Riwaya - Balaa

SIMULIZI: BALAA.
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU: 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA TANO

Katika akili ya Dokta Kilumba alikuwa anajua yule mwanamke aliyeongea na kule baa, Alice baamedi, mwanamke aliyekubaliana nae kule katika baa ya Masoko by night ndiye alikuwa anagonga mlango muda ule. Dokta Kilumba aliusogelea ule mlango bila wasiwasi wowote. Akiwa amejifunga taulo jeupe safi kiunoni, huku juu akiwa kifua wazi.

Dokta Kilumba alipofungua tu mlango alikutana na Balaa! Alikutana na dhoruba kali sana. Alijikuta amesukumwa kwa nguvu na kifua cha kiume cha Dokta Yusha, msukumo ambao ulimrudisha ndani kwa kasi na kumdondosha chini moja kwa moja. Dokta Kilumba hakujiandaa kabisa na tukio lile, alitegemea kukutana na kukumbatiwa na kifua laini cha mrembo Alice, lakini kwa bahati mbaya kabisa alikutana na kitu tofauti, alikutana na kifua kigumu cha kiume, kifua cha Dokta Yusha.

Baada ya anguko lililotokana na msukumo wa kifua cha dokta Yusha. Kwa mwendo wa taratibu dokta Yusha alimfata Dokta Kilumba pale chini. Wakati Dokta Yusha akimfata Dokta Kilumba pale chini, Mwanasheria mlevi alibaki pale mlangoni, alikuwa anafunga mlango wa chumba kile cha kulala wageni kwa ndani. Mambo yote hayo yalifanyika kwa muda mfupi sana, na kwa umakini mkubwa pia.
Dokta Kilumba alibaki ametumbua macho pale chini, sakafuni. Kichwani mwake yalikuwa yanapita maswali mengi sana, bila ya kuwa na majibu. Ingawa Dokta Kilumba alikuwa anawafahamu vizuri watu wale wawili lakini Dokta Kilumba hakujua kabisa watu wale wametokea wapi baada ya kutoweka kwa mm muda mrefu, na wamekijua vipi chumba chake. Dokta Kilumba hakupata muda wa kutafakari zaidi, Kofi la nguvu la mkono wa kulia toka kwa Dokta Yusha lilitua katikati ya uso wa Dokta Kilumba. Dokta Kilumba aliona vimulimuli. Kilikuwa kitendo cha ghafla sana na Dokta Kilumba hakutegemea kabisa kufanyiwa vile na Dokta Yusha....

Dokta Kilumba kikaangoni...atatoka salama?

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA SITA

Hali ilikuwa tete mle ndani kwa upande wa Dokta Kilumba. Vijana wale wawili makini walikuwa wamembana Dokta Kilumba kisawasawa. Mwanasheria mlevi nae alitoka pale mlangoni na kusogea pale walipokuwa Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Siku hiyo Mwanasheria alikuwa hajatia hata tone moja la pombe, lakini mwendo wake ulikuwa wa kilevi. Sauti yake ilikuwa ya kilevi. Ama hakika Mwanasheria mlevi alikuwa ameathiriwa sana na pombe, pombe ilikuwa imeweka kambi katika mishipa yake ya damu. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba.

"Dokta Kilumba, daktari mkuu wa hospitali ya Kinyonga. Daktari msomi uliyekabidhiwa dhima kubwa katika wilaya hii. Dhima ya kuokoa uhai wa wagonjwa. Daktari makini sana, uliyepata mafunzo yako ya udaktari huko katika jiji la Mumbai, India. Daktari mzalendo, uliyekataa kufanya kazi mjini, na kuamua kuja huku wilayani, porini eti kuja kusaidia wananchi maskini wa huku kama ulivyodai mbele ya jopo la madaktari bingwa. Unakumbuka ulikataa kufanya kazi Muhimbili? Ulikataa kufanya kazi katika hospitali ya Taifa, hospitali iliyopo jijini Dar es salaam, unakumbuka Dokta?
Ulikataa dokta, inamaana ulikuwa na mpango huu kabla ndomana uliamua kuja huku kujificha ili ufanye kwa amani ufarauni wako? Una roho mbaya sana Dokta Kilumba,

Zaidi John Kilumba sindo jina lako, nakufahamu vizuri Dokta. Si ulisoma shule ya msingi Kigoma wewe? Au nikwambie mwaka uliomaliza? Jua nakufahamu vizuri sana kabla hujajifahamu.
But to make story short, Dokta Kilumba maisha yako yapo mikononi mwangu, ni bahati mbaya sana kwako kwakuwa maisha yako yapo mikononi mwa mlevi, mlevi niliyekubuhu, mlevi niliyopitia mengi sana katika maisha yangu, kuishi na kifo kwangu ni sawa tu, kwa hiari yako na hii hasa kama bado unatamani kuishi naomba ujibu swali langu kwa ufasaha bila kunidanganya....." Mwanasheria mlevi kwa sauti ya kilevi aliweka nukta na kumeza mate, huku akimwangalia Dokta Kilumba kwa umakini mkubwa. Kiukweli Mwanasheria mlevi aliongea maneno yaliyowashangaza wote mle ndani....

Swali gani hilo analotaka kuuliza Mwanasheria mlevi..Mwanasheria mlevi ni nani mbona anayajua mengi..

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
...Macho yalimtoka pima Dokta Kilumba, mtu wa mwisho aliyetaka kuonana nae katika mji wa kilwa alikuwa ni dk Yusha...
¡è¡è¡è¡è¡è
kule porini Daniel Mwaseba aliendelea kuugulia maumivu pale chini baada ya kupigwa lile teke, wakati huo huo tano, sita na mbili walikonyezana kisha kwa pamoja wakamshika Daniel na kumuinua.....


#mapengo usipokuja kumalizia story yako nitaimalizia hata kama siijui... huwezi kutuweka hapa kiasi hiki...

Umenichekesha hahahaaa umeona anakuchosha tu
 
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA SABA

Kule kambini porini Ngome, hali ya mpelelezi Daniel Mwaseba ilikuwa mbaya sana. Wale majamaa walikuwa walikuwa makatili kweli, walikuwa wamemchakaza Daniel Mwaseba vibaya sana. Walimwacha pale chini akiwa nyang'anyang'a, hatamaniki. Tano toka kundi lile la Six killers, jambazi sugu kabisa alisogea pale alipolala Daniel Mwaseba. Tano alimnyanyua Daniel kwa hasira toka pale chini na kumuweka begani, baada ya kumuweka begani toka akaona bega siyo sehemu sahihi, Tano akagairi, akamtoa begani Daniel na kumnyanyua juu, ilikuwa mithili ya mtu kalibeba pipa tupu. Daniel Mwaseba akiwa hoi bin taaban kule juu alifumbua macho yake, Daniel Mwaseba alifikiria harakaharaka, alitoa na kujumlisha akiwa hewani, baada ya kugawanya na kuzidisha akajua inampasa kufanya kitu kuokoa maisha yake. Tano sugu, alimwachia Daniel taratibu, huku akiutega mguu wake ule mzima ili Daniel Mwaseba afikie katika goti la mguu ule, nia yake kuu ni kumvunja kiuno. Na kweli Daniel Mwaseba alikuwa anashuka kule juu kuelekea katika lile goti zima la Tano. Daniel Mwaseba aligari akiwa hewani.
Aliruka sarakasi huku akiachia teke lililotua katika kidevu cha Tano.
Ilikuwa Balaa!
Lilikuwa pigo la ajabu lililomshangaza kila mmoja mle ndani. Hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu aliouonesha Daniel Mwaseba. Pigo lile la ajabu liliondoka na meno mengine mawili ya Tano. Tano alikuwa amepoteza meno manne sasa. Huku Daniel Mwaseba akitua chini akiwa kasimama imara....

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
Simu: 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA NANE

Daniel Mwaseba alikunja ngumi huku aliwaangalia watu wale kwa zamu na umakini mkubwa sana. Sasa Daniel alikuwa tayari kwa lolote!
Daniel mwaseba alizidisha umakini zaidi maana alijua yuko sehemu hatari sana, tena mbele ya watu hatari sana. Watu ambao kuuwa ni kitu kidogo sana kwao, hawajari, hawaogopi.

Mbili wa Six killers naye kwa umakini mkubwa alisogea pale aliposimama Daniel Mwaseba. Mbili alikuwa makini, alikuwa ashazisikia habari kuhusu Daniel Mwaseba. Kwahiyo alikuwa makini kuzizima mbinu zote za Daniel Mwaseba. Mbili alimsogelea Daniel huku akijifanya kutabasamu.

Wakati uleule Tano wa Six killers naye alikuwa anaamka pale chini, akiwa na ghadhabu pasi na mfano. Hasira za kufanywa namna ile tena mbele ya bosi wake, Don Genge. Tano naye alijizoazoa kwa taabu na kumsogelea Daniel Mwaseba. Ilikuwa kushoto Mbili kulia Tano, mbele ya mpelelezi makini, Daniel Mwaseba.
Patamu hapo!

Ghafla! Mbili wa Six killers alifanya kitu cha ajabu sana. Alidanda chini kwa nguvu. Mdando uliomfanya aruke juu na kuanza kujivingirisha mithili ya feni huku akiachia mapigo mawili kwa nguvu yaitwayo kificho.

"Kificho ni pigo asili yake ni Thailand, pigo ambalo mpigaji anapiga kwa siri hata ukiwa makini kiasi gani kumwangalia huwezi kujua katumia kiungo gani cha mwili kupiga, pigo la kificho likimgusa mpigwaji ni kifo moja kwa moja"

Kwa bahati nzuri Daniel Mwaseba alikuwa anaujua vizuri sana mtindo ule wa kificho. Mwenyewe alishawahu kuutimia mara kadhaa mtindo ule wa kificho. Kumbuka katika simulizi iitwayo mpango wa siri. Siku zote, pigo la kificho huzuiwa kwa kificho. Daniel Mwaseba alifanya hivyo. Alizuia mapigo yale ya kificho kwa kificho. Kati ya watu waliokuwepo pale hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu wa Daniel Mwaseba. Mara zote pigo la kificho huondoka na roho ya mpigwaji. Lakini cha kushangaza Daniel Mwaseba alikuwa bado anapumua baada ya pigo lile la kificho toka kwa Mbili wa Six killers.....

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
Back
Top Bottom