Riwaya: Hatia

RIWAYA: HATIA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA TANO


"Dakika tatu zinazokuja tutakuwa nje, msiwe na papara zozote zile ili tufike salama!!!" alizungumza kwa kumaanisha John Mapulu, Michael alikuwa anatetemeka, alitambua kuwa hakuwa na hatia lakini sasa alikuwa anajiingiza katika hatia ya ukweli. Lakini kipi bora kunyongwa bila hatia au ukiwa na hatia!!! Alijiuliza lakini alikuwa amechelewa sana kupata jibu litakalompa maamuzi sahihi mlango wa pili ukawa wazi.
"JOHN Mapulu….kuja hapa…kuja hapa haraka" ilisikika sauti ya amri ni sauti John aliyoifahamu ilikuwa sauti ya mpelelezi wa kesi yake Sajenti Romagi, mpelelezi aliyesifika kwa ukatiri wake


Mkojo wa moto kabisa ulikuwa umeshapenya katika suruali ya Michael, alikuwa muoga kuliko wenzake hii ni kwa kuwa hakuwahi kuzoea hizo pilika pilika. John alisimama thabiti akakuna kichwa chake kutafuta maamuzi sahihi ama kurejea na kuitikia wito ama kuendelea na safari yao ya hatari kabisa. Hakutakiwa kupoteza hata sekunde kumi!!!! Tatizo!!!
Hatia ya kutoroka ikaanza kumsulubisha palepale kabla hajatimiza lengo!!!
"Twendeni!!!" aliamuru John, akafuatiwa nyuma na kundi la watu watatu wote wanaume lakini mmoja akiwa anatetemeka sana kama mwanamke huyo alikuwa ni Michael. mlango wa kutokea nje ulikuwa umefunguliwa na vijana ambao walikuwa wameziba nyuso zao kwa kutumia vitu kama soksi kubwa hivyo sura zao hazikuonekana. Hawakuzungumza kitu lakini John alielewa kipi kinachoendelea, upepo wa nje majira ya usiku ulipokelewa vilivyo na mapafu ya Michael na kumsahaulisha kosa kubwa alilokuwa amelitenda kosa la kutoroka!!!! Akiwa hajui la kufanya na wapi pa kwenda John Mapulu alimshika mkono wakaanza kutokomea taratibu kuelekea walipojua wao lakini Michael alikuwa kama kipofu anayefuata mkondo.
Hatua kadhaa mbele Michael akiwa ameamini tayari wapo huru bila kupata usumbufu wowote katika giza walimkuta askari aliyekuwa lindoni akiwa amejiegemeza ukutani, John akamshtukia kuwa tayari alikuwa ameuchapa usingizi maeneo yale ilisikika harufu kali ya bangi bila shaka kabla ya kusinzia askari yule alivuta misokoto kadhaa ya mmea huu halali katika nchi ya Jamaika.
Michael ambaye muda wote alikuwa anatetemeka alimshuhudia John akinyata kwa tahadhari kubwa na kumrukia yule askari kilichofuata ni kitendo cha John Mapulu kuwa juu ya askari huku mikono yake ikiwa imelikamata koromeo la huyu kiumbe barabara, baada ya dakika kadhaa akamwacha huru, licha ya kuachiwa huru hakuweza hata kusema neno. Alikuwa maiti!!!
"Washenzi sana hawa!!!" alisema John kisha akampa ishara Michael amfuate, wale waliofungua mlango na akina John wakatoka walikuwa wamepita njia nyingine pamoja na wale wawili wenye kesi ya bunduki waliopata upenyo wa kutoroka pamoja na John baada ya kuamshwa wasaidie kufungua mlango. John tayari alikuwa na bunduki mkononi nani wa kumtisha kiumbe huyu hatari linapokuja suala la kutumia bunduki!!!! Michael alijiona muuaji na anayezidi kupotea njia pumzi za uhuru alizozikurupukia sasa zilikuwa zinamuwasha zaidi ya kawaida. Hatua kwa hatua, mtaa kwa mtaa, hatimaye walikuwa katikati ya kundi la raia wema ndani ya daladala zinazoelekea Nyakato Mecco nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Michael bado alikuwa kipofu!!!


****


Geti dogo lilifunguliwa kidogo, baada ya kuhakikisha aliyetegemewa kuingia ndiye alikuwa mlangoni lilifunguliwa zaidi.
"Mheshimiwa Mapulu!!!! Karibu nyumbani…..kama ndoto vile" sauti nzito ya kiume ilimlaki John aliyejibu kwa tabasamu hafifu.
"Matha yupo au na yeye alikamatwa??" John aliuliza wakati huo ilikuwa yapata saa kumi adhuhuri.
"Matha yupo lakini anakamuliwa na mshkaji mwingine" Alijibiwa kwa njia ya utani akaling'amua hilo akatoa kicheko kidogo.
"Dogo langu hili, linaitwa Michael Msombe muite Dabo M,ukishindwa kabisa muite Dabo" John alimtambulisha Michael kama mtu ambaye anamfahamu siku nyingi sana. Akambatiza jina la Dabo.
"Mambo vipi bro!!!" alisalimia Michael
"Poa Dabo naitwa Bruno…karibu sana"
"Asante sana" alijibu na geti likafungwa.
Haikuwa nyumba iliyotangaza umasikini hata kidogo lakini ilionyesha matumizi mabaya ya pesa kwa samani zisizokuwa na shughuli maalumu kulundikana pale ndani, usiku ule hakuona mtu yeyote zaidi ya Bruno akahisi huenda wamelala wengine lakini haikuwa hivyo hadi panapambazuka hali ilikuwa hivyohivyo.
Michael alishangaa lakini hakuuliza. Asubuhi yule John wa selo aliyekuwa akishindia kapensi kafupi kalikochakaa na wakati mwingine kumwacha uchi wakati akigombania vyakula walivyoletewa mahabusu wengine hakuwa yule tena alikuwa ameng'ara ndani ya nguo ya kulalia rangi nyeupe kabisa mkononi alikuwa na kikombe kikubwa kilichoongezwa uzito na maziwa yaliyokuwa ndani yake. John alikuwa tofauti sana hata rangi yake ilikuwa si ile iliyochafuka na kukosa maji ya kuoga walipokuwa selo.
"Michael kuna mtu yeyote aliyekuwa anafahamu uwepo wako ndani ya selo??."
"Mh!!!! Hapana sidhani" alijibu baada ya kujaribu kufikiri
"Una uhakika kuwa hujawahi kuja kusalimiwa???"
"Hakuwahi kuja mtu yeyote pale kaka, we ulikuwa shahidi" aliendelea kusisitiza. John alitikisa kichwa ishara ya kukubali kisha akaifuata rimoti na kuitazama luninga kuubwa bapa iliyokuwa inamtazama kisha akaminya kitufe ikawaka, hakujishughuisha kuangalia ni chaneli ipi iliyokuwa inaupiga mziki wa zook, akajiondokea.
"Michael!!! Una uhakika na unalosema???" aliuliza tena macho yake mekundu yakiwa yanautazama mdomo wa Michael.
Swali hilo likamshtua Michael kwa nini lilikuwa likiulizwa sana, safari hii akachelewa kidogo kujibu
"Siku ile nilimpa namba za msichana mmoja yule afande sijui kama alipiga ama la lakini hakuwahi hata kuja pale mahabusu." alijibu kwa sauti iliyokuwa na hofu
"Nipe namba ya huyo msichana na kuwa makini sana wakati mwingine unapojibu swali sawa!!!" alifoka kidogo John na Michael akakubali bila kuzungumza chochote. Baada ya kumtajia akaondoka, jambo la kushangaza ni kwamba John akuuliza mara mbilimbili na wala hakuandika hiyo namba mahali popote pale, ni kama alikuwa ameipuuzia hata Michael aliamini hivyo.
Siku hiyo ilipita huku Michael akipewa nguo za kubadilisha ambazo zilimkaa sawa kwenye mwili wake, japokuwa alikuwa na mawazo sana hakusita kukiri kwamba aliifurahia hali ya kuwa huru.


****


Majibu ya askari aliyekuwa na wasiwasi mkubwa machoni mwake yalimkera na kumshangaza sana Joyce Keto, alishindwa kuelewa kwamba ni kweli aliyezungumza naye kwenye simu alikuwa ni askari ama ni mtu alimletea utani. Kwa ghadhabu aliondoka kituoni pale.
Kwa nini nisimpigie simu huyo aliyejifanya askari!!! Alijiuliza Joyce huku akitembea kwa ghadhabu hakuwa na uhakika kama alikuwa akiyumba yumba ama la alichotambua ni kuwa alikuwa akisonga mbele. Moja kwa moja katika duka lililokuwa linauza vocha.
"Nisaidie Tigo ya mia tano!!" alisema Joy na mwenye duka akampatia baada ya kuwa ameisugua. Bila ya kujua ni mara ngapi alikuwa ameingiza ile vocha bila kuwa na umakini aishtushwa na ujumbe uliomtaarifu kuwa namba yake ya simu ilikuwa imefungiwa kutokana na kuingiza namba zisizokuwa sahihi, Joy alitamani kulia, aliitazama simu yake kwa jicho la hasira kama ni yenyewe ilikuwa imefanya makosa hayo ili kumkomesha. Kwa mwendo wa kukata tamaa akaanza kuondoka lakini akasita tena na kurejea dukani.
"Makao makuu ya tigo ni wapi, samahani lakini!!!"
"Bila samahani malkia!!...." alizungumza kwa lafudhi ya kichaga na kisha akamuelekeza Joy wapi ambapo kampuni hiyo ya simu imeweka makao yake.
"Asante sana….kwaheeri!!!" aliaga.
Mwanzoni wazo lake lilikuwa kuondoka moja kwa moja na kuelekea hapo alipoelekezwa lakini njaa ilimkatisha kufanya hivyo, jicho lake liliangaza huku na huko kisha akajifikiria kwa muda pesa aliyokuwa nayo ilimruhusu kula wapi jibu likapatikana kuwa alitakiwa kula chakula cha bei poa sana ili mambo yaende sawia. Mama Fredi mgahawa jipatie chakula safi hapa.
Maandishi hayo yaliyoandikwa kwa mkaa yalimfanya Joyce atabasamu kisha akajiambia "Mahali sahihi pa Joyce kupata chakula chake kwa siku ya leo." akanyata na kuingia kwa mtindo wa kuinama hadi akapata nafasi yake. Bila hata kutaja ni chakula gani alikuwa anahitaji alishangaa mbele yake ukiwekwa wali uliochanganywa na maharage, nyama moja, mchicha na kipande kidogo cha bilinganya, hakutaka kuhoji aliamini huo ndio utaratibu wa mgahawa wa mama huyo aliyekuwa muongeaji sana. Huenda hata ndio sababu ya kuvuta wateja wengi sana katika genge lake.
Baada ya kujiridhisha nafsi yake na chakula hicho kilichomgharimu shilingi elfu moja Joyce Keto alinawa mikono yake na kuondoka.
"Ngoja niandae mahali pa kulala kwanza maana dalili zote zinaonyesha kuwa nitalala Mwanza, na huu ugeni nisije nikapata tabu baadaye." alijishauri na kukubali ushauri huo akaanza kuhangaika huku na huko hadi alipopata nyumba ya kulala wageni iliyomgharimu shilingi elfu kumi ikiwa na choo na bafu ndani.
Hakudumu sana katika chumba hicho baada ya kukizoea kwa dakika kadhaa wazo la kurejea tena Tigo lilimrudia, lakini kabla ya yote alijiweka maliwatoni na kuupasha mwili wake kwa maji baridi nguvu zikamrejea na uchangamfu ukachukua nafasi yake. Kosa dogo alilofanya Joyce liligeuka kuwa kubwa, ni baada ya kujiegesha kitandani na usingizi kumpitia. Alikuja kushtuka jioni ya saa kumi na moja.
Tayari huduma alizotaraji kuzipata tigo hazikuwezekana palikuwa pamefungwa tayari.
"Hee!! Saa kumi na moja." alipayuka kwa nguvu akiwa pale kitandani lakini hakuwepo wa kumjibu hoja yake iliyokuja kwa mtindo wa kushtukiza. Alisimama kama anayetaka kuondoka ili awahi kitu lakini alirejea kivivu pale kitandani hakuwa na pa kwenda. Alijilaza pale alipotoka na kumkaribisha tena jinamizi wa usingizi lakini kabla hajachukua kiti na kuketi simu yake ya mkononi iliita. Ilikuwa namba mpya!! Mh!! Atakuwa mama yake Michael ama…sasa kwa nini atumie namba mpya…au!!!" alijiuliza bila kupata majibu, simu ikakatika!! Mara ikaanza kuita tena
"Hallo!! Mambo vipi dada Joy" upande wa pili ulianza kubwabwaja
"Poa nani mwenzangu samahani nilipoteza…."
Mimi Fredrick, haunifahamu lakini" ilimkatisha sauti ile baada ya kueelewa kuwa alitaka kujitetea kwa kudanganya.
"Wa wapi wewe??"
"Mwanza nimepewa namba yako na Michael yupo matatizoni, umeenda kumwangalia polisi???" iliuliza sauti ile kwa utulivu
"Nimeenda lakini sijamkuta…."
"Wamekwambiaje kwani??"
"Wamesema tu hayupo mi nikaondoka zangu"
"Dah!! Hata sisi wametwambia hivyo..wewe upo wapi sasa maana sisi wenyewe wageni hapa Mwanza"
"Mimi pia mgeni lakini nipo hapa Mitimirefu sehemu inaitwa Resting house, ukishuka tu hapa kituoni unapaona nadhani panafahamika" alijieleza Joy huku akiwa na furaha ya kupata wenzake katika vita moja. Alitambua kuwa ni kaka zake na Michael.
"Haya kama tukiweza tutafika, kwa lolote lile tufahamishane sawa!"
"Msijali nitapenda sana mkifika" alisisitiza Joy. Simu ikakatwa.
Baada ya saa zima akiwa anafanya tafakari mbili tatu alishtushwa na mlango wa chumba chake kugongwa kwa utaratibu maalum.
"Nani tena muda huu!!!" alijiuliza huku akiuendea mlango na kuufungua.
"Una vitu vingine zaidi ya huo mkoba mezani??" lilikuwa swali kutoka kwa sura hizi mbili ngeni kabisa machoni mwa Joy.
"Nyie ni akina nani??" aliuliza lakini hakujibiwa.
"Tuondoke haraka eneo hili" aliambiwa
"Twende wapi…nyie ni akina nani???"
"Ndugu zake Michael, chukua vyako tuondoke". Joyce akatii amri na kukusanya vilivyo vyake na kuanza kuondoka hadi kwenye gari ndogo aina ya corolla safari ya kuelekea asipopajua ikaanza.
"Shem ujue nini yaani hii hali inashangaza sana mh!! Kumbe kweli anayekwenda jela si lazima awe na hatia…" baada ya kimya alikuwa ni John ambaye alikwa anajulikana kwa jina la Fredrick aliyeuvunja ukimya pale ndani. Mh!! Nimekuwa shem tayari!! Alijiuliza Joyce na kumalizia kwa tabasamu la kulazimisha bila kusema lolote.
Baada ya mwendo kidogo John alitoa pipi na kuwagawia wote waliokuwa pale ndani, ni Joyce pekee aliyekurupuka na kuibugia pipi ile, baada ya sekunde kadhaa usingizi mkali ulianza kuyafumba macho yake alijaribu kupambana bila mafanikio kuidhibiti hali ile, dhahiri alionekana kutambua janja hiyo iliyokuwa imechezwa dhidi yake lakini haukuwepo ujanja wowote ule Joyce akapitiwa na jinamizi la usingizi mkali sana.
Alikuwa amewekewa dawa za usingizi katika pipi!!!.
Alikuja kushtuka masaa manne baadaye na kujikuta katika chumba kikubwa cha haja ambacho kilikuwa na hewa safi sana yenye ubaridi bila shaka palikuwa na kiyoyozi.
Joyce alijinyoosha nyoosha huku akiyapikicha macho yake ili kujiweka sawa. Hapa ni wapi?? Alijiuliza, lakini kabla ya kupata jibu alisikia mlango ukifunguliwa kisha akaingia John ambaye alijitambulisha kwa Joy kama Fredrick.
"Mambo vipi Joy naitwa John….jisikie huru upo nyumbani" John alijitambulisha kwa Joy ambaye bado alikuwa anashangaa.
"Nimefikaje hapa….hapa ni wapi??" aliuliza Joyce, John ambaye alikuwa amevaa pensi pamoja na fulana kubwa iliouzidi mwili wake huku miguuni mwake akiwa na raba nyeupe.
"Hapa ndio nyumbani kwetu karibu sana" alisema John huku akiachia tabasamu hafifu.


*****


Michael Msombe alikuwa ametekwa na sinema aliyokuwa anaangalia katika luninga kubwa iliyokuwa sebuleni, hakupatwa na ukiwa wowote kwa kuondoka John na Bruno. Mdadi ulikuwa umemshika pale jambazi kuu lilipokuwa likipigwa na nyota wa filamu hiyo ambaye alikuwa ni Jackie Chan, Michael alikuwa ni kama amezama na kuwa mmoja wa wahusika wa filamu hiyo hadi pale aliposhtuliwa na kikohozi cha kujilazimisha kutoka katika upande wa mlango wa kuingilia.
Macho yake yalihama kutoka katika luninga na kuelekea pale mlangoni.


Alikuwa ni msichana ambaye hakuna mwanaume ambaye angesita kumuita mrembo, nguo fupi aliyokuwa amevaa iliyaruhusu mapaja yake meupe kuchungulia nje, wepesi wa kitambaa cha nguo hiyo ulionyesha mchoro wa chupi aliyokuwa amevaa ikiwa katika mfumo wa bikini, kinguo cha juu saizi ya mtoto wa miaka minne kilihalalisha nusu ya tumbo lake kuwa nje. Matiti yake kifuani yalikuwa na uwezo wa kukinyanyua kinguo hicho kwa umbali mdogo sana huku ule mchomo wa mbele ukionekana kumaanisha kamwe hajawahi kunyonyesha.
Sauti ya Michael ilipotea kabisa akajaribu kuilazimisha irejee ili aweze kumsalimia huyu kiumbe lakini iligoma kabisa. Akagundua kuwa alikuwa ameingiwa na tamaa.
"Mambo!!!!" alisalimiwa Michael kwa sauti laini sana iliyopenya katika masikio yake kisha katika koo na kuilainisha sauti yake hatimaye akajibu
"Safiii….karibu!!!" yule binti akaanza kusogea mahali alipokuwa ameketi Michael akimaanisha ameitikia wito, sehemu zake za nyuma zilikuwa zinatikisika kila hatua aliyopiga. Bila kutambua Michael akajikuta ameingia katika hisia nyingine na maungo yake kujikuta yakiinyanyua suruali yake, kwa haraka sana alichukua kitambaa kilichokuwa mezani na kujifunika lakini alikuwa amechelewa sana. Tabasamu zito kutoka kwa yule binti lilimpumbaza akabaki kama zoba.
"Naitwa Matha….unanifahamu sijui???...lakini haunifahamu"
"Yeah!! Sikufahamu nadhani"
"Ni mchumba wa John..unamjua??"
"Ndio John namjua!!!"
"Wewe unaitwa Michael eeh!!!"
"Umenijuaje kwani???" badala ya kujibu Michael aliuliza huku macho yake yakiendelea kumchunguza kwa chati binti huyu.
Matha Mwakipesile alikuwa amepewa jukumu kubwa la kumfundisha Michael jinsi ya kutumia silaha mbalimbali, John alikuwa ameamua kumchukua rasmi Michael katika shughuli zake za ujambazi.
Matha alimueleza Michael kwa utaratibu kabisa jukumu alilopewa, hali ya Michael iligeuka kuwa ya uoga sana hakuamini kuwa binti mrembo kama Matha anaweza hata kuwa na uwezo wa kushika bunduki sembuse kisu na kuua mtu. Mh!!! Usione ukadhani. Alisema kimya kimya Michael.
Somo alilopewa na Matha halikuwa limemuingia hata kidogo, aliamini sasa alikuwa anapelekwa njia asiyoitaka hata kidogo. Kutoroka!!! Ndio wazo kuu lililomjia lakini atatoroka na kuelekea wapi. Akiwa bado katika mawazo hayo mara aliingia Bruno alikuwa mwingi wa furaha iliyojionyesha waziwazi, alimsabahi Michael kisha akaingia chumbani na kurejea tena baada ya muda mfupi akiwa amebadilisha nguo zake.
"Bruno nahitaji sana kwenda nyumbani, nimekaa hapa imetosha nadhani mama atakuwa akinitafuta sana." Michael alimwambia Bruno baada ya kuwa amekaa kitako.
"John anakuja muda si mrefu utamweleza nadhani itakuwa vyema zaidi mi sijui lolote kuhusu wewe na John" alijibu kwa sauti iliyokuwa na uulizi ndani yake, Michael akatambua kuwa Bruno ameshtuka.


Baada ya masaa kadhaa John alifika na baada ya kuzungumza pembeni na Bruno alimfuata Michael.
"Nimeambiwa ombi lako si baya sana, lakini kabla sijakuruhusu naomba nikukumbushe kitu, unakabiliwa na kesi ya kumuua askari pale kituoni, una kesi kubwa ya kutoroka mahabusu hivyo umehalalisha kuwa ni wewe uliyemuua binti uliyekuwa naye nyumba ya kulala wageni, hizo ni kesi chache za halali zinazokukabili sijui kama zipo za ubakaji na wizi kwa kutumia silaha…kwa ufupi unarudi mtaani kupambana na hukumu ya kunyongwa baada ya fedheha ya kufanywa mke wa mtu gerezani….kama unaamini unaweza kupambana na haya yote peke yako mimi nitakusaidia nauli kesho uende mdogo wangu hata usijali." alieleza John huku macho yake yakiwa yameutazama uso wa Michael aliyekuwa anaukwepesha uso wake kila anapogundua kuwa John anamwangalia.
Baada ya kumaliza kuzungumza hayo John aliyanyuka na kuondoka zake akimwacha Michael akiwa ameduwaa. Neno alilokuwa akilirudia mara kwa mara John kuhusu kuolewa na wanaume wenzake ni hilo lilimsumbua akili Michael hakuwa tayari hata kidogo kwa hiyo fedheha. Macho yalikuwa yamemtoka pima, aliingiwa na hofu ya kutoroka kwa mara ya kwanza!!.
"John!!! Kaka John." aliita Michael kwa nguvu wakati John akikaribia kutokomea.
"Sema dogo!!!"
"Naomba basi walau niwasiliane na mama najua ananitafuta sana mh!!."
"Polisi sio wajinga kama unavyodhani…wewe unamuwazia mtu ambaye kwa sasa anawasaidia upelelezi wa kujua wewe ulipo??? Wewe kumuona mama yako haina tofauti na kuonana na polisi" alijibu John Mapulu kisha akacheka. Neno hilo nalo likamshtua Michael na kuamini kuwa lilikuwa na ukweli ndani yake na mama yake huenda anaweza kumsaliti.
"Kwa hiyo hata Joyce Keto anaweza kuwa anasaidiana na polisi?." alijikuta akiuliza.
"Tena kwa ukaribu sana…nakutakia safari njema Michael" alifungua mlango na kuingia ndani.


Kesho yake Michael hakuondoka!!!!!


****


Moshi wa bangi na sigara vilianza kuizoea damu yake, sumu ya maneno aliyokuwa akilishwa na John Mapulu sasa ilikuwa imesambaa ndani ya damu yake, aliwaona watu wote wanaomzunguka kuwa ni maadui hasa hasa askari.
John alimwelezea Michael jinsi polisi wanavyoua raia wema hovyohovyo, alimpa mikasa mbalimbali ya kutisha hivyo kuikoleza hoja yake kuelekea kwenye ukweli. Taratibu Michael akaanza na sigara hatimaye akajiunga katika mkumbo wa wavuta bangi, kwa jitihada zote aliyapinga matumizi ya unga hilo pekee ndilo alilipigania hadi mwisho.


Mwanzoni alikuwa msindikizaji katika shughuli walizokuwa wakienda kufanya akina John sehemu mbalimbali katika jiji la Mwanza kila baada ya shughuli alipewa nafasi ya kuuliza maswali mawili matatu. Kwa kuwa Michael alikuwa mwingi wa maswali hii ilimuwezesha kuelewa mambo mengi sana katika kipindi kifupi mno.


Tayari alijua mbinu za kuvunja maduka, kuiba magari, na mbaya na kubwa somo la matumizi ya silaha lilikuwa limemkolea.
John Mapulu hakuwa mtu wa masihala linapokuja suala linalomuhusu moja kwa moja, jambo hili hata Michael alilitambua upesi sana kadri alivyokuwa akiishi naye karibu. Mahusiano yaliyokuwepo kati yake na Matha (mpenzi wa John) katika kufundishwa jinsi ya kutumia bunduki yalikuwa yameanza kuvuka kiwango, nafsi ya Michael baada ya kumtamani Joyce Keto bila mafanikio ya kumpata, Joyce mwingine aliyefariki bila kuwa ameelewa azma ya Michael, sasa Michael alikuwa anamtamani Matha japo pia alikuwa hajamwambia, kila siku alikuwa akijizuia na kuuonya mdomo wake usije ukamponza.
Aliamini kwa kumtamkia Matha kuwa anampenda ni sawa na kuanzisha vita na John Mapulu, vita kubwa ambayo wala hakuwa na ubavu wa kuicheza. Wakati fulani Michael aliamini Matha amewekwa karibu yake ili kumchunguza tabia zake hivyo alikuwa makini sana asiweze kuzionyesha hisia zake kwa mrembo huyu.


Matha hakuisha kumvalia nguo za mitego Michael kila wanapokuwa wawili katika chumba maalumu cha mafundisho hayo.
Siku hii jioni tulivu kabisa John na wenzake wakiwa wameingia katika tukio la kuiba pesa benki ambapo hawakutaka kuandamana na Michael kwa sababu ya uchanga wake katika masuala ya uharifu pia hawakuwa na mtaalamu wao wa kike Matha Mwakipesile aliyedai kwamba akili yake haikuwa barabara siku hiyo. Michael kama kawaida akiwa katika burudani yake ya kuangalia filamu, mwilini akiwa na pensi fupi na fulana iliyokatwa mikono alishtuliwa ghafla na ujio wa Matha pale ndani.
"He!! Mwalimu vipi….pole aisee nasikia unaumwa??." Michael alimuanza Matha ambaye kwa sasa walikuwa wamezoeana sana.
"Mh!! Kakwambia nani??"
"Ah!! Nimesikia tu!!!" alijibu huku akisimamisha hiyo filamu kupisha maongezi yake na Matha.
"Ok!! Twende darasani" Matha alimwomba Michael naye akafuata bila ubishi, darasa alilokuwa akipewa na Matha lilimvutia kuipenda bunduki. Walipofika chumba hicho maalumu somo lilianza kama kawaida lakini hawakuchukua muda mrefu Matha akabadili hali ya hewa ya hapo ndani, ni wakati akimfundisha Michael jinsi ya kulenga shabaha akiwa kwa nyuma yake mkono wake wa kushoto ukiwa umekizunguka kiuno cha Michael, zoezi lilisimama ghafla baada ya wawili hawa kujikuta hawaitazami bunduki ila wanatazamana machoni wakiwa wametwaliwa na dalili zote za mahaba mazito.


Mapigo ya moyo ya kila mmoja yalikuwa juu sana, taratibu bunduki ikatuliwa chini, Matha kwa kuutambua uoga wa Michael yeye mwenyewe akajitoa muhanga kusogeza papi (lips) za mdomo wake hadi zikagusana na za Michael, akaupenyeza ulimi wake katikati ya papi za Michael na yeye akaupokea taratibu. Michael alikuwa anatetemeka sana lakini baada ya ndimi zao kukutana akauvaa ujasiri, hapakuwa na godoro pale ndani hivyo wakajikuta katika sakafu iliyokuwa na vigaye, kivazi alichovaa Matha ni kama alimaanisha kitu kwani baada ya kuanguka chini alikigusa nacho mara moja mikanda ikaachia wawili hawa wakawa katika ulimwengu wa mahaba mazito.


***MICHAEL ameangukia katika penzi la MATHA ambaye ana mahusiano na mtu hatari zaidi JOHN MAPULU. Nini hatma ya mchezo huu wa hatari.


***JOYCE KETO naye mikononi mwa JOHN MAPULU…je naye ataishia wapi.


Mr Rocky Wazo Langu nifah
dyuteromaikota
 
  • Thanks
Reactions: ram
RIWAYA: HATIA.
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA SITA

Mapigo ya moyo ya kila mmoja yalikuwa juu sana, taratibu bunduki ikatuliwa chini, Matha kwa kuutambua uoga wa Michael yeye mwenyewe akajitoa muhanga kusogeza papi (lips) za mdomo wake hadi zikagusana na za Michael, akaupenyeza ulimi wake katikati ya papi za Michael na yeye akaupokea taratibu. Michael alikuwa anatetemeka sana lakini baada ya ndimi zao kukutana akauvaa ujasiri, hapakuwa na godoro pale ndani hivyo wakajikuta katika sakafu iliyokuwa na vigaye, kivazi alichovaa Matha ni kama alimaanisha kitu kwani baada ya kuanguka chini alikigusa nacho mara moja mikanda ikaachia wawili hawa wakawa katika ulimwengu wa mahaba mazito.

Matha yule ambaye ana uwezo wa kuua binadamu dakika yoyote ile katika mapambano sasa alikuwa amelala chali mshindi akiwa ni Michael katika kifua chake. Raha walizozipata waliweza kuzielezea wao peke yao maana hapakuwa na shahidi pale ndani zaidi ya mtutu wa bunduki. Hiyo ilikuwa ndiyo siku ambayo Michael kamwe hataisahau kwani ile hali ya kujiamni mbele ya John alihisi inapungua huku akihofia siri hiyo iwapo itavuja ni jinsi gani John atakisambaratisha kichwa chake.
Kwa upande wa Matha hakuonyesha mabadiliko yoyote, hakuwa na uoga hata chembe, na siku iliyofuata alifika hapo nyumbani kwa ajili ya kumfundisha Michael. Darasa likageuka ukumbi wa ngono, Michael alipewa onyo kali.
"Ukikataa tusiendelee kufanya nitamwambia John kuwa unanisumbua kimapenzi, usidhani kuwa atakuhoji kama ni kweli ama la…atakachofanya atachukua bunduki kama hivi na kukufyatua kichwa chako, kama akiwa na huruma sana atakuwekea sumu ufe usingizini….vipi upo tayari kufa??" Matha alimwambia Michael kwa sauti iliyojaa majivuno. Michael hakuwa tayari kufa hivyo akaingia rasmi katika utumwa wa ngono na mpenzi wa muuaji hatari, tena katika nyumba ya muuaji. Raha alizokuwa akizipata wakati wakipashana miili yao joto ilikuwa inayeyuka kila alipokuwa akimfikiria John siku akiugundua huo mchezo mchafu unaoendelea.

****

"John leo nitampeleka huyu dogo kwa mafunzo ya shabaha kule pori!!! Usiku" Matha alimweleza John Mapulu ikiwa majira ya asubuhi baada ya kuwasili pale nyumbani kwa John.
"Vipi lakini uelewa wake anaweza kuingia mzigoni?" Badala ya kujibu naye aliuliza
"Kiaina lakini si wa kuingia mzigoni kwa sasa. Ni moto wa kuotea mbali akishaiva vizuri" Matha alimsifia Michael. Wakati huo na Michael naye alikuwepo pale sebuleni, hakutaka kumwangalia John wala Matha. John alianza kudhani Michael ameogopa sana kusikia habari za porini usiku, wakati Matha alijua kwa nini Michael hakutaka kuwatazama usoni.
Msichana gani huyu hana hata chembe ya aibu!!! Aliwaza Michael.
"Kwa hiyo twende wote ama utaenda na Bruno!!!" aliuliza John
"Mwenyewe ninatosha hata usijali hatutachukua wakati sana, isitoshe Michael si mkorofi" alipanga maneno yake Matha kama karata na yakakubaliwa bila chembe ya wasiwasi na John.
Wakaondoka


*****


Pori kubwa na zito ambalo Michael aliyepelekwa huku akiwa amefunikwa kitambaa usoni, hakulitambua hata kama asingekuwa na kitambaa usoni kwani alikuwa mgeni Mwanza. Walifika porini Michael akiwa na wazo moja tu la kutoroka kabla mambo hayajawa mabaya kwa upande wake, azma ya kuchangia mwili mmoja na mtu mkatili kama John ilikuwa inamtafuna kwa fujo, mwili wake ulioanza kunawiri kutokana na mlo safi na kamili aliokuwa anaupata pale kwa John sasa ulikuwa unaanza kufifia tena.

Matha yeye ni kama raha hizo zilimkubali kwani alizidi kunawiri na kuongeza mvuto wake. Matha alisimamisha gari ndogo aina ya Cresta Michael akashuka na yeye akashuka, hakuwa na wasiwasi wowote juu ya Michael kwani alijiamini kupita maelezo katika suala la kujihami kwa kutumia viungo vya mwili mafunzo aliyoyapata kabla ya kuliasi jeshi la polisi miaka kadhaa nyuma. Nia ya Michael ilikuwa kutoroka lakini hakuona hata njia moja ya kuweza kumtoa pale katika lile pori.
Nitazua mengine hapa!! Aliwaza na kusubiri kuona kilichokuwa kinataka kuendelea.
"Michael!!!" Matha alimwita na kumtoa katika ndoto zake zisizo na mafanikio.
"Naam mama!!!" aliitika kwa nidhamu.
"Njoo huku mara moja!!!" Michael alitii amri, akamfuata Matha alipokuwa anaelekea, fikra zake ni kwamba alikuwa akienda kufundishwa huko kulenga shabaha. Alipokaribia aliamriwa kurudi kinyumenyume hivyo navyo akatii.
"Simama!!" Matha aliamrisha, Michael akatii. Matha akamsogelea Michael na kumtia kitambaa usoni.
"Vipi tena mama??."
"Ndio masharti ya kujifunza shabaha" Matha alitoa sauti ya amri lakini isiyokuwa na kujiamini ndani yake. Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa kisha Michael bila kuwa amejiandaa alichotwa mtama na kujikuta yu katika fundo la majani lililokuwa katika mfumo wa kitanda, kisha akafunguliwa kitambaa usoni, kabla hajasema lolote ulimi wa matha ulipenya katikati ya papi za mdomo wake, ule ubaridi wa ulimi wa Matha ukaubembeleza uoga wa Michael hadi ukasinzia na ujasiri ukaamka. Matha alikuwa kama alivyozaliwa na baada ya dakika mbili Michael naye alikuwa hivyo hivyo. Hii siku ilikuwa ya kipekee kwao kwani walikaa porini masaa mengi sana huku bunduki zikiwa pembeni kama nguo zilivyosahaulika na miili yao ikiwa imenatana.
"Michael nataka uwe mpenzi wangu!!"
"Unasemaje Matha??" aliuliza kama vile hajalisikia swali. Matha hakusema tena aliamini Michael amesikia.
"Hivi unataka niuwawe ndio ufurahie???" Michael alisema kwa sauti iliyojaa hamaki.
"Hautakufa…akuue nani???"
"Matha unauliza aniue nani???...wewe umesema John anaua au sikukusikia??" alihoji Michael kwa ghadhabu, tayari alikuwa amejinasua kutoka mikononi mwa Matha.
"Kama nisipokulinda utauwawa, laini nitakulinda" alijitetea Matha kwa sauti iliyojaa uhitaji wa mahaba.
"Matha ujue unahatarisha maisha yangu, kwanini tusiuache mchezo huu, John hakupi nini kwani??" alilalamika Michael. Matha hakusema neno akaanza kulia, mwanga wa mbalamwezi ulimruhusu Michael kuishuhuda simanzi hii, hakuamini kama maneno yake ndo yamemkasirisha mrembo huyu, kosa kubwa!!! Alipojaribu kumbembeleza huku akisahau kuwa yu uchi alijikuta tena katika mahaba mazito ambayo baada ya hapo yalizaa tabia ya mara kwa mara kudanganya kuwa wanakuja kwa ajili ya mafunzo na kisha kuubadili uwanja wa mafunzo kuwa uwanja wa mahaba. Chumba cha nyumbani waliona hakiwatoshi!!
Nachezea sharubu za simba!!!! Aliwaza Michael.
Lakini angejitoa vipi katika msala huu!!

******

Matha alikurupuka kutoka kitandani alipokuwa amelala na John, mbio mbio alikimbia kuelekea bafuni kuna jambo lilikuwa limemtatiza, lilikuwa jambo geni sana kwake. Alikuwa ana kichefuchefu cha ghafla, hakuwa anaumwa hapo kabla wala hakuwa amekula kitu kibaya usiku uliopita. Alifika na kutapika bafuni, kichefuchefu kikapungua hakutaka tena kurudi kitandani alioga kabisa na kuingia katika chumba kidogo cha mazoezi. Kichefuchefu kikamrudia tena safari hii hakutapika baada ya kukikabili kwa kulamba limao alilolitoa katika jokofu.
Kichefuchefu kikamkimbiza hospitali siku hiyo!!
"Matha Mwakipesile ndo wewe eeh!!!."
"Ndio ni mimi dokta vipi malaria nini??." alifanya utabiri usiokuwa sahihi.
"Hapana hauna Malaria mwanangu.."
"Mh!! Nini sasa hiki Mungu wangu."
"U mjamzito Matha!!!....mwezi mmoja."
"Dokta!!! Be serious!!!"
"Ninamaanisha, vipi kwani hukutegemea au??."
"Yaani siamini maana ni wakati muafaka hii zawadi imekuja." alijibu kwa uchangamfu Matha. Akaaga akaondoka!!!
Alimanusra apate ajali njiani kwa papara alizokuwa nazo katika kuendesha gari kwa mwendo kasi ili awahi mahali. Hakuwa akienda kwa John lakini alikuwa akielekea kwa Michael aliamini kwa namna kubwa sana yeye ndiye muhusika wa hiyo mimba maana hawakuwahi kutumia kinga hata siku moja. Sijui walikuwa wakijiamini vipi!!!!
Matha alikuwa na furaha tele kwani ni mwaka wa nne tangu awe na uhusiano na John Mapulu bila dalili zozote za kupata mtoto. Tangu amtoe usichana wake walipokutana katika msiba wa mama yake mzazi na Matha, uhusiano uliokomaa na kudumu kwa miaka hiyo tele, miaka iliyomhamisha Matha kutoka shuleni na kuingia rasmi katika ujambazi. Akiwa kama kipenzi cha John hakumjua mwanaume mwingine hadi anapoingia kati Michael Msombe.
"Kumbe John hazai!!!" alisema kwa sauti ya chini kama vile kuna mtu pembeni yake alikuwa anamsikiliza.
"Mbona sasa amekuwa mbinafsi kiasi hicho??? Kwa nini hakunambia kuwa ana matatizo, nimejihisi mpweke na kumlaani mama yangu kwa kunizaa mgumba!!! Namchukia John. Kama alinipenda kwa nini ameificha siri hii??" alilalama Matha bila kupata msaada wowote. Breki za gari yake zikafanya kazi yake alipolikaribia geti kisha injini ikazimwa baada ya gari kuwa limeingia maeneo ya Mecco ndani ya nyumba ya John aliyoishi na Bruno!!! John hakuwepo!!! Lakini Michael alikuwepo.
"Michael!!!!."
"Nambie mpenzi wangu." Kwa mara ya kwanza Michael akamwita Matha jina hilo kwa kujiamini. Matha akambusu shingoni kimahaba, wakati huo walikuwa katika chumba chao cha mafunzo ya kutumia bunduki.
"Michael asante sana!!!!."
"Asante kwa lipi huishiwi visa wewe mke wa bosi!!"
"Ah!! Sitaki mie hilo jina utaniudhi sasa hivi!!!" alilalamika kwa sauti ya chini Matha.
"Basi samahani kipetito" Michael alimwambia Matha huku akichukua kichwa chake na kukilaza mapajani mwa Matha.
"Michael nina ujauzito." kama vile aliyepigwa shoti alijikuta akiruka kutoka mapajani mwa Matha na kusimama mlangoni kama anayetaka kukimbia. Matha akaubetua mdomo wake.
"Matha unasemaaje??."
"Kwani ulikuwa unatumia kinga wakati tunafanya??." Swali la Matha likamfadhaisha Michael akawa kama anayetaka kulia lakini chozi lilikuwa mbali sana, sura yake ikawa kama amepigwa ngumi.
"Michael nimekwambia nina mimba yako!!!"
"Sasa Matha hapo mimi nafanyaje unadhani??" alizungumza kwa upole Michael.
"Nakusikiliza wewe!!!."
"Una uhakika kuwa ni ya kwangu???."
"Asilimia zote!!!! John hana uwezo wa kuzalisha" alijibu Matha kwa ujasiri
"Fikiria kwa makini halafu utaniambia tunafanya nini???" alisema Matha kisha akambusu Michael katika papi za mdomo na kumwacha solemba. Mara akarejea na kumkuta Michael akiwa bado amesimama
"Katika mawazo yako yote sahau kuhusu kufanya arbotion, I won't!!!"

*****

Suala la Matha kumkumbusha Michael kuwa sahau kuhusu kitu kinaitwa utoaji mimba lilimchanganya zaidi Michael. Kila alipofikiria kuhusu tatizo la John la kutokuwa na uwezo wa kuzaa Michael alizidi kuchanganyikiwa kwani aliamini kuwa endapo John ataigundua mimba aliyonayo mpenzi wake (Matha) basi mshukiwa wa kwanza kabisa ni yeye (Michael) hilo halikuwa na kipingamizi chochote.
"Na ikiwa hivyo basi nimekwisha mie!!!" Michael alisema kwa sauti ya chini huku kijasho kikipenya katika vinyweleo vya mwili wake kutokea kichwani na kuweka michirizi katika mashavu yake.
Michael hakutafakari na kupata jawabu lolote la maana akaingia chumbani kwake akajiegesha kitandani. Akapitiwa na usingizi!!!
Majira ya saa mbili usiku ndipo alishtuka, mang'amung'amu ya usingizi yalikuwa yakimyumbisha alikuwa akiyapikicha macho yake ili aweze kuona mbele vizuri wakati huo alikuwa anauendea mlango wa chumba chake aweze kuufungua na kutoka nje kiu kilikuwa kimemshika. Alipoufungua mlango ni kama alikuwa amemfungulia mtu ambaye bado alikuwa hajaomba kufunguliwa, Michael alikurupuka kama aliyekuwa amekabwa na jinamizi kisha ghafla akawa ameachiwa. Alikuwa ni John!!
"Vipi dogo…." John aliuliza
"Ahh!! Ni usingizi tu kaka vipi…aah!! Nilikuwa nimelala si unajua" alijibu pasipo kujiamini kijana huyu.
"Jiandae tutoke!!!..nakupa kama dakika kumi na tano fanya fasta" John alimuamuru Michael. Wasiwasi ukamuandama Michael, hakujua huo mtoko ulikuwa wa kwenda wapi. John hakuwa katika mavazi ya kikazi, bali alikuwa ameitundika suti yake nyeusi iliyombana kiasi na kuonyesha kifua chake kilivyoachana katikati, kwa ndani alikuwa na shati jeupe, kiatu cheusi chini kilihitimisha kumfananisha John na bwana harusi na wala si jambazi mzoefu. Hivi tutakuwa tunaenda wapi?? Alijiuliza Michael.
Hakuwa na wa kumpa jibu akaghairi kuliendea jokofu ili apate maji akapiga hatua kadhaa bafuni ili aweze kuoga, hata hivyo ubaridi wa maji ulimsababisha ajijengee hoja kwamba alikuwa msafi na kuhalalisha maamuzi ya kuacha kuoga. Badala yake akanawa uso kujitoa ile ladha ya usingizi usoni mwake, kisha akaliendea sanduku lake lililozuia zipu isijifunge kutokana na wingi wa nguo akatwaa jinsi ya bluu na fulana nyeupe akazitua katika mwili wake baada ya kuwa ametanguliza singlendi nyeupe kwa ndani, kisha akamalizia na raba iliyotawaliwa na weusi kiasi kikubwa na weupe ukichukua nafasi ndogo. Miwani aliyoivaa ilikuwa imempendeza sana kwani ilirandana na kiatu lakini usiku haukuwa wakati muafaka wa kuvaa miwani hiyo, baada ya kugundua hilo aliivua na kuirejesha mahali pake. Marashi!! Alikumbuka wakati anataka kutoka, haraka haraka alirejea na kupulizia kwa chati, aliporidhika akatoka na kuelekea sebuleni.
Hakuwa na haja ya kujitazama kwenye kioo, alikuwa amependeza!!
"Umejiandaa fasta sikutegemea maana nimekushtua sana!!!"
"Nimekacha kuoga!!! Ndo maana nimewahi" alijibu Michael huku akikaa katika ncha ya sofa.
"Twende zetu, huyu Bruno sijui atakuwa wapi muda huu??"
"Hata sijui maana tangu nimelala dah!! Wewe wakati unakuja pale ndo na mimi nilikua naamka, masaa kama manne hivi nilikuwa mfu"
"Shwari…tutampigia simu." alijibu John huku akitangulia na Michael aliyetawaliwa na walakini akimfuata kwa nyuma hadi kwenye gari. Michael hakuingia kwanza alifungua geti gari ikatoka kisha akafunga ndipo akalifuata gari na kupanda.
"Aaah!! Tafadhali bwana mdogo yaani mi nimekuwa dereva wako!!!" alizungumza John kimasikhara baada ya Michael kukaa siti ya nyuma, haikuwa mara ya kwanza Michael kumsikia John akisema hivyo, mara moja akahamia siti ya mbele. Kabla hajakaa John aliondosha pakiti ya sigara iliyokuwa imebakiwa na sigara tatu ndani yake, hiyo ilimaanisha kuwa sigara takribani kumi na saba zilikuwa zimezama na kutoka katika mapafu ya John. Alipenda sana sigara bwana John!! Michael bila kuomba alitwaa naye sigara moja akaiwasha na kuanza kupuliza moshi ndani na nje. Na yeye tayari alikuwa ameathirika japo sio sana na utumwa huu wa sigara.
John alikuwa makini na usukani, kutokea pale Mecco alipinda kushoto kuifuata hoteli na bar ya Cheers kisha akakata kulia akiipita stendi ya Mecco na kuifuata barabara iendayo Nyakato sokoni, hapakuwa na masumbufu ya foleni za hapa na pale hivyo waliwahi sana kufika, baada ya kufika Nyakato sokoni gari ilikata kushoto baada ya kuwa imeingia barabara kuu ya Mwanza maarufu kama Nyerere road, gari liliondoka kwa mwendo mkali lakini salama kuelekea Igoma, NDAMA HOTELS ndipo kilikuwa kituo cha mwisho ambacho John alisimamisha gari lao dogo aina ya corolla. Wakati huo Michael alikuwa anamalizia kipisi kidogo cha sigara ya mwisho wakati wanashuka garini. John hakuwa katika hali ya uchangamfu hali hii ilizidi kumtia mashaka Michael.
"Vipi ina maana amegundua kinachoendelea ama kuna jambo gani linaendelea hapa??" alijiuliza Michael wakati huo John alikuwa akiangaza ni wapi wanaweza kukaa kwa utulivu. Walipata mahali palipokuwa na utulivu walioutaka wakaketi.
"Karibuni!! Karibuni sana" sauti ya muhudumu wa kike aliyetawaliwa na tabasamu bandia usoni maalum kwa ajili ya kazi aliwalaki wawili hawa.
"Asante sana…tutakuita tukikuhitaji!!!" alijibu John bila kumuangalia binti huyu usoni. Binti hakujibu kitu bali tabasamu lake liliyeyuka ghafla akaanza kuondoka.
"Hey!!....Mimi niletee Kilimanjaro, iwe ya moto tafadhali" aliamuru Michael
"Naomba 1800…." Alijibu yule dada ambaye sasa lile tabasamu lililopotea ghafla baada ya kuambiwa ataitwa baadaye sasa lilikuwa limerejea maradufu. Michael hakujibu akamtazama John aliyekuwa ameinama, muhudumu akailewa maana hiyo akamsogelea John bila shaka ni yeye alikuwa na jukumu la kulipia bili.
"Na mimi niletee Castle lite baridi, leta mbili kabisa." John aliagiza huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi yule binti, akaondoka kwa furaha!! Bila shaka walipokea posho kutokana na idadi ya wateja walioweza kuwahudumia kwa siku.
"Michael unamuonaje huyu binti!!!."
"Kivipi yaani."
"Muonekano wake tu!! Ni mrembo eeh!!."
"Kiasi chake, namaanisha yupo katikati!!" alijibu Michael huku akimtazama John na kulazimisha tabasamu ambalo halikujibiwa na John.
"Wasichana wana mambo sana….." kauli hiyo ikamgutua Michael kimawazo.
"Kwanini wasema hivyo…." Aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti chake, viwiko vya mikono yake vikiegemea mezani
"Unajua unaweza kumpenda sana mtu halafu asitambue upendo wako, akatumia upendo huo kukuadhibu……lakini bado unaendelea kumpenda" alianza kujieleza John
"Yeah!! Hiyo inawezekana lakini sijaelewa maana ya kauli yako " aliuliza kwa hofu Michael wakati huu alitoa mikono yake mezani na kuifunga kifuani kwake
"Michael si unajua kuwa wewe ni rafiki yangu sana?"
"Naelewa hilo na ni kaka yangu pia kwani kuna nini??" Michael aliuliza huku akijutia kuuliza vile kwani hakutaka kusikia jibu litakalotoka, hatia iliusaga moyo wake, aliamini kwa maongezi hayo John kuna kitu alikuwa kama hajakigundua basi alikuwa amekihisi kati ya yeye (Michael) na Matha. Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, fulana yake iliyombana ilimwezesha mtu ambaye hata kama si mchunguzi wa masuala ya afya kuligundua hili.

"Shiit!!! Nimeacha mguu wangu ndani ya gari!!!" John alijisonya baada ya kugundua amesahau bunduki yake garini, haukuwa utaratibu wake kutembea bila silaha. Lakini hakujisumbua kusimama na kuifuata. Kauli hiyo ilizidi kumtetemesha Michael.
Ina maana ndio amekuja kunifichulia maovu yangu na kuniua hapahapa!!!! Mungu wangu, lakini nilimwambia Matha kila siku kuwa ananitia matatani ona sasa!!! Aah!! Ona sasa Matha!! Aliwaza Michael kwa uchungu na kuzitupa lawama kwa Matha kabla John hajaendelea kuzungumza
"Eeeh!! Umeuliza kuwa nina maana gani, ujue Michael kuna wakati unafika lazima kila ukweli uwe wazi na uamuzi ufanyike mara moja, na uamuzi mgumu ni ule unaomuumiza aliyeuamua!!!" John aliendelea Michael akawa kimya, alikuwa amekodoa macho funda la mate alilotaka kumeza ni kama lilikuwa linataka kumshinda, koromeo lilionekana kuwa dogo lakini akajilazimisha likapita.
Akayakumbuka maneno ya John Mapulu walipokuwa mahabusu!!!
"Mimi ni mbaya...naua na kusahau mara moja!!"
Mh!! nimeuawawa tayari.



****LAMBALAMBA HUMALIZA BUYU LA ASALI...Michael amemjaza mimba MATHA....mbaya zaidi hataki kuitoa.....itakuwaje?? kwa mara ya kwanza Matha anagundua kuwa John hana uwezo wa kuzaa.
**** JOYCE KETO yupo wapi??
***Na John amempeleka Michael kumueleza jambo gani...JE?? NI SIRI IMEVUJA AMA!!!!



dyuteromaikota Christinah
binti kiziwi magret04 Mr Rocky Wazo Langu nifah
 
Natamani kujua alichoenda kuambiwa, isiwe tu haya majanga aloyasababisha na mrs boss
 
RIWAYA: HATIA
MTUNZI: George Iron Mosenya



SEHEMU YA SABA


"Shiit!!! Nimeacha mguu wangu ndani ya gari!!!" John alijisonya baada ya kugundua amesahau bunduki yake garini, haukuwa utaratibu wake kutembea bila silaha. Lakini hakujisumbua kusimama na kuifuata. Kauli hiyo ilizidi kumtetemesha Michael.
Ina maana ndio amekuja kunifichulia maovu yangu na kuniua hapahapa!!!! Mungu wangu, lakini nilimwambia Matha kila siku kuwa ananitia matatani ona sasa!!! Aah!! Ona sasa Matha!! Aliwaza Michael kwa uchungu na kuzitupa lawama kwa Matha kabla John hajaendelea kuzungumza
"Eeeh!! Umeuliza kuwa nina maana gani, ujue Michael kuna wakati unafika lazima kila ukweli uwe wazi na uamuzi ufanyike mara moja, na uamuzi mgumu ni ule unaomuumiza aliyeuamua!!!" John aliendelea Michael akawa kimya, alikuwa amekodoa macho funda la mate alilotaka kumeza ni kama lilikuwa linataka kumshinda, koromeo lilionekana kuwa dogo lakini akajilazimisha likapita.
"Michael nakupenda sana lakini………" hakuweza kuendelea John muhudumu akawa amefika na vinywaji, akawafungulia , Michael akapiga mafunda mawili kulainisha koo lake, John hakupiga funda lolote bali alitia kiasi fulani kwenye glasi yake, wakati muhudumu huyu anaondoka kupisha faragha ya Michael na John, muhudumu wa kiume kutoka jikoni naye akafika kuwasikiliza.
Paja la mbuzi, weka pilipili, tenganisha sahani, ndizi nne zikaushe vizuri, mwambie huyu aongeze bia. Ni baadhi ya maneno mengi waliyozungumza na hatimaye mada ikawa imesahaulika!!! John hakuendelea na maelezo. Simu aliyopigiwa na Bruno ikawa imeingilia kati.
Michael akapata ahueni!!


*******


Joyce Keto alionekana kuwa kikwazo pekee kwa John Mapulu katika mipango yake ya kujipanga upya katika shughuli zake. Alitambua ni kiasi gani wasichana ni dhaifu. Hivyo kuwa mikononi mwake lilikuwa jambo salama sana.
Iwapo Joyce angetiwa mikononi mwa polisi, lazima angesema lolote analojua kuhusu Michael hali ambayo ingemuweka matatani Michael, kijana ambaye ametokea kushibana naye.
Sasa Joyce alikuwa mikononi mwake katika nyumba ya mafichoni nje kidogo ya mji wa Mwanza. Kama ilivyokuwa kwa Michael. Joyce naye alijazwa chuki na kujihisi yupo hatiani. Hasahasa baada ya kuelezwa kuwa Michael anakabiliwa na kesi ya mauaji.
"Kuonekana kwako tu pale kituoni..unatafutwa sasa ukasaidie upelelezi. Maana Michael alitoroka." John alimwogopesha Joyce. Kisha akamalizia kwa kumueleza juu ya Michael kumkimbia.
"Kwa hiyo mlivyotoroka, amekutoroka na wewe."
John akakubali kwa kutikisa kichwa juu na chini.
Sumu pandikizi ikapenya katika akili ya Joyce. Akawa mtumwa wa kifikra.,
Uhusiano wa kimapenzi ambao Joyce alimueleza John kati yake na Michael haswa ndio ulimfanya John asipendezwe na kitendo cha wawili hao kukutana mapema. Alihofia kusalitiwa. Hivyo alijionya kuwa muangalifu sana.
Akaamua kumuweka Joyce mbali na Michael hadi wakati stahili utakapowadia.






KILICHOJIRI BAADA YA WATUHUMIWA KUTOROKA


Askari wa zamu usiku wa tukio la mauaji na kutoroka mahabusu wa kituo kikuu cha polisi wapatao kumi kwa kulinda maisha yao waliificha siri ya kutoroka kwa mahabusu wanne katika mazingira tatanishi. Pia mauaji ya askari usiku huo huo. Kwa uzembe huo kama wangethubutu kubaki, kifungo cha maisha ilikuwa halali yao kwani watuhumiwa wote wanne waliofanikiwa kutoroka walikuwa wanahusika na mauaji, John akiwa mkongwe anayefahamika kwa kesi hizo, Michael akiwa amesingiziwa lakini ushahidi ukimuhitaji sana kwa upelelezi na wengine wawili wakiwa na kesi ya kuiba na kuua kwa kutumia bunduki.
Kwa watuhumiwa wa kesi nzito kama hizo ni nani angepona kwa kusema kuwa hajui wanne wametoroka toroka vipi??? Bila kushirikishana lakini kila mmoja akijua lake moyoni, wanne kati yao wakaamua kutoroka wawili wakajiua na wanne waliojisalimisha wakaanza kusota rumande na baadaye gerezani Butimba kwa kesi ya kuwasaidia mahabusu kutoroka pia kuhusika katika kuua askari mmoja. Wema waliodhani ni silaha ukawa umewaponza, upelelezi unaendelea ndio kauli pekee iliyosalia wakati wanazidi kuteketea mahabusu. Mmoja baada ya mwingine wakaanza kupoteza maisha kutokana na mateso makali na msongo wa mawazo huku wengine wakigeuzwa wake za watu angali walikuwa mahabusu.
Akabakia askari mmoja huyo alikuja kutoka kwa msamaha wa raisi miezi miwili baadaye baada ya kesi yake kukosa ushahidi wa kutosha, huyu aliweza kuona na kutembea kama aliyekamilika lakini hakuwa na uwezo tena wa kuzaa, mateso aliyopitia tayari yalikuwa yamemvuruga uzazi lakini kubwa zaidi ni kuingiliwa kimwili mara kadhaa na wafungwa wazoefu wakati yupo gerezani akisubiri hukumu yake. Hakurudishwa kazini baada ya msamaha hakuwa na vigezo tena. Uaskari wake ukawa umeishia katika simulizi mbaya na ya kuumiza kama hiyo. Huyu aliyepona aliyebahatika kurejea uraiani alikuwa ni Sajenti Kindo Malugu, hakuwa sajenti tena alibakia kuwa mzee Malugu.
Siku chache kabla ya kukamatwa kwake alipokea taarifa ya mwanae mpendwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, ni baada ya kukumbana na unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa baba yake mdogo aliyekuwa amechukua jukumu la kumlea baada ya mzee Kindo kuhamishwa kikazi kutoka Singida na kuhamishiwa Mwanza.
Baada ya mwanae huyo wa pekee wa kike aliyezungukwa na wenzake wawili wa kiume ambao walikuwa wameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ndio kwanza alikuwa amejitahidi na kumaliza kidato cha sita.
Hakuwa tayari kuolewa bali alitaka kundelea na masomo yake ya chuo kikuu. Mateso, kejeli na dharau kubwa kutoka kwa baba yake mdogo pamoja na mkewe zilikuwa zimemsukuma kutoroka katika mji huo na kwenda mahali alipopajua mwenyewe. Baada ya kupata taarifa hiyo mzee Kindo alinuia kuchukua ruhusa na kurejea nyumbani kushughulikia suala hilo, halikuwa suala dogo hata kidogo ile ilikuwa ni damu yake inatangatanga. Lakini akiwa katika kusubiri ruhusa yake ipitishwe ndipo linatokea tukio la mauaji katika nyumba ya kulala wageni jijini Mwanza.
Hakuwa mmoja kati ya askari walioenda kwenye tukio kwani alikuwa anahangaikia ruhusa lakini alikuwa ni yeye aliyeandika maelezo mafupi ya awali kuhusu mali alizonazo mtuhumiwa kwa wakati ule yaani PPR baada ya Michael kukamatwa. Ruhusa ilizidi kumchelewesha hadi linapotokea tatizo jingine kubwa la kuuwawa kwa askari aliyekuwa lindoni na kutoroka kwa watuhumiwa wanne wa kesi za mauaji, hata siku hii pia alichelewa sana kuingia kazini kwani suala la ruhusa yake lilikuwa bado gumu. Siku hiyo alikuwa zamu, hivyo alikuwa anahusika katika kujibu kitakachoulizwa.
Mwanzoni alikubaliana na wenzake kuhusu kutoroka lakini alipompigia mkewe simu na kumuomba ushauri alipinga vikali na kumsihi asijaribu kutoroka kwani alikuwa na mtihani mwingine wa kumtafuta mwanae je angeuweza vipi huu mtihani wakati asingekuwa huru tena??? Maneno hayo makali yaliyosindikizwa na kilio kisha meseji kadhaa za kumsisitiza asifanye alichokusudia zilibadili mawazo ya Sajenti Kindo, yeye pamoja na askari wengine watatu wakajisalimisha, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuwa huru hadi alipotoka kwa msamaha wa raisi.
"Vua gwanda, vua mkanda, saa na hiyo kofia" haya yalikuwa maneno yaliyowaamrisha siku wanaingia mahabusu, ilikuwa kama utani lakini miaka miwili ikathibitisha si utani ule.
"Mwanangu Joyce, sijui alipatikana???" ni swali la kwanza alilojiuliza mzee huyu, punde tu baada ya kuambiwa yuko huru.
"Poti!! Poti!!...." Kindo alisikia sauti ikimuita wakati akiondoka katika mahakama hiyo ambapo alikuwa amemaliza hatua zote za kuachiwa huru kutokana na msamaha wa Raisi, hakugeuka mara moja kwani aliamini kuwa si yeye aliyekuwa anaitwa. Sauti ile ilipoendelea kusisitiza alisimama na kugeuka. Sura haikuwa ngeni sana machoni mwake lakini hakutaka kuonyesha dalili zozote za kuikumbuka sura hiyo.
"Poti!! Pole sana kaka….nafurahi kukuona mtaani tena dah!! Ya Mungu mengi" mtu huyo mfupi mnene aliyekuwa ananyemelewa na kitambi alizungumza kwa furaha.
"Sijakukumbuka ujue!!!" Kindo alinyanyua mdomo wake na kuzungumza. Bwana yule alifuta tabasamu lake usoni na kuvaa huzuni alimsikitikia Kindo kwani aliamini ni maisha ya kukosa uhuru yalikuwa yamemsababishia hali hiyo ya kukosa kumbukumbu.
"Kura tumekura pakurara je!!!!" badala ya kujibu alitoa kauli hiyo, Sajenti Kindo akashtuka sana kisha akamkumbatia kwa nguvu zake zote mzee huyo, machozi yakawa urembo katika nyuso za wawili hawa.
"Poti Magembe ni wewe kaka???" aliuliza Kindo pasipo kuamini macho yake.
"Ni mimi poti!!! Pole sana kaka, tuliumia sana kukupoteza uraiani" alizungumza kwa huzuni huku akimkagua Kindo kwa macho jinsi alivyozeeka ghafla ndani ya miezi ishirini na nne (24). Walizungumza mengi wakiwa wamesimama wima, Kindo bado alikuwa mkakamavu kiasi licha ya masumbufu ya maisha ya mahabusu bado alikuwa imara. Walikumbushana mengi sana yakiwemo maisha yao ya uaskari tangu wakutane Singida na baadaye Kindo akahamishwa kwenda Mwanza.
"Vipi na wewe ulihamishwa nini??" aliuliza Kindo.
"Ndio hivyo kaka, yaani baada ya wewe kutupwa huko ndani wiki mbili baadaye nikahamishiwa hapa, hivyo niliipata stori yako punde tu baada ya kuhamia hapa. Mazungumzo yalikuwa mengi sana lakini hasahasa kumbukumbu ndio zilitawala.
"Poti hapa nilipo ni kama nashuhudia muujiza nimeachiwa, sina kazi nimefukuzwa tayari, hapa nilikuwa natembea kwenda nisipopajua nashukuru nimekuona, huu mji ninauchukia sana nahitaji sana kurudi nyumbani kwangu huko Singida hapa Mwanza hapana, ngoja nirudi nyumbani…lakini poti!! Mi hapa sina hata nauli, tusizungumzie njaa ninayoisikia hapa hii nitaivumilia…suala ni nauli" alijieleza Kindo kwa sauti ya chini. Magembe akawa amemuelewa.
Kitu cha kwanza walipata chakula ambacho Kindo hakikukifurahia sana, baada ya hapo wakaelekea nyumbani kwa Magembe maeneo ya National housing. Alipumzika kwa siku mbili pale wakati Magembe akihangaika huku na huko hatimaye akapata kiasi cha pesa akampatia Surgent Kindo, akashukuru akaaga na kuondoka.
Siku iliyofuata akaiacha ardhi ya Mwanza.


*****


Maongezi kati ya Michael na John yaliendelea baada ya John kumaliza mazungumzo yake kwenye simu na Bruno mazungumzo yaliyochukua takribani nusu saa huku John akizungumza kwa makini na utulivu asiweze kusikiwa na mtu yeyote. Hali hiyo ilizidi kumtia Michael katika jitimai la nafsi. John aliporejea mezani tayari huduma kutoka jikoni ilikuwa tayari, wakaanza kula na kunywa baada ya hamu kuanza kuwaisha ndipo maongezi yakaendelea.
"Michael naamini una ukaribu flani na Matha!!!" John alisema, lilikuwa shambulizi kubwa sana lililomzidi ujanja Michael akayumba kimawazo lakini hakuanguka, wasiwasi wake ulikuwa wazi sana lakini bahati ilikuwa kwake kwani John alikuwa ameinama akichezea vipande vya mifupa vilivyosalia katika sahani.
"Ndio kwa sasa nipo naye karibu tofauti na mwanzo wakati sijamzoea" alijaribu kujibu mashambulizi Michael.
"Unamchukuliaje kwa jinsi alivyo sasa na kipindi cha nyuma"
Mimba!! Mimba!! Mimba!! Kengere za hatari zililia kichwani mwake.
"Sijaona mabadiliko sana" alijibu huku akiwaza juu ya uwezekano wa swali hilo kuhusisha mimba.
"Michael natamani sana ungejua ni kiasi gani mimi nampenda Matha na nilivyohangaika naye hadi hapa tulipo, ungelijua hilo nadhani ungenionea huruma" aliongea kwa huzuni sana John. Michael akaanza kutetemeka miguu alitamani amtumie ujumbe Matha lakini alihofia huenda tayari simu yake ipo mikononi mwa John hivyo kwa kitendo cha kutuma ujumbe angeongeza maradufu hasira za John.
"Michael Msombe!!!! Nisaidie kitu kimoja tu!! Naamini unakiweza"
"Ni kipi hicho??"
"Unapafahamu kwa Matha??"
Mtego!!!! Alishtuka Michael
"Hapana sipafahamu, sijawahi kwenda" alidanganya Michael kwani aliwahi kukitumia kitanda cha Matha kwa masaa kadhaa kufanya mapenzi na binti huyu mpenzi wa John Mapulu. John alimtazama Michael usoni kwa muda huku akiwa kama anasoma kitu fulani.
"Ok!! Nitakuelekeza….au nitakupeleka…nahitaji msaada wako, wewe ni mwanaume kama mimi" alizungumza John, pombe ilikuwa kidogo imemchangamsha.
"Nimekuelewa kaka" alijibu huku akimeza funda la bia na kukunja sura yake ili kuupokea ukali wake tumboni.
Kimya kikuu kilitawala kwa muda kila mtu alikuwa anawaza na kutenda la kwake hadi walipomaliza na kulipia huduma walizofanyiwa kisha wakaondoka baada ya kuwa wamechukua makopo kadhaa yaliyojazwa bia.
"Endesha!!!!" John alimwomba Michael.
"Sina uzoefu na hizi left hand kaka" alijitetea Michael.
"Ah!! Madereva wa VETA na nyie mna matatizo kweli" alitania John huku akiingia katika kiti cha dereva, safari nyingine ikaanza. Muziki wa hip hop ndio ulitawala ndani ya gari, John aliweza kuimba mistari aliyoifahamu na Michael akijiumauma pale anapoweza hadi gari iliposimama maeneo ya Buzuruga jirani na stendi ya mabasi yaendayo mikoani, ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Nyegezi.
"Unaona lile ghorofa pale, acha hilo linalomeremeta hiyo ni bar, hili la pembeni yake, chumba cha tatu juu, hapo ndipo anakaa Matha, fanya kama surprise sawa" alielekeza John.
"Sasa naenda kufanya nini???" aliuliza Michael. John alijigongesha kichwa chake katika usukani na kusababisha gari ipige honi isiyo na maana, John alikuwa anajishangaa kwani alikuwa hajampa maelekezo yoyote yale Michael.
"Dah!! Mapenzi haya, ok!! Michael kwa maneno yako yote yaliyo kichwani naomba ukamweleze Matha kuwa ninammpenda sana" John alisema kisha akatulia kidogo.
"Najua hakuna rafiki yangu mwingine ambaye ataeleweka kwa Matha lakini wewe naamini atakuelewa, naamini hivyo Michael" John akatulia akamwangalia Michael, macho yake yalikuwa mekundu sana dalili zote za kutaka kulia.
"Ni kitu gani simpi mimi?? Najua amepata kimwanaume kinamzuzua lakini mwambie akumbuke tulipotoka!!!!" alishindwa kuendelea akaanza kulia, Michael akashuka garini akaupunga mkono ishara ya kuaga na kutokomea.


Michael aliamini yupo katika mtego mkubwa kuliko yote maishani mwake, suala la kuagizwa usiku wa saa tano kwenda nyumbani kwa Matha aliamini kuwa ni mpango wa kumtia katika hatia yenye ushahidi wa kutosha ili kuhalalisha hukumu yake. Alitamani sana kumpigia simu Matha lakini bado nafsi yake ilikuwa na mashaka.
"Hapana sipigi simu yoyote ile…nitawapa uhakika mapema sana" alizungumza peke yake. Akiwa na simu yake mkononi badala ya kumpigia Matha alimpigia John, simu yake ikawa inatumika. Akakata baada ya dakika tano John akapiga.
"Vipi mdogo wangu umepotea nini??"
"Umejuaje?? Umesema chumba namba??" alizuga Michael
"Namba tatu upande wa kulia, pembeni yake kuna jiko" alielekeza John baada ya kujilazimisha kucheka kidogo.
"Poa kaka nimeuona mlango, haya baadae" aliaga.
Kwa tahadhari kubwa sana aliufikia mlango, palikuwa kimya sana lakini hilo halikumtisha haikuwa mara ya kwanza kwenda mahali usiku, mara nyingi akiwasindikiza akina John huwa ni usiku. Mlango ulikuwa umerudishiwa kidogo bila shaka muhusika alikuwa hajalala bado. Michael aligonga mlango kwa utaratibu sana. Sauti kutoka usingizini ilimuuliza yeye ni nani hakujibu akausukuma mlango na kuingia ndani.
"Matha!!! U hali gani??"
"Michael!!!!" aliita kwa mshangao mkubwa Matha huku miguu yake tayari ikiwa sakafuni, mikono ikiyapikicha macho yake yaweze kupambana na giza lililokuwa limetanda.
"Upo na nani??"
"Peke yangu kwani vipi???" alihoji Matha kwa sauti ya chini sana huku akiuendea mshumaa na kuuwasha, chumba kikapata mwanga.
"Matha umemfanya nini John"
"Hamna kitu kwani vipi??"
"Una uhakika upo peke yako??"
"Nipo peke yangu jamani sasa haka kachumba na wewe huoni au??" alisema kwa ghadhabu kidogo.
"John ameanza kutushtukia" Michael alisema kisha akaelezea stori yote ya siku hiyo wakiwa na John, Matha alionekana msikivu sana na ambaye huenda angeuliza maswali mengi sana baada ya hiyo simulizi lakini haikuwa hivyo.
"Ujue Michael, huyu John huyu anataka kuchanganyikiwa yule John yule niachie mimi, wewe haumuwezi hata kidogo, yaani yule John…." Matha akiwa anayazungumza hayo alikuwa mbele ya Michael, akiyabinyabinya mabega yake, punde akawa amemkumbatia kabisa, joto kali kutoka kwa Matha, pombe alizokunywa Michael zikaungana kwa pamoja kumshabikia shetani, mapepo yakaruhusiwa kuamka Michael akawa ameagizwa na John kwenda kuzini na Matha, Michael akakisahau kilio cha mwanaume jasiri kama John. Michael akatumia masaa manne kumbembeleza Matha, wakaoga pamoja kwa mara ya kwanza. Walisahau hata mimba iliyokuwa inakua taratibu katika nyumba ya uzazi ya Matha.
"Mwambie John asante sana kwa zawadi eeh!!..mwambie awe anakuagiza kila siku tena usiku ndo inapendeza" Matha alimtania Michael wakati anaondoka. Michael akatikisa kichwa akatabasamu akaondoka. Tayari ilikuwa saa kumi adhuhuri. Kutoka Buzuruga kwenda Mecco ni mbali kiasi lakini Michael aliamua kutembea kwa miguu. Wakati akiwa kwa Matha hofu haikuwepo lakini alipokaribia Mecco, hofu ikamtwaa upya akaanza kumuogopa John, kitendo alichotoka kufanya na Matha kikamtia hatiani tena, hatia ikainyanyasa nafsi yake akaukosa uhuru wa nafsi.
"Hujalala mpaka sasa hivi kaka??" aliuliza Michael baada ya kumkuta John sebuleni akiwa macho anaangalia luninga.
"aaah!! Nilale wakati askari wangu hujarejea bwana!!!" alijibu kwa furaha John .
"Dah!! Nimekuja kwa miguu, si unajua tena daladala hazijaamka bado" alisema kwa utulivu huku naye akichukua nafasi.
"Mh!! Una mambo kaka, nadhani shughuli ilikuwa nzito sana"
"Aah!! Kiasi chake lakini kawaida"
"Si kawaida yaani hadi kufikia suala la kuoga si mchezo ati!!!" alisema John, kauli iliyovunjavunja ujasiri wa Michael, almanusura apige goti kuomba msamaha kwa aliyoyafanya muda mfupi uliopita lakini alisita akabaaki kushangaa.
"Mh!! Aaah!!! Umejuaje kaka" alijipa ujasiri wa bandia na kuuliza.
"Marashi gani ya Matha nisiyoyajua mimi???? Sabuni uliyotumia ni Candy na marashi ni Halloween uongo uongo!!!" alisema kwa utani John ili kumdhihirishia Michael kuwa anamfahamu Matha nje ndani.
"Dah!! Na Matha kanambia hivyo hivyo nikakataa kumuamini mh!! Mnajuana nyie watu si kitoto" alipata uongo wa kujibu Michael.
"Hah!! Matha kakwambia ehee ilikuwaje??" John alikaa vizuri aweze kumsikia Michael vyema.
"Siwawezi nyie…hamuwezi kuibiana kama mnajuana hivyo" alijibu pasipo imani hata kidogo kwani alijua kila kitu tayari John anajua. Michael hakuelewa kuwa kuendelea kusema uwongo ndio yupo sahihi ama auseme ukweli aujue mwisho wa mchezo.
"Nimezungumza na Matha, kwanza amestushwa na imani yako ndogo na amesema kesho niende anipe kitu nikuletee na amesema asante sana kwa Surprise!!!!!" alijilazimisha kufurahi Michael lakini hatia yake iliimeza furaha yote.
"Hata mimi kanitumia meseji!!! Kashtuka sana najua kukuona usiku huu??" aliongezea John. Michael bado hakuelewa kama John alikuwa hajashtukia kinachoendelea ama la!!!
"Vipi kesho muibukie basi au vipi, mi ntakutoa za viroba na nyama choma" kwa sauti iliyojaa ubembelezi John alimsihi Michael.
"Ngoja nikalale maana nimechoka mie, shem kanidekeza hadi nimeoga dah!! Sijui alijuaje kuwa sikuoga wakati natoka" Michael alisema, John akamuunga mkono kwa kicheko kikali cha furaha. Siku ikaisha hivyo tena walakini ukiwa bado umetawala.


Michael aliingia chumbani kwake, hakuamini kama siku hiyo inakatika bila John Mapulu kuusema ukweli wote juu ya uovu aliougundua dhidi yake. Usingizi ulimchukua mapema sana kutokana na uchovu na ulevi wa siku hiyo. Alijilazimisha kuwa na amani ilhali moyoni haikuwepo hata chembe. Michael aliamini kuwa alikuwa mtegoni.
"Mh!! Sijui kama patakucha salama!!" ni wazo la mwisho kichwani mwa Michael kabla hajapitiwa na usingizi mzito.
Majira ya saa nne asubuhi ndipo alishtuka kutoka usingizini lakini alitumia nusu saa nyingine kuuruhusu mwili wake ubanduke kitandani. Njaa ilikuwa inamuuma lakini hakuwa na hamu na kitu kingine zaidi ya supu. Hang over zilikuwa zimemtawala!!
"Oyo!! Huoni au mbwembwe tu!!!" sauti ya John ilimsimamisha Michael aliyekuwa anataka kutoka nje huku akipiga mluzi bila hata kutoa salamu. Michael alisimama na kumwangalia John kwa hofu.
"Ah! Sijakuona wala nini, nawaza tumbo tu hapa nataka nikarekebishe kiaina si unajua tena!!!" alijibu Michael huku akijiegemeza kwenye mlango ambao ulikuwa nusu wazi nusu umefungwa.
"Nilikuchukulia supu na chapati nenda ukacheki jikoni!!" John alimwambia Michael kwa sauti ya upole sana. Kengele za hatari zikalia kichwani mwa Michael. Sumu!!! Aliwaza mara moja kabla ya kushukuru na kujongea jikoni kwa ajili ya hicho alichohifadhiwa.
"Ukimaliza kula uniambie kuna jambo nahitaji tuzungumze!!" John alimwambia Michael ambaye aliupokea ujumbe huu akiwa anakaribia kulifikia jiko. Uoga ulikuwa umeitwaa nafsi yake, kila jambo alilofanyiwa na John alitia walakini ndani yake Hatia iliyokuwa inamkabili ndiyo ilimhangaisha. Kwa mwendo wa kunyata kama mwizi wa njiwa Michael alichukua kipande kidogo cha nyama iliyokuwa katika supu na kurushia paka aliyekuwa akifugwa hapo kwao. Paka alikitafuna kipande kile kwa shangwe zote hata kabla hakijatua chini vizuri kisha akajilambalamba ulimi na kutoa mlio wa nyauuu!!! Huku jicho lake likimtazama Michael kwa matamanio ya kupewa tena kipande cha nyama. Michael alisubiri kwa dakika kadhaa na yule paka naye akisubiri kuongezwa kipande kingine. Paka hakukumbwa na mushkeli yoyote ile. Chakula kilikuwa salama!! Michael alikuwa katika maisha ya mashaka sana!!
"Ah!! Kama ameniwekea sumu juu kwa juu bwana maisha gani haya ya wasiwasi? Bora nife!" alijisemea kwa sauti ya chini Michael huku akiivamia supu ile ambayo ilikuwa ya moto bado, hakujiandalia chakula mezani alimaliza kila kitu pale pale jikoni.
"Asante sana braza maana mh!!!" Michael akiwa na glasi ya maji ya kunywa baridi kabisa alimshukuru John.
"Hapo sasa safiiiiiii!!!!" alizungumza John kwa furaha.
"Ah!! Hapa hata nisipouona mchana poa tu" Michael alijibu huku akichukua nafasi yake katika sofa iliyokuwa ikiangaliana na sofa aliyokalia John.
"Michael nina zawadi yako nahitaji nikupe leo nadhani utafurahia"
"Zawadi kwa lipi kaka nililofanya"
"Jana umetumia muda wako mwingi sana kuzungumza na Matha nimeyaona mabadiliko leo mabadiliko makubwa nilikuwa na Matha asubuhi ya leo hapa!!" John alizungumza huku tabasamu likichanua katika mdomo wake.
"Aaah!! Amakweli leo nimelala sana"
"Kwa suala hilo nahitaji kukupongeza!!!"
"Usijali wewe ni kaka yangu" Michael alisema huku hasira zikiwa zimemtawala ndani ya nafsi yake pepo wa wivu akaanza kumtafuna taratibu, akaanza kuhisi Matha ni mali yake peke yake.
"Hata kama lakini unastahili zawadi" alisisitiza John. Michael hakupinga zaidi ya kukubali kwa shingo upande hiyo zawadi.
"Matha amekuja??? Muda gani na saa ngapi ameondoka?? Au mtego huu?? Eeh!! Mungu nisaidie" baada ya muda mrefu sana kupita Michael alikumbuka kupiga dua.
Au wananichora hawa kasha wanitoe kafara! Alijiuliza.
****


***MICHAEL anazidi kujikita katika penzi la MATHA.
***JOHN hajaushtukia mchezo...anamuamini sana Michael.....
***NINI KITATOKEA SIKU AMBAYO JOHN ATAGUNDUA KUWA MICHAEL ANAMZUNGUKA.
KUMBUKA JOHN NI MTU KATILI NA ANAUA ANAVYOTAKA.


Sangomwile Jullie Z mugaru VAN HEIST
 
Story zako nazipenda maana kila unayosimulia nakuwa najua hayo maeneo kuanzia ya dodoma sasa ya mwanza
 
Ila kweli nimeamini pepo wa ngono ana nguvu....yan michael akiwa na matha anasahau kabisa ukatili wa huyu yohana
 
John vs Michael..., kila mmoja kawa mjanja mjanja, sijui wana lengo gani, ngoja nisubiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom