda kwani alikumsifia sana kwenye hesabu’’ nilidanganya ingawa ni kweli Eric alikuwa mzuri sana kwenye hesabu.
‘’Kweli jama alikuwa kichwa sana kwenye Hesabu, basi siku ya kifo chake Eric aliimba sana nyimbo za mapenzi mchana kutwa na kudai kuwa mapenzi yalikuwa na watu maalum huku akidai kuwa kila mtu alipangiwa kitu kimoja cha kumtesa kwenye uhai wake na ndicho njia yake ya ushindi kwenda kuiona pepo kwake aliona kuwa Mungu alimpa mapenzi kama mtihani wake wa kwenda pepo.Aliniliza mimi mtihani wangu nakumbuka nimlimwambia ‘umbea’ naye akaniambia umbea ni mgumu kuushinda kuliko mapenzi basi kama ningetaka kuushinda niutumie vizuri ama niwe mpelelezi ama hata mtunzi wa kazi za kifasihi hasa riwaya za kijasusi.Kwenye upelelezi nilimkubalia kwani napenda sana kazi hiyo ila kwenye riwaya na Baolojia yangu naona ni uongo tuu, alinipinga sana kwa kuniambia kuwa nchi haina mfumo unaoeleweka ndiyo maana muuguzi anaweza akawa waziri , mwanasayansi akawa kiongozi wa michezo na vitu vingi visivyo na uhusiano .Nilimpinga sana lakini kwa aalinizidi kwa hoja kwani alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa kama wanasiasa kwani alikuwa na hoja zenye nguvu sana.
Baada ya maongezi hayo aliondoka na kwenda mjini akityumia uchochoro mmoja ambao wanafunzi wengi walikuwa wakipenda kuutumia , nakumbuka upo upande wa mashariki ambako kwa sasa pamejengwa mnara wa simu.Hakurudi mzima zaid ya kuiona maiti yake akiwa amegongwa na gari mita chache kutoka kwenye lango la chuo , vipimo vilonesha akiwa amelewa.Ilikuwa asubuhi ya siku iliyofuata nikiamini alikuwa amelala kwenye bweni lingine alikopewa kitanda lnipoitwa na kuulizwa alikokuwa Eric nilishindwa kujieleza hasa kutokana na mshtuko niliokuwa nimeupata niajikuta nikisota mahabusu ambako niliteseka sana.
Niliapa mbele ya dada yangu ambaye ni mama watoto ni kumtafuta huyo msichana na jamaa aliyemnyang’anya mpenzi wake, jina lake aliniambia sema nimelisahau ‘’ Aliongea na kunifanya nizidi kuhaha kwa aliongea kwa uchungu sana na kuonesha alikimaanisha alichokisema.
‘’Mhh pole sana ndugu yangu nitamuuliza Yule mwalimu wake anaweza kunitajia jina la huyo jamaa kama laikuwa akijua ugomvi wao’’ Niliamua kujibalaguza kwa maneno ya uongo nikikwepa kugundulika.
‘’Utakuwa umenisaidia sana’’ ndugu yangu ngoja nikajipange na mtihani’’Aliongea Ludovick akiinuka nami niliinuka na kumsindikiza hadi nje kabla ya kurudi ndani nikiwa na mawazo sana na kulala kwani sikuwa na mtihani mchana.
Jioni nilipokuwa nikielekea mgahawani nikale chakula baada ya tumbo langu kusokota sana likidai mlo nami nikiwa sina hamu ya kula kwani habari ile kuhusu Eric ilininyongonyeza na kuniogofya haswa niliitwa na Ludovick ambaye naye alikuwa akielekea mgahawani.
‘’Vipi za mtihani?’’ Nilimuuliza tukitembea .
‘’Oya nimekumbuka nilipoandika jina la Yule jamaa’’Alilipotezea swali langu na kuibua jambo lililonitesa kutwa.
‘’Kwenye daftari?’’Niliuliza bila kutegemea.
‘’Ndiyo ila nimeliacha Arusha’’ Alinijibu akiwa na furaha, furaha ya kupiga hatua ya kumjua adui yake wakati huo mimi nikijikuta nikiongeza maadui badala ya kumjua adui yangu wa mchana.
‘’Poa ndugu yangu ila unaonaje ukisamehe na kumwachia Mungu?’’Nilijaribu kumshauri.
‘’We! Damu ya mtu kisa mapenzi , siwezi kusamehe hata kama aliyehusika ni ndugu yako sitorudi nyuma kwenye mpango wangu Eric atafurahi sana kule aliko kama mbaya aliyemkimbia amepata adhabu yake’’Aliongea kwa hisia kali Ludovick na kunifanya nizidi kumwogopa.
‘’Pole sana ndugu lakini si wajua visasi havikomi , maana yake nawe kuna watakao kuridhisha nafsi zao na nduguzako watataka kulipa kisasi na kufanya mzunguko wa uhasama usiokoma , ila una nafasi ya kuukata huo mzungu,,,,,’’
‘’We ishia hapo hapo usijifanye nabii hujui maumivu niliyoyapata kutokana na kifo cha Eric’’Alinikatisha Ludovick na kuongea kwa nguvu hali iliyowashtua wanafunzi wengine waliokuwa mgahawani watugeukie.
‘’Poa kaka, ila zingatia ushauri wangu’’Niliongea kinyonge.
‘’Siwezi kuzingatia hata chembe ya ushauri wako’’Ludovick alipwayuka na kusiamaam akiaacha chakula alichoagiza mezani n akufanya wanafunzi wengine kumfuata kujua kulikoni na kama ilivyo kawaida ya wanafunzi wengine waliacha kuagiza chakula na kunifuata kuuliza kulikoni nami niliawajibu kifupi.
‘’Kawaida , hamna tatizo kubwa’’Kisha nikaondoka na kuelekea hostel nilikojilaza na kutafakari mambo mengi.
Kwanza nilijua ile simu haikuwa ya Eric ambaye kwa mujibu wa maelezo ya Ludovick wakati huo alikuwa marehemu, hapo nikakumbuka muwasha simu yangu ambapo nilipokea ujumbe mwingi kutoka kwa Alice aliyenipa pole kwa mitihani. Nikaamua kumpigia nikimuuliza mambo mengi kimtego ili kutaka kujua kama alihusika kwenye lolote lililotokea mchana lakini sikufanikiwa kujua chochote kwani nilimuuliza alivyoitumia siku nzima.Sikuona chembechembe za hofu wala uwezekano wa kuwa na mpango wowote mbaya kwangu.
Jambo la pili lilikuwa ni kuijua ile vita ambayo ni kama niliianzisha lakini kuijua tuu ilikuwa ni hatua kubwa kwangu na kunifanya niwe makini.Nilipata wazo la kushiriisha polisi kwenye suala hilo lakini nikaona ni kama kulisumbua jeshi la polisi kwa kutokuwa na ushahidi wala mahali pa kuanzia, hatimaye nikaamua kupambana kwa mpango wangu.
Jambo la tatu ni kwamba liha ya kujaribu kutumia akili yangu yote sikufanikiwa kuunganisha matukio mawili ya Japhet na Eric na ile simu ya mchana na kunifanya niamini kuwa nilikuwa kwenye vita tatu ingawa sikujua lengo la Yule mtu kusema kuwa angenifuata hata chuoni baada ya maongezi yetu.
Ni kweli hakujua kama simu ilikatwa ama alikuwa amefanya vile kwa kukusudia?’’ Hayo yalikuwa maswali ambayo sikuyapatia majawabu.
Nikachukua uamzi wa kumpia mama Jihn kujua kilichokuwa kikiendelea Arusha lakini hakupatikana hapo hapo nikafanya kitu ambacho sikukipanga wala kutafakari.Nilipiga ile namba iliyokuwa imenipigia mchana na ikawa inaita.
‘’Hallow!’’ Nilisikia sauti nzito niliyohisi kutoka kwa mtu aliyekuwa usingizini.
‘’Hallow , habari!’’Nilijibu nikisikiliza simu kwa makini wakati huo nilikuwa nikirekodi kila simu iliyoingia na kutoka utaratibu ambao nilikuwa nao tangu niliponunua simu.
‘’Salama nani?’’Alijibu akionekana kutekwa na usingizi.
‘’Naam …… ehhee ….unasemaje sikusikii’’Nilijifanya kutomsikia na kukata simu baada ya kugundua tofauti kubwa ya sauti kati yake na niliyekuwa nimeongea naye mchana.
Hapo niliamua kuziama kabisa simu maana nilianza kuhisi kulikuwa na mtu zaidi ya mmoja hasa baada ya kukumbuka ile kauli ya mchana kuwa angenifuata chuoni hakaujiambia bali kula kuwa na mtu ama watu aliokuwa akiwaambia.
‘’Vita, tena vita haswaa’’Nilijisemea kwa sauti ndogo wakati nikizima simu.
Usiku ule ulipita nikiwa na mawazo mengi bila hata kujisomea licha ya kuwa na mtihani asubuhi ya siku iliyofuata hata wanafunzi wengangu tuliokuwa tuilala chumba kimoja waliporejea kutoka darasani nilijifanya kutowasikia na hata waliponiamsha na kuulizia kama nilikuwa na tatizo nilijifanya kuelemewa na usingizi mzito.
Asubuhi nilikurupuka na kufanya usafi wa mwili wangu kwa haraka na kujisomea kwa ajili ya mtihani uliokuwa ukitarajiwa kuanza saa mbili kutoka huo muda ambapo ilikuwa saa moja na nusu.Wengi waliniuliza kuhusu kutofautiana na Ludovick ambaye ufafiki wetu haukumaliza saa kumi sikuwajibu chochotre cha maana zaidi ya kuwataka waniache nijiandae kwa mtihani uliokuwa mbele yangu.
Mchana baada ya kumaliza mtihani nilirejea bwenini na kulala nikiwaza yaliyokuwa yakiniandama kwa wakati ule.Hapo nikakumbuka simu na kuiwasha lakini tofauti na nilivyotegemea sikupokea ujumbe wowote wakati nilikuwa nimeshazoea kupokea ujumbe kutoka kwa Alice akinitakia mtihani mwema ama akinipa pole , pia nilikuwa nimeshazoea kupokea ujumbe kutoka wka wazazi wangu waliokuwa Lindi.Nikaamua kuwapigia simu wazazi na kuongea nao kwa muda mrefu sana kabla ya kumpigia Alice ambaye naye niliongea nanye sana.
Wakati naongea na Alice , Ludovick aliingia na kunisalimu kwa ishara na kukaa pembeni akisubiri nimalize kuongea lakini niliamua kumkatisha Alice kwa madai kuwa nilikuwa naingia darasani na kumsikiliza Ludovick ambaye akili yangu iliniambioa kuwa nilikuwa na jambo.
‘’We unamdanganya shemeji darasa gani unaloingia?’’Aliniuliza Ludovick akicheka.
‘’Ahh hawa bila kuwadanganya unaweza usifanye kazi maana wao wanajiona ni watoto mara ohh ‘’nilikuwa naosha kijiko kimedondoka’’ mara ‘’nina kazi nyingi’’ , ukimuuliza nini atakuambia kuvua nguo na kuoga na hapo kajitahidi maana huweza kukutajia nguo moja moja na akaanza kutaja hatua hadi afike aseme kuoga utadhani anasafiri kwa moguu kwenda Dar’’ Niliongea na kumfanya Ludovick acheke haswaa hapo nikaanza kuhisi ile chuki ilikuwa imepungua.
‘’Hahahahhaaa! Ila kweli hawa nao wamezidi?’’ Aliongea akijifuta machozi yaliyotokana na kicheko.
‘’Haya bhana niambie Ludo vipi ‘pepa’ limekaaje?’’ Niliamua kubadili mada.
‘’Ahha wamekaza sana mku’’
‘’Pole sie hawakutukazia ile uvivu wa kusoma ulitufanya tukose hata cha kuandika’’
‘’Haaahahaaaaa! Hata mie naweza sema wamekaza kumbe uvivu tuu wa kushika madaftari’’Alinijibu akicheka na kunifanya niamini kuwa binadamu wote wakali sema wakikutana na kichocheo kwani sikuamini kama aliyekuwa amesusa hata kula jana yake ndiye niliykuwa naye wakati ule.
‘’Hahahahahaaaa wengine wanatungia sifa’’Niliendelea utani.
‘’Poa ila kilichonileta hapa si habari za hao walimu na mitihani yao’’Alibadili mada hata mwonekano wake akionekana kutotaka utabni tena.
‘’Kipi kimekuleta ama zile habari za jana?’’ Nilimuulizanikijiamini kwa nje lakini moyo wangu ni kama ulikuwa ukishindana kifua kutaka kutoka.
‘’Hakuna nyingine ni zile zile’’ Alisita kisha akaendelea.
‘’Kuna jambo nimetafakari sana na walau nimepata pa kuanzia’’
‘’Pakuanzia?’’ nilimuuliza huku bila kujielewa jasho jembamba likiwa limepita kutoka kwapani na nililihisi lilipofika kiunoni.
‘’Ndiyo nimepata njia nyingine ya kumpata aliyesababisha kifo cha Eric’’
‘’ Ipi hiyo?’’ Nilimuuliza kwa wahka.
‘’Usiogope mkuu taratibu tuu wala usiwe na papara’’Aliongea akiinuka na kwenda kufunga mlango wa kile chumba tulimokuwemo.
Nilitetemeka hasa nilipouona uso wake ambao haukuwa na chembe ya uoga.
‘’Mbona unafunga mlango?’’nliuliza huku nikiwa na mashaka huku nikizuia mtetemeko wa mwili uliokuwa umeshanitoa kijasho chembemaba kwa uoga.‘’Ni suala muhimu na la siri ‘’Alinijibu na kukaa pembeni yangu.‘’Siri,kuna siri ya watu wawili?’’‘’Hakuna siri hata kwa huyo mmoja, labda hata huyommoja akiwa haijui hapo ndipo tutasema pana siri’’‘’Unataka kuniambia hata mwenyewe umeamua kuniambia kwa kuwa siyo siri tena?’’‘’Ninachotaka kukuambia ni cha siri ila si siri’’‘’Siyo siri bali ni cha siri, mbona sikuelewi dadavua kidogo hapo’’Nilimuuliza huku nikiendelea kuusaili uso wake kujua kama palikuwa na baya moyoni mwake lililojitokeza usoni.‘’Nina maanisha kuwa hiki ninachotaka kukuambia siyo siri bali ni ‘cha siri’ yaani kinahitaji usiri ‘asiambiwe asiyehusika’, Umeelewa?’’ Niliitikia kwa kupandisha na kushusha kichwa na kumwacha aendelee.‘’Umelewa kweli?’’ Aliniuliza na kunikazia macho yake ambayo licha ya kuwa madogo lakini yalionekna kuwa na ujasiri ndani mwake.‘’Ndiyo , nimekuelewa bwana unauliza kama mwalimu wa ‘Zoology’ kusema utakuja kunipa mtihani siri na siri zake zina maana nyingi sema unanilazimisha kukariri maana yako uliyojitungia’’Nilimjibu kibabe kidogo kwani niliona kama alikuwa akinipotezea muda wangu kwa kuzunguka zunguka bila kuniam bia kilichokuwa kimemleta mle ndani.‘’Nina maana yangu kukupa maana ya siri maana nikija kusikia hili jambo sehemu nyingine utakuwa adui yangu mkubwa zaidi ya yule aliyemuua rafiki yangu Eric’’Aliongea bila mzaha na alipotaja jina la Eric kmoyo wangu ulikuwa kama umetoka nje na kurudi sehemu yake tena.‘’Haya endelea na siri yako ndugu’’Nilimjibu huku nikioana ule ni kama mtego wake wa kutaka kuhakikisha kama ndiye niliyekuwa mgomvi wa Eric lakini suala la kuniona kama muaaji na si msasabishaji wa tabia iliyopelekea kifo cha eric liliniumiza kichwa na kuniogofya haswa.‘’Nilikutana na aliyesababisha ugomvi kati ya Eric nahuyo jamaa aliyekuwa akisoma naye’’Alisita lna kunitazama usoni.‘’Enhee! Lini tena?’’Nilimuuliza niificha hofu ya si tuuya kutajwa jina langu bali usalama wa huyo msichana.‘’Imepita miaka mitano hivi ,ilikuwa Moshi mjini sikumgundua hadi siku moja alipoamua kunisimuliza kisa kilichomfanya aachane na mwanaume aliyekuwa naye’’‘’ MIaka mitano? ilikuwaje?’’Wahka ulizidi kunipanda.‘’Nilikutana naye mjini na nikamtupia ndoano akazungusha wee baadaye akanasa na tukaanza kula maisha siku moja ndo akaniambia kitu kilichomfanya ayajutia maisha na hata huko mbinguni aliko atakuwa nakumbuka ‘’Aliongea Ludovick akionesha hasira zake waziwazi.‘’Mbinguni kwani alifariki?’’Nilimuuliza nikiwa na hofu kubwa moyoni lakini nikiificha kwa juhudi zangu zote.‘’Atakuwa amekufa kwani alikuwa na ujauzito wangu kama haukutoka’’Aliongea kwa kujiamini huku akionekana kuzidiwa na hasira.‘’Na ujauzito? Kama haukutoka? Mbona sikuelewi?’’ nilimuuliza nikiwa kama nimechanganyikiwa.‘’We unaonekana huna kifua pasi wacha uyajue hayotuu mie naenda na nikisikia hata hicho kidogo kutoka kwa mtu mwingine nakuhakikishia kuwa utakuwa adui yangu namba moja mbele ya muuaji wa rafiki na shemeji yangu Eric’’ Aliongea kwa hasira na kutoka akipishana na mwanafunzi mwenzangu aliyekuwa akikaa ndani ya kile chumba ,nilioka haraka kumkimbilia na kumtaka anieeleze lilejambo lakini alikataa katakata na kuniamia tuu aakimaliza mitihani ataenda kutafuta jina la aliyemwita muuaji wa rafiki yake japokuwa hakuwa muuaji wa moja kwa moja ambaye ni mimi.Akili ilifanya kazui haraka haraka na kuwaza kwa nini alidai kuwa alitaka ajue jina la huyo mtu ili iweje na atajuaje kama atakuwa hai ama mfu na kuniongezea maswali mengi kichwani mwangu.‘’Ina maana ananihisi hivyo anatafuta uhakika?’’‘’Na kama hanihisi na hajanigundua anatafuta hilo jina la nini?’’Nilijiuliza maswali mawili ambayo yanitesa sana siku nzima na kunikosesha usingizi huku nikijitahidi kufuatilia nyendo za Ludovick kwa siri kwani kuondoka kwake shuleni kungeonesha kuwa hatari ya kujulikana na kuwa adui yake kungeniweka hatarini.Siku ile ikapita , siku nyingine ikapita na nyingine nazo zikapita hatimaye wiki mbili zilipita kwa kasi kubwa huku nikiendelea kukutana na Ludovick ambaye hatuongelea tena habari za Eric zaidi ya masomo na mambo mengine hivyo kunifanya niendelee kuwaza mengi sana uhai wangu niliuona ukiwa hatarini kupotea kwa sababu ya kisasi cha mtu, kisasi mabacho nilikiona si sahihi na halali kwangu.Nilibaki sina amani hadi siku moja kabla ya kuondoka shuleni tukijipanga kuondoka chuoni kwa ajili ya kwenda kumalizia likizo ya mwisho kabla ya kurudi chuoni kwa ajili ya kumalizia muhula wa mwisho na kuhitimu.Siku hiyo niliitumia sana kuongea na Alice simuni akinitaka niende Arusha nikae naye wiki nzima kisha niende nyumbani kwangu nilonakama bahati kwa Alice kutaka kuwa nami kwa muda wa wiki nzima tena kwa gharama zake ,sikufikiria ule msemo kuwa ‘Hakuna cha bure duniani’ niliuongezea maneno machache mbele na kuwa ‘ila kwa wachache wenye bahati’ na kuufanya usomeke ‘HAKUNA CHA BURE DUNIANI ILA KWA WACHACHE WENYE BAHATI’.Ingawa nilikuwa na furaha sana sikujisahaulisha juuya ile simu ya vitisho na habari za Ludovick na sualalake la kisasi, hapo nikajikuta nikifikiri zaidi na zaidi na kujikuta nikishangilia moyoni baada ya kupata ambacho niliamini ilikuwa ni njia aliyopanga kuitumia Ludovick baada ya kujua jina langu.‘’Nikuingia mtandaoni na kulitafuta jina langu hivyo angeletewa taarifa zangu zote na kujua kuwa nilikuwa wapi’’Hilo ndilo nililigundua.‘’Sasa?’’‘’Akili ni nywele , ni kumuwahi kwa njia yake’’Nilijiuliza na kujijibu kisha nikaingia mtandaoni na kutafuta taarifa zake ambapo nilipata kujua mengi hata ambayo sikuyategemea.Kwenye taarifa za kuchaguliwa kufika chuoni pale nilikutana na Anuani yake ambayo ilimwonesha kuwa likuwa mwenyeji wa Arusha, sikuihia hapo nikaingia kwenye mtandao wa facebook ambapo nilikutana na picha nyingi sana ambazo alikuwa amepiga akiwa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha .Nikazipakua na kuzihifadhi simuni na kushusha pumzi ndefu nikijisemea kwa sauti ya chini.‘’NITARUDI ARUSHA’’Siku iliyofuata niliwahi uamka na kupanda gari la kwanza lililonifikishamjini ambako nako nilipanda gari la kwanza nilifika Arusha mjini saa moja kasoro na moja kwa moja nilifika nyumbani kwa akina Johnnikionanan na mama yake akitaka kuelekea sokoni .‘’Ujio wangu ukamrudisha na baada ya salamu na maongezi machache nilimwonesha picha zile za Ludovick nikiwa na lengo la kutaka kujua maeneo aliyokuwa akiishi nikimdanganya kuwa alikuwa ni ndugu yangu niliyekuwa nikimtafuta pale Arusha.Ajabu alipoziona zile picha alishtuka.‘’Unamfahamu huyu?’’Aliniuliza huku akijitahidi kukumbuka kitu.‘’Ndiyo ni ndugu yangu’’Nilimjibu nikimwangalia lakini nilishuhudia kitu cha ajabu usoni pake.Machozi…
"Mbona hivyo dada?" Nilimuuliza baada ya kumwona akiendelea kulia huku akiwa ameehikilia tumbo lake.
"Tu...t...tu..tumbo" Aliongea mama John na kuanguka chini kisha kutulia.
Sikujua uhusiano hali ile na zile picha zangu hivyo nikajikuta nikichanganyikiwa, nilimwinua pale chinina kumkalisha nikiegamizakichwa chakeukutani.Wakati niiifikiria cha kufanya mara niiisikia sauti ya Japhet ambaye alionekana kufurahia uwepo wangu akiwa hana habari za mwenyeji wake kuwa katika hali mbaya.
Aliponikaribia akanirukia na kunikumbatia, lakini ghafla ainiachia nakumfutamama John aliyekuwa pale chiniametumbua macho.
"Umemfanya nini tena?"Aliniuliza kwa tuhuma maana kuniuliza nilichomfanya badala ya kilichompata nilitafsiri kama ishara ya kutoaminika naye licha msaada mkubwa niliokuwa nimewapa.
"Nasema umemfanya nini?"Japhety alizidi kupwayuka na kumfanya hata John aliyekuwa ndani aje mbio mbio.
"Sijamfanya chochote amelalakika tumbo na kunguka" Nikijaribu kumwelewesha Japhety aliyefura kwa hasira huku nikianza kuamini kuwahakuwa akimwamiji yeyote maishani mwake.
" Kuanguka ? Mbona hajawahi kutuangukia sisi na kilichokuleta hapa asubuhi hii ni kipi?" Japhety aliendelea kunishutumu kwa maswali yake wakati huo John alikuwa amemkumbatiamama yake pale chini akilia.
"Tuite gari tumpleke hospitali halafu hayo mengine tutayaongea ndugu.
"Na wewe kwa akili yako, gari ya nani tutakayoita huku uchochoroni muda huu?"Japhety aliendelea kunisuta.
Haraka haraka nikamwinua mama John nakumbeba nikifuata upande wa barabarani na kusimamisha kwa namna ya ajabu gari iliyokuwa ikipita kwani nilipitiliza hadi barabarani na kuifanya gari hiyo isimame nusu mita mbele ya miguu yangu nikipokea msonyo na tusi kubwa la nguoni kishanikaulizwa shida yangu.
"Enhee tukusaidie nini?"
"Mgonjwa, mgonjwa amezidiwa naomba msaada wa kufikishwa hospitalini" Niliongea nikiusogelea mlango wa gari ambao ulifunguliwa kwa haraka sana nadhani kutokana na kuchoka kwangu na hali ya mgonjwa ilivyokuwa.
Wakati huo Japhety na John walikuwa wameshafika.
"Haya ingia twende" Aliniamrisha.
"Wanangu"Nilingea nikimtaka awachukue na akina John hadi huko hospitalini kwani kwa kuwaacha pale bado ningewaachia maswali mengi juu yangu kwani akili zao zilishaanza kuwaambia kuwa nilikuwa mtu mbaya kwao licha ya msaada niliokuwa nimewapatia huko nyuma.
"Mwahishe mgonjwa kwanza watatufuata kwa miguu" Aliongea na kugeuza gari kurudi alikotoka.
"Mount Meru" Aliongea akichungulia dirishani akiwaelekeza akina Japhety na kuondoka gari kwa kasi.
Nilimtazama mama John ambaye kichwa chake kilikuwa juu ya mapaja yangu nikifikiria siku ile nilivyokuwa nimeianza vibaya.Nikajishangaa kwa ujasiri na uwezo wa kuubeba mwili wa mama John ambao wakati ule ulikuwa umeshaanza kuumiza misuli ya mapaja yangu.
Nilimwangalia macho yake makubwa bado yalionesha kukosa nguvu kabisa ya kuinua hata kope.
" Atakuwa hata hahudhurii kliniki huyo ona alivyochoka" Aliongea yule mwenye gari bila kunigeukia.
"Kliniki ya nini?"
" Kwa hiyo hata mwanao uliyemwacha kule ilitokea tuu bahati akajifungua?" Alizidi kuuliza maswali ambayo sikuyaelewa kabisa.
"Mwanangu? yule si mwanangu ni mtoto wa huyu binti" Niliongea nikibabaika ,wakati huo tulikuwa tukiingia hospitalini.
"Kwa hiyo mnalala tuu na mabinti za watu bila kufuatilia afya zao ,ona sasa unaweza hata kuuziwa mbuzi kwenye gunia huyo binti ni mjamzito na ujauzito unaonekana hata kama nisingekuwa daktari ningeu gundua" Aliongea yule mtu akiniangalia usoni na kujiachia maswali mengi yaliyokosa majibu.
" Ina maana mama John ni mjamzito?"Nilijiuliza kwa sauti bila kujua kwani nilihisi nimewaza lakini jibu la yule mtu ambaye niligundua kuwa alikuwa daktari lilinifanya nijue kuwa nilikuwa nimezungumza kwa sauti.
"Ndiyo mjamzito tena ujamzito mkubwa tuu sema kwa mwili wake ni vigumu kumgundua" Alinijibu swali ambalo nilikuwa najiuliza mwenyewe kujithibitishia nilichokuwa nimekisikia .
"Mhh" Niliguna na kukaa kimya nikimsubiri yule daktari anifungulie mlango.
"Usigune ni majukumu tuu hayo , tumeletwa duniani tuongezeke ilausirudie mara nyingine kutohudhuria na mkeo kliniki" Aliongea yule daktari akiwaita wahudumu kwa ishara na kuja kunifungulia mlango na dakika moja baadaye wauguzi wawili wakikuja kasi wakiwa na kitanda cha kuvuta.
"Sawa daktari" Niliitikia kinyonye wakati huo wale wauguzi walikuwa wameshamchukua mama John kwenye kile kitanda na kwenda naye ndani.
"Sawa mie naelekea nyumbani nikapumzike"Aliongea yule daktari na kutoa gari kwa kasi.
Kilisogea hadi kwenye benchi la mbao lilikuwa na watu wachache sana ambao niligundua kuwa walikuwa kwenye fikra ambazo ziliwafanya hata wasisikie salamu yangu.
Nami nikakaa pale nikirudisha akili yangu kwa mgonjwa wangu ambaye sikujua kama angekuwa mzima lakini jambo jipya ambalo liliibuliwa na yule daktari lilinifanya nifikiri sana.
Ujauzito, kwanza nilifikiri kuhusu muhusika wa ujauzito huo angenielewaje, angenishukuru ama angenishuku kuhusika kuiba tunda lake lakini zile tuhuma za Japhety na wasiwasi wake nazo zilinifanya nizidi kunyong'onyea pale kwenye benchi.Nilipokumbuka pia kilichokuwa kimenirudisha Arusha , hapo nilikuta fikra zangu zikikosa uelekeo kabisa.
Mara akaja Japhety akihema na kuniita kwa ishara nami nikainuka kutaka kumfuata lakini kabla sijapiga hatua alikuja muuguzi ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wamekuja kumchukua mama John pale garini na kuniita pembeni.
" We ndo mume wa yule binti?"
"Binti?" Niliuliza kusudi ili niipe akili yangu kufikiria zaidi.
" Ndiyo yule uliyemleta"
"Mhhh ....."
"Ndiyo nesi kuna tatizo lolote"Niliamua kukubali baada ya kufikiri kidogo kwani kukataa kungenifanya nitoe majibu ambayo yangeongeza maswali mengi zaidi ya kumtaka mume wa mama John ingawa jibu lile nalo lingeniweka kwenye wakati mgumu wa kuiibu maswali ambayo yangetaka majibu sahihi zaidi.
" Sawa , alikuwa ikihudhuria kliniki wapi?" Alijiuliza swali ambalo hata sikutegemea kuulizwa hivyo kunifanya nijute kudanganya.

Enheee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom