Riwaya - Balaa

Haya hata napengo nae anatutenda hivi! siamini! nadhani ana mkwamo kidogo coz namuaminia yeye na Willy gamba si wa kuremba.
 
Jaman mnisamehe buree, ..mambo tu yanaingiliana...nikitoa kitabu tawaambia...poleni kwa kuwakwaza:D
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY.
SIMU! 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI MOJA

"Naitwa Alfred Duto, afisa wa jeshi la polisi, mko chini ya ulinzi" Askari mmoja alitamka huku akiwa kashikilia kitambulisho chake cha kazi imara mkononi.
Daniel Mwaseba na Tano wote walinyoosha mikono juu. kila mmoja akiuchukulia ujio wa askari wale kwa namna tofauti, wakati mpelelezi Daniel akiupokea ujio wa askari wale kwa tabasamu. Kwa sababu ujio wa Polisi wale ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwake. Kwakuwa yeye alikuwa ni askari pia, hivyo walikuja askari wenzake. Lakini kwa Tano lilikuwa ni pigo kubwa sana, kuingia katika mikono ya polisi ni kitu alichokuwa hataki hata kufikiria.

"Haya tokeni nje haraka!" Askari mmoja aliamrisha kwa sauti ya amri.
"Naitwa Daniel Mwaseba"

Askari wote watatu walistuka kusikia jina hilo.
Daniel alishusha mkono mmoja na kutia mfukoni, alitoka na kitambulisho chake cha kazi. Sasa Polisi wakawa makini na yule jamaa mwengine. Huku wakitoa midomo ya bunduki zao kwa Daniel.

Kumbe purukushani zao na makelele wakati wanapigana zilisikiwa na Mhudumu kule nje. Mhudumu ambaye alimpigia simu Meneja wake kumueleza juu ya hofu yake na chumba namba saba, chumba alichofikia Daniel Mwaseba. Meneja nae aliamua kutoa taarifa polisi.

Sasa walikuwa Askari wanne, wakitoka nje na Mhalifu. Kutoka katika hoteli ya kitalii ya Kimbilio, hoteli aliyofikia Daniel Mwaseba, haikuwa mbali kabisa na kituo cha polisi Masoko. Ilikuwa ni pua na mdomo. Walitumia miguu tu kumfikisha Tano kituoni.

Walipofika kituoni Tano aliendelea na Kiburi chake. Hakueleza kitu chochote zaidi ya kusema yeye anaitwa Tano wa Six Killers. Alipewa mateso makali sana na askari Polisi. Mateso ambayo hayakumfanya Tano atoboe siri zake ama siri za kundi la six Killers na mpango wao haramu. Tano aliendelea kuwa bubu. Alilala kituoni siku ile, huku Daniel Mwaseba akirudi mtaani kuendelea na upelelezi wa mauaji na kupotea kwa wanafunzi. Huku akiwa na msamiati mpya kichwani mwake ambao alishindwa kuutambua.

'Six killers'

Kesho yake asubuhi Tano alipelekwa mahabusu, Gereza la wilaya ya Kilwa. Alipakiwa kwenye gari la polisi akiwa kafungwa pingu mkononi. Huku bunduki mbili zikitazama kichwa chake. Gari ilioondoka kwa kasi kubwa sana huku ikipiga ving'ora. Tano alizungusha macho yake huku na huko, kutafuta nafasi ya kutoroka, na ilikuwa hivyo. Tano wa Six killers akiwa hoehae aliiona nafasi akiyoitafuta...

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI MBILI

Tano alijilegeza kidogo ikawa laini kama mlenda kisha akaanguka kwenye bodi ya gari. Askari wote walipatwa na mshangao mkuu, waliacha kumuelekezea ile midomo hatari ya bunduki, walimsogelea huku bunduki zao zikining'inia mabegani.
Lilikuwa kosa la mwaka!
Tano akiwa kajilegeza vilevile alijirusha nje ya ile gari na kushuka katika barabara ya lami.
Balaa!
Tano alifikia vibaya sana katika barabara ya lami, kumbuka gari lilikuwa linatembea kwa kasi kubwa sana. Pia Tano alikuwa amefungwa pingu mikononi. Lakini Tano hakujari hilo hata chembe.
Wale Askari walibaki midomo wazi, na bunduki zao mkononi zikiwa zinawashangaa. Hawakuwa na ujanja wa kuruka kwa kasi ile, ilikuwa ni zaidi ya hatari. Askari walipigapiga bodi ya gari ile ili kumuamrisha dereva apunguze mwendo, maskini dereva hakusikia chochote, mwendo ule ukichanganya na kelele za king'ora, ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Walimuacha Mhalifu hataru sana njiani, wao wakiendelea na kasi yao ya kutisha kuelekea gerezani!

Tano, kwa sasa alikuwa ametapakaa damu mwili mzima, akiwa na maumivu kila sehemu ya mwili wake, maumivu ya kupewa kichapo na Daniel Mwaseba, maumivu ya kuruka katika barabara ya wakati gari ikiwa kasi, tena na kuangukia kwenye lami. Tano alikuwa na roho ya paka! Kwa kutambaa ingawa kwa shida sana alijisogeza pembeni ya barabara, alikuwa na maumivu makali sana, kiasi kwamba alikuwa anashindwa kunyanyuka. Nasema ilimpasa ashindwe kunyanyuka lakini Tano wa Six Killers alijitahidi kunyanyuka, maana kuendelea kukaa mahala pale ilikuwa ni hatari sana kwake. Jamaa alijitahidi kunyanyuka, aliweza, Tano alinyanyuka kwa mwendo wa kusuasua alijisogeza pembeni zaidi ya barabara.

Gari ya polisi ilikuwa inaingia katika viwanja vya gereza la Kilwa. Dereva alipiga kona kwa mbwembwe nyingi huku akifunga breki kali sana. Laiti angejua kama mhalifu Tano hakuwepo kule nyuma ya gari....

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI NA TATU

Gari lilisimama. Taarifa mbaya kabisa ikapenya katika masikio ya dereva. Kwamba mhalifu Tano alijirusha toka katika ile gari wakati ikiwa katika mwendo mkali. Ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa hata sekunde kumi, dereva alirudi kwa haraka katika usukani wa gari ya Polisi na kuligeuza gari kwa haraka pia, kurudi pale mahali ambapo alijirusha Tano. Dakika nne na sekunde thelathini tu zilitosha kuwafikisha pale, askari walishuka haraka haraka kabla gari haijasimama vizuri na kuanza kumsaka Tano. Walichakua katika nyasi zote lakini Tano hakuonekana! Askari waliishiwa nguvu, kwa jinsi Tano alivyojirusha na kufikia na mwendokasi waliyotumia kurudi pale walitegemea kumkuta Tano palepale barabarani. Hayo yalikuwa mawazo yao, lakini Tano hakuwepo kabisa pale barabarani, hata dalili tu kama kulikuwa na kiumbe.

Huko porini Ngome hali ilikuwa ya taharuki sana. Tangu jana yake usiku Tano alikuwa hajarejea kambini. Waliamini Tano amepotea kama alivyopotea Sita. Sasa wanapotea vipi, wanaenda wapi, hakuna aliyekuwa na majibu. Walitafuta sehemu zote walikodhani labda atakuwepo lakini Tano hawakumpata. Mwishowe walienda mahali ambako Tano aliwaambia ataenda usiku, katika baa ya Tiga Tisa. Six killers wote wanne walienda katika baa ya Tiga Tisa. Walikaa meza moja na kuanza kuchunguza mazingira ya pale baa. Hawakupata lolote la maana. Mwishowe Moja aliamua kumuita Mhudumu mmoja ili amuulizie kama alimuona jamaa yao hapo. Kwa bahati mbaya Mhudumu aliyemuita Moja nd'o yuleyule aliyeongea na Daniel Mwaseba kabla. Nd'o yuleyule aliyefanikisha Tano kukamatwa. Mhudumu muoga sana anapokutana na wanaume kama hawa. Haikuwa kazi ngumu kwa vijana mahiri wa six killers kutambua kwamba Mhudumu yule anayajua mengi. Wakaamua nae wamchukue....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI NA NNE

Kwa bahati mbaya kabisa Mhudumu wa baa ya Tigatisa akaingia katika mikono isiyo salama. Mikono hatari ya kundi baya na katili sana kuwahi kutokea katika historia ya Kilwa, kundi la Six Killers. Mhudumu nae akapelekwa porini bila kujua ukatili wa sehemu anakopolekwa na jamaa wale. Na majaa hao makatili sasa walikaa sebuleni na kuwaza na kujadiliana nini cha kufanya baada ya matokeo mabaya sana.

Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu kabisa Tano wa six killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa amejificha katika mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na kurudi kambini kwao, porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano alikuwa anapita katika maumivu makali sana. Alikuwa na vidonda mwili mzima, vidonda ambavyo sasa vilikuwa vinapitiwa na na ladha ya chumvichumvi toka katika mikoko ya pwani.

Askari walirudi kituoni, kutoa taarifa kwamba Jambazi aliyejulikana kwa jina la Tano alikuwa amewarotoka. Kwa haraka sana habari hizo mbaya zikafikishwa kwa Daniel Mwaseba huku askari wakimwaga mtaani kama njugu kumsaka Tano wa six Killers. Daniel Mwaseba alipopigiwa simu, hakujibu kitu chochote kuhusu ile simu zaidi ya kuitikia tu tena kwa sauti ndogo sana.

Mpaka saa sita usiku inaingia ilimkuta Tano pale katika mikoko, muda huo giza lilikuwa la kutisha sana, usiku ukichanganya na uwepo wa mikoko iliyoshonana.
Muda huo wa saa sita ndipo Tano alishuka juu ya mkoko na kuelekea porini Ngome kwa kupitia pori kwa pori.

Hakujua, Tano hakujua!

Nyuma yake hatua kama kumi na saba, kulikuwa na mtu makini anamfata. Mtu ambaye alilijua lile ficho lake muda mrefu sana. Mtu huyo hakutaka kumkamata. Shida yake ilikuwa ni kutaka kujua tu uelekeo wa Tano utakuwa wapi. Yeye alikuwa na shida ya kuyafahamu makazi ya yule jamaa, aliyejiita Tano. Na sasa ndio alikuwa anafanikiwa kuuona uelekeo wa Tano, na kwa umakini mkubwa alikuwa anamfuata Tano kwa nyuma, bila Tano kuhisi jambo lolote....


ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU! 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI NA TANO

Masaa matatu yalitosha kumfikisha jambazi Tano kambini kwao huko porini Ngome. Bila kujua kabisa kama nyuma yake kulikuwa na mtu ambaye aliyekuwa akikanyaga kila sehemu ambapo alitoa mguu wake.
Mtu huyo akiyemfata Tano kwa nyuma alikuwa makini sana, asiyeruhusu kufanya makosa katika kazi yake. Mpelelezi namba moja nchini Tanzania aliyekuwa anaitwa Daniel Mwaseba.
Daniel Mwaseba alitilia shaka uwezo wa mtu yule mapema sana. Aliamua kulifatilia kwa nyuma lile gari pale tu lilipotoka kituo cha polisi likiwa na Tano ndani yake. Daniel Mwaseba alishuhudia vizuri sana jinsi Tano wa six Killers alivyojirusha wakati gari linatembea kwa kasi kubwa sana! Daniel alishangaa sana umahiri wa jambazi Tano. Kwa mwendo uliokuwa linatembea gari lile la jeshi la polisi na kwa jinsi Tano alivyojirusha angekuwa mtu mtu dhaifu kama mimi na wewe angepasuka vibaya sana. Lakini Tano hakuwa mimi na wewe, alikuwa mtu hatari zaidi ya hatari yenyewe.
Pamoja na kujirusha namna ile lakini Tano hakuumia kwa kiasi hiko. Daniel akimshuhudia jinsi Tano alivyokuwa anajikokota na kujificha katikati ya mikoko. Bila kujua kama alikuwa anafuatwa na mtu nyuma yake. Daniel Mwaseba alihakikisha hafanyi kosa lolote kama ilivyo ada yake. Na kweli hakufanya kosa. Wakati Tano wa six killers kajibana katikati ya mikoko, Daniel Mwaseba nae alijibana kwenye mikoko umbali sio mrefu sana na alipojibana Tano. Alikuwa na uwezo wa kumkamata lakini hakutaka kumkamata. Nia yake ilikuwa ni kuona uelekeo wa yule jamaa itakuwa wapi, Daniel Mwaseba alihisi Tano lazima ataenda kwenye maficho yao. Na hicho ndicho kitu ambacho Daniel Mwaseba alichokuwa anakihitaji sana..

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA.
MWANDISHI; HALFANI SUDY.
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA THEMANINI NA SITA

Wahenga walisema subira yavuta heri, na kweli. Saa sita ya usiku alimshuhudia yule jamaa akitoka kwenye mikoko alipojificha. Masaa yote matatu aliyokuwa anayatumia kujiburuza kuelekea porini ngome, Daniel Mwaseba alikuwa nyuma yake. Tano alikuwa kachoka sana, mchoko ulioambatana na maumivu kila sehemu ya mwili wake. Alikuwa anajiburuza kwa shida sana! Daniel Mwaseba alihakikisha hatoi ukelele wowote ule wa kuweza kumsitua yule jamaa. Ilikuwa ni mwendo wa kimyakimya. Porini ilikuwa giza sana, lakini kwa mara nyingine tena Dokta Yusha aliuona umahiri wa yule jamaa aliyekwenda kwa jina la Tano, pamoja na kuwa nyang'anyang'a lakini jamaa alichanja mbuga, na kufika kambini kwao.

Daniel Mwaseba kwa macho yake mawili aliushuhudia ukuta mkubwa sana uliojengwa kule porini. Kimoyomoyo alitabasamu, akijua pale ndipo maficho ya wale watu wabaya. Sehemu sahihi aliyokuwa anatamani kuijua, na sasa aliijua. Alimshuhudia yule jamaa akihangaika kubonyeza kitufe fulani pale mlango, na baada ya dakika kama tano geti lilifunguliwa. Na yule jamaa aliingia ndani ya ule ukuta kwa mwendo wake uleule wa kujiburuza, kisha geti lilifungwa tena. Daniel Mwaseba aliyashuhudia yote hayo akiwa kajibanza nyuma ya mti mmoja.

Ndani ya nyumba kundi la Six killers lilikuwa katika mshangao. Walishangaa Tano kurejea tena kambini. Kila mmoja alikuwa na swali lake la kumuuliza Tano, mtu aliyerudi kimaajabu sana kambini, akiwa na vidonda kadhaa mwilini mwake, lakini hawakuweza kumuuliza chochote. Ruhusa ya kuuliza maswali alikuwa nayo kiongozi wa kundi lile pekee, Don Genge.....

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Mkiona kimya ujue nimetingwa na majukumu yakimaisha hivyo acheni papara hii itaruka hapa Hapa..niombeeni uzima tu..pole kwa nilio wakwaza.Nawapenda wote.
 
Back
Top Bottom