Riwaya: Hatia

Yani hapa kila kona ina majanga..., ila nmecheka sana pale Minja alipoenda kwa Rashidi, jamaa kaweka mbwembwe hatariii, eti sogeza gari hadi mlangoni...,
 
RIWAYA: HATIA
MTUNZI: George Iron.




SEHEMU YA KUMI NA MBILI


"Hapana sivyo!!! ila huyo John huyo John Mapulu namfahamu hana uwezo wa kuzaa iweje useme mkewe ana ujauzito?" aliuliza kwa sauti ya chini Rashid, macho yakamtoka Minja akabakia na pande la nyama mdomoni bila kutafuna, kauli ile ilikuwa imefungua akili yake kwa kiasi kikubwa.
Akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa bila kusema lolote. Kisha akatikisa kichwa kumaanisha kuwa ametambua jambo. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka tamaa ya pesa ya kichaga ikamwingia, ikamtuma kumchenga Rashid ili aweze kula peke yake.
"Ah!! wanawake wa mjini hao, hebu achana naye" alisema Minja. Rashid akaafiki, baada ya nusu saa wakaagana. Safari hii kila mmoja aliondoka kivyake.




****


Matha baada ya kumhadaa Minja na kumsimamisha kazi aliamua kutokuwa mbinafsi na kumshirikisha suala hilo Michael ambaye mara nyingi alikuwa msikilizaji. Lakini katika maongezi ya siku hiyo hakuwa ameridhia maamuzi hayo yaliyotaka kufanywa na Matha, yaani kumtafutia kazi nyingine Minja ili kumuweka mbali na John.
"Na vipi siku akikutana na John, au akimpigia simu???" aliuliza Michael, Matha akakiri kuwa hali bado ni tete.
"Minja sio mropokaji ni muelewa sana" alijaribu kutetea Matha, Michael akakubali kwa shingo upande.
"Akithubutu kunichezea nitamuua!!!" alijisemea kwa sauti ya chini lakini Michael aliweza kumsikia.
"Kuliko kuua ni heri tutoroke Matha!!" alishauri Michael, Matha akamkazia macho, Michael akawahi kukwepesha macho yake. Matha akaaga na kuondoka, John na Bruno hawakuwa nyumbani.
Huo ni uoga wa kunguru!!! Akawaza Matha juu ya kauli ya Michael kuhusu kutoroka.


****


Ukaidi wa Minja mbele ya John ilikuwa dharau kubwa sana, John alijua lazima kuna kitu, hisia za kwamba Minja anaweza kuwa 'informer' na huenda ameishtukia dili yao ya kwenda kuiba Supermarket. John akawaeleza wasiwasi huo wenzake, hisia za John zikawashtua wenzake, mara moja msako Minja ukaanza. Sehemu ya kwanza kabisa ilikuwa kazini kwa Minja yaani sheli ambapo hakuwepo. Msako haukuishia hapo lilikuwa jeshi la watu wanne wenye mioyo ya kuua.
Minja alikuwa katika hatia asiyoitambua.
John alikuwa amekerwa sana na dharau aliyofanyiwa. Msako huu kwa upande wa John ulikuwa kwa faida ya Matha, alitaka kujua kuwa ni kwa jinsi gani Minja amemfahamu Matha tena kwa majina yote mawili kiufasaha.
"Au Matha ana uhusiano naye jamaa ananifanyia jeuri!!!" alihisi John, wivu ukachukua nafasi yake ukaanza kuikwaruza nafsi ya John, hasira ikajikaribisha katika kiti kilichokuwa wazi katika moyo wake.
"Nitamuua kwa mkono wangu!!!" aliapiza baada ya kumkosa pale sheli kwa mara ya tatu.
Wenzake na John walichukulia kuwa hizo ni hasira za kawaida ambazo John alikuwanazo lakini haikuwa hivyo ni wivu wa mapenzi ulikuwa unamshambulia tena shambulio la nguvu na la ghafla.
Msako ukatoka pale sheli na kuhamia nyumbani kwake, ramani ilikuwa tayari mkononi mwa kundi hili.
Wakashauriana waende usiku!!!!


*****


Kitanda kilikuwa hakilaliki, si kwa sababu ya godoro lililokuwa limechakaa sana bali kutokana na mgogoro wa nafsi, mke wa Rashid aliigundua hali hiyo kwa mumewe ambaye siku hiyo alipendezesha chumba kwa harufu ya bia tofauti na siku nyingine ambazo hunuka pombe za kienyeji.
"Baba Karim!!!....vipi mbona hulali"
"Sina tu usingizi mke wangu" alijibu kwa sauti ya kukwaruza.
Rashid alikuwa katika dimbwi kubwa la mawazo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Minja. Umasikini ulikuwa unamtia katika fedheha kubwa, alidharauliwa na wala hakupendwa na mtu yeyote maana hakuwa na msaada wowote kwao. Wazo la utajiri kupitia kuusema ukweli unaomuhusu mke wa John lilimwingia lakini kisu kilikuwa kimeshikiliwa na Minja. Tamaa ikamwingia Rashid akatamani akishike yeye kisu hicho.
"Nitamweleza Minja na kama akikataa je?" alijiuliza.
"Akikataa nitaenda mwenyewe kwa John Mapulu" alijipatia jibu.
Mgogoro mkubwa wa nafsi ukautwaa usingizi wake, maumivu ya kichwa yakayeyusha usingizi wake. Rashid akaamua kuamka na kukaa kitandani, wakati huo mke wake alikuwa amelala tayari.
Nimeuchoka umasikini!!! alisema kwa nguvu kisha akajaribu tena kuutafuta usingizi.
Safari hii usingizi ulimchukua.
Siku iliyofuata akaamua iwe siku ya vitendo hakutaka kuchelewa zaidi. Kwa kuwa alipajua nyumbani kwa Minja aliamua kwenda usiku baada ya kuwa ametoka lindoni majira ya saa kumi na mbili jioni.
Siku nzima lindoni Rashid alikuwa anatazama vitu vya thamani huku akiamini kuwa iwapo Minja atakubaliana naye basi baada ya muda mfupi atakuwa na uwezo wa kuvinunua.
Ujio wa Minja nyumbani kwake siku moja iliyopita ulimzidishia tamaa zaidi ya kuipata pesa, miaka yake 40 aliyokuwanayo bado ilimruhusu kuwa na tamaa za kimwili, Rashid aliwatamani wanawake waliokuwa wakipishana katika maduka mbalimbali kununua vitu vya gharama.
"Nikizipata hawa watakuwa wananiheshimu na pia watakuwa wakinisalimia, hebu tazama wanavyonipita kama hawanioni vile!!!" Aliwaza Rashid, donge la hasira likamkaa kooni akajilazimisha kumeza mate lakini hayakupita. Akasonya!!
Alitamani jioni iweze kufika aijaribu bahati yake ya kupata pesa.
Jioni ilifika akaaga na kurejea nyumbani, hapo pia hakukaa sana alimuaga mkewe kuwa anatoka kisha akatoweka!! Hakusema anakwenda wapi.






*****




Chumba cha Minja kilikuwa kimya sana wakati anaingia, alijaribu kuita lakini hakupewa jibu lolote, lile giza lilimlazimu kutumia simu yake ya tochi kuweza kuona vyema ndani.
Chumba kilikuwa na harufu nzuri za manukato jambo ambalo halikuwa kawaida hata kidogo.
Jeuri ya pesa!!! aliwaza Rashid huku akichukua nafasi na kukaa.
Baada ya dakika kadhaa pakiwa na giza hivyo hivyo alisikia vishindo vya watu vikiingia ndani. Miale mikali ya tochi ilitua katika macho yake, alitumia viganja vyake kujikinga.
Maumivu makali katika paji la uso wake aliyasikilizia huku mwili wake ukiwa ardhini.
"Kwa nini leo hujaingia kazini??, kwa nini umeacha kazi tangu tufike siku zile??" Alisikia maswali yakimuelekea.
"Ni juzi tu ndio sijaenda jamani!!! sijaacha kazi, hata leo mchana nilikuwepo" alijitetea.
John alipatwa na ghadhabu akiwa nje ya chumba kile akiangalia hali ya usalama.huku akipuliza sigara yake.
"---- huyo anawadanganya!!!" alikoroma kwa sauti ya hasira tena yenye kisilani, wivu juu ya mpenzi wake ulimtwaa kwa kiasi kikubwa. Aliamini kuwa yule ndani ya chumba kile alikuwa ni Minja.
Waliokuwa wameingia ndani waliposikia kauli inayoitwa kudanganywa moja kwa moja wakajua kuwa aliyekuwa mbele yao ni adui.
Dakika tano pekee zilitosha kumbadilisha Rashid na kuwa tayari kwa kuhamia kaburini. Ilikuwa ni kabali baabkubwa iliyomzidi nguvu mlinzi huyu ambaye hata chakula cha usiku alikuwa hajapata.
Timu nzima ya John ikajua kuwa imemuangamiza Minja.
Tamaa zikawa zimemponza Rashid, utajiri alioutaka ukawa umeingia shubiri. Mchezo asioujua mwanzo wake ukawa umetwaa uhai wake.
Rashid akatokomea na tamaa yake!!


******




Minja akiwa na jeuri ya pesa ambayo sasa ilikuwa imebaki kama shilingi elfu sitini. Aliichukia sana hali ya chumba chake kutokuwa na umeme, siku hiyo hakutaka kuuvuta moshi mkali wa kibatari, giza lilivyoanza kuwa totoro akaamua kutoka, kwa kuwa hakuwa na chochote cha thamani kinachoweza kuwavutia wezi aliurudishia mlango wa chumba chake na kutoweka, alikuwa amevalia nguo mpya alizokuwa amenunua siku hiyo, aliamini kuwa alikuwa amependeza sana. Pesa zile kidogo zilikuwa zinamuwasha, taratibu huku akiepuka kuchafua kiatu chake kilichokuwa kimeng'arishwa haswa alizipiga hatua hadi akafika katika 'bar' maarufu pande za Mabatini iliyokwenda kwa jina la 'Corner bar', akachagua meza ambayo ilikuwa tupu ikiwa imepambwa na viti vinne visivyokuwa na watu.
"We mwanamke!!!" alikoroma Minja, muhudumu akajikimbiza mara moja akasimama mbele ya Minja.
"Kasto laga (Castle lagger)" alibwatuka.
Muhudumu akachukua pesa na kuondoka kisha akarejea na kinywaji, Minja alianza kunywa taratibu kama mwanaume asiyekuwa na hofu ya pesa kumuishia. Baada ya pombe kumkaa sawa kichwani alipata ujasiri wa kwenda kumhadaa muhudumu ambaye alikuwa anashangaa shangaa huku na kule kutazama kama kuna mteja atamuita kwa ajili ya kutoa huduma.
"Njoo saa nne!!" yule muhudumu alimpa ahadi hiyo Minja. Minja hakutaka kurejea katika kijumba chake alichokuwa anakichukia kwa siku hiyo kutokana na giza lililokuwepo. Alichofanya ni kuhamia 'bar' nyingine huku akienda sawa na muda.
Saa nne kamili alikuwa amerejea 'Corner bar', muhudumu alikuwa tayari amevua sare zake. Akatokomea na Minja kama mpenzi wake wa siku nyingi sana.
Safari yao ikaishia nyumba ya kulala wageni.
"Mi silali lakini mwisho saa saba"
"Usijali" alijibu Minja huku akizivua nguo zake haraka haraka.
"Kwanza nipe pesa yangu kabisa!!"
"Shilingi ngapi??"
"Elfu tano"
Minja akatoa elfu kumi akampatia.
"Sihitaji chenji baki nayo" alisema kwa ujivuni Minja baada ya yule binti kuulizia kama Minja anayo 5000 iliyoshikana.
Binti akatabasamu na yeye akaanza kuzipunguza nguo zake mwilini. Tayari kwa kutoa huduma.
Hakuna aliyekumbuka suala la kutumia kinga, na hakuna aliyejutia baada ya tendo.
Saa sita usiku Minja alikuwa anarejea nyumbani kwake, alijihisi mwepesi na aliyechangamka sana baada ya tendo hilo alilokuwa amelikosa kwa siku nyingi sana.


Alipokikaribia kibanda chake furaha yake ilianza kupungua kwa kasi, alilitambua joto lililokuwa linamnyanyasa katika kijumba chake ambacho hakikuwa na 'sealingboard'. Alitamani kurejea katika nyumba ya kulala wageni ila akakumbuka kuwa alilipia kwa masaa kadhaa tu na wala si kulala hadi asubuhi.
Akapiga kite cha hasira kisha akaingia katika kijumba chake cha kupanga kama amelazimishwa hivi. Giza lilimpokea, lakini kwa kutumia uzoefu wa eneo hilo alipapasa hadi akakifikia kitanda chake akajibwaga bila kushusha neti. Usingizi haukumpitia kwa wepesi alipanga mipango kabambe ya siku inayofuata.
"Hivi nianzie na John ama nile pesa za Matha!!!" Alijiuliza huku akijipiga bega lake kupambana na mbu waliokuwa wanamzengea. Minja alikuwa katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi, kauli aliyokuwa amepewa na rafiki yake Rashid juu ya tatizo la John la kutozaa na kijitambulisho cha ujauzito wa Matha vitu hivi vilimtia kizunguzungu, akajiuliza ni nini cha kufanya. Hakika alikuwa masikini na hii kwake aliiona kama bahati ya walau kuukwaa huu ugonjwa unaotawala Tanzania, ugonjwa wa umasikini, ugonjwa uliokosa tiba ya kudumu.


Tamaa za kuwa na mahusiano na Matha zilimtawala, roho mpenda sifa alimkaa mwilini akashindwa kubanduka.
"Matha atake asitake atakuwa mpenzi wangu wa siri....na kama akikataa namueleza John ukweli" Alijisemea Minja huku akizikumbuka raha alizozipata na yule muhudumu wa 'bar' katika nyumba ya kulala wageni. Aliamini kuwa sasa atakuwa akizipata raha hizo bila kulipia bali kulipwa.
Hali ya hewa ilibadilika taratibu, ulianza kuvuma upepo ambao ulipunguza joto kidogo pale ndani, kisha ikafuata miungurumo. Bila shaka ilikuwa dalili ya mvua.
Minja alikereka kutokana na hali hiyo kwani dari la chumba chake lilikuwa linavuja. Kwa mara nyingine alipiga tena kite cha hasira.
Miale ya radi za hapa na pale ilileta mwanga pale ndani, Minja akaona kitu ambacho hakukitilia maanani sana kwani aliamini yalikuwa mawazo tu.
Alikuwa ameiona sura ya Rashid mbele yake.
Rashi cha ulevi!! Huyu jamaa anakunywa pombe huyu!! Alisema kwa sauti ya juu kidogo kisha akacheka.
Akapuuzia akiamini ni mawazo tu, akaendelea kuwaza na kuwazua, mwanga wa radi ulipopiga tena, Minja akaamini hapakuwa na mawazo ya namna hiyo, kulikuwa na kitu chini ya kimeza chake.
Mara moja akaiwasha simu yake akapapasa kidogo akapata kiberiti akakiwasha kimshumaa kilichokuwa kinakaribia kuisha. Kama vile amesukumwa kwa mitambo maalum alijikuta anajibamiza kitandani akasimama tuli akiwa ameyakodoa macho yake.
Alikuwa ni Rashid akiwa amekodoa macho na kutoa ulimi nje!!! Hakuwa Rashid tena alikuwa hayati Rashid.
Minja alitamani kumeza mate kulainisha koo ili aweze kupiga kelele lakini kinywa kilikuwa kimekauka sana ikashindikana. Upepo ukavuma tena. Mshumaa ukazimika!!! Hofu ikaongezeka, haikuwa ndoto tena Minja alikuwa chumba kimoja na maiti. Alitamani kukimbia lakini akajivika ujasiri alikuwa anatetemeka akapapasa tena akakipata kiberiti akawasha tena mshumaa, ukawaka. Akapiga hatua, akafika mahali ulipokuwa mwili wa Rashid.
"Minja! Minja! usimguse!!! utaacha ushahidi" Sauti ya ndani (Conciousness) ikamwambia Minja, akashtuka akasimama wima akaanza kurudi nyuma, joto katika suruali yake mpya lilitoa jawabu la mkojo uliopita bila idhini maalumu kutoka kwa muhusika.
Upepo ulivuma tena, mshumaa ukazima Minja hakuuwasha tena.
Wazo la kukimbia likavamia ubongo wake, wazo hilo likaambatana na milango ya jela. Minja akatetereka kidogo aanguke akahimili kuendelea kusimama. Harufu ya kwenda jela ikamtuma kukimbia, hakuna kitu alichokiogopa kama polisi bila kuchukua chochote zaidi ya pesa alizokuwa amezihifadhi chini ya godoro lake Minja alitoka usiku uleule bila kumwambia yeyote.
Hatia ya mauaji ikatembea naye kila hatua aliyokuwa akinyanyua. Ladha tamu ya pesa yake ikapotea, mawazo ya utajiri yakayeyuka.
Minja akawa mfuasi wa Hatia, kila mara Hatia ilivyochachamaa ndivyo ndugu yake aitwae hofu alikurupuka na kumtetemesha Minja. Jasho likawa linamvuja 'Singlend' yake ikazidiwa ikaruhusu na shati lake kuubeba mzigo wa jasho. Minja hakujua ni wapi anaelekea. Alichowaza wakati huo ni kutoroka!!! Hatia ikawa inampa suluba takatifu!!


*****


John Mapulu baada ya tukio hilo la mauaji alitaka kurejea nyumbani kwake lakini akakumbuka kuwa zilikuwa zimepita siku mbili hajaenda kumjulia hali Joyce Keto katika kasri lao jingine walilolipata kwa shughuli za kijambazi. Aliagana na wenzake akaelekea Nyasaka, jirani na shule ya mwanzo na upili ya Jerry's.
Ulikuwa ni usiku sana lakini John aliamua kuwa kwa usiku huo azungumze na Joyce kuhusu Michael Msombe. Hatia iliyokuwa inamkabili kuhusu ujauzito wa Joyce ilikuwa imemzidi uzito akaamua kuigawa kwa Joyce ili aone kama nafsi yake itakuwa huru, kwa kiasi kikubwa kifo cha Minja kilikuwa kimempa ahueni, aliamini kuwa mwanaume huyo kuna jambo la siri alikuwa anafanya na Matha, hivyo hata kabla hajalifahamu ni vyema alikuwa amemwondoa duniani.
John hakuwa tayari kumshuhudia Matha na mwanaume mwingine. Alikuwa anampenda sana, japo hakuwa na uwezo wa kumzalisha. Hiyo pia ilimsumbua kichwa kwani Matha hakuwa akijua lolote juu ya tatizo hilo..
Bahati nzuri Joyce alikuwa hajalala hadi muda huo kuna mfululizo wa sinema ya 'Nikita' alikuwa anaitazama. Ni yeye aliyekwenda kumfungulia John mlango.
Sura ya Joyce Keto ilimsababisha John kukosa ujasiri wa kuzungumza naye juu ya suala la Michael, ujasiri wote ukawa umeyeyuka!!!
"Mambo bro!!"
"Poa Joy, hulali wewe"
"Nimelala sana mchana, hata sina usingizi kwa sasa"
"Aaah!! ok!!" alijibu John huku akichukua nafasi katika moja ya sofa pale sebuleni.
John alikaa bila kusema lolote kwa dakika mbili, Joyce alikuwa bize anatazama mtiririko ule wa 'Nikita'.
"Rajab yupo!!" aliuliza.
"Yeah!! watakuwepo lakini walilala mapema"
"Basi utamwambia nilikuja" alisema John kisha akasimama na kuaga.
Ujasiri wa John ulikuwa umeyeyuka, alikuwa amepata wazo la kwenda kwa Matha aliamini huenda ndiye mtu sahihi wa kugawana naye ile hatia, japo Matha alikuwa hajui kama Michael alikuwa na uhusiano na Joyce ama la. John alikanyaga mafuta ya gari kwa kujitawala hadi akafika Buzuluga. Akazima injini ya gari yake katika moja ya sehemu za kuhifadhi magari akatembea kwa mwendo wa miguu kuanza kuzipanda ngazi ambazo zingemfikisha katika chumba cha Matha ghorofani.
"Kesho saa kumi jioni nitakutafuta"
"Uwe na namba hiyo hiyo usiweke ile ya zamani"
"Usijali usijali"
"Hakitaharibika kitu!!"
Ilisikika sauti ya Matha ikijibishana katika simu na mtu ambaye sauti yake haikusikika bali ilikoroma kumaanisha kwamba alikuwa ni mwanaume, John alisikia kila neno alilosema Matha kwa sababu ilikuwa ni usiku sana na kila mtu alikuwa amelala.
Wivu ukamvamia!! ukampiga mtama akaanguka, akajikongoja akainuka. Wivu aliodhani ameuzika kwa kumuua Minja ulikuwa umefufuka tena. Hasira zilipanda zikapita kipimo, John akauma meno kupambana na ghadhabu yake. Kinyumenyume akarejea hatua kadhaa, akataka kuondoka mara anataka kuendelea agonge hodi akawa anaenda mbele na kurudi nyuma.
Akawa kama kichaa hivi!! hatimaye akaamua kuondoka. Alikuwa amechukia sana japo hakuwa na uhakika huyo mwanaume ni nani kwa Matha.
"Matha kwanini ananifanyia hivi??" alijiuliza John wakati anaitoa gari sehemu alipokuwa ameihifadhi.
"Unasemaje bosi!!" aliulizwa na aliyehusika na kuingia na kutoka kwa magari. Kumbe alivyoongea alisikika. John hakujibu kitu akaondoka zake. Akaamua kuelekea nyumbani, mawazo tele yakamtawala, alimfikiria mwanaume aliyetaka kuingia katika anga zake kwa kumchukua Matha wake.
Kesho nitamjua lazima, saa kumi jioni!!!! alifikiria John huku akizidi kuiendesha gari yake kwa umakini.


*****




Kelele za simu yake alizifananisha na ule mlio wa 'alarm' akajiuliza aliitegesha kwa sababu zipi za maana. Akabonyeza kitufe bila kufumbua macho ikaacha kutoa mlio, baada ya dakika moja mlio ukaanza tena akaamka akiwa ametaharuki, aliamini simu ile haikuwa ikimtendea haki, macho makubwa yaliyokuwa yamekodoa yalitua katika simu yake.
Haikuwa alarm kama alivyodhani, ilikuwa namba mpya inampigia. Kidogo Matha aipuuzie lakini pia aliamua apokee ili ampe vidonge vyake mpigaji ambaye hajui kuwa ule ni usiku.
Matha alipopokea alikutana na sauti ya kiume iliyokuwa katika uoga.
"Mi Minja..nahitaji sana kuonana nawe" Sauti hiyo ikampasua donge la usingizi likayeyuka, akakaa kitako, na hakujua kama amekaa uchi. Minja hakuielezea shida yake katika simu alihitaji kumuona Matha, ndipo Matha akampa ahadi wakutane siku inayofuata majira ya saa kumi jioni. Kumbe wakati wote wa mazungumzo sikio la John lilikuwa makini kunasa kila kitu.
Hofu kuu ilimtanda Matha hakujua ni nini kimeharibika ghafla kiasi hicho, alitaka kumpigia Michael lakini akasita alihofia huenda angeweza kuwa karibu na John.
Hatia kuu ikamkaba kooni, akainuka akachukua maji yasiyochemshwa katika moja ya ndoo zilizokuwa ndani akajaribu kunywa, yalikuwa ya moto tena yenye chumvi akajilazimisha kumeza funda moja.
Hakuongeza tena!!! akakaa kitandani, kichwa kikaanza kumuuma. Alijutia mengi sana lakini, kubwa lililomnyanyasa ni mimba aliyokuwa nayo.
Matha akatanabai kwamba yupo katika vita kubwa sana, halafu yeye hana silaha wala hajaamua kujihami.
Akaisogelea kabati yake akatoa bunduki yake akaitazama kwa jicho la upendo kisha akaibusu. Akachukua na kisu chake akakibusu pia.
Nitamuua Minja nipunguze mateso haya!!!! alijiapiza Matha kisha akazirudisha silaha zake pahala pake.
Baada ya hapo alirejea kitandani akafanya sala fupi kumuomba Mungu amuepushe na balaa lililopo mbele yake, sala ilikuwa katika mtindo wa kubahatisha kwani alikuwa na siku nyingi sana hajaenda kanisani. Aliulazimisha usingizi kwa kujigeuza hapa na pale hatimaye kifo hicho cha muda kikampitia.
Asubuhi na mapema tayari Matha alikuwa amedamka, alifanya usafi wa hapa na pale kisha akajitosa bafuni akapambana na maji ya baridi, tayari ilikuwa saa mbili asubuhi akajipamba kidogo, akavaa suruali yake na blauzi chini akaweka viatu vya wazi akaufunga mlango akaondoka na kuingia katika mizunguko isiyokuwa rasmi ilimradi tu muda usogee na kuifikia saa kumi.
Hapa na pale hatimaye ilitimu saa nane na nusu, funguo zilikuwa zinatekenya kitasa cha mlango wake, mlango ukafunguka akaingia ndani.
"Upo wapi muda huu??" aliuliza kwenye simu.
"Nipo huku Makoroboi"
"Tukutane hapo kwenye maduka ya nguo karibu na geti la kuingia chuoni" alitoa maelekezo Matha, Minja upande wa pili akawa ameelewa tayari, simu ikakatwa.
Matha akaingia kuoga tena kwa mara ya pili, akajipamba tena akatia kisu pamoja na bastola yake katika mkoba wake, akauweka kwapani akajiangalia kwenye kioo kisha akatoka.




*****


John alifika na kujitupia katika kitanda chake bila kuvua viatu, alikuwa anashambuliwa na wivu mkali, alikuwa na hasira kali juu ya mwizi wa mpenzi wake. John Mapulu alikuwa anajiuliza ni nani huyo alikuwa na ujasiri wa kumgusa sharubu, midomo ikawa inatetemeka usingizi ukakataa kukaribia pale alipokuwa. Akasimama akajongea hadi sebuleni akaliendea jokofu akafungua akakutana na chupa ya kilevi, akaitwaa akaimimina katika glasi akainywa kwa vurugu, akawasha luninga akakutana na mechi ya mpira wa miguu akazimisha. Akaendelea kuubugia kwa fujo. Katika mawazo ya hapa na pale akapitiwa na usingizi hadi saa moja asubuhi aliposhtuka.
Alikodoa macho hapa na pale hakuna aliyekuwa ameamka hapo ndani, akaitwaa ile chupa ya mvinyo akaiweka juu ya jokofu akarejea chumbani kwake.
Akili yake ilikuwa katika mvutano mkubwa sana, siku hiyo ilikuwa ndio siku ya tukio la kwenda kuiba Supermarket kwa kutumia silaha lakini siku hiyo pia lilikuwepo tukio kubwa sana la kwenda kumfumania Matha. John akachekecha mawazo hapa na pale akaamua kuchagua moja. Kwenda kufumania!!!
Akanyanyua simu yake akabonyeza namba za mkuu wa kitengo cha maandalizi ya tukio la wizi.
"Mambo vipi kaka" alisalimia John kwa unyonge.
"Shwari kaka, vipi kwema"
"Ebwana si shwari sana, nitachelewa kuja huko, kichwa kinanisumbua sana" alidanganya John. Upande wa pili haukupinga akakubaliwa. Akakata simu.
Usingizi ulimchukua tena hadi saa nane mchana alivyoamka, akafanya maandalizi yake bila kumshirikisha mtu yeyote.
Saa tisa kasorobo tayari alikuwa maeneo yaliyomruhusu kuitazama vyema nyumba aliyokuwa akiishi Matha, ilimchukua dakika arobaini kumshuhudia Matha akitoka katika chumba chake. Laiti kama asingekuwa amelikariri umbo la Matha asingeweza kumtambua na angesubiri kwa muda mrefu bila kumuona. Matha alikuwa amevalia baibui la staili ya kininja alikuwa anaonekana macho peke yake. Hali hiyo ilimtikisa John, akazidi kuamini kuwa Matha alikuwa anaenda kufanya jambo baya.
Matha bila kujua kuwa anafatiliwa alielekea barabarani akaangaza hapa na pale akanyanyua mkono wake wa kuume akaita taksi, haraka haraka dereva aliyekuwa amemuona Matha aliifikisha gari yake Matha akaingia ndani.
John akasubiri ile teksi ilivyoanza kuondoka naye akaingia katika teksi aliyokuwa amekodi.
"Fuata gari hiyo!!" alitoa maelekezo hayo John, dereva akafuata maelekezo. Gari mbili zikawa zinafuatana bila gari ya mbele kuwa na habari juu ya hilo, John alikuwa amevaa miwani nyekundu kuziba macho yake yaliyokuwa mekundu sana, hakutaka kumtisha dereva.


*****




***WIVU umempelekea JOHN kuamua kumuua MINJA lakini bahati mbaya inamuangukia RASHID nakufa na umasikini wake.
***MINJA anajikuta katika HATIA ya mauaji...harufu ya jela inampa wazo kuu la kukimbia.......
***MATHA anapigiwa simu na mwanaume usiku...JOHN anasikia mazungumzo haya...WIVU unamkumba tena anaamua kufuatilia ni nani mwizi wake.
***MATHA ametembea na kisu na bastola...je? anaenda kuua ama???


HATIA INASUMBUA WAHUSIKA WOTE WA RIWAYA HII


Khantwe KABERWA2013 mbalu Honey Faith Sangomwile Jullie Z mugaru VAN HEIST binti kiziwi Donatila
 
RIWAYA: HATIA
MTUNZI: George Iron


SEHEMU YA KUMI NA TATU


Matha bila kujua kuwa anafuatiliwa alielekea barabarani akaangaza hapa na pale akanyanyua mkono wake wa kuume akaita taksi, haraka haraka dereva aliyekuwa amemuona Matha aliifikisha gari yake Matha akaingia ndani.
John akasubiri ile teksi ilivyoanza kuondoka naye akaingia katika teksi aliyokuwa amekodi.
"Fuata gari hiyo!!" alitoa maelekezo hayo John, dereva akafuata maelekezo. Gari mbili zikawa zinafuatana bila gari ya mbele kuwa na habari juu ya hilo, John alikuwa amevaa miwani nyekundu kuziba macho yake yaliyokuwa mekundu sana, hakutaka kumtisha dereva.


*****


Adrian alikuwa amekaa nje ya duka kubwa la kuuza nguo maeneo ya Makoroboi, umeme ulikuwa umekatika na biashara haikuwa nzuri sana siku hiyo. Adrian alikuwa anaperuzi katika gazeti la michezo alilokuwa amenunua muda mrefu uliopita.
Ubovu wa biashara wa siku hiyo haukumshtua sana Adrian kwani alikuwa na uhakika kuwa maduka mengine matano yaliyokuwa yamezagaa jijini Mwanza yangekuwa na biashara nzuri siku hiyo.
Mzee Mhina Mboje alikuwa amemuamini sana kijana wake huyu wa pili kuzaliwa, japo aliwahi kuikataa shule alipokuwa kidato cha tatu lakini akili yake katika kutafuta maisha ilikuwa inavutia wengi sana na kuwapa wivu. Adrian sasa alikuwa anasimamia maduka yote ya baba yake huku lile la Makoroboi likiwa mali yake binafsi. Adrian aliwahi sana kujipanga kimaisha kwani tayari alikuwa ameondoka nyumbani miaka mingi iliyopita na kuamua kufanya maisha ya kupanga.
Mwanzoni alikuwa anakaa na mdogo wake wa kiume lakini baada ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi aliamua kumrudisha mdogo wake nyumbani kwa wazazi ili aupate uhuru zaidi wa kujivinjari na binti huyu. Kwa kuwa ulikuwa upendo wake wa kwanza alikuwa akimsikiliza sana binti huyo ambaye alikuwa bado ni bikra, mapenzi yao ya kitoto toto waliyajua wao wenyewe. Adrian hakuruhusiwa kufanya lolote katika mwili wa huyu binti zaidi ya kumbusu shavuni tu na kuishia kucheza cheza.
Adrian hakuruhusiwa pia kutangaza kwa mtu yeyote juu ya uhusiano huu eti kisa tu baba yake binti alikuwa mkali sana. Upendo wa dhati ukawa umejijenga.
Ile hali ya Adrian kuukana uhusiano wake mbele ya watu ili kumfurahisha mpenzi wake huyo ilikuja kumgharimu sana. Akatokea mwanaume aliyekubuhu akamlaghai huyu binti ambaye ni Matha, alikuwa ni John Mapulu aliyemnyang'anya Adrian Mhina tonge mdomoni. Matha akahamishia upendo wake kwa John ambaye alikuwa ameitoa bikra yake. Adrian akabaki kama zezeta asijue la kufanya lakini hatimaye akazoea baada ya wawili hawa kuhamia sehemu nyingine kabisa mbali na yeye.
Kumbukumbu juu ya Matha zikasahaulika pia kutokana na mchumba wake ambaye walikuwa wanatarajia kuoana baada ya mwezi mmoja kwani walikuwa na mwaka mzima tangu waishi maisha ya uchumba huyu alikuwa ni Monica Lewis, dada zake walikuwa wakimpenda sana na hii ndio ilikuwa chachu ya kumshawishi Adrian kuoa.
Mara kwa mara Monica alikuwa analala nyumbani kwa Adrian, na hata kabla ya kutambulishana kwa wazazi tayari Monica alikuwa ameshiriki katika tendo la ndoa na Adrian, ujanja aliofanyiwa na Matha miaka iliyopita hakutaka tena kumwamini mwanamke.
Mwezi mmoja kabla ya ndoa tayari Monica alikuwa mjamzito, jambo hilo walilitambua wao peke yao, hawakutaka wazazi watambue hali hiyo ya wao kupata mtoto nje ya ndoa.
"Mambo vipi kaka" alisalimiwa Adrian akiwa bado ameinamia gazeti lake.
"Poa karibu!!" alijibu huku akiunyanyua uso wake. Hakutaka sana kumuangalia mtu aliyekuwa mbele yake kwa sababu alikuwa ameficha uso wake.
"Unanikaribisha unanijua kwani??" aliuliza yule binti ndani ya baibui, Adrian akacheka.
"Adrian!!! Za siku!!"
"Mh!! Kwani we nani"
"Matha!!! Jamani" alijitambulisha. Kumbukumbu ya sauti ile ya kupendeza ikarejea katika kichwa cha Adrian. Kabla hajajua la kufanya, Matha alimsogelea na kumkumbatia. Adrian hakuamini alichokuwa anakiona mbele yake, Matha akasikika kama analia, kilio hicho kikafuta hasira zote alizokuwanazo Adrian, joto lililopenya katika baibui na kumuingia Adrian likaibua hisia za upendo.
Walikumbatiana kwa dakika nzima. Kisha baada ya kuachiana Matha alijifunua kidogo, Adrian akaona vishimo katika mashavu ya Matha.
Upendo maradufu ukamvaa!!!
Matha akawa katika majuto ya hatia iliyokuwa inamkabili kwa yote aliyomtendea Adrian miaka iliyopita. Kwa mbaali akausikia mguso wa kimapenzi kutoka kwa Adrian. Akaanza kupatwa na hofu huenda Adrian bado ana hasira, lakini haikuwa hivyo!!!!
Walizungumza kwa dakika kadhaa kisha Matha akamwachia namba yake kijana huyu mwenyeji wa Tanga aliyekulia jijini Mwanza.
Yote hayo yaliyokuwa yanatokea yalishuhudiwa na jicho kali lililokuwa nyuma ya miwani, jicho la John Mapulu. Alitamani kumfyatua palepale yule mwanaume lakini alijikaza, akauzuia wivu usipitilize. Akawa amemtambua mwizi wake akapanda teksi na kuondoka, wakati huo na wawili hawa walikuwa wameagana.
Laiti kama angesubiri kidogo tu angepata kufahamu kuwa mpenzi wake huyo anakwenda kukutana na Minja anayeaminika kuwa alikufa usiku uliopita.
Lakini John Mapulu hakuwa na subira.


John alirejea nyumbani kwake, hakutaka tena kwenda kwenye tukio la ujambazi akili yake ilikuwa imechanganyikiwa kabisa. Uchungu alioupata Adrian miaka mitatu iliyopita sasa ulikuwa umemgeukia yeye.
Wakati anamnyakua Matha mikononi mwa Adrian alijiona kidume sasa na yeye alikuwa katika majaribu ya namna ya kipekee.
"Kama mwanzoni nilimchukulia Matha wake sasa wakati huu naitwaa roho yake, mshamba kama yule hawezi kumchukua Matha kirahisi hivyo, nitamuua!!!" aliapa John kwa sauti ya juu.
Alikuwa kama amechanganyikiwa!!!
Wivu ukawa unamtesa!!!




******




"Tukutane hapo nje ya chuo cha biashara (CBE)"
"Sawa dada" alijibu Minja. Matha akapiga hatua kadhaa akawa amefika hapo chuoni. Minja alikuwa ameanza kukasirika baada ya kuwa anapiga simu ya Matha halafu haipokelewi.
"Ingia ndani!!!" Matha alimuamrisha Minja bila kumuangalia usoni. Hiyo ilikuwa ni mbinu ya kuepusha kama yupo mtu anawafuatilia asiweze kugundua lolote. Laiti kama angejua aliyekuwa anawafatilia tayari amepata jibu na kuondoka hata asingeweza kujihangaisha hivyo.
Minja aliingia akaa katika meza moja, baada ya dakika mbili Matha naye akafika.
"Samahani kaka naweza kukaa hapa?" alizuga, Minja akashangaa. Matha akajiongeza akakaa.
"Chooni wapi kaka samahani" aliuliza kwa sauti ya juu ili majirani waweze kumsikia.
Minja akashangaa tena.
Matha akamuuliza mtu mwingine akaelekezwa akaenda uani.
Aliporejea alikaa alipokuwa Minja. Aliamini kuwa tayari amewapoteza baadhi ya watu.
"Ehee!! Kuna tatizo gani?"
"Yaani sijui nisemeje"
"Umeniita kufanya nini kama hujui la kusema" aliunguruma Matha, Minja akaogopa.
"Usiku kuna mtu ameuwawa ndani kwangu" alijitutumua na kumueleza kila kitu kilivyokuwa. Matha akawa ameelewa kuwa dhumuni lilikuwa ni kuuwawa kwa Minja.
"Laiti kama John angempata jana basi najua mambo yangekuwa mabaya……" aliwaza Matha huku walau hofu ya John kugundua tatizo hilo ikianza kupungua, lakini uwepo wa Minja jijini Mwanza ungekuwa bado ni tatizo. Matha hakuona tena haja ya kumuua Minja kwani alimuona kama hana hatia yoyote ile tena.
"Unatakiwa uondoke haraka hapa Mwanza"
"Sasa naenda wapi dadangu nisaidie"
"Hujui pa kwenda, basi utaenda jela" alisema Matha, Minja akatetemeka kusikia hivyo.
"Chukua hii, kesho uondoke!!!" Matha alimkabidhi Minja shilingi laki moja.
Laiti kama angejua kuwa Minja kuna jambo zito analifahamu wala asingekubali aondoke hai jijini Mwanza.
Asubuhi iliyofuata Minja akaondoka kuelekea Singida, alitegemea kufikia kwa rafiki yake ambaye waliwahi kufanya shughuli za udalali pamoja jijini Dar es salaam. Amani ikarejea moyoni mwake, akajihisi kuwa hana hatia tena. Akawa amesahau kuwa hatia humfuata muhusika popote atakapoenda.
Hatia ilipanda naye katika basi kuelekea Singida!!!!
Hatia haimuachi muhusika mpaka mwisho wa uhai wake, hatia huingia na mtu wake kaburini!!!




******




Adrian aliwahi sana kufunga duka siku hiyo, aliikatisha ahadi aliyokuwa nayo ya kutoka jioni ya siku hiyo na mpenzi wake (Monica). Kitendo cha kumuona Matha kwa mara nyingine tena kilikuwa kimeamsha ari fulani katika nafsi yake.
Alifika nyumbani kwake akaoga na kisha akaingia kitandani. Aliyawaza maisha yake na Matha miaka ya nyuma katika nyumba hiyohiyo hadi siku alipomsaliti na kuondoka na John. Zilikuwa ni hisia za kipekee zilizojawa na historia ambayo Monica hakuwa nayo kwani walikutana ukubwani.
Ile hali ya kukosa nafasi ya kuitoa bikra ya Matha ilimtesa sana lakini bado aliona si bure anaweza kuthubutu kumtoroka Monica kisha walau afanye mapenzi na Matha kama njia ya kupunguza machungu aliyoyapata wakati ule.
Adrian akaamua kumpigia simu Matha. Simu iliita kidogo ikapokelewa, alikuwa ni Matha katika sauti iliyochangamka sana. Adrian alilitambua hilo akajijengea kujiamini sana. Walizungumza mengi sana, na kuishia katika mazungumzo yaliyohusisha penzi lao la wakati ule. Mazungumzo hayo yaliibua hisia kwa kila mmoja, Matha akawa wa kwanza kulia, Adrian Mhina akaligundua hilo akajaribu kumbembeleza sana lakini kwa kuwa alikuwa yupo kwenye simu ilikuwa ni kazi bure.
"Adrian nahitaji kukuona!!!!" Matha alijikuta akitamka kwa hisia kali. Adrian hakuamini alijua kuwa Matha anatania. Lakini kadri alivyorudia mara kwa mara ndipo aliamini kuwa alikuwa anamaanisha mpenzi huyu wa zamani.
Kwa kuwa alikuwa ameoga tayari, alivaa pensi ambayo hupendelea kuivaa jioni, juu akavaa fulana iliyokuwa inambana na kuonyesha kifua chake jinsi kilivyokuwa kimejigawanya katikati, chini akavaa viatu vya wazi.
Akachukua pochi yake, akatazama ndani yake palikuwa na kadi ya benki (ATM) na noti kadhaa za shilingi elfu kumi na elfu tano.
Hizo zilimtosha kwa ajili ya kuchukua teksi iliyomfikisha maeneo ya PPF Tower, akazama katika mashine ya kutoa pesa akajitwalia kiasi alichotaka, kisha akapanda tena hiyo teksi iliyokuwa inamsubiri.
"Tunaelekea wapi bosi!!!" alitamka yule dereva, Adrian akatabasamu kusikia anaitwa bosi, tabasamu lake likaruhusu meno yake yaliyoathiriwa na utafunaji wa vitu vyenye sukari kuonekana.
"Millenium Hotel Nyegezi" alijibu kwa sauti nzito na tulivu.
Safari ikaanza!!!


Matha alikuwa anamaanisha alichokuwa anamwambia Adrian kwenye simu, picha za Michael na John Mapulu zilitokea mara kwa mara lakini hazikuweza kukizuia kivuli cha Adrian Mhina. Alijua ni kweli anafanya usaliti lakini, ile hatia ya kumtenda Adrian miaka kadhaa iliyopita ikawa inamuadhibu. Matha akajikuta anafanya maamuzi ya ajabu!! Maamuzi ya kuificha na kuifuta hatia hiyo kwa kumpa penzi Adrian.
"John alimdhulumu Adrian, Michael amemwibia John, na Adrian anachukua kwa Michael….ah!! wote weziiii" alisema Matha wakati akiikaribia hoteli ya Millenium iliyopo maeneo ya Nyegezi jijini Mwanza.
Matha alianguka kifuani mwa Adrian baada ya kuwa wameingia chumbani, Adrian alimpokea kwa kumbatizi lenye huba ndani yake. Machozi yakamtoka Matha na kukilowanisha kifua cha Adrian, Adrian hakuwa jasiri na yeye akatokwa machozi. Walikuwa wanavuta fikra za miaka iliyopita.
Baada ya kuachiana, kila mmoja alimtazama mwenzake, halafu kwa pamoja wakautazama mlango kumbe ulikuwa unapiga kengele ya kuwapa taarifa ya kuwa upo wazi, wakatabasamu Matha akaenda kuufunga vizuri.
Wakati anaenda mlangoni Adrian alipata fursa ya kumwangalia vizuri jinsi alivyokuwa ameumbika, hakuwa na shaka hata kidogo kuwa alikuwa na haki ya kumtoroka Monica siku hiyo na kuzini nje. Matha alikuwa ni mrembo haswaa, wakati anaufunga mlango aliinama kidogo, kikaonekana kicheni kinang'ara katika kiuno chake.
Macho yakamtoka Adrian, alijua kuwa Matha alifanya maksudi kwani tangu zamani hizo alikuwa anafahamu ni kwa jinsi gani yeye (Adrian) ni mfuasi wa kiurembo hicho.
Wakati Matha anarejea katika mwendo wa kunyata na yeye Adrian alielekea Matha alipotoka, akachomoa kikadi kilichokuwa pembeni kidogo ya mlango. Taa zote zikazima!!! Kiyoyozi kikawaka!!!
Teknolojia ina mambo!!!!
Akarudi kwa hisia za kupapasa akafika na kumkuta Matha bado amesimama. Akamkumbatia tena na kumbusu.
"Asante Adrian!!!" alishukuru Matha kwa sauti ya kimahaba.
Katika chumba hicho hakuongelewa Michael, John wala Monica.
Kila mmoja alijua kuwa alikuwa anaiba!!!!






*****




Monica alikuwa anampenda sana Adrian sio tu kwa kuwa alikuwa na pesa na pia anatoka familia ya kitajiri la!! Moyo wa kujali aliokuwanao Adrian ulimvutia zaidi. Japo wasichana wengi walidhani kuwa Monica amefuata pesa kwa Adrian.
Siku hii Monica alikuwa anataka kuzungumza na Adrian juu ya ndoa yao ambayo ilikuwa imekaribia na huo ujauzito aliokuwanao.
Suala la kuitunza siri ya ujauzito huo ilikuwa imemchosha hivyo alihitaji kumshauri Adrian kuwa wawe wawazi.
Adrian aliporejea tu kutoka Nairobi alipokuwa amefuata mzigo wa nguo mpya. Monica alimuomba waonane, Adrian akawa amempangia Monica siku hii ambayo alikutana na Matha. Ile hali ya Adrian kuhairisha ghafla miadi hiyo wakati yeye Monica akiwa amejipanga na kuwaaga wazazi wake ilimshtua na kumkera sana, alijiuliza maswali mengi.
"Mara anaumwa!!! Sijui hajisikii vizuri!!!...kuna ukweli hapa au mume wangu amenichoka!!!" alijiuliza. Hakutaka kumwambia mtu yeyote kuwa Adrian amehairisha ahadi yake. Aliona aibu kwa wadogo zake wa kike ambao kila siku walikuwa wakimwonea wivu.
Monica akawaza sana mwishowe akaamua kwenda kwa Adrian bila taarifa.
"Isijekuwa ana kasichana leo hapo kwake….yaani sijui nitamfanyaje!!!" aliwaza Monica, wakati huo ilikuwa saa nne usiku.
Kimya kimya huku mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio aliifikia nyumba ya Adrian. Akanyata hadi mlangoni.
Akatega sikio hakusikia lolote lakini pumzi zikipishana hapa na pale. Kabla ya kugonga mlango akaiondoa kanga yake aliyokuwa amevaa akabakia na kisketi kifupi sana, lengo likiwa kumtega Adrian.
Akaikunja kanga na kuitia katika mkoba, akajaribu kufungua mlango ukawa haujafungwa, akausukuma taratibu ndani taa ilikuwa imezimwa, akapiga hatua mpaka ndani.
"koh….koh….koh…" akakohoa baada ya kukutana harufu ya sigara, wakati anaiendea taa akasikia kitu cha baridi kabisa kikimgusa shingoni.
"We Adrian wewe!!! Hebu acha ujinga…ina maana kumbe….." kabla hajamaliza alisikia kitu kizito kikitua mgongoni mwake, hakikuwa chuma lakini mkono wa mtu, viatu virefu alivyokuwa amevaa vikamtegua mguu wakati anajaribu kutafuta balansi. Akapiga ukelele wa nguvu ukelele wa maumivu.
Mara taa ikawashwa, hakuwa Adrian!!! Ilikuwa sura ngeni kabisa machoni mwake.
"Shkamoo" alisalimia kwa uoga, akajibiwa kwa tabasamu feki, macho mekundu.
"Wewe ni nani yake Ady" aliulizwa.
"Nani mimi?" aliuliza na yeye il-hali wapo wawili tu hapo ndani. Akapokea pigo jingine usoni akatoa kelele tena. Kelele hazikuwa na msaada wowote kwani nyumba ya Adrian ilikuwa imejitenga sana.
"Mke wake…naniii mchumba" alijibu Monica. Uso wake tayari ulikuwa mwekundu na alikuwa anajitahidi kuizuia damu inayomtoka isiendelee kutoka kwa kujilamba midomo.
Jibu hilo lilikuwa baya sana mbele ya mtu aliyekuwa mbele yake. Mwanzoni alikuwa ameishikilia bunduki lakini sasa akaiweka kando akamvagaa yule msichana akamchania chania nguo zake, kisketi, bikini, sidiria na blauzi Monica akawa uchi wa mnyama. Lakini mbele yake alikuwepo mnyama mwingine John Mapulu. Kama vile simba anavyomvagaa swala ndivyo John alifanya akamvagaa na kuanza kumbaka Monica kwa kulazimisha, nguvu alizokuwanazo zilimshinda Monica ambaye alikuwa hajaandaliwa, maumivu yakamzidi damu nazo zikamvuja sana.
"Nisamehe!!!"
"Akusamehe nani?? Unajua Adrian yupo wapi na anafanya nini??" aliuliza John huku akiendelea kumbaka Monica.
Baada ya kumbaka alimtembezea mwaliko wa kipigo kikali sana. Monica akapasuka pasuka.
John hakuwa na huruma!!! Tayari alijua kuwa yu hatiani hivyo ongezeko la hatia nyingine kwake halikuwa tatizo. Maana hatia moja ukiongeza nyingine jibu bado ni HATIA.
Alitambua kuwa ameua tayari!! Akavaa nguo zake na kutoweka bila kizuizi chochote, akimwacha Monica nusu mfu nusu hai.






*****




Matha na Adrian waliamka kwa ajili ya kujiandaa majira ya saa kumi na moja alfajiri.
Wote walikuwa hawawezi kutazamana usoni. Hakuna aliyeweza kuzungumzia kuhusu usiku uliopita. Kila mmoja alijidai hajui kinachoendelea.
Adrian aliwahi bafuni akabonyeza kitufe katika moja ya kona ya bafu maji yakaanza kupata joto, alipohakikisha joto hilo ni sahihi akaenda na kumchukua Matha wakaingia kuoga wote. Huko walikuwa kama watoto wadogo, mara wafinyane wamwagiane maji wabebane waogeshane ilimradi tu burudani.
Walitumia saa zima bafuni na wote walitoka wakiwa na furaha.
"Twende ukapaone kwangu najua umepasahau tayari, maana lile ghorofa la mzee Kimaro limevunjwa tayari yaani huwezi kupakumbuka"
"Siwezi kupotea hata iweje, sasa nitakuja peke yangu kesho!!" aliahidi Matha katika hali ya kubishana. Adrian akakubaliana naye kwamba kesho ataenda mwenyewe. Waliagana kwa kukumbatiana pale chumbani kisha wakateremka na kwenda kupata kifungua kinywa halafu wakapanda teksi iliyomfikisha Matha hadi Buzuluga stendi na kisha kuondoka na Adrian kuelekea Isamilo.
Wakapungiana mikono ya heri.
Adrian alipoagana na Matha ndipo alipata upenyo kidogo wa kumfikiria Monica, kwanza alimchukulia kama msichana ambaye ameingilia mapenzi yake na Matha. Aliamini Monica ndiye alipaswa kuwa mpenzi wa John halafu yeye na Matha waendelee kama zamani.
Suala la Matha kuwa bado hajazaa lilizidi kumtia hamasa Adrian na kuamini kabisa kuwa alipangwa kwa ajili yake kiumbe huyu. Uchungu wa bikra ya Matha kutolewa na mtu mwingine tayari ulikuwa umepoozwa usiku uliyopita, penzi alilopata kwa Matha lilikuwa limekifuta kidonda kile, wazo la kuendelea kuwa na Matha katika mapenzi lilivamia kichwa chake, likamyumbisha kimsimamo akaanza kuziona siku za kufunga ndoa na Monica zikizidi kusogea. Adrian akaanza kumuona Monica kuwa si mwanamke sahihi tena kwake.
Adrian alitaka kumkwapua Matha, jumla jumla.
Akiwa katika mawazo hayo akaikumbuka mimba aliyokuwa nayo Monica. Jambo hilo likamfadhaisha sana alijua hicho ndio kilikuwa kiunganishi baina yao.
Naenda kumshauri aitoe!!!! Aliijiwa na wazo hilo la kishetani.
Lakini kabla ya kumwambia aitoe hebu ngoja kwanza nikazungumze na mzee juu ya kuhairisha ndoa hii kwanza. Adrian aliwaza hivyo kwani alikuwa anaamini mzee wake alikuwa anampenda sana hivyo atamsikiliza na kumsaidia.
"Hebu ingia huku Kirumba kwanza" Adrian alimwamuru dereva aende upande alioutaka. Huko ndipo alikuwa anakaa mzee Mhina na familia yake, hapo hapo nyumbani mzee Mhina alikuwa na ofisi yake ndogo.
Adrian alifika na kuingia moja kwa moja ndani akawasalimia ndugu zake kisha akaenda kidogo kudeka kwa mama yake kabla ya kuingia ofisini kwa baba yake.
"Simba hilooo!!!" alikoroma mzee Mhina akimsifia mtoto wake. Adrian alizipokea zile sifa kwa kicheko kidogo kisha akamsalimia mzee wake kwa kumshika mkono halafu akakaa.
"Umetutenga sana simbaaaa!!!!"
"Majukumu baba!!!!" alijibu Adrian.
"Anakuja Monica tu, ana juhudi sana yule mtoto wangu" maneno hayo yaliyotoka katika kinywa cha Mzee Mhina yalimchoma sana Adrian kwani alijua ni kiasi gani familia yake ilikuwa inampenda Monica.
"Monica akija ni sawa nimekuja mimi" alijibu kwa sauti ya chini Adrian.
"Haya niambie mguu huo najua ni kwangu"
"Ndio mguu huu kwako kuna jambo nahitaji tuzungumze kidogo ni kuhusu ndoa yangu mimi na Monica" Mzee Mhina akashtuka kidogo, akaacha kazi alizokuwa anafanya akaondoa miwani yake machoni akamtazama Adrian.
"Umempiga mtoto wa watu eeh!!" alibashiri. Adrian hakujibu akatabasamu!!!
"Bora ingekuwa hivyo tungeyamaliza wawili"
"Nini sasa tatizo…."
Kabla mzee Mhina hajamaliza kuzungumza alikatishwa na simu ya Adrian.
"Ah!! Namba mpya hizi zinaniboa sana" alilalamika huku akijiweka sawa koo kwa ajili ya kupokea simu ile.
"Adrian Mhina nani mwenzangu!!!"
"Naitwa Jose kuna tatizo hapa kwako!!!"
"Tatizo tatizo gani??" alihoji kwa mshangao mkubwa Adrian, mzee Mhina alikuwa makini kana kwamba alikuwa anausikia upande wa pili unavyojieleza.
"Mkeo… ni mkeo…..hebu njoo" kauli hiyo ikamnyanyua kutoka katika kiti alichokuwa amekaa, akaanza kupambana na joto kali lililomkumba ghafla. Mzee Mhina naye akasimama wima na kumsogelea mwanaye.
"Adrian nini kimetokea kwani"
"Hata sielewi wananiambia mke wangu sijui, hebu ngoja niende baba"
"Tunaenda wote hebu ngoja" mzee Mhina aliingia ndani akachukua funguo za gari lake akamuaga mama Adrian bila kumwambia lolote linaloendelea.
Injini za gari zilizimwa mbali kidogo na nyumba aliyokuwa anaishi Adrian kwani umati ulikuwa mkubwa sana, Adrian alikuwa anatetemeka sana lakini mzee Mhina ukongwe ulimsaidia aliweza kupambana na presha ile.
"Mungu Wangu sijui kama ni mzima yule" walisikika watu wakizungumza. Adrian aliyasikia hayo, mzee Mhina akawa makini amemshika mkono kwani aliamini kuwa kuna tatizo kubwa ambalo mwanae hawezi kulihimili.
Na kweli hakuwa amewaza vibaya mzee huyu, punde tu baada ya kuuona mwili wa mpenzi wake Monica ukiwa umezungukwa na damu pande zote lakini ukiwa umesitiriwa kwa upande wa kanga Adrian alilegea na kupoteza fahamu palepale. Likaanza zoezi la kumpepea pasipo mafanikio.




****ADRIAN anaanza kunogewa na penzi lake la utotoni kwa MATHA...sasa anataka kumdhulumu JOHN MAPULU jumla....akiwa bado katika mwanzo wa harakati..linatokea tukio baya nyumbani kwake...MONICA anabakwa!!! MSHTUKO!!!


****JOHN MAPULU amebaka huku akiamini kuwa ADRIAN ndiye mwizi wake namba moja....anaapa kumwondoa duniani..je? atatimiza!!!!


****MINJA amesafiri na hatia yake kukimbilia Singida..je!! hatia imekubali kubaki Mwanza na kumwacha huru MINJA!!!!

NYIRO master09
Khantwe KABERWA2013 mbalu Honey Faith Sangomwile Jullie Z mugaru VAN HEIST binti kiziwi Donatila
 
Last edited by a moderator:
Inapendeza sana kusoma hadithi inayotaja maeneo unayoishi na kuyajua kwa undani
Big UP
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom